Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 2,488
- 6,969
Wakuu,
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Afisa Utafiti wa LHRC, Fundikila Wazambi wakati anawasilisha ripoti ya mwaka amesema kati ya mwaka 2021 hadi 2025, kituo hicho kimekusanya na kuthibitisha jumla ya visa 197 vya utekaji na upoteaji wa watu, idadi ambayo imeelezwa kuwa kubwa na inayohitaji hatua za haraka.
"Swala jingine kuu ambalo liliathiri haki za binadamu kwa mwaka 2025 ni swala zima la utekaji na upoteaji wa watu. Na takwimu hizi zinaonyesha matukio haya yaliongezeka kwa mwaka 2025 kwa visa ambavyo tumevikusanya kwa kipindi cha miaka mitano, vimefikia 197."
Katika kuonyesha uzito wa suala hilo, Wazambi ametolea mfano tukio la Sheikh Jabel Haidar Jabel, ambaye alitekwa na baadaye kupatikana akiwa ameuawa, tukio lililozua mjadala mpana na shutuma kutoka kwa wadau mbalimbali wa haki za binadamu.