Nini tathmini yako kwa CHADEMA 2012 Walipofanikiwa, Walipokosea na Mapendekezo 2013?

Karibuni masijala

JF-Expert Member
Sep 13, 2012
409
0
Wanabodi heshima kwenu.
Mwaka unaishia sisi kama Jf wa jukwaa la Siasa mwaka 2012 chama kikuu cha Upinzani au kinachounda Kambi Rasmi katika Uwakilishi wetu bungeni tulikishuhudia kikiendesha siasa za majukwaani kwa njia ya mikutano na upashaji wa habari kwa kutumia jukwaa hili.
Vilevile siasa za ndani ya bunge zikiongozwa na Mwenyekiti Mhe Mbowe, Tundu Lissu na wabunge wenzake
Makao makuu wakiongozwa na Rais wa Ukweli Katibu mkuu Dr. Slaa Safu yake wakiibua mikakati kama vile M4C na mingineyo kuchochea mabadiliko.
Nini tathimini yako
1. Kwa harakati za CHADEMA ndani ya bunge na nje ya bunge.
2. Unawapongeza kwa yapi waliyofanikisha kuchochea mabadiliko.
Nakumbuka jk aliamua mpaka kubadili baraza la mawaziri, piga chini muhando,kuibua ufisadi mpya Uswiss, madai ya tembo piga chini maige, nk
3.Mikakati na mambo walivyoyaendesha
4. Walipokuangusha au waliposhindwa
Kuwa huru kuwapongeza, Kuwakosoa walipokosea na Ushashauri wako kwa mwaka 2013 wa muhimu wazo huweza leta mabadiliko chanya
 
Makupa

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
3,403
2,000

Cdm wameumbuka sana 2012 hasa baada ya kupatikana kwa taarifa kuwa Dr Slaa bado ni mwana ccm damu
 
dada jane

JF-Expert Member
Dec 8, 2011
565
0
Pongezi kwa kuendelea kujitanua mpk vijijini japo bado maeneo mengine. Ila kijijini kwangu wamefika nilijivunia sana. Kazi kwangu kuendeleza vuguvugu kwa wazee.
 
Concrete

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
3,605
0
Kwa ujumla ni mafanikio makubwa sana hasa ndani ya Bunge, Chaguzi ndogo na M4C.

*KASORO
1/Utendaji duni wa baraza la wanawake.

2/Uhaba wa nembo za chama(Bendera, Stika nk)

3/Uchache wa matangazo kupitia vyombo vya habari hususani radio na TV

*MAPENDEKEZO
1/Kuharakisha uanzishwaji wa CHADEMA media hususani Radio.

2/Kuchapishwa haraka sana kwa Kalenda na stika zenye Nembo za Chadema na kusambazwa nchi nzima mapema kabla ya January 2013.

3/Kuandaa mkakati kabambe maalum kwa ajili ya kuwafikia zaidi wanawake ili waiunge mkono CHADEMA.

4/Kuendelea na harakati za M4C tena kwa kasi zaidi.

5/Kuanza kuandaa mikakati na wagombea kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka2014
 
chitambikwa

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
3,940
2,000
Chama kinafanya vizuri sana. Wachumia tumbo wameendelea kujiondoa chamani na nguvu kubwa ya ccm na ujambazi wake wameshindwa kukiua bali wamekitangaza zaidi kimataifa na hasa vijijini .
Bado hatuna fedha za kutosha lakini kwa kuwa tuna watu ndo cha muhimu sana. Tunahitaji kufanya kazi kubwa zaidi ili kukijenga na kukiimarisha na kwa sasa ni taasisi kubwa sana . Nakiona kama kina wapelelezi wakali kama wa Israeli
 
Curriculum Specialist

JF-Expert Member
Oct 8, 2007
2,731
0
Chadema imekuwa kwa kasi mwaka 2012 imekuwa tishio zaidi kwa CCM, imefanya kazi za kukumbukwa bungeni na nje ya Bunge, mapendekezo tuendelee kujiimarisha zaidi, na kuwa na mbinu mpya za kupambana za CCM! CCM wanakuja na mbinu mpya za propaganda ambazo wanazitumia tunahitaji kujipanga zaidi kuziyeyusha propaganda zao! Tuendelee kumtegemea Mwenyezi Mungu muweza wa yote, kwa pamoja 2013 tutaizika CCM jumla!
 
ndomyana

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
4,951
2,000
M4C kukubalika lindi na mtwara kwangu niliwapa hongera sana.

Kuchemka dk slaa jembe letu kujibishana na vuvuzela nape kuhusu kua na kadi ya ccm apo alichemka sana make majibu kama hayo tunayo toka mwaka 2010 ko karipandisha vuvuzela chat
 
meningitis

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
8,333
2,000
m4c ni mbinu muruwa iliyopeleka mauti kwa ccm.cha muhimu ni kuhakikisha ndani ya siku moja kunakuwa na m4c's katika kila mkoa.
Bado nashauri uandaliwe utaratibu wa kuhakikisha vijana hasa wa vyuoni wanapata fursa ya kupiga na kulinda kura hapo 2015.
Pia tuendelee kuwakumbusha wananchi juu ya ufisadi,mafisadi ni athari zake katika maisha yetu.
 
Karibuni masijala

JF-Expert Member
Sep 13, 2012
409
0
Chadema heko walijinga kwa kutumia wabunge na viongoz wake bungeni walitimiza wajibu umakini wa mnyika, lissu, msingwa na wote kweli bunge tulifurahia uwepo wao
mahakamani na matakwa ya kisheria wakili marufu na mzalendo kimongolo pokea heko zetu hasa kesi ya lema ungeweza kufisadiwa lakini umesimamia haki, Mhe Tundu lissu na Mabere marando mtambo Feki wa chemba na mtoto wa baba mwanaasha uliwaumbua
 
Karibuni masijala

JF-Expert Member
Sep 13, 2012
409
0
Chadema heko walijipanga vyem. kwa kutumia wabunge na viongoz wake 1.Bungeni walitimiza wajibu umakini wa mnyika, lissu, msingwa na wote kweli bunge tulifurahia uwepo wao
2.mahakamani na matakwa ya kisheria wakili marufu na mzalendo kimongolo pokea heko zetu hasa kesi ya lema ungeweza kufisadiwa lakini umesimamia haki, Mhe Tundu lissu na Mabere marando mtambo Feki wa chemba na mtoto wa baba mwanaasha uliwaumbua.
3.Uongoz wa Dr Slaa usiokuwa na makundi na usiotetereka ukiwa ummeshinda katibu mwenzake mukama hongereni ssm wao ni kupigana chini
4. Watanzania kwa mikutano programs zenu tumeamini ni chama cha demokrasia na maendeleo na cha chaguo la mtanzania 5. Wabunge hamkutuangusha ni shibuda na zitto tunawasiwasi na mchana chadema usiku ssm
MAPENDEKEZO 2013
1. Mikakati ya siasa za vijijini ndo kuna watu wengi na uchaguzi wa serikali za mitaa 2014
2. Changisheni ili kuanzisha TV na redio ya chama kama ssm itabana anzishe mwanachama TAMBUENI ssm imefanikiwa kuzima wamiliki wasiwape nafas kurusha matangazo TV,Nk
 
Aristides Pastory

JF-Expert Member
Feb 7, 2012
348
0
Kazi iliyofanywa ni nzuri mno mwaka 2012 .

USHAURI >>>

Naomba Mwaka 2013 Kasi iongezwe zaidi ya Ufunguzi wa Matawi haswa Vijijini .

Majimbo ambayo yanaonekana hayakupitiwa na M4C naomba uongozi uchukue jukumu la kupiga kambi ikiwezekana mwezi mzima kama ilivyofanyika pale MOROGORO .

Huku Dar es salaam yapo Maeneo yanasubiri M4C mfano: MBAGALA pamoja na Kata zake zote , TEMEKE .
 
MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,792
2,000
Naunga Mkono hoja hizi

- Upelelezi mkali kama wa Israel ili kugundua hujuma dhidi ya Chadema kabla hazijatekelezwa....
-Kalenda, badge, na sticker kabla ya Jan 2013
-Kuandaa viongozi wa kugombea 2014
-Vibaraka tuwajue kupitia hapa JF na tuwasambaze katika magazeti
-M4C ipangwe na ifanyike kwa Nguvu zaidi. Pia wazo la kufanya M4c kwa siku moja mikoa yote ni nzuri
-M4C ifanyike na Viongozi wa Kitaifa/Wabunge waende sehemu ambazo ni za vijijini zaidi.... ambazo M4C haijulikani
-Viongozi waache kupigania madaraka (uchu wa madaraka) badala yake washiriki M4C
-CDM media
 
Domy

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
4,696
2,000
Kwa upande wangu nimefanikiwa kuwashawishi rafiki zangu na ukoo wangu wote kuwa na kadi ya chadema.

Kwa upande wa chadema tumefanikiwa kuona serikali iliyoko madarakani inatekeleza sera za chadema!

Vile vile tunafurahi kuona Rais wa wananchi Dr W.P.Slaa akiwakosesha usingizi CCM.
 
Du Bois ideas

JF-Expert Member
Feb 1, 2011
427
0
Wamejitahidi sana katika kutoa elimu ya uraia kwa nchi kubwa namna hii angalau kila mtu anajua thanami yake katika chaguzi mbalimbali na maamuzi katika sera za taifa n.k. Ushauri wangu waendele kujiimarisha hasa vijijini na kuimarisha ofisi nchi nzima na kupanga mikakati ya ushindi katika chaguzi za serikali za mitaa 2015 na uchaguzi mkuu 2015
 
UPIU

JF-Expert Member
Jun 26, 2012
602
0
Kwa ujumla ni mafanikio makubwa sana hasa ndani ya Bunge, Chaguzi ndogo na M4C.

*KASORO
1/Utendaji duni wa baraza la wanawake.

2/Uhaba wa nembo za chama(Bendera, Stika nk)

3/Uchache wa matangazo kupitia vyombo vya habari hususani radio na TV

*MAPENDEKEZO
1/Kuharakisha uanzishwaji wa CHADEMA media hususani Radio.

2/Kuchapishwa haraka sana kwa Kalenda na stika zenye Nembo za Chadema na kusambazwa nchi nzima mapema kabla ya January 2013.

3/Kuandaa mkakati kabambe maalum kwa ajili ya kuwafikia zaidi wanawake ili waiunge mkono CHADEMA.

4/Kuendelea na harakati za M4C tena kwa kasi zaidi.

5/Kuanza kuandaa mikakati na wagombea kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka2014

Mkuu kwa sasa CHADEMA inakuwa katika decreasing rate, inaitajika Chama kishinde uchaguzi wowote utakaoitishwa ili kilete matumaini ya uhai, kama umaarufu wake ulivyopanda baada ya kushinda uchaguzi wa Arumeru
 
ungonella wa ukweli

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
4,211
0
Kwa ujumla ni mafanikio makubwa sana hasa ndani ya Bunge, Chaguzi ndogo na M4C.

*KASORO
1/Utendaji duni wa baraza la wanawake.

2/Uhaba wa nembo za chama(Bendera, Stika nk)

3/Uchache wa matangazo kupitia vyombo vya habari hususani radio na TV

*MAPENDEKEZO
1/Kuharakisha uanzishwaji wa CHADEMA media hususani Radio.

2/Kuchapishwa haraka sana kwa Kalenda na stika zenye Nembo za Chadema na kusambazwa nchi nzima mapema kabla ya January 2013.

3/Kuandaa mkakati kabambe maalum kwa ajili ya kuwafikia zaidi wanawake ili waiunge mkono CHADEMA.

4/Kuendelea na harakati za M4C tena kwa kasi zaidi.

5/Kuanza kuandaa mikakati na wagombea kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka2014
mkuu pamoja sana hasa suala la media na kuhamasisha wanawake kujiunga na chama!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom