Nipo njia panda kuhusiana na kampuni ya interchicks

nicholas1

New Member
May 28, 2016
4
4
Habarini wana jamvi?Naitwa Nicholas naishi morogoro,nashughulika na biashara na ufugaji.Kifupi ni kwamba nimepata tatizo katika kuku wa nyama niliowachukua kutokakampuni ya interchick kupitia wakala wao hapa morogoro ambao ni duka la madawa linaitwa Imuka.Yaani hadi sasa bandani kwangu kuku zaidi ya 50 wanakufa ovyo na hao kuku nimejaribu kuwachunguza sijaona ugonjwa wowote.

Ilinibidi niende duka nililochukulia vifaranga wao wanachonijibu ni kuwa inaonekana batch tuliochukua haikuwa sawa kwani tayari kuna wenzangu zaidi ya watano wameripoti tatizo kama hilo.Mimi nilichukua tarehe 25 mwezi wa nane yaani hadi leo hao kuku wana wiki mbili... Nitaendelea kesho.

Naendelea, Sasa nahitaji kupata angalau namba ya hawa jamaa wa interchick kwani nikiwapigia kwa simu yao ya ttcl hawapokei na hii hali si mimi peke yangu kuna wafugaji wenzangu wengi wameathirika na tatizo hili.Nachoshangaa ni kuwa kwa nini tatizo linalotokana na kampuni lituathiri sisi wafugaji hasa sisi ambao ni wadogo.?

Hadi sasa bandani kwangu tayari kuku 123 pamoja na wale 50 wa mwanzo na nilichukua kuku 150.Kwa stahili hii tutafanikiwa kupigana na umaskini na kuenda na kasi ya maendeleo tunayoyataka?

Ninachoomba cha ziada ni ushauri wa nini cha kufanya kuhusiana na hili au kama kuna muwakilishi wa kampuni hii tuwasiliane kwa namba hii 0719974886
 
Bora wewe ni wanyama' wamayai ndio hawafai kabisa interchiks ni kampun ya hovyo kabisa hawa jamaa hawana wataalamu hata chakula chao ni shida kuku wanadonoana
 
Mkuu achana na hao interchick, zamani walikuwa vizuri Ila siku hizi ni bomu tupu. Hata ukiwapata hawarudishi hela yako.
 
Nashukuru Mungu, mimi natotolesha mwenyewe na nina tengeneza chakula mwenyewe kwa kufuata formula toka kwa wataalam.
 
Habarini wana jamvi?Naitwa Nicholas naishi morogoro,nashughulika na biashara na ufugaji.Kifupi ni kwamba nimepata tatizo katika kuku wa nyama niliowachukua kutokakampuni ya interchick kupitia wakala wao hapa morogoro ambao ni duka la madawa linaitwa Imuka.Yaani hadi sasa bandani kwangu kuku zaidi ya 50 wanakufa ovyo na hao kuku nimejaribu kuwachunguza sijaona ugonjwa wowote.

Ilinibidi niende duka nililochukulia vifaranga wao wanachonijibu ni kuwa inaonekana batch tuliochukua haikuwa sawa kwani tayari kuna wenzangu zaidi ya watano wameripoti tatizo kama hilo.Mimi nilichukua tarehe 25 mwezi wa nane yaani hadi leo hao kuku wana wiki mbili... Nitaendelea kesho.

Naendelea, Sasa nahitaji kupata angalau namba ya hawa jamaa wa interchick kwani nikiwapigia kwa simu yao ya ttcl hawapokei na hii hali si mimi peke yangu kuna wafugaji wenzangu wengi wameathirika na tatizo hili.Nachoshangaa ni kuwa kwa nini tatizo linalotokana na kampuni lituathiri sisi wafugaji hasa sisi ambao ni wadogo.?

Hadi sasa bandani kwangu tayari kuku 123 pamoja na wale 50 wa mwanzo na nilichukua kuku 150.Kwa stahili hii tutafanikiwa kupigana na umaskini na kuenda na kasi ya maendeleo tunayoyataka?

Ninachoomba cha ziada ni ushauri wa nini cha kufanya kuhusiana na hili au kama kuna muwakilishi wa kampuni hii tuwasiliane kwa namba hii 0719974886
chukua mkuza chick.wako vizuri ni wanzania wenzetu
 
Bora wewe ni wanyama' wamayai ndio hawafai kabisa interchiks ni kampun ya hovyo kabisa hawa jamaa hawana wataalamu hata chakula chao ni shida kuku wanadonoana
Hili tatizo naona liko kwenye kampuni zote, mi nilifuga napoko wakafa kuku 1000 wa mayai na walikuwa ndo wameanza kutaga nilipata hasara ya ajabu sitaki hata kukumbuka! Ukienda kulamika wanasingizia ni tatizo lako mfugaji wakati unakuta ni zaidi ya watu watano mmekumbwa na hilo tatizo! Sielewi hatima yetu wafugaji ni nini kama hawa jamaa wanaturudisha nyuma kihivyo! Serikali yetu nayo naona Inahitaji kuangalia kwa jicho la pili upande huu wa ufugaji ili kujua jinsi ya kuwabana hawa jamaa wawe walau wanaturudishia fidia..imagine umekopa benki si ndo mwanzo wa kufilisika wajameni? Ukienda kwenye maabara za mkoa unaulizwa kuku ji wa kampuni gani ukitaja mbili kati ya hizo unaambiwa ni typhod ila ukitaja mfano wametoka kenchick kenya unaambiwa ni marecks ina maana wameshateka mpaka hao wanaotuchunguzia hao kuku hivyo hupati pahala pa kwenda kudai fidia
 
Chukua vile vya Arusha vya TPF vizuri sana hasa mbegu yao nzito, hao vifaranga kawachukulie Dr's report ujue sababu kama chanzo sio kwako, kawadai waonyeshe report
 
lkn pia usipo safisha banda lako vzr pia inatokea tatizo kama hilo japo hio kampuni kweli haiko vzr kihivyo. nakumbuka miaka miwili iliopita tulikua tunachukua hapo interchick vifaranga 120 vilikufa baada ya uchunguzi ikaonekana kunakosa limefanyika walivyokua wanatotoleza kwaio waliwalipa watu wengi sana vifaranga wengine
 
Back
Top Bottom