Nini sababu ya kuogopana kati ya Ke/Me?

Nini sababu ya kuogopana kati ya Ke/Me?

Konda wa bodaboda

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2014
Posts
7,981
Reaction score
4,174
Hii nimeiona kwa vijana wengi walio wengi bila kujali jinsia zao.

Unakuta upo kazini, chuoni, shuleni au hata kanisani na mtaani tu unakuwa unahitaji ukaribu fulani na mtu wa jinsia tofauti na yako, labda ni ukaribu wa kiofisi au hata kimahusiano ila unajikuta unapata kigugumizi kumuomba mbadilishane mawasiliano ya simu.

Hali hii inakuwa ngumu sana kwa upande wa jinsia ya kike kwani huwawia vigumu sana kufikia hatua kumuomba namba mpinzani wake(jinsia ya kiume) namba ya simu hata anahitaji kwa sababu ambazo sio za kimapenzi.

Sasa kama watu mnafanya kazi, kusoma au hata kushirikiana shughuli za hapa na pale kwanini muogopane?

Unakuta jamaa anaogopa kumuomba mdada namba direct, anaamua kumtumia mtu kuipata wakati yupo naye karibu kama nilivyosema hapo awali.

Kama hili ni tatizo, hebu wahusika mseme hapa nini sababu ya hilo tatizo.
 
Confidence hawana ndio maana... Wengi unakuta hawajiamini tu..ila mie huwaga sinaga muda wa kuwaza 'rejection' ..nikitaka namba nafata tu.. Tena mademu wengi wanapenda wanaume wenye confidence..so ukimfata direct unajiongezea point ..
Yote tisa, kumi usisahau kwenda kumpigia kura Lowasa 25 oct #Mabadiliko yatawapa watanzania confidence.
 
Sijajua kwann.hata me huwa najikuta naogopa gopa kumuanza ila kama na ye hana zile mapozi basi unakuta napata confidence haraka
 
Ngoja nirudishe kumbukumbu nyuma...ole wake alowahi kunireject


Hahaa hilo swali lako la uchokozi

i believe watu wote tumewahi experience some kind of rejections in our lives..
rejections hata kama painful zinatufanya tuwe more humble....
na kuwa humble kunatufanya tuwe better people...

we hujawahi?
 
mtu mnaonana karibu kila siku tena hata ni workmate sasa uombe namba ya nini...?
kama unataka kuanzisha mahusiano ya kimapenzi ni bora uanze kwa kukutana naye face to face, mwambie then ndio mambo ya namba yafuate baadaye...
 
Back
Top Bottom