Nisaidieni mawazo pls

M-bongotz

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
1,729
386
Wadau hebu nisaidieni..

Traditionally mwanaume ndio mwenye jukumu la kutunza watoto, lakini hivi ni sawa kama mama wa watoto nae ana kipato kuacha kununua hata kiatu cha mtoto wake mwenyewe wa kumzaa akisubiri kuwa baba mtoto atabeba jukumu?.,hebu wenye experience zaidi na masuala haya mnisaidie jamani.
 

Roulette

JF-Expert Member
Dec 15, 2010
5,592
5,336
Huo ni ujinga. siku hizi wote wanafanya kazi coz mtu mmoja hatoshi kuitunza familia. lazima kusaidiana. sasa hizo hela zake ni za nini kama sio za watoto?
 

Jestina

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
4,838
1,699
utajiju hilo ni jukumu la mwanaume,mwanamke hela yake ni ya kuendea saloon kutengeneza kucha na kununua viwalo vipya apendeze akuvutie.
 

M-bongotz

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
1,729
386
utajiju hilo ni jukumu la mwanaume,mwanamke hela yake ni ya kuendea saloon kutengeneza kucha na kununua viwalo vipya apendeze akuvutie.

Astaghafirulah.,hata wewe Jestina unasema hivyo, kwa maisha kweli unadhani ni rahisi kuyaendesha solo?
 

shosti

JF-Expert Member
Dec 21, 2010
4,914
1,497
ana wazimu huyo...mtoto alivyo mtamu jamani una pesa unashindwa kumnunulia kitu!
 

Nailyne

JF-Expert Member
Dec 11, 2010
350
111
si bure ukiona hadi mwanamke anakataa kununua viatu vya mtoto wake..,liko jambo hujatueleza,hakuna mwanamke bahili linapofika suala la mtoto wake
 

Ave Ave Maria

JF-Expert Member
Apr 22, 2011
10,735
5,613
Sio sawa, kwa nini asichangie katika familia yake wakati ana uwezo wa kufanya hivyo? Siku nyingine mwambie awanumulie kwanza watoto alafu yeye atembee peku akisubiri pesa ya mumewe itoke mfukoni na ya kwake akaifiche shimoni!
 

Speaker

JF-Expert Member
Aug 12, 2010
6,327
2,227
sio sahihi bana,haki sawa kwa wote.
Ila kama ulikua unajidai kuwa nazo toka mwanzo na
hutaki mwenzako ashiriki ndo itakula kwako
 

M-bongotz

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
1,729
386
si bure ukiona hadi mwanamke anakataa kununua viatu vya mtoto wake..,liko jambo hujatueleza,hakuna mwanamke bahili linapofika suala la mtoto wake

Hakuna lolote, ni hulka tu ya ubahili ya huyu mdada.,kwani pamoja na kwamba hataki kusaidia kuhudumia wanae lakini hata hela ya kununua mafuta yake ya kujipaka anaomba kwa mumewe.
 

fabinyo

JF-Expert Member
Aug 5, 2011
2,828
1,656
.......sikuhizi mambo ni kusaidia,huyo ni mbinafsi na atakuwa anajenga kwao kimya kimya!!!
 

Evarm

JF-Expert Member
Aug 30, 2010
1,850
1,244
utajiju hilo ni jukumu la mwanaume,mwanamke hela yake ni ya kuendea saloon kutengeneza kucha na kununua viwalo vipya apendeze akuvutie.

Hii si kweli maisha ni kusaidiana, na ndio maana kwenye kiapo cha ndoa huapa kwamba mme na mke watapendana kwenye raha na shida
 

Mamaya

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
4,102
2,065
utajiju hilo ni jukumu la mwanaume,mwanamke hela yake ni ya kuendea saloon kutengeneza kucha na kununua viwalo vipya apendeze akuvutie.

wewe nawe ni dizain ya huyo mwanamke anayelalamikiwa hapa, haufai hata kidogo. Ning'ekuwa mi ndo b.frnd wako kwa point hii tu ning'ekupiga chini bila kuchelewa manake utakuja kuwa kupe kwangu.
 

babalao

Forum Spammer
Mar 11, 2006
427
56
Ukiona katika familia kuna malalamiko kama hayo kwanza itakuwa imepungukiwa upendo lazima kuna kasoro. Kuna familia ambayo kulikuwa na malalamiko kama hayo lakini nilipowasuluhisha niligundua tatizo lilikuwa siyo pesa ila ni kukosekana upendo, kuheshimiana na mawasiliano kwani kutokana na kukuosekana mawasiliano mwanamme alifikia hatua ya kumtumia mke wake matumizi kwa M PESA wakati wanakaa ndani ya nyumba moja. Baada ya kuwasuluhisha tatizo hilo lilikwisha. Sasa ndugu yangu nikuulize jee wewe wakati unamuoa mkeo ulikuwa unampenda na yeye alikuwa anakupenda? AU Mlilazimishwa kuoana? Kama swala dogo la viatu vya mtoto linawashinda kulitatua inabidi mtafakari. Itabidi ukae na huyo shemeji muuangalie uhusiano wenu ili mjue mmejikwaa wapi mkitatua tatizo lenu halisi mtaishi vizuri kuna kitu hapo siyo hivihivi tu!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom