Nioe mwanamke aliye zaa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nioe mwanamke aliye zaa?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by TEGEMEA, Mar 16, 2012.

 1. T

  TEGEMEA JF-Expert Member

  #1
  Mar 16, 2012
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nilifiwa na mke wangu,aliniachia mtoto mmoja wakike(6 yrs).Alifariki wakati wa kujifungua mtoto wetu wa pili. katika mizunguko yangu nimekutana na mwanamke ambaye alizaliswa(mtoto wakike 3yrs).je nina weza kufunga nae ndoa?.ushauri tafadhali.
   
 2. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  ndio, mnaweza kufunga ndoa....kama mmependana......
   
 3. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #3
  Mar 16, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Kwanza fatilia ujue kwa nini anaishi bila mume?
  Usije kuingie choo cha kike then akaku-JAFETI KASSEBA.
   
 4. Ipyanah

  Ipyanah Member

  #4
  Mar 16, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 99
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Mmeshapima!? Mnapendana, hamna sheria inayowazuia kutofunga ndoa. OA.
   
 5. T

  TEGEMEA JF-Expert Member

  #5
  Mar 16, 2012
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nina mpango wa kwenda kupima.mimi pamoja naye.
   
 6. T

  TEGEMEA JF-Expert Member

  #6
  Mar 16, 2012
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante sana.ninaendelea kufuatilia history yake.
   
 7. sister

  sister JF-Expert Member

  #7
  Mar 16, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 9,026
  Likes Received: 3,932
  Trophy Points: 280
  mnaweza sa long as mnapendana.
   
 8. T

  TEGEMEA JF-Expert Member

  #8
  Mar 16, 2012
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimekusoma.asante.
   
 9. Smarter

  Smarter JF-Expert Member

  #9
  Mar 16, 2012
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 455
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ndio Oa, Haina shida as wewe pia Umezaa.

   
 10. T

  TEGEMEA JF-Expert Member

  #10
  Mar 16, 2012
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimekusoma asante.
   
 11. Mirhea

  Mirhea JF-Expert Member

  #11
  Mar 16, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 317
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kama mnapendana poa.
   
 12. Mamushka

  Mamushka JF-Expert Member

  #12
  Mar 16, 2012
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 1,609
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mkeo alikufa kwa sababu gani? Ugonjwa? na kama ugonjwa ugonjwa gani? na ulishapimaA? kama kitu kingine sawa manaake usijekalia kumchunguza mwenzio kumbe wewe pia sio salama. Na kama umnapendana kwa nini usite na wakati wote mna watoto? Ukiskia amani moyoni mwako muoe, ila kama unasitasita, acha tu, kwani hata usipomuoa wewe ataolewa na mume mwingine, hapo mshirikishe Mungu pia, kwani kupata mtu atakae kulelea mtoto wako kama wa kwake inabidi na Mungu ashiriki hapo/
   
 13. T

  TEGEMEA JF-Expert Member

  #13
  Mar 16, 2012
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante sana kwa ushauri wako.mungu akubariki.Mke wangu alifariki wakati anajifungua mtoto wetu wa pili.
   
 14. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #14
  Mar 16, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Its complicated, sio rahisi kama inavyoonekana kwa nje.
  Inahitaji watu matured sana kiakili kuoana kama wote wana watoto.

  Haya mambo ya ku-abuse watoto huanzia hapa.
   
 15. k

  kisukari JF-Expert Member

  #15
  Mar 16, 2012
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,753
  Likes Received: 1,038
  Trophy Points: 280
  hakuna ubaya,kama mnapendana.ingawa huwa ngumu kwenye kulea watoto.wanaweza wakaoneana wivu,huyu baba angu na huyu mama angu.inachotakiwa,mpendane vizuri,na watoto msiwabague
   
 16. T

  TEGEMEA JF-Expert Member

  #16
  Mar 16, 2012
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Je mmoja wa wanandoa akiwa mpya kwenye ndoa(hakuwahi kuoa/kuolewa) hapo hakuna abuse ya watoto wa mwenzake?
   
 17. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #17
  Mar 16, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,869
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280
  ana mapenzi na mwanao?
   
 18. farkhina

  farkhina Platinum Member

  #18
  Mar 16, 2012
  Joined: Mar 14, 2012
  Messages: 12,831
  Likes Received: 775
  Trophy Points: 280
  Hilo ndo jibu lipo wazi kabisa
   
 19. WaliNazi

  WaliNazi JF-Expert Member

  #19
  Mar 16, 2012
  Joined: Mar 7, 2012
  Messages: 853
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Oa fasta.....kama mmependana lakini.....
   
 20. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #20
  Mar 16, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,268
  Trophy Points: 280
  Huyo mwanamke kama alizaa na mtu mwingine je huyo mwanaume yuko hai? na kama yuko hai ni nini sababu za wao kutokuwa pamoja? hapa mjomba unaingia choo kike, ni ngumu sana watu kuyagunduwa makosa haya hasa ukiwa tayari umeshaonjeshwa tunda la katikati.

  Hivi pata picha siku huyo binti yake siku anaolewa sasa mpo kwenye shereha za harusi halafu pale mbele high table mke wako anakaa na mwanaume mwingine maana ndio baba mzazi wa huyo binti!......kuna fedheha nyingine huwa tunazitafuta wenyewe.
   
Loading...