Nipeni maarifa kuhusu biashara ya kuprint Tshirt

kokudo

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
2,546
1,662
Wakuu Habari za majukumu, naomba kujua kuhusu hii biashara ya kuprint Tshirt hasa ile local ambayo wanatumia ki unao flani hivi.

Nachotaka kujua, namna unavyoweza kujifunza kukitumia hicho kifaa je logo kabla hujai print unaifitisha vipi kwenye hicho kimachine?

Mwenye darasa tafadhali tufungue macho.

=======

Jinsi ya kuchapa/kuprint fulana(t-shirt) kwa kutumia vifaa vinavyopatikana kirahisi.

print1.jpg

Uchapishaji fulana kwa kutumia Screen inaweza kuonekana ngumu, lakini katika njia ya kuchapa kwa kutumia screen nyumbani ni rahisi. uchapishaji kwa kutumia Screen ni njia nzuri ya kuchapa mashati mengi kwa aina ileile ya logo au maneno. Hizi ndizo hatua Unazotakiwa kuzifuata kwa mtiririko ili kufanikiwa kuwa mmoja kati ya wachapaji wazuri wa Tisheti(fulana).

Mahitaji
Kitanzi/pete duara ya plastiki au mbao(Embroidery hoop) - Tumia kwa kuzingatia ukubwa unaoendana na dizaini yako. Zinaweza kupatikana katika maduka yanayouza vifaa vya upambaji kwa mikono (craft shop).

• Pazia nyavu(Gauzy curtain) - Tumia pazia lenye uwazi au kitambaa chembamba. Kutumia kitambaa chenye mashimo madogo hutoa matokeo bora zaidi.

• Wino wa uchapishaji au rangi nyeusi ya kitambaa -Vyote hivi vinaweza kupatikana katika duka hila (Craft shop).

• Rangi mpira - Angalia kwa ukosee kupaka rangi katika kona nyembana usizo tarajia. (Hii ni kwa ajili ya kujaza nafasi hasi juu ya screen). Mimi nimefanya majaribio kadhaa na kuamua kwamba rangi ya mpira hufanya kazi hii kwa bora zaidi.

Karatasi nyeupe (safi na isiyokuwa na maandishi) na rangi ya maji.

Brashi ndogo ya sponji /brashi sifongo

• Kipande cha kadi ngumu au plastiki kilichochongwa Logo au maneno yanayotakiwa kuchapwa(print)

•Tisheti


Rangi maji(Watercolor) na Brashi ya kupakia rangi

Baada ya kukusanya vifaa vyako, hebu tuanze...

Kuchagua Dizaini

Kwanza, itabidi kuchagua dizaini ya unachotaka kuchapa. Buni na uchague dizaini ambayo itakuwa rahisi kwako kufuatilia juu. Miundo rahisi huchukua wino kwa urahisi pia. Unaweza kuchora picha wewe mwenyewe, au kupata picha unayoipenda mtandaoni.

Tumia mhariri picha(image editor) kwenye kompyuta yako kwa kurekebisha ukubwa wa picha kuwa sahihi/unaohitajika. Itakuwa haja ya picha hiyo kutosha katika kitanzi chako (embroidery hoop). Printi picha hiyo katika karatasi iliyo wazi (empty paper).
Kuandaa screen yako
Nyoosha na trim screen.

Nyoosha pazia nyavu(gauzy curtain) yako juu ya kitanzi(embroidery loop)kimoja halafu juu yake weka kitanzi kingine kinacholingana kabisa na kitanzi kilichotangulia chini. Hakikisha screen yako inavutwa na kukazwa/kuwambwa vizuri. Rekebisha Panapohitajika mpaka ikaze kama kichwa cha ngoma. Kata sehemu ya nyavu iliyojitokeza/iliyozidi zaidi kwa kutumia mkasi.

Fuatiliza Dizaini(picha au neno) juu ya kitanzi chako
Kuwa makini katika kufuatiliza dizaini.

Weka kipande chako cha karatasi juu ya meza ambayo unafanyia kazi. Weka kitanzi(embroidery hoop) juu ya picha kiasi kwamba picha inaonekana katikati na anza kufuatilia. Unahitaji kufuatilia kwa penseli juujuu kiasi kwamba hakuna mabaki mengi ya risasi ya penseli yanayobaki katika screen. Hatua hii inaweza kuchukua dakika chache, kulingana na jinsi picha ilivyo rahisi. Kama unafuatilia herufi, hakikisha kufanya mistari mizuri na nyoofu.

Kufuatiliza yaweza kuwa vigumu kwa baadhi ya watu. Kama hii ni kesi, unaweza kuprint picha au dizaini yako katika karatasi ambiso na kuikata. Karatasi ambiso(Self adhesive paper) zinapatikana katika idara nyingi na maduka hila (craft shops). Weka karatasi yako iliyokatwa vizuri kwenye screen na ibane vizuri chini, Pia hakikisha kingo(edges) zake zimekatwa vizuri.

Paka rangi mpira kwenye Screen yako
Paka rangi mpira(latex paint) juu ya screen yako (screen hii ni imekamilika na ipo nje ya hoop baada ya mradi kukamilika)

(Katika picha hii, screen imeondolewa kutoka kwenye kitanzi/embroidery hoop baada ya mradi kukamilika . Paka rangi screen yako na embroidery hoop/kitanzi kikiwa juu yake. )

Tumia rangi ya mpira(latex paint) ili kufunika nafasi zote ambazo hutaki kuprint/kuchapa. Ni muhimu sana kuhakikisha kwamba unafunika nafasi zote hasi. Ili kuwa na uhakika , angalia kupitia screen katika mwanga ili kujaribu kuchunguza sehemu yoyote iliyokosewa. Kama umefuatiliza dizain yako, tumia brashi ndogo kwa ajili ya nafasi ndogo.

Acha rangi ikauke, hii inaweza kuchukua saa moja mpaka masaa matano, kutegemea na kiasi cha rangi kilichotumika. Ikishakauka, jaribu screen yako kwa kuiweka kwenye kipande wazi cha karatasi na upake rangi ya maji nyembamba(thin watercolor) juu ya screen nzima kwa kutumia brashi inayofaa. Picha itakayotokea kwenye karatasi yako ndiyo itaonekana kwenye vazi utakalochapa. Rekebisha makosa yoyote kwa kuongeza zaidi rangi na kupima tena kabla ya kuprint/kuchapa.

Chapa/Print Fulana au nguo yako
Pakaa wino au rangi kwenye nguo (fulana au shati), kwa kutumia brashi ndogo ya sponji kwa kiasi sawa juu ya dizaini yako yote.

Weka t-shirt juu ya uso bapa kabisa (Flat surface). Ingiza kipande cha kadibodi kati ya mbele na nyuma ya shati ambapo utakuwa unachapa. Hii ni kuzuia wino kuvuja upande wa pili wa nguo yako.

Weka screen sehemu ambapo unataka kuchapa/kuprint juu ya shati. Tumia brashi sifongo yako kupakaa rangi/wino kote juu ya picha yako. Ukishamaliza kabisa, vuta taratibu screen yako kutoka juu ya nguo. Unaweza pia kutumia rangi ya kitambaa(fabric paint) katika hatua hii.

Acha wino/rangi ikauke kwa usiku mzima. Inaweza kuwa salama kufua katika 'washer' baada kukauka vizuri. Sasa una screen unayoweza kutumia kuprint/kuchapa aina hiihii ya logo tena na tena.

Nakutakia ujasiriamali wema kwa kazi bora za mikono yako.
 
Ngoja nichokoze mada

Mahitaji muhimu
Vibao vyenye squares au mstatili
Ways wa mesh
Misumar
Nyundo
Mkasi
Rangi ya kuprintia
Photo emulsion( original au utengeneze mwenyewe,pia panasomo lake hapa namna ya kutengeneza)
Draya ya wanawake kukaushia nywele
Jiki
Mafuta ya taa/ mafuta ya nazi
Sponji
Beseni
Squiza
Kibao au plaudi ya kuwekea t-shirt wakat wa kupeint.

Kama unatengeneza mwenyewe photo emission, Viti muhimu ni
Gundi
Maji
Sensitizer
Pigment

Wakuu hivyo ndio Viti muhimu vinavyohitajika, ukiwa navyo hivyo unaweza kuanza kazi ya kuchanga kwa kutengeneza photo emmosion na kibao na Mambo mengine yakaendelea.

Pia unatakiwa kujua chimbo lake ni liko wapi la hivyo vitu.

Nawasalimu kwa jina la jamhur ya muungano Tanzania.......kazi iendeleeee
 
Ngoja nichokoze mada....
Mahitaji muhimu
Vibao vyenye squares au mstatili
Ways wa mesh
Misumar
Nyundo
Mkasi
Rangi ya kuprintia
Photo emulsion( original au utengeneze mwenyewe,pia panasomo lake hapa namna ya kutengeneza)
Draya ya wanawake kukaushia nywele
Jiki
Mafuta ya taa/ mafuta ya nazi
Sponji
Beseni
Squiza
Kibao au plaudi ya kuwekea t-shirt wakat wa kupeint.

Kama unatengeneza mwenyewe photo emission, Viti muhimu ni
Gundi
Maji
Sensitizer
Pigment


Wakuu hivyo ndio Viti muhimu vinavyohitajika, ukiwa navyo hivyo unaweza kuanza kazi ya kuchanga kwa kutengeneza photo emmosion na kibao na Mambo mengine yakaendelea.
Pia unatakiwa kujua chimbo lake ni liko wapi la hivyo vitu.

Nawasalimu kwa jina la jamhur ya muungano Tanzania.......kazi iendeleeee
Duh umechokoza vizuri sana.
 
Back
Top Bottom