Mama shurti akupokee mzigo wowote hata smartphone yatosha, kisha unatakiwa uketi upumzike na mama akuvue viatu, halafu anakuacha unarelax, huku akikuandalia maji ya kuoga ya uvuguvugu kwa mbali tayari kwa mkulu uoge.
Ukiishakoga unakaribishwa msosi kwa sauti ya mahaba kali kabisa yasema, "poti nkande tayari" huku tabasamu likiwa lakuangalia machoni na mkulu unaitikia kwa furaha maana una uhakika wa msosi, hata kama ni ugali wa mhogo na mboga moja ya majani yaitwa mchunga na bilauli ya maji ya nanasi pembeni.
Wakti wa kula mwala wote maana yeye alikuwa anasubiri wee mchana kutwa mgosi wa ndima mwenyewe urejee home.
Basi mwala wote huku mkiwa mnabadilishana mawazo ya hapa na pale, ni raha sana.