Nini mtazamo wako kuhusu Clouds FM kuiga ubunifu wa E-FM?

hao washafika ukingoni,mbaya zaidi progam wa vipindi nayo hana uwezo,kazoea kuiga iga tu,nasikia wanataka kurudisha AFRIKA BAMBATAA,kisha wawe wanapita kila BAR
 
E fm ni kituo cha radio ambacho hakina muda mrefu tangu kianzishwe lakini kimejipatia umaarufu mkubwa Jijini Dar es Salaam na Pwani kutokana na ubunifu ktk utoaji wa matangazo yao na swaga za watangazaji wake mahiri ktk vipindi vyao ambao baadhi yao wametoka clouds fm.

Pamoja na uchanga wa kituo hicho (E fm), kituo kingine ambacho ni kikubwa nchini ambacho kinasikika karibu nchi nzima kwa masafa ya fm na Duniani kote kupitia mtandao kimekuwa kikiiga ubunifu wa radio E fm na kufanya kama vile ni ubunifu wao.

Mifano ya vitu vilivyoigwa na clouds fm ambavyo awali vilifanywa na Efm ni pamoja na kufanya kipindi nje ya studio. Efm wana kitu kinaitwa Nje ndani naona Clouds fm nao wameiga hiyo kwa kufanya kipindi cha leo cha sports Xtra huko Tandale.

Mbali na hilo Efm waliwahi kuandaa tamasha la waendesha bodaboda na bajaji kule kijitonyama, lakn baada ya tangazo la E fm clouds kupitia radio ya choice fm waliibuka na tangazo lao lenye tarehe hiyohiyo kufanya tamasha la walaji chips huko mbagala.

Baada ya matamasha haya Efm kwa kutumia Jingo ya Wimbo wa Mwana FA "Ahsanteni kwa kuja" waliwashukuru wote waliofika kwenye tamasha lao pale kijitonyama jambo lisilo la kawaida kwa kutumia jingo hiyohiyo choice fm (clouds media) walitumia kuwashukuru waliohudhuria tamasha lao pia.

Clouds media kupitia radio zake walikuwa hawawathamini kabisa wasanii wa singeli lakn baada ya E fm kuufanya aina hiyo ya mziki kama ndo mziki rasmi wa kituo hicho, clouds media kupitia Choice wameanza kupiga singeli na wameenda mbali hadi kuwajumuisha wasanii hao wa singeli kwenye matamasha yao llikiwemo tamasha lao kubwa la fiesta.

Kingine Efm walikuwa na kitu kinaitwa kapu la sikukuu, ambapo wanapiga jingo ktk kipindi fulani halafu wasanii wanapiga simu wakipatia muda jingo ilipopigwa na kipindi husika na watangazaji basi wanajishindia hilo kapu Clouds nao wakaja na kitu kinacgofanana na hiki (sikumbuki jina lake) ila nakumbuka walikua wanataja namba ww unatakiwa useme hizo namba zilitajwa kipindi gani, muda gani na watangazaji walikuwa akina nani.

Mimi naona kwa uigaji huu, clouds inajipotezea umaarufu pia inapoteza wasikilizaji. Na hilo linajidhirisha hapa mjini ukitembea mitaani ni E fm sehemu nyingi ukilinganisha na siku za nyuma.

Sasa sijui Efm ikisambaa mikoani itakuaje. Efm walikuwa na kitu inaitwa Sakasaka, Shika ndinga na sasa hivi wameanzisha Efm Jogging Club Ninawasiwasi Clouds huenda wako mbioni kuiga.

Efm wana msemo wao "Huu mchezo hauhitaji hasira". Nilishangaa siku nikausikia huu msemo kwa Kipanya wa Power Breakfast.

Nini mtazamo wako juu ya hii kitu.?
Ndugu Habari zote ulizoweka hapo ni za uzushi na kutunga Fanya research kabla ya kupotosha tamasha la Chips yai pamoja na tamasha la Waendesha bajaji yalifanyika siku mmoja ,
pili kurusha vipindi live nje ya clouds havikuanza leo toka 2012 link hiyo hapo http://gsengo.blogspot.com/2012/04/clouds-fm-yazindua-mpango-mpya-wa.html
clouds%2Bfm1.jpg

Kama unasifia E-fm fanya hivyo na sio kupotosha Jukwa
 
Ndugu Habari zote ulizoweka hapo ni za uzushi na kutunga Fanya research kabla ya kupotosha tamasha la Chips yai pamoja na tamasha la Waendesha bajaji yalifanyika siku mmoja ,
pili kurusha vipindi live nje ya clouds havikuanza leo toka 2012 link hiyo hapo http://gsengo.blogspot.com/2012/04/clouds-fm-yazindua-mpango-mpya-wa.html
clouds%2Bfm1.jpg

Kama unasifia E-fm fanya hivyo na sio kupotosha Jukwa
e.fm huwa wana rusha kipindi cha joto la asubuhi kila ijumaa nje ya studio halafu kuna kuwa n wasanii wa singeli kitu ambacho week hii sports xtra wameiga halafu clouds kurusha vipindi kwa nje walikuwa wanafanya kukiwa n kitu au tukio maalumu either mahujiano n kiongoz flan au tamsha au kampen maalumu
 
Wakuu hebu tuongee kwa hoja sio blah blah, hivi kiukweli kabisa kutoka moyoni unaweza kuyajua haya yooooooooote kuwa Clouds wanaiga kama huisikilizi hiyo radio .............Kwanini tusiseme kuwa na wao E.FM imeiga kuanzisha Radio ..............Tuseme pia E.FM imeiga kupiga Bongo fleva kutoka kwa Radio one ambao ndio waanzilishi ............Tuseme pia E.FM imewaiga Clouds mtindo wa utangazaji wa watangazaji kuwa watatu na zaidi studioni hii kitu haikuwepo kabla ya Clouds ..........Tuseme pia E.FM imewaiga Radio One kwa mtindo wao wa kuwachukua watangazaji kutoka radio nyingine maana Radio one ndio walioanza mchezo huo kuwachukua watangazaji wa RTD (TBC) ............Tuseme pia kuwa E.FM imewaiga Clouds mtindo wa radio stations kuandaa matamasha,maana kabla ya Clouds hapakuwa na Radio stations zinazoanzisha matamasha ......... Tuseme pia E.FM imewaiga Clouds kwa mtindo wao wa vipindi vya michezo kuwa zaidi ya robo saa (dakika 15) kabla ya Clouds hapakuwa na Radio inayorusha kipindi cha michezo kwa muda zaidi ya robo saa ?????? LETENI HOJA ACHENI BLAH BLAH,KAMA NI KUIGA HATA NYINYI/SISI TUNAIGA KUVAA MAANA KABLA YA WAZUNGU KUBUNI NGUO BINADAMU ALITEMBEA UCHI,KIPI AMBACHO WEWE SASA HIVI UNAKIFANYA AMBACHO UIGI ............ HATA UKINI QUOTE TAYARI NA WEWE UMEIGA KUTOKA KWA WABUNIFU, ACHENI UJINGA NA UPUMBAVU WENU.
 
Huu mchezo hauhitaji hasira...kipanya anaupenda sana huu aliutumia kwenye social media kipindi kile cha tamasha la chips na huku komaa concert
 
e.fm huwa wana rusha kipindi cha joto la asubuhi kila ijumaa nje ya studio halafu kuna kuwa n wasanii wa singeli kitu ambacho week hii sports xtra wameiga halafu clouds kurusha vipindi kwa nje walikuwa wanafanya kukiwa n kitu au tukio maalumu either mahujiano n kiongoz flan au tamsha au kampen maalumu
Unafahamu Ndondo Cup? kumbe hata hujui kwanini walifanyia Nje unawajua Msosi FC ya Tandale?

Kama hujui kaa kimya
 
Tangu waanze kuhoji Mashoga kwenye kituo chao cha Clouds TV walizidi kuporomoka maradufu,na nyie E fm msije iga huo upuuzi.
Wanatafuta wasikilizaji hawa na majizzo mjanja mno kupitia huo udhaifu wanaouleta clouds majizzo anajichukulia listerners kibao hapo
 
Clouds ilikuwa zamani, saiv haina kitu ikibid iuze masafa au ibadirishe jina la kitu. Mwanzo waliwaonea sana timesfm, timesfm walipo anza kutangaxa mziki wa naijeria clouds wakadaki.. Efm na kisengeli na pale wakadakia il waonekane wao ndo wanausapot huo mziki. Ila kwa bahati mbaya wamechemka.
Hii ishu ya times ni kweli kabisaa nakumbuka skelewu niliisikiaga sana ikipata airtime times jamaa walipomleta davido ndio nao wakaanza zigonga za naija ila kukumbuka davido alipaswa fanya tamasha na times mwisho wa picha wakageuza kibao na kumchukua wao tena kwenye fiesta
 
Back
Top Bottom