Nioe mwanamke aliye zaa?

Huyo mwanamke kama alizaa na mtu mwingine je huyo mwanaume yuko hai? na kama yuko hai ni nini sababu za wao kutokuwa pamoja? hapa mjomba unaingia choo kike, ni ngumu sana watu kuyagunduwa makosa haya hasa ukiwa tayari umeshaonjeshwa tunda la katikati.

Hivi pata picha siku huyo binti yake siku anaolewa sasa mpo kwenye shereha za harusi halafu pale mbele high table mke wako anakaa na mwanaume mwingine maana ndio baba mzazi wa huyo binti!......kuna fedheha nyingine huwa tunazitafuta wenyewe.

Ndio maana tupo JF.nakushukurusana kwa mawazo yako.
 
haina tatizo ila angalia huyo mwanamama kama atakuwa na upendo kwa mwanao ...,,msome vizuri kwanza na ukimuoa tafadhari uwe karibu na mwanao sana maaana ni ngumu kwa nguvu za kibinadamu
 
Mimi nilifiwa na mke wangu,aliniachia mtoto mmoja wakike(6 yrs).Alifariki wakati wa kujifungua mtoto wetu wa pili. katika mizunguko yangu nimekutana na mwanamke ambaye alizaliswa(mtoto wakike 3yrs).je nina weza kufunga nae ndoa?.ushauri tafadhali.
Wazee walisema "Ndowa ni kutia mkono kizani" Wewe peleka mkono tu kwa kutarajia mafanikio la ukingatwa na ng'e utajiuguza na kujaribu tena!
 
Haina tatizo mradi wenyewe mnaona mahali mnapo elekea.
Ila hilo neno kuzalishwa si neno zuri,ni msamiati ambao unaweza kutumika kwa wanyama na si binadamu,hii huwa ni katika kujaribu tu kumshusha/kumuhukumu mwanamke ambaye ana mtoto,
na pia huenda umelibeba hilo neno kichwani na kila ukifikiria unaona ni issue kubwa kwamba "kazalishwa".

Pia siku zote mtoto/watoto always ni baraka na wakati unapokea mmoja kutoka kwake
unampa yeye wawili.Good luck.
 
kuoa ruksa, ila unapaswa kujiuliza kwanza huyo binti ujauzito aliupata katika mazingira gani? Aliyempachika hyo mimba ilikuwaje kamwacha ilihali anamlelea mwanae? usije ukakusanya shida ukafa siku sio zako kwa stress!
 
Man angalia sana hawa waliozaa si mchezo.bora uendelee nae kwanza kumsoma.Kama unaweza kula nae tu mpaka hakuna cha ndoa
 
Man angalia sana hawa waliozaa si mchezo.bora uendelee nae kwanza kumsoma.Kama unaweza kula nae tu mpaka hakuna cha ndoa

Bora kuoa aliyezaa kuliko bikra.... Aliyezaa hasa kabla ya kuolewa anajua maisha sanaaa, kuliko vikojoz!!!!
 
ndio, mnaweza kufunga ndoa....kama mmependana......

Labda kwa vile umeshaoa zamani, lakini inaelekea wewe bado kijana kwa nini uoe kayamba-mwana mke ambaye ameshazaa!!! Aliyemzalisha kwa nini hakumuoa? Tafuta msichana achana na vilivyoanguka kwenye mchanga, uokote na kupuliza mchanga utoke halafu ule!!!
 
its awkey,. kwanza ukitaka kuoa ambae hajazaa utakuwa unamuonea coz wewe ushazaa. so aliezaa ndo saiz yako. ila mkapime kwanza.
 
its awkey,. kwanza ukitaka kuoa ambae hajazaa utakuwa unamuonea coz wewe ushazaa. so aliezaa ndo saiz yako. ila mkapime kwanza.
 
Uko kwako na huyo mkeo afu tena anakuja baba mtt ili kumwona mwanae afu tena mama anaondoka nae kumsindikiza ww utajisiaje? Naomba utueleza status ya huyo mme aliyemzalisha yuko wapi na kaoa au kafa? kama hajaoa na yuko hai je waliachanaje. Kwa ugonvi au kazi zilitenganisha kijiografia?. Hapo akili kichwani mwako.
 
Never trust anything used.

na yeye muomba ushauri kashakua used kwa hiyo asioe. kaka nakushauri kama mmependana na unaona anafaa oa unaweza ukaoa ambaye hajazaa ikawa ni tabu tu kama ni mtazamaji wa channel E.entertaiment kuna kipindi cha keeping up with the kardashian mama yake kim kardashian kaolewa akiwa na watoto wanne na aliyemuoa naye anao wanne lakini wameishi wakapata wawili wengine wanaishi kwa furaha iweje hao wawili wawafikirishe ndoa ni maelewano muda mwingine mawazo ya watu yaweza kuwa sumu
 
Labda kwa vile umeshaoa zamani, lakini inaelekea wewe bado kijana kwa nini uoe kayamba-mwana mke ambaye ameshazaa!!! Aliyemzalisha kwa nini hakumuoa? Tafuta msichana achana na vilivyoanguka kwenye mchanga, uokote na kupuliza mchanga utoke halafu ule!!!

ucpende kuhukumu kwa usichokijua waweza kuta alibakwa au ndo wanaume uchwara wamemwaribia maisha tusipende kuweka fallacy conclusion mi ni mwanamke na wanayotendea wanawake na baadhi ya wanaume yananikera sana ya kuwapa ujauzito na kuwatelekeza halafu vilaza wengine wanaongea ***** tu.
 
Baba wa mtoto akija kumsalimia mtoto hali itakuwaje.?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom