Nini siri ya baadhi ya watu kutozeeka mapema?

Nini siri ya baadhi ya watu kutozeeka mapema?

Baba/Mama tafuta ela uzee utausikia kwenye redio mbao, Muangalie Mama nasibu chombo mpya usipoangalia vizuri unaweza sema kigoli umnyapie.
[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Hii ni kutokana na kucheka sana hasa pale wanaposahisha mitihani sometime majibu ya wanafunzi yanafurahisha
Wanacheka maswali yalotungwa na kujibiwa na wanafunzi
 
Nilipata muda wa kwenda kutembea katika moja ya shule nilizosoma ambapo ni takriban miaka 9 sasa toka niondoke hapo.

Kuna watu nimewakuta hapo ambao niliwaacha walinishangaza sana, wamebadilika miaka tu lakini kimuonekano wako vile vile kama nilivowaacha miaka 9 nyuma na kuna wengine wamezeeka na mvi kibao, nilipata shauku ya kutaka kujua siri iliyopo ila muda haukua rafiki kwangu hivyo nimeona sio mbaya kuuliza kwenu wakuu sababu ni nini, ni vitu vya kurithi ama kuna namna mtu anaweza ishi ikamfanya awe hivyo?
Una maana walimu hawazeeki au?
 
Wanacheka jinsi baadhi ya wanafunzi walivyojibu maswali. Nilishakaa jirani na mwalimu wa Biology form 2 akiwa anasahisha mitihani anacheka peke yake ndani
Hata ww lazma ungecheka tu mtu anajitungia mtihani wake famasiala nn
 
Wali na Ugali,hasahasa unga wa Sembe na maandazi ni hatari Kwa ngozi yako!!
Mboga za majani na matunda ni suluhu ya uzee Kwa Sasa.
Punguza ulaji wa vyakula vyenye Wanga na Nyama hivyo mbadala wake uwe Matunda na Mbogamboga
Matunda na mboga mboga tu utapataje nguvu? Wewe ni vegetarian?
 
Nitaweza kuacha wali kweli mm

Maisha bila wali yangekuwaje duh
Mi mwenyewe siwezi

images.jpg
 
Kuna huyo babu toka miaka ya 1998 nipo katoto yuko vile vile mpaka leo, sasa mama yangu ambae ana miaka 50+ anakwambia huyo babu yupo hivyo hivyo toka wao bado wadogo. Mpaka leo hajabadilika chochote na anatembea vizuri tuu kweli Mungu kweli wa ajabu na kambariki sana.
 
Nitaweza kuacha wali kweli mm

Maisha bila wali yangekuwaje duh
Alafu ukutane na kiporo cha wali maharage asubuhi na chai ya moto weee kama ni hivyo acha nizeeke tu kwanza mimi wali maharage ndio umenikuza eti nije niukane ukubwani hapana
 
Kuna huyo babu toka miaka ya 1998 nipo katoto yuko vile vile mpaka leo, sasa mama yangu ambae ana miaka 50+ anakwambia huyo babu yupo hivyo hivyo toka wao bado wadogo. Mpaka leo hajabadilika chochote na anatembea vizuri tuu kweli Mungu kweli wa ajabu na kambariki sana.
Ulishawahi muuliza siri ya mafanikio?
 
Back
Top Bottom