w0rM
Member
- May 3, 2011
- 68
- 164
Wakuu salama
Innocent Bashungwa ambaye jana ameteuliwa kuwa Waziri wa Ujenzi amekuwa Waziri anayehamishwa Wizara mara nyingi sana. Nini hasa kipo nyuma ya Bashungwa kuhamishwa Wizara kila mara?
Ukiangalia tangu atotolewe kuwa Naibu Waziri wa Kilimo na kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara mnamo Juni 8, 2019 hadi sasa amekuwa Waziri katika Wizara 5 (Kipindi cha miaka 4).
Kwenye Wizara ya Viwanda na Biashara ndio Wizara pekee alikaa kwa zaidi ya mwaka moja.
Juni 8, 2019 - aliteuliwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara (miezi 22)
Machi 31, 2021 - Aliteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo (miezi 9)
Januari 8, 2022 - Aliteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) (miezi 9)
Octoba 2, 2022 - Aliteuliwa kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (miezi 11)
Na jana Agosti 30, 2023 Rais Samia amemteuwa kuwa Waziri wa Ujenzi.
Nini siri ya Bashungwa kuhamishwa kwenye Wizara hizi? Hii ya sasa atamaliza mwaka?