Nini tofauti kati ya CHADEMA na utawala wa Idd Amin?

Nini tofauti kati ya CHADEMA na utawala wa Idd Amin?

Wanaowaona chadema ni heroes ni wale ambao wanaamini au wameahidiwa nafasi wakishika dola,
Wengine ni brainwashed hopeless people tu

Mkuu, jaribu kuwa makini na maandishi yako. Mbona unaandika kama uliyekata tamaa. Brainwashed hopeless people?! Nyumbani kwenu, yaani ndugu zako na au wazazi wako hakuna anayeisapoti CDM? Muungwana hawezi tumia maneno ya namna hii. Kama hukubaliani na CDM just ignore them and lead your own life. Mimi si mwanachama wa chama chochote cha siasa lakini maneno yako yanaonekana ulikuwa na matarajio fulani wakati unajiunga CDM na sasa hivi huo uchungu wa kutokufikia matarajio na matamanio yako ndo unakunyung'unya. Pole sana ndugu yangu.
Hata kile unachokilinganisha kati ya CDM na Idi Amin kwa mtu ambaye hana hasira na mchambuzi mzuri wa masuala ya siasa na utawala hawezi kuleta suala kama hili katika jamvi hili kwa mjadala. Maandishi yako yanaonesha jinsi gani ulivoumizwa na CDM na huna jinsi ya kuwafanya CDM au mtu aliyekutenda. Kuna watu wengine pia wanatapika au kushikwa na tumbo hata la kuhara wanaposikia na kuyaona yanayotokea chini ya utawala cha chama chako kipenzi. Take a break and camp in a national park for week and on your return you will be a different person. Utakuwa huna stress kabisa. Pole sana. Haya ndo maisha.
 
Nimekaa nimejiuliza maswali mengi kuhusu namna utawala wa CHADEMA ulivyo na nimeshindwa kuelewa. Ndani ya CHADEMA ni dhambi kuhoji lolote baya likifanywa na wakuu wa chama Ndani ya CHADEMA mgombea urais anachaguliwa na mtu mmoja tu Ndani ya CHADEMA kuna kashfa nyingi sana ambazo ni marufuku kuzijadili wala kuhoji na ukuionekana unataka kudadisi basi utaitwa msaliti. Tukumbuke kuwa kauli mbiu ya CHADEMA ni demokrasia huru na haki, Hivi wanelewa kweli maana ya demokrasia au wanaimba tu kama nyimbo za kizaire? CHADEMA wananikumbusha Idd Amin wakati wa utawala wake Uganda, ilikuwa ukisema lolote baya dhidi yake basi hautachukua raundi kesho yake watatkukuta kama sio kwenye friji basi kando kando ya barabara umekufa. Chadema wao wanapenda kuwanyooshea vidole CCM na kuwahimiza wafuasi wao ambao wame wa brainwash kuandamana kila kukicha na kufanya vurugu pale wanapopata cha kuongea wakati wao yakitokea kwao husema wamesingiziwa Pia kuna jambo moja linalonitia mashaka hapa. Hawa CHADEMA ki
 
Hebu nitajie wengine waliowahi kunufaika na hiyo mikopo zaidi ya mtu mmoja tu aliejikopesha

Kwani kuna waajiriwa wangapi wa CDM...?? Kuna ubaya gani mmoja akikopeshwa na mwingine asipokopeshwa? Ukopeshaji wa fedha siku zote unaangalia creditworthness ya mtu, sio kila mtu anakopesheka.
 
Jaman jaman, JF ni for the great thinkers, sasa jamaa amepoteza sifa, c aende BBM au FB akachat mapenzi?
 
nimekaa nimejiuliza maswali mengi kuhusu namna utawala wa chadema ulivyo na nimeshindwa kuelewa.

Ndani ya chadema ni dhambi kuhoji lolote baya likifanywa na wakuu wa chama
ndani ya chadema mgombea urais anachaguliwa na mtu mmoja tu
ndani ya chadema kuna kashfa nyingi sana ambazo ni marufuku kuzijadili wala kuhoji na ukuionekana unataka kudadisi basi utaitwa msaliti.

Tukumbuke kuwa kauli mbiu ya chadema ni demokrasia huru na haki, hivi wanelewa kweli maana ya demokrasia au wanaimba tu kama nyimbo za kizaire?

Chadema wananikumbusha idd amin wakati wa utawala wake uganda, ilikuwa ukisema lolote baya dhidi yake basi hautachukua raundi kesho yake watatkukuta kama sio kwenye friji basi kando kando ya barabara umekufa.
Chadema wao wanapenda kuwanyooshea vidole ccm na kuwahimiza wafuasi wao ambao wame wa brainwash kuandamana kila kukicha na kufanya vurugu pale wanapopata cha kuongea wakati wao yakitokea kwao husema wamesingiziwa

pia kuna jambo moja linalonitia mashaka hapa.
Hawa chadema kila kukicha wanajenga chuki kati ya wananchi na polisi. Hii ina maana kuwa kama chadema wakipewa dola basi polisi wote itabidi wafukuzwe na wataunda polisi mpya. Unaandaa kuwafukuza walinzi wa usalama wenye mafunzo ya kijeshi matokeo yake unayajua???

Hii ni hatari sana kwani hawa watu wanweza kuja kuwa hatari kuliko hata amin kwani sasa hawana dola ni huwezi kuwahoji, jee wakichukua nchi tutapona kweli?

Hii ndharia ya kutetea na kuficha madhambi ni hatari sana kwa taifa letu
idi-amin-dada-9183487-1-402.jpg

MNAWAHOJI KAMA MOVIE NI YA KWAO AU? WAKATI MAJIBU MNAYO
mtaangaika sana mwaka huu kuitengenezea kila aina ya filamu zinazonuka vichwani mwenu.. Wanainchi wanataka maisha bora si kelele zenu na chadema mpaka mnasahau majukumu yenu
 
Boss,
Mimi sio mtu wa kutumwa kama unavyofikiri, mimi najituma mwenyewe.
Ninachoeleza hapa ni kwa faida yako wewe na vijana wengine ambao mko brainwashed hamjui hatima yenu.
Ngoja nikuulize swali.
Umewahi kukopa hela za ruzuku ujikimu mahitaji yako?

Vyama vyote vilivyoanzishwa na kudai uhuru ni Dictators !! sasa Chadema hapo wapo??!!
 
Kwenye Msafara wa magamba na Ke.ge kumbe bado mmo!!au umetumwa na Nape kuandika haya!

Pole sana Kijana na mawazo yako haya!

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Pole Chris Lukosi siku utakpopona yale magonjwa saba tuliyotajiwa na Dr. Alex ndipo tutaanza kukuchukulia maanani lakini kwa sasa bado tunaendelea kukupa pole ili uendelee kujiuguza hadi upone.
 
Last edited by a moderator:
Idd Amin was a great Leader for Ugandans!they are admiring him till date!!Go ask Ugandans!!
 
Nimekaa nimejiuliza maswali mengi kuhusu namna utawala wa CHADEMA ulivyo na nimeshindwa kuelewa.

Ndani ya CHADEMA ni dhambi kuhoji lolote baya likifanywa na wakuu wa chama
Ndani ya CHADEMA mgombea urais anachaguliwa na mtu mmoja tu
Ndani ya CHADEMA kuna kashfa nyingi sana ambazo ni marufuku kuzijadili wala kuhoji na ukuionekana unataka kudadisi basi utaitwa msaliti.

Tukumbuke kuwa kauli mbiu ya CHADEMA ni demokrasia huru na haki, Hivi wanelewa kweli maana ya demokrasia au wanaimba tu kama nyimbo za kizaire?

CHADEMA wananikumbusha Idd Amin wakati wa utawala wake Uganda, ilikuwa ukisema lolote baya dhidi yake basi hautachukua raundi kesho yake watatkukuta kama sio kwenye friji basi kando kando ya barabara umekufa.
Chadema wao wanapenda kuwanyooshea vidole CCM na kuwahimiza wafuasi wao ambao wame wa brainwash kuandamana kila kukicha na kufanya vurugu pale wanapopata cha kuongea wakati wao yakitokea kwao husema wamesingiziwa

Pia kuna jambo moja linalonitia mashaka hapa.
Hawa CHADEMA kila kukicha wanajenga chuki kati ya wananchi na polisi. Hii ina maana kuwa kama CHADEMA wakipewa dola basi polisi wote itabidi wafukuzwe na wataunda polisi mpya. unaandaa kuwafukuza walinzi wa usalama wenye mafunzo ya kijeshi matokeo yake unayajua???

Hii ni hatari sana kwani hawa watu wanweza kuja kuwa hatari kuliko hata Amin kwani sasa hawana dola ni huwezi kuwahoji, jee wakichukua nchi tutapona kweli?

Hii ndharia ya kutetea na kuficha madhambi ni hatari sana kwa taifa letu
Idi-Amin-Dada-9183487-1-402.jpg
Kwa mwenendo huu nahisi kijana huyu ataishia Mirembe muda si mrefu ujao! Hivi kuna mfananisho wa aina anayosema au ni obscession zake? Lukosi, ni heri kukaa kimya kuliko kuropoka maana unawapa nafasi watu kuyafahamu mapungufu uliyonayo katika namna zako za kufikiri.
Mimi sikufahamu na wala sijawahi kulumbana nawe hata siku moja lakini leo nimekuelewa ulivyo; yaani uelewa wako mfinyu!
Labda ungeeleweka kama hapo kwenye CHADEMA ungeweka CCM maana CHADEMA hawajawahi shika dola yoyote duniani! Unatia huruma.
Nadhani ipo siku utachukua kamba ujieu pale utakaposikia mabwzna zako wa sasa (CCM) wameangukia pua na CHADEMA kimekuwa ndiyo chama tawala.
Watanzania wengi wanaiona CCM kama chama cha kibabe, ujambazi, ulaghai, udini, kiukoo, kushkaji, kimafia,kihalifu kiiimla na ...taja tzkataka zote.
Inauma sana kuona chama kilichokuwa kipenzi cha kila mtanzania miaka ishirini tu iliyopita sasa kimekufa, kinanuka, hakitamaniki na kinabezwa hata na wanafunzi wa shule za msingi!
Hivi ni nani aliyeiroga CCM? Hivi kuna yeyote aliyefikiria kwamba kwa kitambo kifupi tu CCM wangetorokwa na wanachama kiasi cha kuwashawishi kwa kuwanunua kama ulivyonunuluwa wewe na wenzako kina Tambwe, Kaburu, Mwampamba, Shonza na wengine lukuki? Kuna aliyefikiria CCM ingeuka genge la mamafia wanaowateka wale wasiokubaliana na sera zao, kuwatesa, kuwabambikia kesi na hata kuwaua? Yupo aliyefikiria CCM ingefikia hatua ya kuwahonga wananchi vijipesa, maji, fulana na rushwa mbalimbali ili angalau wafanikishe mikutaano yao?
Sasa wanafungia magazeti, wanawajeruhi waandishi, wanawateka nyara, wanakwapua hadi Benki Kuu walikojaza koo zao, wanahaha kuficha milungula waliyodai nakulipwa ili kuuhujumu uchumi wa nchi wanayojifanya kuipenda!
Pole sana Lukosi kwa kujivua nguo na kuwavua nguo hao mabwana zako. Ama kweli shida haina adabu. Endelea kumtumikia kafiri ili uende choo.
 
Boss,
Mimi sio mtu wa kutumwa kama unavyofikiri, mimi najituma mwenyewe.
Ninachoeleza hapa ni kwa faida yako wewe na vijana wengine ambao mko brainwashed hamjui hatima yenu.
Ngoja nikuulize swali.
Umewahi kukopa hela za ruzuku ujikimu mahitaji yako?
Hakika unajidhalilisha sana. Sio siri wala sikutegemea kama siku moja utakua na akili kama hizi. Kuna mambo mengi sana
nilitegemea kupata kutoka kwako lakini dah! Lukos tuliza akili ndugu yangu.
 
Nimekaa nimejiuliza maswali mengi kuhusu namna utawala wa CHADEMA ulivyo na nimeshindwa kuelewa.

Ndani ya CHADEMA ni dhambi kuhoji lolote baya likifanywa na wakuu wa chama
Ndani ya CHADEMA mgombea urais anachaguliwa na mtu mmoja tu
Ndani ya CHADEMA kuna kashfa nyingi sana ambazo ni marufuku kuzijadili wala kuhoji na ukuionekana unataka kudadisi basi utaitwa msaliti.

Tukumbuke kuwa kauli mbiu ya CHADEMA ni demokrasia huru na haki, Hivi wanelewa kweli maana ya demokrasia au wanaimba tu kama nyimbo za kizaire?

CHADEMA wananikumbusha Idd Amin wakati wa utawala wake Uganda, ilikuwa ukisema lolote baya dhidi yake basi hautachukua raundi kesho yake watatkukuta kama sio kwenye friji basi kando kando ya barabara umekufa.
Chadema wao wanapenda kuwanyooshea vidole CCM na kuwahimiza wafuasi wao ambao wame wa brainwash kuandamana kila kukicha na kufanya vurugu pale wanapopata cha kuongea wakati wao yakitokea kwao husema wamesingiziwa

Pia kuna jambo moja linalonitia mashaka hapa.
Hawa CHADEMA kila kukicha wanajenga chuki kati ya wananchi na polisi. Hii ina maana kuwa kama CHADEMA wakipewa dola basi polisi wote itabidi wafukuzwe na wataunda polisi mpya. unaandaa kuwafukuza walinzi wa usalama wenye mafunzo ya kijeshi matokeo yake unayajua???

Hii ni hatari sana kwani hawa watu wanweza kuja kuwa hatari kuliko hata Amin kwani sasa hawana dola ni huwezi kuwahoji, jee wakichukua nchi tutapona kweli?

Hii ndharia ya kutetea na kuficha madhambi ni hatari sana kwa taifa letu
Idi-Amin-Dada-9183487-1-402.jpg

kojoa ulale.ya ndan ya chama cdm waachie wenyewe.we kama sio mWana cdm kwa nin uwashwe
 
mgonjwa sasa ameingia, mgonjwa wa magonjwa 7, dr njoo umtibu, maana hapa hamna hoja cwez kujibu kwa hoja, kuna pumba wacha nijibu mashudu. Njaa ikizidi sana, huondoa maarifa.
 
Chris Lukosi, hebu soma ushuhuda wa mawaziri ambao ni wanachama wa CCM jinsi ambavyo sauti yoyote inayojaribu kupinga ufisadi inavyozimwa kwa uovu mkubwa na nguvu za dola.

Kama una haraka soma pekundu tu.

Jiulize kwa nini jeshi la polisi halifanyii kazi matukio hayo ya Mwakyembe na Mwandosya?

Kuna watu wako kwa ajili ya kula nchi hii. Yeyote anayewasumbua, iwe chama au mtu binafsi anashughulikiwa. Hata kama ni mwana CCM mwenzao na waziri katika serikali yao.

Hawataki kuambiwa ukweli, na wewe umeanza kutumika kama chombo cha kuendeleza uovu huo.

Usinunuliwe kwa bei rahisi. Waulize Sitta, Mwakyembe, Mwandosya n.k.

Nadhani hapa umeona ulinganisho wako na utawala wa Idd Amin una ukweli fulani hapa nchini......
quote_icon.png
By Lunyungu

  • Muuaji wake alitoa taarifa za mpango
  • Profesa Mwandosya asema wote walipimwa yaleyale
  • Sugu amtaka Dk. Mwakyembe CHADEMA
  • Sitta aponda siasa za Tanzania

Raia Mwema | Toleo la 260 | 26 Sep 2012

SHUHUDA zilizotolewa wakati wa ibada ya shukrani ya Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, zilikuwa ujumbe tosha kuhusu kuwapo kwa mitandao ya kiharamia iliyolifikisha Taifa pabaya.

Ibada hiyo ya shukrani ilifanyika katika Kanisa la Kiinjili la Moravian Tanzania, Usharika wa Nduli katika Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya Jumapili iliyopita, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali, wakiwamo mawaziri, wabunge na viongozi wa Serikali na vyama vya kisiasa mkoani Mbeya.

Kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, wananchi wamekuwa na hamu ya kufahamu hasa ugonjwa uliomsibu mwanasiasa huyo huku ikiaminika miongoni mwa wengi, wakiwamo viongozi wa kisiasa, kwamba ulitokana na sumu ambayo hata hivyo mazingira ya kupewa kwake imebaki kuwa ni kitendawili hadi leo.

Kila aliyepata nafasi ya kuzungumza alibainisha utukufu wa Mungu ulivyodhihirika katika matukio mbalimbali nchini, hususan, yaliyohusu mikasa dhidi ya baadhi ya viongozi wa kisiasa nchini, hivyo kufichua dhambi ambazo waliamini kuwa hazikufahamika, na wananchi kutoufahamu ukweli wa madhila yaliyowasibu viongozi wao.

Dk. Mwakyembe aliamua kumshukuru Mungu kutokana na mambo makuu aliyosema alimtendea katika miaka mitatu iliyopita ikiwa ni pamoja na kumuokoa kwenye ajali mbaya ya gari iliyotokea mkoani Iringa, Mei 2009, na njama za kumuua yeye pamoja na baadhi ya viongozi wengine wa kisiasa, dini na watu mashuhuri nchini, matukio yote hayo yakiwa yametolewa taarifa katika Jeshi la Polisi lakini yakiachwa bila kufanyiwa kazi.

Lakini lililoshtua zaidi ni ugonjwa wa ajabu uliompata mwaka jana kiasi cha Serikali kulazimika kumkimbiza katika Hospitali ya Apollo nchini India ambako walifanikiwa kubaini kuwapo kwa kemikali kwenye ute katika mifupa yake (bone marrow), ambazo ndizo zilikuwa zikisababisha kuharibika kwa ngozi yake pamoja na kunyonyoka nywele.

Katika ushuhuda wake, Waziri Nchi, Ofisi ya Rais, Profesa Mark Mwandosya ambaye naye alihudhuria ibada hiyo, alisema pamoja na mambo mengine kwamba kilichomshangaza ni kuona vipimo alivyofanyiwa Dk. Mwakyembe ni vile vile alivyofanyiwa yeye na hivyo kubainisha kuwapo kwa mahusiano katika ugonjwa waliougua.

Profesa Mwandosya ndiye aliyetangulia kwenda katika Hospitali hiyo ya Apollo nchini India, ambapo awali alitarajia kutumia juma moja tu asifahamu ukubwa wa tatizo lililokuwa likimkabili. Akiwa hospitalini hapo ilibainika Waziri huyo kukabiliwa tatizo kubwa zaidi ya alivyotarajia hivyo kulazimika kukaa kwa zaidi ya miezi sita akitibiwa.

“Nikiwa India nikampigia simu kumuomba msamaha kwa kutomuaga, na nikamuomba anapokuja jimboni kwake apitie na Busokelo (Jimbo la Rungwe Mashariki kwa Profesa Mwandosya), lakini baadaye kidogo nikashangaa kuambiwa naye kaletwa India kwa matibabu,” alisema Mwandosya na kuongeza: “Siri ambayo sikuwahi kuieleza ni kwamba, vipimo walivyomfanyia ni vile vile walivyonifanyia mimi.”

Kuugua kwa mawaziri hao wawili kwa wakati mmoja, tena wenye kutambulika kama mtu na ndogo wake, wakiwa wanatoka mkoa mmoja, majimbo yaliyo jirani yenye kukaliwa na watu wa jamii moja, kulizua sintofahamu ambayo hadi sasa haifahamiki iwapo wananchi wa Mkoa wa Mbeya wamesamehe.

Hali halisi, pamoja na kutowekwa bayana, ni kwamba wananchi walio wengi mkoani humo hawana imani na Serikali yao pamoja na chama tawala, mazungumzo yao yanathibitisha hilo, hususan, pale wanapohoji kulikoni kila mzawa wa Mkoa huo anapoibuka, hukutwa na masahibu ya kutisha.

Mazungumzo kuhusu madhira yanayowakuta wazawa wa mkoa huo ni jambo la kawaida kuyakuta maofisini, vijiweni na maeneo mbalimbali ya mikusanyiko, ambapo huyataja majina kuanzia marehemu Stephen Kibona, waziri wa fedha wa zamani, ambaye hadi leo hawaamini kwamba kifo chake kilikuwa ni cha kawaida.

Hawaishii hapo, wanayakumbuka majina ya kina marehemu Profesa Jwani Mwaikusa aliyeuawa kikatili kwa kupingwa risasi nyumbani kwake jijini Dar es Salaam, Profesa Mwandosya na Dk Mwakyembe walionusurika kifo kutokana na ugonjwa wa ajabu uliowakuta, na hivi karibuni zaidi, Dk Stevev Ulimkoka, aliyeongoza mgomo wa madaktari akaishia kutekwa na kufanyiwa ukatili wa kutisha akinusurika kufikwa na mauti katika mazingira ya kimiujiza.

Mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa Kituo cha Channel Ten mkoani Iringa na Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani humo, marehemu Daudi Mwangosi, yamezidisha hasira ya wananchi hao dhidi ya Serikali, wakiamini kuwa ni mpango mahsusi wa kuwamaliza wazawa wa mkoa huo wenye kujitokeza na kujenga majina nchini.

“Mwaka 2009 nilipata ajali mbaya kati ya Makambako na Iringa mjini. Kitu ambacho sitokisahau milele ni kwamba niligongwa na lori,” alisimulia Dk. Mwakyembe Jumapili.

Alisema pamoja na tukio hilo na matukio mengi mengine yaliyomwandama na kuyaripoti katika Jeshi la Polisi, lakini amekuwa akishangazwa na watendaji katika jeshi hilo kwa kuyasemea matukio hayo pasipo kuyafanyia uchunguzi jambo ambalo limekuwa likimkera na kupoteza imani kwalo.

Dk. Mwakyembe ambaye alitumia nafasi hiyo kuwaelezea wananchi wa jimbo lake namna anavyoandamwa kuuawa pamoja na ugonjwa wa ajabu uliompata ghafla na kusema matukio yote hayo yamekuwa yakipotoshwa vibaya na watendaji wakuu wa ndani ya Polisi.

Aidha, alisema miongoni mwa walioshuhudia ajali hiyo ni Mkurugenzi wa Taasisi moja ya elimu yenye kuendesha shule za sekondari na vyuo katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, Mboka Mwambusi, ambaye akiwa na mchumba wake wakati huo wakielekea jijini Dar es Salaam walimkuta Dk. Mwakyembe akiwa mahuttuti huku dereva wake, Jose Msuya akitokwa damu, na kuwakimbiza hospitali ya Mkoa wa Iringa.

“Polisi tuliyemkuta aliniambia niondoke, kwani Dk. Mwakyembe hakuwa mzima tena, alishafariki. Namshukuru ndugu yangu Jose, alinisisitizia kuwa alikuwa hai, nimharakishe hospitali, nikamshusha abiria niliyekuwa naye, nikashusha michele na ndizi, tukampakia na kumkimbiza hospitali,” alisimulia Mkurugenzi huyo.

Kwa mujibu wa Mwambusi ajali hiyo ya Dk. Mwakyembe aliyoipata Iringa, ni miongoni mwa matukio ambayo hatayasahau katika maisha yake, akisema litaendelea kudumu katika kumbukumbu zake milele.

Lakini lililoshitua wengi waliohudhuria katika ibada hiyo ni simulizi ya Dk Mwakyembe kuhusu jinsi alivyofuatwa na mtu aliyepangwa kumuua, hiyo ikiwa ni Desemba 28, mwaka 2009.

Alisema:
“Niliandaliwa mpango wa kuuawa kati ya Iringa na Mbeya. Aliyepangwa kuniua ni mhalifu sugu, lakini Mungu alijiinua, muuaji alinifuata akaniambia unaenda safari ya Kyela, usiende, ukienda nitakuua.”

Katika maelezo yake hayo ambayo yaliwaacha wahudhuriaji wa ibada hiyo ya shukrani wakiwa wamepigwa butwaa, alisema muaaji huyo alimweleza mpango mzima wa mauaji ulivyopangwa na kumpa uhuru wa kumrekodi maelezo yake, ambayo ameyahifadhi hadi leo.

Katika matukio yote yaliyomsibu ndani ya miaka hiyo mitatu, Dk. Mwakyembe alisema amekuwa akilitaarifu Jeshi la Polisi, lakini anasema pia kwamba wakati wote hawakuchukua hatua zozote zaidi ya kuendesha juhudi za kuficha ukweli.

Pengine lililowaumiza walio wengi ni ugonjwa aliougua, ambao anasema katika mazingira ya kushangaza kumekuwapo na juhudi za kuupotosha umma.

“Mwaka 2011 niliugua, cha kusikitisha niliugua wakati huo huo na kaka yangu Profesa Mark Mwandosya. Mungu ni mwema, alitunyanyua vitandani, leo tunatembea. Mimi na kaka yangu Mwandosya ni ushahidi juu ya utukufu wa Mungu,” alisema Dk. Mwakyembe.

Katika kile kinachosababisha wananchi wengi, akiwamo yeye mwenyewe, waamini kuwa ugonjwa uliomsibu ni wa ajabu, hali aliyokuwa nayo alipofikishwa India anasema iliwatisha hata madaktari waliokuwa wakimhudumia.

“Daktari aliyenitibu, aliniambia amefanya kazi yake hiyo ya udaktari kwa zaidi ya miaka 27, lakini hakuwahi kuona ugonjwa wa aina ile,” alisema Dk. Mwakyembe.
Aliongeza:
“Sitta alipofika kuniona, nilisikitika sana kwa nini alikuja. Ndiyo maana aliporudi alikuja na kilio kwa Polisi akiwataka wachunguze, wakamgeuzia kibao... walisau kuwa Sitta (Samuel) ni mwanasheria aliyebobea.”

Katika ushuhuda wake, Waziri wa Afrika Mashariki,
Samwel Sitta alihitimisha ibada hiyo kwa kuhoji: “Mungu hapendi uongo, na ukweli hauna tabia ya kujificha, ipo siku utadhihirika. Ikiwa Polisi walikuwa wanachunguza ugonjwa uliomsibu Dk. Mwakyembe, kwanini hawakwenda kwenye hospitali aliyokuwa akitibiwa?”

Waziri Sitta aliendelea kufichua udhaifu wa ndani ya siasa za Tanzania akisema:
“Tatizo la nchi zetu hizi za Afrika ni siasa ya kiwango cha chini, viongozi wanajali maslahi yao na si maslahi mapana ya umma. Wapo watu, tunasheherekea hapa wao wamenuna, na wanafahamika, tutapambana na ubinafsi, tutapambana na ufisadi.”

Ibada hiyo ilikusanya watu mbalimbali mashuhuri na miongoni mwa waliozungumza ni pamoja na
Mbunge wa Kahama, James Lembeli, ambaye alibainisha kuwa matatizo yote aliyoyapata Dk. Mwakyembe yalitokana na tabia yake ya kuwa mkweli.

Kauli hiyo iliungwa mkono na Mbunge wa Mbarali, Modestus Kilufi na Mbunge wa Nzega, Dk. Hamis Kigwangala, huku Kilufi akibainisha kuwa tatizo la siasa za Tanzania ni kwamba wenye kusimamia ukweli huwa hawapendwi.

Akizungumza katika ibada hiyo, Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi alimshauri Dk. Mwakyembe kuachana na Chama cha Mapinduzi (CCM) na badala yake ahamie chama chake cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akidai kuwa misimamo yake (Dk. Mwakyembe) haiendeni na ile ya chama chake.

“Kitu chochote ambacho hakijakuua, kinakupa nguvu zaidi. Kinachotuunganisha mimi na Dk. Mwakyembe, wote tuna ambition sawa, kusimamia maslahi ya Mbeya na Taifa letu kwa ujumla,” alisema Mbilinyi.

Kiasi cha shilingi milioni 41.8 zilipatikana katika ibada hiyo ya shukrani kama sadaka kwa Mwenyezi Mungu, ikiwa ni sehemu ya waliohudhuria ibada hiyo kumuunga mkono Dk. Mwakyembe katika shukrani yake kwa Mungu kwa mambo makuu aliyomtendea, ikiwamo kumwepusha na kifo katika vipindi tofauti.

Kiasi hicho cha fedha kilichokusanywa wakati wa ibada hiyo ya shukrani, kimeelekezwa kutumika kwenye kukamilisha ujenzi wa jengo jipya la Kanisa la Usharika huo wa Nduli pamoja na ukarabati wa jengo la zamani litakalotumika kuendesha miradi ya maendeleo ya kina mama kijijini Ikolo, ikiwamo upishi na ushonaji.

Viongozi wengine waliohudhuria ibada hiyo ni pamoja na Naibu Waziri wa Elimu, Philip Mulugo, Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk Charles Tizeba, aliyekuwa waziri wa maliasili na utalii, Ezekiel Maige na Mbunge Viti Maalumu, Hilda Ngoye.
 
Mkuu ugonjwa wako umefika pabaya!

Ukiwa mtaani hasa maeneo ya mijini ni dadra sana kusikia mtu anaisifia CCM, wapo watu wanapenda CCM iendelee kuwa madarakani ingawa watu hao huwa hawasemi wazi. Unaweza ukawaona kwenye mitandao ya kijamii kwa kutumia Nick names.

Zifuatazo ni sababu zinazofanya baadhi ya Watanzania kulilia CCM ibaki madarakani pamoja na umasikini, ufisadi uliokithiri kufikia hatua ya kushika nafasi ya pili kwa ufisadi Afrika mashariki, point moja tu baada ya uganda.

1. Watu hao kwa sasa wananufaika na mfumo wa sasa, kwani ni mfumo ambao uko loose,kundi hili ni waajiriwa serikalini. Wafanyakazi wa Serikali wamefanikiwa kuvuna pesa za wizi serikalini wanaomba hali iendelee kuwa kama ilivyo, CCM iendelee kutawala .

Wengi wetu tunawafahamu rafiki zetu walioko serikalini bila kujali kuwa wana nafasi za juu au za chini wamefanikiwa kutajirika ghafla, tunawafahamu lakini hakuna mahali pa kuripot kwakuwa system nzima ni Corrupt.

2. Wako wafanyabiashara wanaokwepa kodi, serikali imegubikwa na rushwa kwa hiyo hawawezi kukusanya kodi, kila kitu kinakwenda kwa dili au ten %. Hawa nao wanasema kidumu chama cha mapinduzi

3. Wako ambao wamezaliwa kwenye familia tajiri, wakiamka asubuhi wanajiuliza ama wale soseji au mayai. Friji zao Zimejaa kuku, samaki nk. Pia wanachagua watoke na aina gani ya gari. Kundi hili halifahamu vizuri umasikini uliowagubika watanzania, shida wanazisikia kwenye vyombo vya habari, maisha yao hawajichanganyi na masikini kabisa, wanasoma shule na vyuo vya kitajiri kwa hiyo umasikini hawaujui. Kwa hiyo hawaoni kosa la CCM

4. Masikini lakini wanaipenda CCM mpaka kesho. Kundi hili liko vijijini. Linaipenda CCM kwa sababu ya kukosa elimu ya uraia, au hawapati habari kabisa. Shughuli yao kubwa ni kulinda nyani wasivamie mashamba yao. Kundi hili halijui maana ya maendeleo, wanatamani hata shule zisiwepo ili watoto wachunge ng’ombe na kulima, wakivuna mazao ya kutosha wakala wakashiba hata kama hawana shilingi ya kununua ndala wao usema CCM oyeeeee

5. Kuna kundi ambalo lenyewe limedanganywa kwa uvumi au kwa mazoea tu. Kwamba bila CCM kutakuwa na vita, linasema CCM imenilea hadi hapa nilipo. Kundi ili liko tayari kuchagua hata fisadi au jiwe ilimradi tu atokee CCM. Kundi hili linafahamu kabisa kuwa serikali haifanyi vizuri lakini kwa mazoea lenyewe limeendelea kuomba CCM ibaki madarakani ili amani iendelee kuwepo.

6. Imani. Kundi hili ni mchanganyiko wa wasomi na wasiosoma. Hawa kwa sababu ya imani kali kwa dini limehamua kuweka dini mbele lakini maendeleo baadae. Kundi hili linafahamu kabisa madudu ya CCM lakini limeendelea kuwa na msimamo kwa CCM. Kundi hili udanganywa kirahisi kwa propaganda za CCM kwamba Chama fulani ni cha dini fulani. Bila kujali msitakhabali wa nchi uamua kushabikia CCM lakini baada ya miaka mitano huwa halioni mabadiliko ya kimaendeleo. Kundi hili ndilo linalochelewesha mapinduzi ya nchi, kundi hili ukesha likiomba CCM iweke mtu wa dini yake bila kujali uwezo wa kiongozi husika, wako tayari hata kupigia kura mgombea mwenye mtindio wa ubongo ilimradi awe wa dini yake.

7. Mafisadi papa. Hili ni kundi ambalo ni chafu kabisa, halina hata dini. Limeiba pesa nyingi za Watanzania bila kujali kuwa kila siku kuna masikini wanakufa kwa kukosa dawa mahosipitalini. Kundi hili kwa kutumia nguvu ya pesa za wizi linatamani ligawie kila mtanzani laki moja ili wapigie kura CCM. Kundi hili linahitaji CCM idumu ili lipate security ya mali zake, liko tayari hata kuua au kung'oa mtu kucha anaehatarisha CCM kuanguka. Linahofu kuwa chama kingine kikiingia madarakani litafilisiwa na kupelekwa mahakamani. Ni kundi lenye nguvu kubwa hata sasa ndani ya CCM
 
Ukiwa mtaani hasa maeneo ya mijini ni dadra sana kusikia mtu anaisifia CCM, wapo watu wanapenda CCM iendelee kuwa madarakani ingawa watu hao huwa hawasemi wazi. Unaweza ukawaona kwenye mitandao ya kijamii kwa kutumia Nick names.

Zifuatazo ni sababu zinazofanya baadhi ya Watanzania kulilia CCM ibaki madarakani pamoja na umasikini, ufisadi uliokithiri kufikia hatua ya kushika nafasi ya pili kwa ufisadi Afrika mashariki, point moja tu baada ya uganda.

1. Watu hao kwa sasa wananufaika na mfumo wa sasa, kwani ni mfumo ambao uko loose,kundi hili ni waajiriwa serikalini. Wafanyakazi wa Serikali wamefanikiwa kuvuna pesa za wizi serikalini wanaomba hali iendelee kuwa kama ilivyo, CCM iendelee kutawala .

Wengi wetu tunawafahamu rafiki zetu walioko serikalini bila kujali kuwa wana nafasi za juu au za chini wamefanikiwa kutajirika ghafla, tunawafahamu lakini hakuna mahali pa kuripot kwakuwa system nzima ni Corrupt.

2. Wako wafanyabiashara wanaokwepa kodi, serikali imegubikwa na rushwa kwa hiyo hawawezi kukusanya kodi, kila kitu kinakwenda kwa dili au ten %. Hawa nao wanasema kidumu chama cha mapinduzi

3. Wako ambao wamezaliwa kwenye familia tajiri, wakiamka asubuhi wanajiuliza ama wale soseji au mayai. Friji zao Zimejaa kuku, samaki nk. Pia wanachagua watoke na aina gani ya gari. Kundi hili halifahamu vizuri umasikini uliowagubika watanzania, shida wanazisikia kwenye vyombo vya habari, maisha yao hawajichanganyi na masikini kabisa, wanasoma shule na vyuo vya kitajiri kwa hiyo umasikini hawaujui. Kwa hiyo hawaoni kosa la CCM

4. Masikini lakini wanaipenda CCM mpaka kesho. Kundi hili liko vijijini. Linaipenda CCM kwa sababu ya kukosa elimu ya uraia, au hawapati habari kabisa. Shughuli yao kubwa ni kulinda nyani wasivamie mashamba yao. Kundi hili halijui maana ya maendeleo, wanatamani hata shule zisiwepo ili watoto wachunge ng'ombe na kulima, wakivuna mazao ya kutosha wakala wakashiba hata kama hawana shilingi ya kununua ndala wao usema CCM oyeeeee

5. Kuna kundi ambalo lenyewe limedanganywa kwa uvumi au kwa mazoea tu. Kwamba bila CCM kutakuwa na vita, linasema CCM imenilea hadi hapa nilipo. Kundi ili liko tayari kuchagua hata fisadi au jiwe ilimradi tu atokee CCM. Kundi hili linafahamu kabisa kuwa serikali haifanyi vizuri lakini kwa mazoea lenyewe limeendelea kuomba CCM ibaki madarakani ili amani iendelee kuwepo.

6. Imani. Kundi hili ni mchanganyiko wa wasomi na wasiosoma. Hawa kwa sababu ya imani kali kwa dini limehamua kuweka dini mbele lakini maendeleo baadae. Kundi hili linafahamu kabisa madudu ya CCM lakini limeendelea kuwa na msimamo kwa CCM. Kundi hili udanganywa kirahisi kwa propaganda za CCM kwamba Chama fulani ni cha dini fulani. Bila kujali msitakhabali wa nchi uamua kushabikia CCM lakini baada ya miaka mitano huwa halioni mabadiliko ya kimaendeleo. Kundi hili ndilo linalochelewesha mapinduzi ya nchi, kundi hili ukesha likiomba CCM iweke mtu wa dini yake bila kujali uwezo wa kiongozi husika, wako tayari hata kupigia kura mgombea mwenye mtindio wa ubongo ilimradi awe wa dini yake.

7. Mafisadi papa. Hili ni kundi ambalo ni chafu kabisa, halina hata dini. Limeiba pesa nyingi za Watanzania bila kujali kuwa kila siku kuna masikini wanakufa kwa kukosa dawa mahosipitalini. Kundi hili kwa kutumia nguvu ya pesa za wizi linatamani ligawie kila mtanzani laki moja ili wapigie kura CCM. Kundi hili linahitaji CCM idumu ili lipate security ya mali zake, liko tayari hata kuua au kung'oa mtu kucha anaehatarisha CCM kuanguka. Linahofu kuwa chama kingine kikiingia madarakani litafilisiwa na kupelekwa mahakamani. Ni kundi lenye nguvu kubwa hata sasa ndani ya CCM
 
Chris Lukosi hivi ukiambiwa wewe
Ni kati ya vijana wanaofikiria kwa kutumia makalio sio kwamba umetukanwa ila umeambiwa ukweli yaani Elimu yako ni kama haikusaidii kwani tunawasiwasi kwamba huko ulikuwa ukisoma au ulikuwa ukifanya kazi za ndani,au unapersonal issues na viongozi wa Chadema,

Kwa akili ndogo tu za mtu ambae hakwenda shule hauwezi kulinganisha Chadema na Utawala wa Amini kama kweli ni msomi yaani ni akili za kipumbavu huna tofauti na Juliana Shonza kwa kuwa yeye ni mwanamke lakini anakuzidi akili

Unachosema unakihoji na haujibiwi ni kipi yaani unayoyaandika hayakutofautishi na mpumbavu ambae hajaenda shule

Eleza moja unachokigombea na viongozi wa Chadema ni nini make utaonekana mpumbavu zaidi ya ulivyo sasa pamoja na kujiona mjanja,wewe unaongea ujinga sababu umekosa kazi sasa unataka kujipendekeza ili upewe cheo,ni fikra za kitoto kwa kufikiria kwamba utukane ili upewe cheo
Jiajiri tafuta kazi kukaa kwenye laptop mchana kutwa haitakusaidia kutoa matusi all the time
Usitake watu wakuamulie ujinga wako kwa kuongea upuuzi wako

Tumia elimu yako ili ujulikane kwamba ni educated person
 
Back
Top Bottom