Kuna msichana ana miaka kuminatano(15) na mwengine ana miaka ishirininatatu(23) wote wapo ready au tayari ,mwenye umri wa miaka 15 amemaliza la saba na amepasi lakini atakuwa tayari kuolewa akishapitisha miezi sita na ni makubaliano ambayo hayana wasiwasi yameshakubalika kwa pande zote wazazi wazee na yeye mwenyewe ,huyu wa miaka 23 yeye anafundisha yaani ni mwalimu.
Njemba inayotaka kuoa ina miaka 42 ila anaonekana ni mdogo kiumbo, wapo wanaoshauri bora huyu alie na miaka 15 eti ataweza kumlea na kumfundisha pia ana ladha na sauti zinazopishana kwa kuvutia na kusononeka kuliko wa miaka 23 na kumponda yule wa miaka 23 wakisema anaijua dunia vilivyo na hasa alivyokuwa msomi kutakuwepo na mbinde ilivyokuwa ni mtoto wa mjini na ameshapita hadi formsix na chuo cha ualimu ila wanaomtilia na kumuunga mkono huyu wa miaka 23 wanasema atakuwa ameshaijua dunia vilivyo na hivyo uamuzi wake wa kukubali kuolewa ni uamuzi mzuri unaofikiwa na wakike wanaotimiliza miaka hiyo(ukubwa) na kumponda yule wa miaka kumi na tano kwa kuwa huwa wanabadilika hasa watimiapo miaka 21 na wanakuwa rahisi kuanza kubishana na huwa hawakataziki.
Wana JF nini ushauri ,mawazo na uchambuzi wenu ???
Hutakiwi kumaka au kuuliza yanahitajika maelezo na sababu zako ili tuweze kujadili.
unataka mjadala upi? hata huo ni mmojawapo.
Hutakiwi kumaka au kuuliza yanahitajika maelezo na sababu zako ili tuweze kujadili.
Sass samahan bosi kama nimekukwaza..lakini si unasikia serikali kila siku inasisitiza watoto wa kike wapelekwe skuli wapewe darsa, iwasaidie maishani? Sasa haya mambo ya kukubali wakubali wazazi wake, kuolewa aolewe mwingine ni mambo ya karne hii?
Halafu haiwezekani binti averaged 15yrs old Tanzanian CHILD amvutie mtu ambaye hana TAATHIRA YA U-PEDOFILIA, kiasi cha kutaka kumuoa..
Hayo ni maoni yangu tu..
mwenye umri wa miaka 15 amemaliza la saba na amepasi lakini atakuwa tayari kuolewa akishapitisha miezi sita...
huyu wa miaka 23 yeye anafundisha yaani ni mwalimu ...na ameshapita hadi form six na chuo cha ualimu
1) Miaka 15 bado ni mtoto kisheria na kisayansi
a) Mambo ya sheria yatakuwa na utata niyaache
b) Kisayansi umri huu ndio wanapata matatizo sana ya uzazi na husababisha hata kifo wakati mwingine kwa sababu bado wanakua.
2) Mtoto pia amefaulu, mbona wanataka kumpoteza?
3) Pia huyu mzee wa miaka 42 na mtoto wa miaka 15 mbona wamepishana sana? By the time anafikia miaka 60 "fimbo lugoda" haifanyi kazi vizuri "mtoto" ndio atakuwa na miaka 33 ndio kipindi anahitaji hasa "tendo" matokeo yake ni huyo mzee kuachwa solemba kwa kuwa hatamtosheleza, au ataletewa magonjwa n.k.
4) Wote hawamfai, lakini kama ni lazima achague kati ya hao, amchukue wa miaka 23.
Tatizo ni sheria ya Ndoa ya Tanzania ya 1973 ambayo inaleta utata. Sheria hiyo inasema kwamba binti wa miaka 15 anaweza kufunga ndoa kwa kupata ridhaa ya wazazi au mlezi wake.
Hiki kifungu kinaenda kupingana na kile cha makosa ya kujaamiana(1998) ambayo inasema kwamba mtoto chini ya miaka 18 hawezi kukubali kufanya mapenzi na ukifanya naye mapenzi basi inachukuliwa kwama umembaka(statutory rape).
Tukija kwenye suala la tafsiri za sheri hizi mbili, basi napenda kusema kwamba kulingana na sheria ya tafsiri ya sheria(tanzania) inabainisha kwamba sheria iliyopitishwa karibuni itaweza kuchukuliwa kama tafsiri sahihi ( subject to arguments).
Huyo jamaa, anatakiwa ajiweke katika viatu vya mzazi huyo na kujiuliza kama angekuwa binti yake angeweza kuwmoza kwa jamaa wa miaka 42?
Hitimisho langu ni kwamba jamaa ni mbakaji mtarajiwa na aangalie mkondo wa sheria unamfuata. Pili binti huyo kafaulu kwenda sekondari(kulingana na maelezo ya mtoa hoja) kwa hiyo ni kutaka kumwalibia maisha yake.
Tatu, sote hapa barazani tunatakiwa kukemea vitendo kama hivi vya ubazazi kwa nguvu zote.
Bw. Mwiba hakuna cha kujadili hapo. Miaka kumi na tano-kwa sheria zozote zile dunia hii - huyo ni mtoto. Jee hivi kweli tunaowa watoto siku hizi? Lete mada yenye maana tujadili siyo hii.Hutakiwi kumaka au kuuliza yanahitajika maelezo na sababu zako ili tuweze kujadili.
Hiki kifungu kinaenda kupingana na kile cha makosa ya kujaamiana(1998) ambayo inasema kwamba mtoto chini ya miaka 18 hawezi kukubali kufanya mapenzi na ukifanya naye mapenzi basi inachukuliwa kwama umembaka(statutory rape).
Amehusu PembaMwiba nyinyi wazaramo nini mkuu???