Wadau naombeni ushauri wenu nipo njia panda,Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 29 sasa,nipo njia panda katika kutoa maaamuzi,nina wachumba wawili lakini sijui ni yupi nimchague awe mwenza wangu wa maisha, mmoja amenizidi umri yeye kwa sasa ana miaka 34.
Yeye tangu utotoni tulikuwa tunaishi jirani, tulizoeana sana kama kaka na dada na familia zetu zinajuana vizuri, kwa bahati nzuri mimi nilipokuwa masomoni nchini Africa ya kusini, na yeye pia alikuwa anafanya kazi nchini humo, kwa hiyo tukazidi kuwa marafiki, lakini mwaka 2007 tukajikuta tunaangukia kuwa wapenzi, kwa kweli tulipendana sana na kuzidi kuwa karibu sana, na kusema kweli huyo dada ni dada asiye na makuu na pia anajiheshimu sana,
Tuliendelea na mapenzi yetu mpaka mwaka 2008 mwishoni ambako mimi nilimaliza masomo yangu na yeye pia akawa anamaliza mkataba wake wa kufanya kazi nchini humo.wote tukarudi nyumbani Tanzania, lakini mimi mwanzoni wa 2009 nikapata nafasi ya kwenda USA kuendelea na masomo zaidi, na kumuacha yeye Tanzania kwa kuwa alikuwa anafanya kazi tayari.
Kwa bahati mbaya au sijui nzuri, nilipofika US kuna msichana mmoja ambaye alikuwa rafiki yangu high school Tanzania, mimi nilikuwa Shaban Robert na yeye alikuwa Mziziima , Yeye ana umri wa miaka 26.Alinipokea na kusema kweli huyo msichana nilimpenda sana tena sana tangu tulipokuwa high schoool japokuwa sikuwahi kumwambia,tukawa marafiki tena.
lakini katika huo urafiki wetu tukajikuta tunangukia kuwa wapenzi, kusema ukweli sijawahi kupenda kama ninavyompenda huyu msichana. na nakubali kuwa nilifanya kosa kubwa la kutomueleza ukweli kuwa mimi tanzania nimeacha mtu.
Lakini mwishoni wa 2009 yeye alimaliza shule na wazazi wake wakamtafutia kazi Tanzania kwa hiyo ikambidi aniache mimi nikimaliza masomo na yeye kurudi Tanzania, kwa matumaini ya kuwa nikimaliza na mimi nitarudi Tanzania tufunge pingu za maisha.Hapo ndio tatizo linapokuja, wote wawili wananisubiri nirudi, japokuwa yule wa kwanza haijawahi pita siku bila kunipigia simu, na pia najua ananipenda sana lakini naogopa naona amenizidi sana umri inaweza kuleta matatizo hapo baadaye.
Japokuwa yeye tunajuana vizuri sana nje ndani, na anajiheshimu sana tena sana na hata mama yake anajua mimi ndie mchumba wake pia uwa ananipigia simu naongea na mama yake pia , Lakini mimi nampenda sana huyu wa pili japokuwa huyu wa pili yeye inaweza pita hata siku tatu hajanipigia simu wala messegi, na pia naona kama yuko desperate sana na kuolewa, maana anataka kufanya mambo kwa haraka sana, mpaka nakuwa nahisi anaweza pata mtu huko nyumbani ambaye tayari ameshasettle akamuoa.
japokuwa naye mama yake ananijua mimi ndie mchumba wake na hata dada yake na kaka yake wanajua hilo,nilikuwa niiende tanzania likizo mwezi huu lakini nimearisha kwa kuogopa itakuwaje nikifika Tanzania maana wote wananisubiri, na huyu wa pili alitaka sana nije eti anitambulishe kwa wazazi wake na mimi nimtambulishe kwa ndugu zangu, hapo ndio roho yake itatulia maana kwa sasa hana uhakika kama mimi ni wake kweli.
Na juzi huyu wa pili kanipigia simu anasema kwa kuwa siendi Tanzania yeye atakuja huku US mwezi wa tisa ili eti nimpe mimba then tuwe na kitu ambacho kitatufanya tuwe pamoja.Na yule dada wa kwanza naye anataka kuja huku x-mas japokuwa yeye ajasema kama anataka mimba au lah ila nahisi naye ni hilo hilo anataka, sasa hapo ndio maisha yangu yanapokuwa magumu mpaka nakosa raha naombeni sana ushauri wenu wadau tafadhari japokuwa najua mimi ndie nimejitakia yote hayo lakini naombeni ushauri, yupi ananifaa kati ya hao nichukue uamuzi?