Chadema hatuna sera ila tunaenda na matukio. CCM wakisema sisi tunapinga au kama kuna tukio CCM wanaliunga mkono sisi Chadema lazima tupinge hiyo ndiyo sera yetu kwa sasa. Ndio maana tulipinga kwa nguvu zote suala la makinikia, kutumbuliwa kwa mafisadi, vyeti feki, ujenzi wa SGR na "flyovers' za Ubungo na Tazara, Lowasa kukutana na Magufuli tulipinga pia. CCM wakiwa upande huu sisi tunaenda upande mwingine hiyo ndiyo kazi ya upinzani kama alivyosema mheshiwa sana ndugu Msingwa mbunge wa Iringa. Kwa kifupi sera yetu ni kupinga, matusi, kuharibu uzalendo, na kusifia au kuunga matamko yote yanayoshambulia serikali na mwisho ni kuwaunga mkono wote wanaoiba rasilimali za nchi yetu hasa madini kwa kisingizio cha kutupatia ajira.