Nini tofauti ya msomi na asiye msomi?

Nini tofauti ya msomi na asiye msomi?

Werevu ni wa kuzaliwa nao kama ilivyo upumbavu.

Mwerevu hata asipoenda shule hubaki kuwa mwerevu, mpumbavu hata akiwa na vyeti vingi na majina marefu kama ulivyoanisha bado ataendelea kuwa mpumbavu hata akivaa suti na tai.
Asante najifunza vitu kwenu wadau wa JF 🙏🙏
Msukuma, Kishimba, Mnyika huenda wanazo za kuzaliwa kuliko wale wapumbavu uliowatunzia heshima kwa kuficha majina yao.
Wanazo za kuzaliwa 👍
 
You can be a professor but still "an adiot "
Unaweza ukawa Professor PhD holder wa Kilimo cha Karanga na Alzeti Chuo Kikuu cha Kilimo SUA ila ukiletwa kwenye angle ya Matibabu ya Magonjwa ya Moyo, Uti wa Mgongo, FIGO, INI na Kibofu cha Mkojo wewe unaonekana ni kilaza yaani empty hujui kitu in detail pamoja na kua professor mpaka upigwe brush kuondoaa ujinga kichwani ila sio mpumbavu
 
Katika hotuba na mafundisho Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alisisitiza kuwa tofauti ya msingi kati ya mjinga na mpumbavu inatokana na uwezo wa mtu kupokea na kuelewa mambo
  • Mjinga: Ni yule anayekosa maarifa au asiyejua jambo fulani, lakini anafundishika. Akielezwa ukweli au kupewa elimu anaelewa na kubadilika.
Shukran umefafanua vyema 🤝
  • Mpumbavu: Ni yule asiyefundishika (kichwa ngumu). Hata ukimweleza na kumuelimisha vipi, haambiliki, hataki kubadilika, na anaendelea na msimamo wake wa makosa.
Hili neno Mpumbavu hata mimi nikiri sikua najua maana yake vizuri Asante mkuu🙏
 
Kuna tofauti kati ya elimu na kuelimika,unaweza ukawa na elimu ila ukawa hujaelimika,elimu yako inakua haijakukomboa kifikra,

Pia tambua kua kuna formal education na informal education,elimu ya darasani na elimu ya mtaani,

Akili ni kile kinachobaki baada ya kuondoa kile ulichofundishwa darasani,

Usichanganye kati ya elimu na inteligence,ni vitu viwili tofauti kabisa,

Education is the structured acquisition of knowledge and credentials.
Intelligence is the innate or developed capacity to think critically, adapt, and apply knowledge in real-world scenarios
Asante kaka 👏👏
Hapa nipo darasani asanteni 🙏
 
Genius ni mtu yeyote anayejua jinsi ya kukabiliana na asiyoyajua.

Fikiria hivi.

Mpumbavu anafika mlangoni, anaona mlango umefungwa —
anaanza kugonga ukuta badala ya kutafuta ufumbuzi.

Mwenye akili anafika mlangoni, anaona mlango umefungwa —
anaanza kutafuta ufunguo, au namna yoyote ya kuweza kufungua mlango.

Genius anafika mlangoni, anaona mlango umefungwa —
anasimama then anajiuliza swali ambalo wengine hawakufikiria kabisa.

"Kwa nini huu mlango umefungwa?"

Angalia tofauti ilipo hapo.

Mpumbavu anapigana na hali yenyewe badala ya kutafuta namna ya kukabiliana na hali.

Mwenye akili anatafuta namna ya kukabiliana na hali lakini hajajiuliza kwanini hali ipo hivyo.

Genius anajiuliza kwanza kwanini hali ipo hivyo? ndipo atafute namna ya kusolve tatizo.

Tofauti utaiona hapo.
 
Lengo kuu la shule ni kujenga wananchi bora. Shule inapaswa ifundishe watu ustaarabu, nidhamu, udadisi na mawasiliano bora.

Bahati mbaya kwenye nchi zetu masikini, hatuwezi kumudu kutoa elimu ya namna hii.
Kwahiyo elimu yetu baado inaitaji maboresho
Kwahiyo kimsingi na kinadharia shule zinapaswa zitoe upumbavu, ila kwa muktadha wa kiafrika hilo halitokei. Ukiona mtu ana utofauti flani basi ujue ni mazingira yamembadilisha.
Ukiona tofauti ujue ni mazingira ya membadilisha 👍
 
Genius ni mtu yeyote anayejua jinsi ya kukabiliana na asiyoyajua.

Fikiria hivi.

Mpumbavu anafika mlangoni, anaona mlango umefungwa —
anaanza kugonga ukuta badala ya kutafuta ufumbuzi.

Mwenye akili anafika mlangoni, anaona mlango umefungwa —
anaanza kutafuta ufunguo, au namna yoyote ya kuweza kufungua mlango.

Genius anafika mlangoni, anaona mlango umefungwa —
anasimama then anajiuliza swali ambalo wengine hawakufikiria kabisa.

"Kwa nini huu mlango umefungwa?"

Angalia tofauti ilipo hapo.

Mpumbavu anapigana na hali yenyewe badala ya kutafuta namna ya kukabiliana na hali.

Mwenye akili anatafuta namna ya kukabiliana na hali lakini hajajiuliza kwanini hali ipo hivyo.

Genius anajiuliza kwanza kwanini hali ipo hivyo? ndipo atafute namna ya kusolve tatizo.

Tofauti utaiona hapo.
🫡🫡🫡👏👏👏 asante kaka kama una cha kuongeza ongeza nisome tena
 
Again Dada , umeweka hoja Kali na naona watu wameheshimu point Yako.

Jibu langu Mimi ni kwamba kiasili kila mtu anakosea hata wasomi na asiye msomi. Pia mazingira yanaweza kuadhiri matendo na maneno ya mtu.Mfano kiongozi msomi itabidi aongee mambo ya kijinga ili kuepuka wakubwa wasije ona yey ni msaliti kwao.

Hata Mimi Huwa nakosea japo Nina uelewa wa mambo.
 
Again Dada , umeweka hoja Kali na naona watu wameheshimu point Yako.
Wapo vizuri sana
Jibu langu Mimi ni kwamba kiasili kila mtu anakosea hata wasomi na asiye msomi. Pia mazingira yanaweza kuadhiri matendo na maneno ya mtu.Mfano kiongozi msomi itabidi aongee mambo ya kijinga ili kuepuka wakubwa wasije ona yey ni msaliti kwao.
Kwa hiyo wengine sio kwamba ni wapumbavu ila mazingira yanawafanya waonekane hivyo
Hata Mimi Huwa nakosea japo Nina uelewa wa mambo.
Hakuna mtu mkamilifu kaka angu
 
Sasa kama mtu msomi kakesha kutengeneza mabomu kwa utaalamu anaojua mwenye na aliyemfundisha, Lakini hajui pa kuyatumia huoni ni tatizo.!?
Umefanya nimecheka😅😅

Unataka kusema wakati anakesha kuyatengeza hajui ni wapi pa kuyatumia
Mkuu si anatengeneza ili afanye biashara au?
 
Back
Top Bottom