Nini msimamo wa CHADEMA kuhusu Azimio la Arusha?

Nini msimamo wa CHADEMA kuhusu Azimio la Arusha?

Vyema Mkuu wangu Highlander, nadhani tunakubaliana hapa kuwa serikali kwa kutumia mikopo na masharti waliyoyamudu, walishaanza kuonesha tumaini la kutunusuru kabla ya mvurugo wa AZ.
Suala la watumishi wa umma (viongozi) kujishughulisha na biashara unasema si tatizo kwako ila tu wangehojiwa walichonacho kabla na baada! Hofu yangu ni hii, heshima ya mtu leo hii inajengwa na alichonacho. Aje kama wale wote madarakani wakaamua kutunga sheria kulinda biashara zao? Ndicho kinachotokea leo! Hakimu na waziri wana-share hisa, mimi kapuku sina nayemjua. Wakati huo tumeruhusu ushindani wa kibiashara, unadhani nitapata fursa sawa kama zao?
Nimekupata Mkuu Highlander kuhusu Demokrasia. Hakika uliyotoa ndio maana asili ya demokrasia. Kama unavyosema kuwa iliyopo leo, IMECHAKACHULIWA! Tena ni kwa makusudi. Sina ugomvi na Demokrasia hiyo! Hata wewe Mkuu wangu Demokrasia unayoitaka, si hii nayosemea mimi! Si hii iliyopo. Hii ni BATILI-IMECHAKACHULIWA. Na ndiyo tuliyoletewa na IMF/WB, na ndiyo tunayoshinikizwa kuifuata! Hizi ni NJAMA ZAO ZA WAZI. Ndio maana nilisema, chunguza maneno haya mawili HAKI na UHURU under misingi ya Demokrasia iliyopo leo! Utaona uvundo na HILA za IMF. Mimi sizitaki!
Mkuu Highlander, japo ilikuwa kama umefunga hoja ya Biashara, naomba kwa heshima yako nikurudishe nyuma. Mkuu unasema Kanuni kuu ya biashara ni kupata FAIDA. SAWA. Lakini niulize hapa, je kuna chochote afanyacho mtu hakijasimama katika kupata faida? Ni kweli, biashara ni kupata faida. Hata kula nikupata faida, hata kulala nako! Kwanini iwe kwa biashara tu? Je hiyo si kanuni ya jumla ya maisha?
Kwanza Faida ni nini katika biashara? Je, hiyo faida iwe kwa nani? Je, ni kwa muuzaji tu ama na mnunuaji? Faida hiyo inabagua?
Kwa misingi ya UTU wa mtu mweusi, kwanza...
(a) Faida katika biashara, ni uwezo wake wa kuwa ENDELEVU "SUSTAINABILITY" wakati Faida under Democratic principles ni SURPLUS.
(b) Gharama za kufanya biashara iwe endelevu ni hii, THE PROFIT MUST BE SHARED kati ya wahusika wote. HAKUNA FAIDA KAMA HAITO-BE SHARED. The profit must be shared Mkuu wangu! Ni kwa misingi ya UTU wa mtu mweusi. Hiyo ndio gharama halisi.
(c) How then to share the Profit? Hapo ndipo naposema Nyakati na Mazingira husika ndiyo yanayopaswa kuamua hilo. Ni kwa kuangalia demands kulingana na Mazingira na Nyakati za wote na kupewa reasonable share zao. Je, mazingira yetu na nyakati zinafanana duniani kote? HAPANA.
Katika misingi ya Demokrasia iliyopo, faida ni kwa muuzaji tu with no consideration to wanunuzi. Hili lipo wazi, hata hapo ulipo kuna zaidi ya mifano kumi mbele yako. Mzungu alifanikiwa sana kutupindulia mambo. YANATUFUNGA LEO.
Ni hayo Mkuu wangu;
Mungu wetu yu tayari kutushindia vitani. Anaita sasa!
 
Last edited by a moderator:
Unasema Hakimu na waziri wana-share hisa, mimi kapuku sina nayemjua. Wakati huo tumeruhusu ushindani wa kibiashara, unadhani nitapata fursa sawa kama zao? Jibu ni kwamba tupo katika tope. Kitakachotutoa katika tope hili si Upole. Hawa watu unaowataja hapa wamekwisha jilimbikizia mali nyingi sana ndani na nje, tunahitaji sana maudhui fulanifulani mazuri ya Azimio la Arusha yarudi kulinusuru Taifa.

Lakini kwa sababu sera huwa naneno tu kwenye maandishi, kuna hatari ya kushindwa katika jitihada hii ya kutafuta usawa wa kipato. Hapa njia ninayoiona ni kuwalazimisha hawa watu kuachia hizi mali walizoziiba. Hatutaweza kwa maneno matupu. Naweza nisilitamke hapa, lakini ndiyo njia iliyobaki. Na mtekelezaji hawezi kuwa aliyesababisha tatizo. Atakuwa mtu mwingine. Si lazima liitwe Azimio la Arusha kwa sababu dispensetion imebadilika, lakini malengo yatafanana. Safari hii Mkoloni ni mweusi mwenzetu. Tatizo siyo dogo. Ni kubwa.

Una mkoloni mweusi upande wa kuume: Ana mashule ya sekondari rundo kila moja ikiingiza mamilioni ya fedha kwa mwaka, ana viwanja vya kuegesha magari katika kila wilaya ya Tanzania, na majumba ya kukodisha, ana ada za wanachama, ana misaada ya wafanyabiashara wakubwa aliowawezesha yeye kupata utajiri ule kwa njia haramu, ana dola. Halaf upande wa kushoto unaye mshindani wake ambaye nguvu pekee aliyo nayo ni kikundi cha watu waoga; watu ambao wanatetemeka kwa hofu wanapoangalia hazina ya maguvu na mtaji vilivyopo upande wa pili. Wanatetemeka wakiviangalia.

Kazi iliyo mbele yetu ni kubwa sana, ni hatari, ni ngumu. Kitu pekee kitasaidiapo kidogo ni 'collective rage' kutoka kwa wananchi chini ya chama au hata vyama vinavyokubalika. Wakoloni wetu wanalijua hili--ndiyo maana wanavuruga mikutano ya kuhamasisha wananchi. It's not going to be as easy as we may want. Hawa watu kwa kutumia utajiri wetu wenyewe waliotuibia wanao uwezo hata wa kununua mamluki waingie nchini kutupiga tunyamaze waendelee kuiba.

Azimio la Arusha jipya ni ndoto nzuri, lakini haitapatikana na kuwa kitu halisi kirahisi!

Mkuu JingalaFalsafa, Niombe ruksa yako kutangaza kuwa niliwahi kuwa na mwalimu wa kozi moja philosophy miaka mingi iliyopita. Hoja yako kwenye eneo la biashara na dhana ya faida limenikumbusa kozi ile na mwalimu yule. Alitwambia "Philosophy is sometimes like chasing a black cat in the dark!"

Umenifurahisha katika mzunguko wa kuchambua dhana ya faida, ambapo hata hivyo katika hitimisho bado umeonekana kukubaliana na kila mwenye kuchambua faida. Faida, kwa kiingereza cha lugha za biashara inaitwa Utility. Utility ni ule mridhiko unaoupata katika kitu ulichopata. Ukiwa Tandale, unaweza kununua baiskeli ya shilingi 50,000 Manzese kwa shilingi 100,000 na ikawa na Utility kwako. Pesa ulioyotoa haina maana sana kwako. Lakini Muuzaji wa Baiskeli ataona kapata kitu kikubwa sana katika ile 100,000 uliyompa wewe ambaye unaona ile 100,000 haina utility iliyopo katika baskeli. Ni kweli, kama unavyosema, maisha yote ni kufukuzia faida, hata kama dhana ya faida ni very subjective. Lakini ukimkata faida sana mtu atajua kwa sabu panauma; na pengine ndiyo maana tuna ugomvi na hawa tunahisi wamekata kupita kiasi kiwango cha faida ya maisha tuliyo nayo hapa nchini.

Labda hapa mwisho niombe tukubaliane kwamba hatujapata muafaka kwenye mtizamo wa IMF na World Bank. Wewe unaona wao ndo chanzo cha ujio wa Azimio la Zanzibar, wao ndo chanzo cha rushwa iliyokithiri ndani ya nchi yetu, na kwamba wao ndo chanzo cha udhaifu wa utawala tunaouona. Mimi nawaona IMF na World Bank wakiwa tasisi zilizotutoa shimoni, na kwamba matatizo yaliyopo katika dispensation ya siasa za uchumi wetu ya sasa yameletwa na Hulka ya ulafi iliyopo katika wale tuliowapatia nafasi ya kutuongoza. Naomba tukubaliane kutokukubaliana kwenye hili.
 
Nawaomba radhi tena kwa kutorudi kwa wakati kuchangia hoja muhimu zilizotolewa humu na wadau mbalimbali. Pia nasikitika kwamba sijapata bahati ya kumkuta mzee wetu Edwin mtei humu lakini ni matumaini yangu kwamba akipata nafasi atajumuika nasi tena katika mjadala huu muhimu. Bado naendelea kusoma michango ya watu mbalimbali na nitarudi kujadili baadhi ya hoja lakini kwa vile the general atmosphere ya mjadala is well understood, nina machache ya kujadili lakini pia nina maswali muhimu ya kumuuliza mzee Edwin Mtei pamoja na wadau wengine husika katika mjadala.


Mijadala mingi juu ya Azimio la Arusha imekuwa inatawaliwa zaidi na hoja juu ya "WHAT WENT WRONG", huku mijadala juu ya "WHAT WENT RIGHT", ikipewa nafasi ndogo sana. Vilevile kwa kiasi Fulani, mijadala inayohusiana na Azimio la Arusha imekuwa inatawaliwa na chuki (kidini, kikanda, kikabila) na pia kusukumwa zaidi na ushabiki wa kisiasa, hasa dhidi ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kuliko objectivism. Wahusika katika haya wanajisahau kwamba njia sahihi ya kulielewa Azimio la Arusha ni kupitia objectivism (sio subjectivism). Ushauri wangu kwahiyo ni kwamba - tujadili azimio la arusha kwa framework ifuatayo:


Kwanza – Ni Malengo au madhumuni ya Azimio la Arusha.
Pili – Ni Mchakato uliotumiwa kutekeleza sera za Azimio la Arusha, na
Tatu – Ni Matokeo ya Utekelezaji wa sera za Azimio la Arusha.


Swali langu linalofuata kwenu wadau bila ya kumsahau mzee Edwin mtei ni je – tatizo lenu juu ya azimio la arusha lilikuwa wapi hasa na kama bado lipo, ni katika eneo lipi hasa:


Je, ni kwenye MALENGO/MADHUMUNI ya Azimio La Arusha?
Je, ni kwenye UTEKELEZAJI wa sera za azimio la Arusha? Au
Je, ni kwenye MATOKEO ya Utekelezaji wa Sera za Azimio la Arusha?


Ili kuwapa nafasi nzuri zaidi ya kuja na majibu yaliyojitosheleza, pengine ni muhimu nijadili yafuatayo:


Mzee Edwin Mtei, nadhani unaelewa fika kwamba kufikia mwaka 1961, hali ya uchumi na maisha ya watangayika ilikuwa ni tofauti sana ikilinganishwa na makoloni mengine kama vile Kenya, Zimbabwe n.k. Kwani kwa kutazama historia hata ya kiwango cha elimu ya msingi, katika Tanganyika, ukoloni uliishia na mjerumani mapema sana, na baada ya hapo, Tanganyika ikawekwa chini ya uangalizi wa Mwingereza. Kutokaa na hali hii, Mwingereza hakuwekeza lolote la maana in terms of Human Capital and Physical Infrastructure katika Tanganyika tofauti na maeneo mengine ambayo kwake yalikuwa ni makoloni yake rasmi. Matokeo yake ni kwamba kufikia mwaka 1961, Tanganyika kama taifa lilikuwa nyuma sana kimaendeleo, na takwimu zinasema kwamba by 1960, almost 90% of Tanganyika was rural, primitive and illiterate. Iwapo tunakubaliana hadi hapa, basi nadhani pia tutakubaliana katika yafuatayo:


Mafanikio ya TAA na baadae TANU yalitokana na juhudi kubwa za viongozi husika kuwaunganisha watanganyika, huku ahadi mbalimbali zikitolewa juu ya faida zitakazopatikana baada ya uhuru. Nadhani katika suala la ahadi za ukombozi na utekelezaji wake, Mzee wetu Mzee Edwin Mtei ni suala la Dejavu kwako kwani Chadema imefanikiwa sana kuwapa matumaini watanzania juu ya faida za ukombozi iwapo watakiunga mkono Chadema 2015 kuing'oa CCM madarakani kwa hoja ambayo inakubaliwa na wengi, i.e. CCM imeshindwa kumkomboa mtanzania. Lakini huo ni mjadala mwingine, nikirudi kwenye hoja yangu ya msingi, mzee mtei, nadhani utakubaliana nami kwamba – after 1961, the success or failure of Tanganyika as a state was going to be judged by her ability to deliver the services promised during the liberation struggle, na utekelezaji huu was to become one of the key components of legitimacy ya TANU na Serikali yake in the eyes of watanganyika. Nadhani ni kutokana na ukweli huu ndio maana mzee wetu Edwin mtei na wengine wachache (tofauti na watu kama Oscar Kambona na wengineo) waliamua kumuunga mkono Mwalimu na Azimio La arusha kwani it was almost impossible for TANU to deliver the goods promised wakati wa harakati za ukombozi kwa kutegemea mfumo uliorithiwa kutoka kwa mkoloni. Kama sipo sahihi katika hili, nasimama kupingwa;


Hoja yangu ya pili –


Nadhani mzee wetu Edwin mtei na wadau wengine pia mtakubaliana na mimi kwamba economic crisis that hit our country, first in 1973-4 na baadae 1978-9 haikusababishwa na ujamaa per se bali combination of a variety of factors. Kumekuwepo upotoshaji mkubwa sana juu ya hili. Sidhani kama kuna haja ya mimi kujadili internal and external factors zilizopelekea Tanzania kutumbukia katika economic crisis lakini the bottom line hapa ni kwamba – ujamaa haukubadilisha sana mfumo wa uchumi ulioachwa na mkoloni ambao ulitegemea uzalishaji wa mazao ya biashara for export in order to finance the needed imports for kilimo, industrialization and delivery of social services. Sana sana ujamaa ulijaribu kuja na ‘a more organized way to sustain such a colonial pattern', huku Mwalimu akiwa na matumaini kwamba tofauti na zamani ambapo benefits za sekta ya kilimo zilimufaisha mkoloni peke yake, chini ya Azimio la Arusha, Mwalimu aliamini kwa dhati kabisa kwamba Tanganyika ingekuwa katika nafasi nzuri to undergo an agricultural transformation ambapo the end result ni mapinduzi ya viwanda. Tulifanikiwa japo kidogo towards that end na nitajadili hili la industrialization mwishoni kwa mtindo wa swali kwa mzee wetu Edwin mtei na wadau wengine.


Hoja yangu ya tatu –


Hoja hii inaendana na ya pili hapo juu na ni kwamba tofauti na wengi wanavyopotosha na pia kupotoka, Ujamaa haukuwa ukomunisti na sidhani kama nina haja ya kufafanua hili. Vinginevyo, kutokana na ukweli huu, ndio maana Mzee Edwin Mtei na wengine mnaelewa kwamba nchi za magharibi pamoja na Benki ya Dunia chini ya Mcmanara ziliunga mkono sana Azimio la Arusha,kiasi cha kwamba ilifikia wakati Tanzania ikawa ni moja ya mataifa yaliyokuwa yanayopokea misaada kwa wingi sana duniani, na ilifikia wakati tukawa only second to Israel. Je, where did this AID go? Huo ni mjadala mwingine na nadhani mzee Edwin mtei ataendelea kuwepo ili kwa pamoja tujadiliane juu ya hilo hapo baadae.


Pengine ili kujenga vizuri muktadha wa mjadala, ni vyema tujikumbushe kidogo some of the key elements za Azimio la Arusha:



  1. Nationalization of private interests, hasa mabenki na Bima;
  2. Nationalization of most of food processing factories…
  3. Nationalization of manufacturing and trading companies…
  4. Nationalization of import and export whole selling enterprises
  5. Nationalization of commercial buildings kupitia NHC;
  6. Mwalimu kufungia kufuli exploitation of our natural resources mpaka pale tutakapokuwa tayari;
  7. Provision of social services kwa wananchi hasa elimu, afya n.k;
  8. Leadership code iliyolenga taifa kupata viongozi wenye uadilifu, uzalendo na wawajibikaji…


Kulikuwa na faida na hasara katika mengi ya hapo juu lakini kwa sasa ningependa kujikita zaidi katika suala la saba i.e. "provision of social services….", kwani kama nilivyojadili awali juu ya historia ya taifa letu, hasa changamoto za kisiasa, kijamii na kiuchumi kama taifa uhuru on independence eve, haikuwa jambo rahisi kwa TANU kukwepa suala la provision of social services kwa umma by the state na nadhani mzee Edwin mtei atakubaliana na mimi katika hilo. Iwapo mzee mtei na wengineo mnakubaliana nami katika hoja hii, basi nina uhakika pia mtakubaliana nami katika hoja ifuatayo:


Provision of social services chini ya Ujamaa iliendelea kutegemea sana Foreign AID licha ya jitihada za serikali kujitahidi to finance it from our own sources. Tusisahau hapa pia kwamba explosion in population growth ilikuwa ni moja ya sababu kubwa sana juu ya kwanini delivery of social delivery kwa umma by the state iliendelea kukabiliwa na changamoto kubwa sana karibia throughout the Ujamaa period, ingawa aidha out of ignorance or arrogance, watanzania wengi wanapuuzia this fact. As of 1961, population ya Tanganyika ilikuwa around nine (9) million, huku majority – almost 90% wakiwa vijijini and as backwards/primitive and illiterate as of early 19[SUP]th[/SUP] century mkoloni alipoanza ku establish Tanganyika as a territory. Nikirudi kwenye hoja yangu ya msingi – sababu ya serikali kuendelea kutegemea foreign AID kutoa huduma za kijamii kwa wananchi (maji, afya, elimu n.k), ilikuwa pamoja na ukweli kwamba uchumi wetu ulikuwa ukitegemea sana mazao ya kilimo for exports, na kilichokuwa kinapatikana wasn't enough to support the needs of the surging population.


Kwa maana nyingine, ilibidi tuendelee kutegemea AID katika kutoa huduma za msingi za kijamii kutokana na the fact kwamba our internal economic organization did not provide the material resources to finance such social services and the related programmes. Madhara yake ikawa ni further reinforcement of dependency ya nchi yetu kwani terms of trade were not as favorable, Balance of Payments position iliendelea kuyumba, na kupelekea huku deni la taifa kuanza kupanda kwa kasi. Mzee Mtei anaelewa fika kwamba ni kutokana na hali hii, wahisani wakaona kwamba the only way forward for our economy to make a turnaround was to abandon sera ya ujamaa and adopt Structural Adjustments Policies.


Vinginevyo nadhani mzee Mtei atakubaliana na mimi kwamba yeye kama kiongozi aliendelea kwa na imani na Azimio la Arusha kwa muda mrefu na ndio maana aliendelea kuitumikia serikali ya Mwalimu Nyerere katika key positions za jikoni kabisa kiuchumi – Gavana wa benki kuu na waziri wa fedha katika nyakati tofauti. Kwa maana hii, at least in the medium term, aliliunga mkono azimio la arusha, at least Madhumuni ya Azimio la Arusha, kwani suala la Mchakato na Matokeo ni yeye pekee mweney uwezo wa kulisemea. Vinginevyo kuna kila dalili kwamba tofauti iliyojitokeza baina ya mtei na Nyerere ilikuwa way and above madhumuni, pengine ilikuwa ni umuhimu wa mageuzi ili kuokoa the staggering economy, suala ambalo Mwalimu Nyerere hakukubaliana nalo lakini kwa hoja nzuri tu ambazo tutajadili baadae kwani madhara ya SAPs tunayaona leo.



Naomba nisisitize tena kwamba – chini ya ujamaa, ilifikia hatua uchumi ukaanza kwenda kombo lakini sio kwa sababu we adopted Azimio la Arusha bali kutokana na sababu mbalimbali za ndani na nje ya nchi, lakini muhimu ikiwa ni pamoja the underlying fragility of our economy/ structural weaknesses, of our economy tatizo ambalo bado lipo leo hii mwaka wa 28 wa soko huria na ubepari. Ushahidi juu ya hili ni kwa kuangalia the fact kwamba pamoja na sisi kupitia phase ya Ujamaa, wenzetu ambao waliendelea na soko huria tokeo uhuru wao leo hii hawana lolote la kujivunia kwamba wamepiga hatua zaidi yetu. Sana sana mataifa mengi katika afrika yanakosa the necessary ingredient ya economic development ambayo ni social cohesion, unity and leace. Vinginevyo, its such an irony kwamba mataifa kama Kenya, Zimbabwe, Nigeria n.k, wote yapo classified as Low Income Countries kama Tanzania!!!


Hoja yangu ya nne –


Ni muhimu tukaelewa kwamba pamoja na uwepo wa azimio la arusha, this didn't affect the fundamental productive basis of the economy of Tanganyika kwani, it was still colonial in nature. Ndio maana former colonial powers wengi pamoja na WorldBank waliunga mkonoU jamaa. Kwa maana nyingine – pamoja na basic industrial strategy ya Tanganyika katika miaka ya mwanzo ya 1970s, bado the new industrial capacity wasn't well integrated with local skills and resources; This led to even greater reliance on cash crops for foreign exchange earnings ili to finance importation of machinery, spare parts, oil and expertise, among other things, which were key for agricultural development and industrialization; Our dependence on narrow line of products maana yake ikawa kwamba – kufikia mwishoni mwa 1970s (when the second wave of economic crisis hit on a global scale), we began to feel the effects of the deteriorating terms of trade - kuanguka kwa mapato ya mazao kama vile katani n.k. Katani kwa mfano wakati Fulani ilikuwa ni provider wa foreign earning from exports by almost 50%. Hapa pia ningependa kuongezea hili:


Kuna hoja kutoka kwa baadhi ya watanzania kwamba azimio la arusha liliua productivity katika kilimo. Kwa kiasi Fulani upo ukweli katika hili lakini ni muhimu pia ieleweke kwamba kuwa na high productivity katika kilimo sio mwarubaini wa matatizo yetu ya msingi ambayo basis yake ilikuwa na inaendelea kuwa the structural weaknesses of our economy, lani sio Tanzania tu bali nchi nyingi zinazoendelea (LDCs). Tufahamu kwamba hata kwa mataifa makubwa kama USA na mengineo, Sekta ya Kilimo ni very strategic and sensitive, kwahiyo hata kama nchi maskini zina mazao mengi na bora ambayo yamezalishwa kwa efficiency ya hali ya juu, bado suala la politics katika sekta hii mfano protectionism n.k, can affect mafanikio yetu na kilimo. Vile vile kuna suala la devaluation ambapo huwa tunalazimishwa na mataifa makubwa kupunguza thamani ya sarafu yetu ili bidhaa zetu za mazao ya kilimo ziwe na soko zuri zaidi huko nje.


Protectionism and devaluation policies hazijali kama taifa maskini liliwekeza kikamilifu katika kilimo na kufanikiwa kuzalisha mazao yake kwa efficiency ya hali ya juu. Vile vile, bei za mazao ya kilimo (perishables) ni very volatile by nature, tofauti na bei za durable consumer goods; ndio maana mkakati wa Mwalimu ulikuwa ni kutumia kilimo kama daraja la kuelekea towards industrialization, hence enable Tanzania kuingia into higher value chains za commodity production.


Mzee Edwin mtei – tofauti ya msimamo baina yako na Mwalimu in the 1980s ilitokana na msimamo wako kwamba kulikuwa na haja kwa nchi kuingia katika mageuzi ili kuiokoa isiporomoke zaidi kwani uchumi wetu ulikuwa in the brink of collapsing; This was fair enough and justified. Lakini, as part of the package ya SAPs of which you strongly supported and later coordinated kupitia Dawati la Tanzania kule IMF, Washington, ilikuwa ni masuala ya Liberalization, Marketization and Privatization, ndio maana nasisitiza umuhimu wako kwenda public na kukiri kwamba soko huria lina mapungufu makubwa ambayo Azimio la Arusha iwapo lingesimamiwa vizuri katika maeneo kadhaa (sio maeneo yote kwani kulikuwa pia na mapungufu mengi sana), basi taifa letu lingekuwa katika unafuu kuliko ilivyo sasa. Specifically, ningependa kumuuliza mzee Edwin Mtei na wdau husika maswali yafuatavyo:



  • Je, ukiwa chini ya IMF baada ya kuondoka Tanzania na kwenda kufanya nao kazi Washington in 1980s baada ya kupingana na Mwalimu, unadhani ni wapi mlikosea na kupelekea nchi kutumbukia zaidi katika matatizo na kufikia kuwa nchi ya tatu kutoka mwisho kwa umaskini duniani wakati wa utawala wa mwinyi in early 1990s? Kwa vile tuna tabia yak u focus on what went wrong chini ya ujamaa, nadhani angalau on this one utatumia muda wako mchache kujadili juu ya what went wrong under SAPs.


  • Swali la pili kwa mzee Edwin Mtei na wadau husika, je - kwanini IMF/WorldBank walitushinikiza tufute sera za Mwalimu juu ya serikali kujihusishwa na utoaji wa huduma muhimu za jamii kwa wananchi, only for IMF/WorldBank kurudia logic ya Mwalimu baadae (hadi sasa)? Moja ya tofauti yako na Mwalimu in the 1980s ilikuwa ni pamoja na Mwalimu kusisitiza juu ya umuhimu wa serikali kupewa another chance to implement sera za Ujamaa kwa msaada wa wahisani bila major disruptions, jambo ambalo ulilipinga, lakini katika miaka hii, moja ya pillars kuu za Chama chako cha Chadema ni kutoa huduma za kijamii kama zile chini ya ujamaa – BURE.


  • Swali la tatu kwa mzee Edwin mtei na wadau wengine ni je - Kwanini Liberalization, Marketization and Privatization chini ya usimamizi wa IMF na WorldBank have led to de-industrialization in Tanzania?/vimeua viwanda Tanzania?


Chini ya azimio la arusha, mass goods industries kama vile viwanda vya leather, textile, oil and other food processing industries were established with formidable success!! And strange enough, fedha zilizotumika zaidi kujenga na kuendesha viwanda hivi zilitokana na jasho la wakulima na wafanyakazi, sio waweekzaji kupitia Foreign Direct Investment i.e. utilized zaidi local capital than foreign capital. Lakini ujio wa soko huria - Liberalization, Marketization and Privatization, ukaenda kupora, tena mchana kweupe, assets zilizojengwa na watanzania walala hoi; Lakini mbaya zaidi, uporaji huu badala ya kwenda endeleza viwanda husika, badala yake led to de – industrialization. Viwanda tajwa hapo juu were the hardest hit when protectionism was lifted under the supervision of IMF and World bank.


Nitarudi kujadili hoja nyingine.

Cc Edwin mtei, cagl, jingalafalsafa, EMT, nguruvi3, highlander et al…
 
Tuko pamoja katika hilo Mkuu wangu. Ninaamini kabisa, Mbwa mwizi na mroho, aliyeiba kifaranga cha kuku mdomoni mwake, kamwe hatokiacha kwa kwa kuumkemea tu, ni hadi pale utakapompiga jiwe, hata kama hatotaka kukiachia, atapanua kinywa kulia BWEEEEEE! Na kifaranga kitaanguka! Mimi naamini AA likifanyiwa maboresho kidogo, ni jiwe tosha kwa wakoloni si hawa weusi tu bali na mabwana zao wa nje! Mkuu wangu wewe unasema tulichambue AA, na tutokee na hayo fulani fulani. Ni sawa, lakini KATIKA KULICHAMBUA HLO KAMWE MSITUMIE VIGEZO VYA KULINDA DEMOKRASIA ILIYOPO, MTAPOTEA. Kigezo ni kimoja tu, relevance yake kwa Mazingira na Nyakati zetu. Ninaamini mtapata zaidi ya 90% mazuri, mwishowe mtagundua kinachotakiwa kufanywa ni MABORESHO TU.
Turudi kwenye mada, Mkuu GAGL, ametaka kujuzwa CDM ina msimamo gani juu ya AA maana yeye ana imani nalo. Kwangu kila kitu ni HESABU tu, kama CDM watataka kuliishi AA ni lazima wajikatae leo! Waseme wao si CDM hii tena! Na waue sera zao, waunde mpya. Walizonazo leo, ni zile za AZ, ambayo wewe Mkuu Highlander na mimi, tumekubaliana kwamba AZ linanuka uozo. Mzoga, hakuna kitokacho humo kimfaacho mtu kutia kinywani mwake.
MAENDELEO NI HESABU MKUU WANGU! Ukishazitega vizuri, kila kitu kinaenda vizuri, ila ukikosea tu japo kidogo...UTATESEKA SANA. Kama ilivyo kwa maendeleo yetu, vivyo hivyo, UNYONGE(umasikini) WETU NI HESABU PIA.
Mungu wetu anaita sasa!
Mungu wetu anaita sasa.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu JingalaFalsafa, haya ya leo naona niyajibu haraka:

WEWE: unasema tulichambue AA, na tutokee na hayo fulani fulani. Ni sawa, lakini KATIKA KULICHAMBUA HLO KAMWE MSITUMIE VIGEZO VYA KULINDA DEMOKRASIA ILIYOPO, MTAPOTEA. Kigezo ni kimoja tu, relevance yake kwa Mazingira na Nyakati zetu. Ninaamini mtapata zaidi ya 90% mazuri, mwishowe mtagundua kinachotakiwa kufanywa ni MABORESHO TU.

MIMI: Unajifunga katika neno "mazingira ya nyakati zetu." Hatuwezi kukwepa kulinda Demokrasia iliyopo kwa sababu ndiyo mazingira yenyewe yaliyopo sasa ndugu yangu. Ukiacha kuzungumzia Demokrasia iliyop sasa utatoa document isiyokuwa na releveance kabisa kwa hizi nyakati tulizo nazo.

WEWE:
Turudi kwenye mada, Mkuu GAGL, ametaka kujuzwa CDM ina msimamo gani juu ya AA maana yeye ana imani nalo. Kwangu kila kitu ni HESABU tu, kama CDM watataka kuliishi AA ni lazima wajikatae leo! Waseme wao si CDM hii tena! Na waue sera zao, waunde mpya. Walizonazo leo, ni zile za AZ, ambayo wewe Mkuu Highlander na mimi, tumekubaliana kwamba AZ linanuka uozo. Mzoga, hakuna kitokacho humo kimfaacho mtu kutia kinywani mwake.

MIMI: Hapa pia umesahau kitu muhimu. CDM ni chama kilichozaliwa Tanzania, kina Watanzania ambao historia ya nchi hii ni ya kwao sawasawa kabisa na wenzao waliopo CCM na katika vyama vingine. Kile ambacho CCM inaweza kuboresha kutoka katika historia ya taifa hili ndo hicho ambacho CDM, CUF, NCCR-Mageuzi au hata Mtikila na DP yake wanaweza kufanya. Azimio la Arusha ilikuwa sera ya TANU. Tanu ilikuwa ya nani. Ya CCM? Wrong!!! TANU ilikuwa yetu wote! CDM wana sera ya Mrengo wa Kati. Hii ni sera ya Ki-Social Democrat. Sera hii inaruhusu kuibapo kidogo mambo fulanifulani ya Ujamaa. Hapo juu kwenye redi nakupinga kwa nguvu zangu zote. Na kwa taarifa yako sasa, naamini asilimia 90 au zaidi ya waanzilishi wa CDM ni X-members wa TANU. Hiki chama ni mtoto wa TANU. Ulizia kama Brown Ngwilulupi alikuwa mwanachama wa TANU au la. Ulizia kama akina mzee Shang'o kutoka Singida, na akina Shanga wa Kilimanjaro walikuwa Wanachana wa TANU au la. Ulizia uanachama wa Bob Makani katika TANU, na Mtei, na habari za yule Mama wa Kinyakyusa alikuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake CCM (jina limenitoka) aliyetoka CCM akawapo katika kamati anzilishi ya CDM; huyu aliwahi kuwa mwana TANU? Alikuwapo na Col. Marealle nadhani, kama sijasahau. Wote wana TANU kwa asili yao. Hiki chama hakiwezi kukwepa damu ya TANU aslani. Walid Aman Kabourou tu ndo sina hakika na link yake na TANU. Ujue mitizamo ya mtoto inakuwa molded wakati wa formative stage miaka ya Mwanzo. Hawa watu formative stage zao kisiasa zilikuwa TANU tupu. Sidhani kama watakosa harufu hiyo.

Mkuu, Azimio la Arusha malengo yake makuu yalikuwa Uadilifu, Haki na Usawa. Hakuna Uadilifu, Haki na Usawa katika uharo unaitwa Azimio la Zanzibar. Ni kukichafua CDM kukihusisha na ile HILA kubwa ya ufisadi inaitwa AZ. Uadilifu, Haki na Usawa vinatekelezeka katika sera za Social Democratic principle. Yanafanyika Ujerumani, yanafanyika Uingereza, Obama anayafanya kule Marekani sasa.

 
Nimesoma bandiko lako refu la mwisho Mchambuzi. Katika maelezo yako ya page sita unakwepa masuala yote ya msingi kuhusu Uchumi wetu.

1. Umeshindwa kabisa kujadili nafasi ya Rushwa katika kutibua uchumi
2. Umeshindwa kabisa kujadili nafasi ya udhaifu wa uongozi (management incompetence) katika kuharibu uchumi
3. Unasema IMF na World Bank wameua viwanda vyetu kwa kulazimisha Privatization: Kumbe kauli hii imekosa kabisa
upana wa tafakuri. Kilichoua viwanda vyetu ni PSRC. PSRC walipewa hadidu za rejea kubinafsisha viwanda vyetu
viendelee kuzalisha bidhaa za awali. Hawakufanya due diligence ya kutosha wakawapa matapeli viwanda vyetu
na matapeli hawa wakavigeuza kuwa magodown. Ujue ukosefu wa due dligence haukuwa bahati mbaya lakini.
PSRC walikuwa wanakatiwa pochi wanyamaze.

Kingine ni kwamba viwanda vyetu vingi vilijengwa kwa whims. Havikujengwa "demand-driven." Katika mfumo tulio nao
sasa, mtu hajengi kiwanda pasipokuwa na demand ya uhakika ya produce inayotoka pale kiwandani. Mtu atafanya
ujenzi wa kiwanda akimaliza kufanya utafiti wa soko lilivyokaa kwanza, nani mshindani wake, je biashara yake itakuwa
sustainable, anajenga. Kuna viwanda vimekufa kwa sababu vilijengwa pasipo market analysis sahihi au ya kutosha.
Kuna bidhaa local haziwezi kushindana na cheap imports. Atayejenga kiwanda sasa atajiuliza kama anaweza
kushindana na cheap imports na kwa ujanja upi. Vya sasa vikijengwa vitadumu. IMF na World Bank wanaingiaje
kwenye Management incompetence ya wale wanaopewa kazi na CCM kusimamia uchumi? You are not serious.

Kun amahali unasema mijadala yetu inayohusiana na Azimio la Arusha imekuwa inatawaliwa na chuki (kidini, kikanda, kikabila) na pia kusukumwa zaidi na ushabiki wa kisiasa, hasa dhidi ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kuliko objectivity. Mimi sijaona haya kwenye uzi huu. Tumekuwa very sobber nadhani. Ni kweli kwamba baadhi ya characteristics za Azimio la Arusha zilikuwa ni

  1. Massive nationalizations
  2. Kufungia kufuli exploitation ya natural resources zetu mpaka pale tutakapokuwa tayari;
  3. Provision of social services kwa wananchi hasa elimu, afya n.k;
  4. Leadership code iliyolenga taifa kupata viongozi wenye uadilifu, uzalendo na wawajibikaji…

Sababu kubwa ya haya ilikuwa kujenga jamii yenye haki na usawa, na kuziba gap kubwa lilikokuwapo kati ya wenye nacho na wale wasokuwa nacho. Hii ilikuwa nia njema ninavyoona mimi. Rushwa na management incompetence katika utawala wa CCM vimerudisha hali iliyokuwapo wakati tunapata Uhuru. Gap kati ya wenye nacho na wasio nacho imepanuka sana tena. Hii inalazimisha Azimio la Arusha kurudi kwa mtindo fulani. I don't care nani anatekeleza hili, lakini hili gap ni lazima kulipunguza kama tunataka kudumisha amani hapa. Unataka kujua what went right with Azimio la Arusha? Fikra za kuwanyanyua wanyonge kilikuwa kitu "right." Kufanya hiki ni sahihi no matter unakipatia jina gani, au nani anakifanya.

Umeongelea Kilimo. hapa pia CCM meanza kuonesha management incompetence yake ya kila siku. Protectionism haina tatizo kwa lengo la kulinda maslahi ya wenye nchi. Leo tupo Milioni 45 unagawia mabepari ekari 400 kila mmoja walime maua na mchele kupeleka kwao. Mwaka 3000 tukiwa milini 90 ardhi itatoka wapi? Nyinyi watu mnaumwa ujue. Kazi kutafuta visingizio tu; oo, IMF wameua viwanda, oo, hatuna fedha za kufanya kilimo cha kisasa, kwa hiyo turuhusu Iran na Saudia na Kuwait, na Holland, na Afrika ya Kusini, na Australia waje wapewe nusu ya ardhi yetu walime kilimo cha kisasa. Huu ni ujinga! Huko mbele tutaanza kuomba kibali tupewe viplot kwa kukodi katika haya maeneo ya wageni ndani ya nchi yetu wenyewe. Nyinyi watu mnaumwa. Fanya Google, tafuta madhara ya Minifundios katika Lotifundios kule South America na India ndo utajua mnakotupeleka na hii mis-interpretation ya soko huria.

CC: JingalaFalsafa, Mchambuzi, Wayne, Melky Msechu, Tango73, nderingosha, Edwin Mtei, habibu bakili, GAGL




Swali zuri lakini nadhani halitajibiwa kwa sababu za kisiasa au litajibiwa kisiasa;tangia kifo cha azimio la arusha,nchi imekosa dira na tumepoteza uhuru wetu wa kujiamulia jinsi gani ya kuendesha nchi kwani madereva ni IMF na Worlbank;Kama alivyofanya Mwalimu kuomba radhi watanzania juu ya mapungufu ya azimio la arusha, Mzee Mtei nae anatakiwa azungumzie hili na pengine kuomba msamaha juu ya mapungufu ya sera za IFIs ambazo yeye alikuwa mmoja wa waasisi miaka ya mwanzo ya themanini;huo ndio ustaarabu; ni ajabu Mzee Mtei anaendelea kukaa kimya wakati ni dhahiri sasa kwamba kwa mtanzania wa kawaida,pamoja na mapungufu mengi ya ujuamaa,miaka 18 ya azimio la arusha ilikuwa bora na ya matumaini kuliko miaka 28 ya ubepari na soko huria tunayoendelea nayo leo hii; let's be objective and rational on this subject,tusiweke ushabiki wa kisiasa and display our ignorance and arrogance;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Highlander,

Are you an economist by any chance? Hivi kweli kiini cha tatizo letu la umaskini ni sababu ya ccm na rushwa? Is that how you want to debate about hali yetu ya mbaya ya uchumi and expect to come up with a meaningful solution? Kweli bandiko langu ni refu na inaonyesha limekukera kwani umerudia kusema hivyo zaidi ya mara moja,niwie radhi kwa hilo lakini mjadala wako katika majibu yako did not address key issues that I raised:

Kwanza nilijadili kwamba wengi tuna tabia ya kuwa subjective na mijadala ya azimio la arusha kwa kumshambulia mwalimu, na sikusema hayo yamejotokeza humu, lakini kwa vile wewe bado mgeni, umekosa mijadala yetu mingi humu for the past six years;

Pili,nikaja na ushauri kwamba ili tuweze elewa uzuri na mapungufu ya azimio la arusha, ni vyema tuligawanye katika sehemu kuu tatu-Malengo,Mchakato wa utekelezaji na Matokeo;

Tatu, nikajadili kwamba tumekuwa na tabia ya kujadili what went wrong with AR,tutumie muda mwingi pia kuanhgalia what went right;

Nne, nikajadili juu ya umuhimu wetu kujadili pia what went wrong with SAPs under the auspices of the IFIs huku nikielekeza maswali kadhaa kwa mzee edwin mtei na wadau wengine;

Tano,nikatumia muda mrefu kujadili kwamba mgogoro wa kiuchumi uliopelekea ujio wa SAPs haukutokana na ujamaa kimsingi bali a variety of external and internal factors, 1973-4 na 1978-9;

Sita nikajadili juu ya umuhimu wa kutambua kwamba azimio la arusha was almost inevitable by giving an historic account ya uchumi wetu kabla ya uhuru; pia nikaelezea kwanini leo hii sisi na kenya,nigeria etc tupo kundi moja as low income countries licha ya sisi kupitia ujamaa tofauti na wenzetu,thus strengthening my argument kwamba root cause ya umaskini Tanzania na afrika kwa ujumla is beyond ujamaa in tanzania;

Saba nikajadili role ya worldbank na imf katika kuzorotesha uchumi wetu na wa Nchi maskini kwa ujumla; inaonekana hauna uelewa wa kutosha to look beyond rushwa na ufisadi,haya just compliment a much bigger problem that sucks us to the bone; ukipata muda soma nobel laurettes kama prof stiglitz,prof amartya sen etc ambao ni well reputable na walikuwa very senior worldbank na wanaelezea jinsi gani globalization has so many discontents that frustrates economies in poor countries;

Nane na msisitizo kwako - jitahidi kuangalia matatizo yetu kiuchumi beyond CCM kwani hata chadema wakienda ikulu 2015 watatekeleza yale yale ya Ccm, tofauti itakuwa tu ufanisi na uwajibikaji but it won't solve the inherent structural weaknesses facing our economies, ndio maana to IFIs, they care less nani anaenda ikulu 2015; nimejadili sana hili,ukipata muda tembelea my homepage humu JF;

Mwisho niseme mawili - kwanza, you are taking the debate of industrilization out of context na pia unajichanganya unapojadili kwamba IFIs have no role played kutuangusha; kwako tatizo ni ccm, psrc na pia mambo mengine ambayo ukiyasoma btn the line, tunarudia pale pale - the unfair global capitalist system ambapo sisi ni kama we are made to play on the periphery for ever huku a few wakicheza in the centre;do you know how psrc came about? It was part of the reforms package iliyolazimishwa kwetu, soma zaidi juu ya Aid conditionality;Pia hapa nia swali: hivi do you know kwamba nje ya south africa and mauritious, no other country in Sub saharan africa imefanikiwa na mapinduzi ya viwanda? Do you know why?

Pili na mwisho, kuna sehemu umetupotosha kuhusiana na itikadi ya chadema kwamba ni mrengo wa kati na kwamba eti ni social democrats; you are very wrong,ukipata muda tembelea uzi wangu titled:nape,mnyika na itatiro,itikadi zenu wapi?

Vinginevyo if you want to discuss economics, I am an economist but also have a background in economic development,nasema haya kwa vile umetamka kwamba sijajadili mambo ya msingi ya uchumi; nilikuwa na sababu za msingi kama nilivyojadili lakini sio kwamna sina uelewa wa uchumi, hasa kuhusiana na mazingira ya Tanzania; Till then, bado nasubiri mawazo yako kama yapo juu ya maswali na hoja za msingi nilizojadili katika bandiko langu lililo kuchosha kwa urefu; again apologies for that;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Umefanya vema kujitambulisha kuwa ni Economist. Nafurahi kujua najadili suala hili muhimu na economist. Well, mimi siyo economist, ila nimefanya kazi ya Ualimu on and off katika maisha yangu--darasani na kwenye makaratasi sometime.

Hoja unazozileta hapa ni hoja za Maeconomist walioharibu uchumi wa Taifa letu kwa kutafuta matatizo ya uchumi wa Taifa hili outside the country, badala ya kufanya introspection. Hawana (au niseme hamna) hata chembe ya aibu kuendelea kulaumu external factors, na kung'ang'ania kutafuta hata hizo solution za hayo matatizo yetu outside the country! Hizi ni economics mfu. Mkuu Mchambuzi, sijaona hata sehemu moja katika hoja zako tangu tumeanza ulipofanya introspection kukiri internal weaknesses zetu.

Our problems have always been caused by External forces. Nikupe Footnote hapa: Tafuta kitabu hiki, "Management of Public Enterprises in Developing Countries: The Tanzania Experience", By Juma Volter Mwapachu, Oxford & IBH Publishing Company, @ 1983. Hakuna hata haja ya kutaja Ukurasa kwa sabu kitabu chote kinashuhudia Economics mfu za hapa nchini. Ni kweli umetumia muda mrefu kujadili kwamba mgogoro wa kiuchumi uliopelekea ujio wa SAPs haukutokana na ujamaa kimsingi bali a variety of external and internal factors, 1973-4 na 1978-9.

Mwenzetu unasema 1973 -74 palikuwa na external factors? Mbona unaruka effect ya kulazimisha watu kulima pamoja katika vijiji vya ujamaa badala ya kuwapelekea mbolea wakuze mashamba yao binafsi waongeze output kulekule walikokuwa. Una-blame external factors wakati distabilzation ya agriculture ilifanywa na Ma economist wa aina yako kwa kuforce watu ku-abandon kilimo kwa mtindo waliouzowea. Mimi naona absence ya fikra sahihi za Economics kuwa chanzo cha matatizo kuanzia 1967 hadi 1977; decade hiyo.

This mis-manager of the economy, au nimwite Mchawi, hakuwa nje ya nchi. Mchawi tulikuwa naye hapahapa nchini, na bado yupo! Naweza kusamehe depression iliyoanzia 1978-79. Vita ilikuwa force majeure. This external factor naikubali! Na kama nilivyosema awali, effect za vita ndiyo kiini hasa cha depression iliyotulazimisha kuanza dozi ya IMF na World Bank, dozi ambaye imeleta faida kubwa sana kwa taifa--kama isingekuwa uwepo wa tatizo la Rushwa na hawa Maeconomist wanatafuta external factors kwa kila tatizo internal.
 
Mjadala mzuri highlander,nitarudi punde kujadii hoja zako muhimu na za msingi;l

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Very Interesting Topic...Nimefarijika na michango ya watu tofauti humu jamvini. Generally speaking Azimio la Arusha was too ideological despite ya baadhi ya maazui ambayo yamejikita katika kujenga uzalendo na umoja wa Taifa letu.

Fikra kama vile chama kushika hatamu (party supremacy) zimekiuka kanuni hizo. Mipango inayowapa binadamu au kikundi cha binadamu mamlaka makuu-enzi-kuu-(supremecy) ni mpango usiolingana na kanuni za usawa, demokrasia na Maendeleo.

Ujamaa na kujitegemea ni maneno mawili yasiyo na uhusiano ni sawa na kuchanganya maji na mafuta (completely immiscible). Katika hali ya kawaida katika kipindi cha miaka mitano toka kupata uhuru kuanza kuhubiri siasa ya kujitegemea bila kujenga misingi imara ya uchumi ni maneno matamu yasiyo na kanuni imara za kiutendaji.

Shabaha kuu za azimio la Arusha chini ya siasa ya Ujamaa na Kujitegemea inahitaji nguvu, amri kali na utawala wa aina ya kijeshi. Siasa hizi hazijazingatia ule ukweli wa binadamu na hisia za ndania za asili ya watu. Ni siasa za kufikirika zaidi.

Mashamba ya jumla (collective or communal farms) kuanzia vijiji vya ushirika mpaka kufikia kijiji cha ujamaa ni zao la misingi dhaifu ya kukua kwa uchumi na hatimaye maendeleo nadi ya Taifa letu.

Utaifishaji na umilikaji wa shughuli tofauti za umma nje ya NJIA KUU ZA UCHUMI umechelewesha na kudhoofisha maendeleo ndani ya taifa letu.
 
Highlander,

Kwanza niwie radhi iwapo baadhi ya matamshi yangu yanakuletea kero za hapa na pale, sikusidii hilo, bali ni sehemu ya mapungufu yangu kama Binadamu; Pili, nina amini kwa dhati kabisa kwamba sote tuna uchungu mkubwa na nchi yetu, ila tofauti kubwa baina yangu na wewe ni juu ya root-cause ya tatizo letu la umaskini lakini vile vile kuhusu the way forward; Huu ndio upinzani tunaotakiwa kuwa nao ambao ni ushindani wa hoja, sio wa viroja kama wana CCM wengi wanavyoendesha mijadala yao kutetea mafanikio ya CCM; Ni dhahiri mafanikio yapo lakini yanafunikwa na mapungufu, lakini mbaya zaidi kiburi cha viongozi na hulka ya ufisadi; Na hii inanipeleka kwenye hoja yangu nyingine kwamba:

Mimi sio kwamba napingana na wewe kuhusiana na role of ufisadi katika kuangamiza uchumi wetu; Nachofanya ni kujaribu to paint a picture beyond ufisadi ili watanzania baadae waje kuelewa je ni kwanini imechukua muda mrefu kwa Chadema kuikomboa nchi assuming Chadema inafanikiwa kuchukuwa nchi 2015, 2020 au 2025; Nadhani utakubaliana na mimi kwamba support kubwa ya umma kwa chadema has more to do na imani kwamba nchi haijaendelea kutokana na ufisadi, na kwamba CCM ikitoka tu, na ufisadi kushughulikiwa, basi umaskini utapungua kwa kasi; Nasema haya from experience yangu na wananchi huku vijiweni, na hili ni timing bomb kwa Chadema na nilishajadili sana juu ya changamoto hii kwa chadema na kutoa maoni jinsi gani Chadema inaweza kujiepusha na bomu hili mapema; Kwahiyo naomba uelewe kwamba hoja yangu kuangalia beyond ufisadi is against this background, na sio vinginevyo.

Nikiendelea na hoja ya ufisadi japo kidogo, ni muhimu niseme kwamba, hoja kwamba "Rais anaangushwa na wasaidizi wenzake" ilikuwa more relevant chini ya utawala wa Nyerere kuliko awamu zilizomfuatia baadae! Tofauti na wengi wanavyopenda kuamini kwamba Nyerere alikuwa haambiliki, ukweli ni kwamba miongoni mwa marais wote wa nchi, hakuna Rais aliyekuwa msikivu kwa wasaidizi na washauri wake kama Mwalimu. Mifan katika hili ni mingi, kuanzia jinsi gani alikuwa na utamaduni wa kupeleka hoja zake Mlimani (UDSM) ili kupata challenges na more inputs, na instances nyingine nyingi. Vile vile katika suala zima la Vijiji vya ujamaa, idea kwa kweli haikuwa mbaya, ubovu ulikuja katika utekelezaji ambapo Mwalimu alitegemea sana wasaidizi na viongozi wa ngazi za chini kutekeleza malengo husika, na wengi ya hawa walikuwa hawana elimu, utaalamu na uzalendo kwa Tanzania.

Kuna mifano mingi sana jinsi gani watendaji wengi walikuwa wanafukuzwa kazi baada ya Mwalimu kupewa ripoti juu ya utendaji wao waovyo; Kwa mfano wapo watendaji ambao walikuwa wanaendesha operesheni vijiji vya ujamaa kwa mabavu, kiburi na ubinafsi, kwa kulazimisha wanavijiji kuhama kwa nguvu, kuchoma nyumba zao n.k. Mwalimu never ordered watu kuchomewa nyumba zao moto hata siku moja na hali ilipozidi kuwa mbaya, ni Mwalimu ndiye aliyeingilia kati na kusimamisha operesheni ya vijiji vya ujamaa kwa kukiri kwamba imeshindwa;

Nikiwa bado katika hoja hii ya wasaidizi wa Mwalimu, ufisadi na rushwa chini ya Mwalimu sio kwamba haukuwepo, bali tofauti kati ya sasa na wakati wa Mwalimu ni kwamba ufisadi chini ya Mwalimu ulikemewa na kulikuwa na vyombo vyenye meno kudhibiti. Kwa maana nyingine, hata hao mafisadi walijua wazi kabisa Mwalimu alikuwa anachukia rushwa kwa dhati na alikuwa tayari kuchukulia hatua kiongozi yeyoye Yule ambae alionekana kuwa na mienendo ya kifisadi; Wewe na wengine humu tayari mmelijadili hili kwa kina kwa sura mbalimbali; lakini pamoja na yote haya, bado mafisadi walifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuhujumu mashirika yetu ya umma, miradi ya maendeleo n.k ambayo walipewa kuiongoza na kusimamia; Tukumbuke kwamba Ujio wa Ujamaa haina maana kwamba mabepari wa ndani na nje walitoweka kwani waliendelea kuwepo on the periphery to challenge ujamaa kwa kutumia watu wengi ambao walikuwa wanaaminika na utawala wa Mwalimu. Nia ilikuwa ni kuhakikisha kwamba kunajengwa mazingira kuonyesha kwamba Ujamaa umeshindwa; All in all, Mwalimu alifanya makosa mengi na alikiri kukosea kwa mfano, aliwahi kusema kwamba yapo mengi ya kijinga aliyafanya lakini pia yapo ya maana aliyafanya chini ya Ujamaa, na akashangaa kwanini waliompokea nchi wanaacha ya maana na kufanya ya kijinga. All in all, Mwalimu didn't profit from politics, and that's this should have so much weight in debates kuhusiana na mafanikio na mapungufu ya Ujamaa.

Mkuu highlander, kwa vile haupendi posts ndefu, naomba kwa sasa nigotee hapa lakini muda sio mrefu narudi na bandiko linguine kujadili hoja yako muhimu juu ya jinsi gani tuna kila sababu ya kujilaumu kuhusiana na kuanguka kwa ujamaa, hasa from an economic point of view. Kwa sasa naomba nisisitize tena kwamba sio kwamba mimi napingana na hilo, kwani ni dhahiri tatizo la ujamaa lilikuwa katika utekelezaji, sio katika malengo. Na ndio maana nikashauri tuvunje vunje azimio la arusha katika vipengele vitatu – (1) Malengo (2) Mchakato na (3) Matokeo, ili tuweze kuja na mjadala wenye tija, na nikauliza maswali kadhaa ambayo bado sijapata majibu au maoni kutoka kwenu. Nisisitize tena kwamba Ujamaa ulifeli kutokana na factors nyingi ambazo zilikuwa cross cutting between nje na ndani, na inawezekana kabisa kwamba the overriding factors zilikuwa za nje au za ndani depending on how mtu anajenga hoja.

Mwisho, pamoja na background yangu katika masuala ya uchumi na maendeleo, naomba nikueleze tu kwamba wewe kusema kwamba ni wachumi wa aina yangu ndio wameiangusha nchi yetu sio sahihi sana kwani Azimio la Arusha lilifikia peak yake sijafikisha hata miaka mitano ya kuzaliwa. Kwahiyo naujadili ujamaa kutokana na elimu yangu kuanzia msingi sekondani n.k, lakini pia uzoefu wangu katika mazingira mbalimbali, bila ya kusahau tabia ya kupenda kujisomea, ambayo nimegundua hata wewe unayo. Ndio maana mjadala huu umekuwa na tija sana.

Nitarudi in a few minutes kutoa maoni yangu specifically kuhusiana na jinsi gani we poorly managed uchumi wakati wa ujamaa kwani nikiendelea kwenye bandiko hili sidhani kama utapenda kutokana na urefu wa bandiko;
 
Kwanza nianze kwa kumshukuru Mkuu wangu Mchambuzi kwa bandiko lake zuri. Liko more detailed nakiri binafsi siwezi kufikia kupata data/takwimu hizo, ila nashukuru kuziona hapa, hongera kwa kazi nzuri. Hakika ni kazi nzuri Mkuu wangu na ni darasa tosha kwangu. NINASHUKURU!
Kwako Mkuu wangu Highlander. Utakuwa hujanielewa,unaposema kwamba mimi nimezunguka katika hoja yangu ya biashara, na mwishowe nimetokea sehemu ile ile kuwa ninakubaliana na kila mwenye kuchambua faida. SI KWELI. Hoja yako ilidai kuwa, kanuni ya biashara ya USA na ile ya Afrika au Asia, ni sawa! Kwani wote ni kupata FAIDA. Nikakutalia kwa kukuambia, FAIDA si kanuni ya biashara tu, bali ni kanuni ya maisha kwa ujumla. Nikakuambia tena kuwa, kanuni za biashara hutegemeana na Mazingira na Nyakati za eneo husika, mazingira na nyakati hizo kamwe haziwezi kufanana dunia yote, hivyo haiwezekani kuzaa kitu kimoja kote! NEVER! Hivyo Mkuu wangu kamwe usidhani katika mazingira na nyakati sawa kutakuwa na tafsiri tofautitofauti za faida na zote zikawa sahihi, big NO! Pia Mkuu hapa ndio unapopotea kabisa kwa kudanganyika na kitabu cha watu wezi, kamwe FAIDA si MRIDHIKO! KATUKATU NINAKATAA. Hao ni waongozwao na ID/HULKA ndio wanaodai hivyo, WABINAFSI. Kamwe hakuna Faida kama haitomfikiria jirani yako! Hivi hujui kama kuna machifu waliridhika kupewa shanga na wakoloni ili wauze aridhi yao? Je hiyo ni faida? Hujui kuwa athari yake ni jirani yake kukosa kipande cha kulima mwanae akafa njaa, mwishowe akaona hasira akanoa mkuki wake kumuua yeye chifu na mzungu wake! Je ni faida au hasara kwa chifu? Ndio maana nimesema katika misingi ya UTU wa mtu mweusi FAIDA lazima iwe shared, kwani Faida ni UENDELEVU. Unapokiuka hapa, ni mawili aidha umuue jirani yako ama jirani yako akuue wewe! Very simple logic! Wewe na mimi tunalalamika sana leo, ni kwa imani hii batili kuwa Faida ni SURPLUS kwa muuzaji na MRIDHIKO kwa mnunuzi.
Mkuu wangu naona unahamaki sana inapotajwa CDM, niliposema CDM ijikatae si kwao pekee yao tu, ni hata CCM hii ya leo! Ndio maana wapo wanaohoji kwanini CCM isirudie misingi yake ya zamani, au kwanini CDM isirudie misingi ya AA? Sawa na Cuf, NCCR na wengineo! Naogopa Mkuu wangu Highlander, kama vile hauko huru katika mjadala huu, kama vile unafungwa sana na imani yako kwa CDM na kukerwa kwako na CCM.
Mkuu wangu Highlander, unadai kuwa viwanda vyetu vilikufa kutokana na kukosekana kwa upembuzi yakinifu wa soko. SAWA. Ni moja ya sababu. Lakini umeongeza pia kuwa tumejenga viwanda wakati hatuwezi kushindana na Cheap Imports sokoni, na umeohoji kuwa hapo IMF inahusikaje? Umesahau kuwa hizo cheap imports zisingekuwepo kama kusingekuwa na sera zilizoruhusu hayo! Sera hizo hazikuwepo kipindi cha AA, bali fikra za AZ ndizo zilizoleta hayo. Who initiated them to AZ kama si IMF, walikuwa na lengo gani kama si kuua viwanda vyetu na kutengeneza soko la viwanda vyao? Walijua kabisa kuwa hatuna teknolojia wala mtaji wa kutosha, wakata tushindane nao sokoni! Na kwa mashinikizo kuwa tusipofanya hivi basi nao hawatatufanyia vile. Unadhani walifanya hayo kwa bahati mbaya tu? Unathubutuje kusema IMF haikuwa na HILA nasi? Hivi Mkuu wangu, unajua chochote kuhusu Ukoloni Mamboleo?
IMF haiwezi kwepa lawama kwa incompetence ya viongozi wetu. Simple logic..."AA created competent leaders ndani ya CCM kwa miiko thabiti, AZ being initiated by IMF killed AA na miiko yake, kisha ikaibuka Incompetent leaders ndani ya CCM ya leo" Pia ukumbuke kuwa AZ si watu ingekuwa watu tungesubiri wafe tu, lakini AZ ni SERA ni FIKRA KAMILI. Je, hujui kama zilitoka IMF? Sera hizo zinabebwa na propaganda kuu "Demokrarisia" ambayo ni mama wa Privatization, multpartism aliyemzaa CDM na CCM wa leo, marketization n.k Mkuu wangu, unadhani hao Iran, Kuwait na Saudia wamejijia tu? Ukweli ni wezi tena maharamia wakubwa, sasa ukitaka kuthibitisha hawakuja tu kiholela, nenda kawapige mawe au na mbwa wako uwakamate, uone IMF na agents nyingine za UN watatufanya nini? Kama hawana hila nasi, kwanini wasituunge mkono kuwatimua! Zipo sera zilizowaruhusu kuja, zimeletwa na IMF kupitia AZ mama wa CCM ya leo na CDM yako. Nilishakuambia kuwa, hakuna kitokacho katika mzoga kimfaacho mtu kula. Kama unaamini AZ ni uharo, nikuambie tu CDM nayo kama ilivyo CCM hii imetoka humo!
Mungu wetu anaita sasa!
 
Last edited by a moderator:
Naomba mtafute kamanda yeyote aliye karibu nawe Mkuu GAGL kachukue kadi yako ya CHADEMA.

Kitu ambacho wengi wanakitamani katika Azimio na Arusha si jina la azimio lile, bali wanatamani maudhui yake fulani-fulani mazuri kwa taifa hili. Si kila kitu katika Azimio la Arusha kilikuwa sawa. Azimio la Arusha lilikuwa na Utopia nyingi sana mule, nikianzia na dhana kwamba mtu anaweza kuacha profit motive kabisa, kitu ambacho hakiwezekani. Kumbe kilichotakiwa kuonekana katika Azimio la Arusha ilikuwa dhamira ya ku-moderate profit motive. Mataifa yaliyoendelea yanafanya hivyo. Unaruhusu profit motive kushamiri, ila unai-moderate. Sera za CHADEMA zinatafuta kutumia profit motive kujenga uchumi wa taifa, lakini profit motive moderated.

Spirit ya kujikana reasonably, (narudhia: kujikana reasonably), ilikuwapo katika Azimio la Arusha. Kutaka wengine nao wapate faida katika yanayofanyika ndani ya taifa, hili lilikuwapo. Uadilifu katika utendaji ndani ya chama na serikali, hili pia lilikuwapo katika Azimio la Arusha. Na haya yanahubiriwa na wataalam wa mahubiri ya siasa katika CHADEMA.

Mi nionavyo, kikubwa katika Azimio la Arusha kinachostahili kukienzi ni Maudhui ya uadilifu katika kulinda maslahi ya kwako--wewe mtu binafsi--lakini kwa mtizamo kwamba wewe ni sehemu ya walio wengi, hivyo kwamba unafanya kazi unayoifanya kwa niaba ya wengi; yaani kwamba umepewa jukumu la kulinda maslahi makuu ya Taifa kwa ujumla wake, badala ya kulinda maslahi binafsi kwanza mtu anapokuwa katika nafasi yoyote ile ya uongozi. Chadema wanahubiri haya. Linda maslahi ya taifa kwanza. Mengine yafuate. Kwa hiyo hata kama hawatafufua Azimio la Arusha neno kwa neno kwa sababu lilikuwa na kasoro zake pia, maudhui katika Azimio la Arusha yenye nia njema kwa taifa tayari wanayahubiri.

Kwa maana hiyo, kama wewe ni mpenzi wa Azimio la Arusha, nina hakika utakuwa unalipenda Azimio lile kwa sababu ya maudhui yake mema. Maudhui ya uadilifu, maudhui ya kulinda masalahi makuu ya taifa kwa ujumla wake; kulinda maslahi ya Taifa kwanza kabla ya kulinda maslahi binafsi mtu anapokuwa katika nafasi yoyote ile ya uongozi. Haya Chadema inahubiri tayari na kwa kiasi kikubwa wanajitahidi kutekeleza mahubiri yao wao binafsi. Nilisikia John Mnyika anatembelea 'Vitz kobe' ndogo badala ya Prado. Niliipenda sana hii!

Wale unaosikia wamekiacha CHADEMA na kurudi CCM ni wale ambao walienda CHADEMA kutafuta ajira; wale ambao walienda kule kutafuta mianya ya utajirisho, wakidhani CHADEMA ni kama CCM. Walipokuta pale kuna kujitolea kwingi sana wakaona hapafai na kurudi kule ambako siasa malengo yake ni ajira ya utajirisho kwa hela halali na haramu. CHADEMA inatekeleza maudhui mema ya Azimio la Arusha nionavyo mimi. Hawawezi kutekeleza kila kilichokuwapo katika Azimio la Arusha kwa sababu si kila kitu kilikuwa sawa mule. Mengine hayakuwa sawa wakati ule, hayawezi kuwa sawa leo. Lakini pia Azimio la Arusha ilikuwa sera ya TANU. Chadema si TANU, japo inaweza ikawa KAMA TANU katika mambo fulanifulani. Huwezi kuzaa mtoto akafanana na wewe kwa kiiiiila kitu. Yapo mengine yatakuwa ya kwake yeye kama yeye.

Kachukue kadi mkuu. Ingia kwenye vita ya kurudisha heshima ya nchi yetu na utajiri wake mikononi mwetu. Go!
Wako wana CCM wengi hawakubaliani na chama chao kukiuka misingi mikuu ya Azimio la Arusha. Je huoni kuna haja ya cdm kutoa rasmi msimamo wake kuhusu Azimio la Arusha ili wanachama hao waweze kufana uamuzi mgumu?
 
Swali zuri lakini nadhani halitajibiwa kwa sababu za kisiasa au litajibiwa kisiasa;tangia kifo cha azimio la arusha,nchi imekosa dira na tumepoteza uhuru wetu wa kujiamulia jinsi gani ya kuendesha nchi kwani madereva ni IMF na Worlbank;Kama alivyofanya Mwalimu kuomba radhi watanzania juu ya mapungufu ya azimio la arusha, Mzee Mtei nae anatakiwa azungumzie hili na pengine kuomba msamaha juu ya mapungufu ya sera za IFIs ambazo yeye alikuwa mmoja wa waasisi miaka ya mwanzo ya themanini;huo ndio ustaarabu; ni ajabu Mzee Mtei anaendelea kukaa kimya wakati ni dhahiri sasa kwamba kwa mtanzania wa kawaida,pamoja na mapungufu mengi ya ujuamaa,miaka 18 ya azimio la arusha ilikuwa bora na ya matumaini kuliko miaka 28 ya ubepari na soko huria tunayoendelea nayo leo hii; let's be objective and rational on this subject,tusiweke ushabiki wa kisiasa and display our ignorance and arrogance;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Mchabuzi uko sawa, ubepari uchwara haujaleta matumaini mema kwa watanzania kama ujamaa. Bado hatujapata formula au itikadi mbadala na ujamaa.
 
Sehemu ya Kwanza: Tathmini Yangu ya Azimio La Arusha

Nianze kwa kusisitiza tena na tena na tena kwamba mjadala wowote juu ya Azimio la Arusha hautakuwa na maana bila ya juhudi zetu za makusudi to unpack it na kuligawanya katika maeneo matatu kama ifuatavyo:


  1. Malengo ya Azimio La Arusha
  2. Utekelezaji wa Azimio La Arusha
  3. Matokeo Ya Utekelezaji wa Sera Za Azimio La Arusha

Hii ndio framework ambayo nilishauri tuifuate katika mjadala lakini kwa sababu zisizojulikana, wengi wetu tunaikwepa, na ni katika hali hii (sio tu katika mjadala huu), wengi wetu tunaishia kulijadili AR objectively, hasa kwa kumshambulia Mwalimu binafsi lakini pia kwa kujikita zaidi katika mjadala wa "What Went Wrong Under Ujamaa" huku tukipuuzia mjadala on "What Went Right Under Ujamaa." Ningependa kuingia moja kwa moja katika hoja:

What Went Right Under Ujamaa?

Yapo mengi na nitajitahidi kujadili yale muhimu.


  • We had a very favorable rate of economic growth miaka ya 1960s – 1970s, kwa mfano, Between uhuru (1961) na 1978 our annual per capita growth rate ilikuwa around 3% na GDP growth rate (annual) during the same period i.e. 1961 – 1978, ilikuwa ni around 6%; Hii ni kwa mujibu wa takwimu za BOT (1983) wakati mzee Edwin mtei akiwa bado ni waziri wetu wa fedha.


  • Pia katika kipindi hiki cha 1961 – 1978, taifa lili maintain stable price levels (inflation rate) in single digits.


  • Thamani ya shillingi yetu kwa dola ilikuwa juu sana – kuanzia 1961 hadi 1974, dollar moja ilibakia katika kiwango cha T.sh 7.142 (shilingi saba!!!); Mwaka 1975 ikaanza kupanda kidogo (Tsh. 7.413), mwaka 1976 ( Tsh. 8.379) mwaka 1977 (T.sh 8.274);


  • Sekta ya Kilimo ilikuwa kwa kasi nzuri sana kati ya 1965 na 1979 i.e. 4% between 1965 and 1969, 2% kati ya 1970-74 and 8% kati ya 1975-79; In fact, kwa karibia miaka kumi na moja, kwa wastani, sekta ya kilimo ilikuwa kwa kasi kuliko ongezeko la watu (around 3% per annum!!), hivyo food security was not a problem kwa zaidi ya miaka kumi;


  • Vilevile, average growth rate ya production ya mazao kwa ajili ya soko ilikuwa very impressive hasa kwa mazao kama mahindi, chai, tumbaku, it only began to decline 1978/9 kutokana na UKAME!!;


  • Producer prices for majority of crops – yani bei kwa wakulima wa mazao yote ya chakula na ya biashara, was constantly raising hadi kufikia peak 1977/78 baada ya tatizo la ukame kuanza kujitokeza!


  • Sekta ya Viwanda ilionyesha positive growth kwa ujumla kuanzia 1961 hadi 1978 ilipoanza kuporomoka; Mchango wa sekta ya viwanda kwa pato la taifa (GDP) iliongezeka from around 4% in 1961 to around 9.8% in 1971 na kufikia over 10% 1972 – 74, kabla ya kuanza kuporomoka kuanzia 1978; sababu za kuporomoka tutajadili baadae;


  • Vinginevyo mafanikio mengine ilikuwa ni pamoja na literacy rate kupanda sana na kuwa miongoni mwa nchi zinazoongoza Afrika; child mortality rate kupungua kutokea 248 kati ya watu 1,000 mwaka 1960, na kufikia 200 mwaka 1980; Pia infant mortality rate ilishuka kutokea 144 mwaka 1960 na kufikia 101 mwaka 1980; Vile vile life expectancy iliongezeka kutokea miaka 41 mwaka 1960, kufikia miaka 45 mwaka 1975, na miaka 52 mwaka 1980; Miaka 33 baadae chini ya soko huria, (2013), life expectancy yetu kiwango cha enzi za ujamaa!!! Otherwise hii positive trend ilitokana na mkazo wa Azimio la Arusha kuwekeza katika huduma za jamii na pia the accumulated financial reserves chini ya utawala wa Mwalimu;

Ni muhimu nisisitize tena hapa kwamba pamoja na Mwalimu kuingiza nchi katika Ujamaa kupitia Azimio la Arusha (1967), WorldBank iliendelea kuwa mstari wa mbele in terms of policy guidance and development strategies in general.


  • Niingie kwenye eneo muhimu sana la government/public investments. Wakati wa Ujamaa (hasa mid 1960s to late 1970s), levels of investments in the economy as percent of GDP ilikuwa ni nzuri na ya kuridhisha kwani on average ilikuwa around 20% to 27% of the GDP; Kuna uzi wangu mwingine unaojadili deni la taifa ambapo nilijadili kwa kina kuhusiana na nidhamu ya serikali katika mapato na matumizi ya fedha za umma (fiscal discipline); katika mjadala huo, nilipinga hoja za wanasiasa wa ccm kwamba taifa letu lipo salama in terms of debt burden kwa kigezo cha Debt per GDP ratio. Wanasiasa wetu hawa uchwara wamekuwa wanajenga hoja kwamba ratio yetu kuwa chini ya 50% (around 47%) means tupo salama kuliko mataifa kama Japan ambao ratio yao ni karibia 200%, huku taifa kama marekani likiwa na uwiano at around 110%; Nilipinga hoja hii kwamba ni ya upotoshaji wa hali ya juu na uzi huo ni kama ufuatao:
https://www.jamiiforums.com/great-t...e-wanasiasa-wachumi-na-wachumi-wanasiasa.html

Nachotaka kusisitiza hapa ni kwamba – chini ya ujamaa kulikuwa na nidhamu zaidi katika suala zima la usimamizi wa mapato na matumizi ya fedha za umma, hasa kwa kufuatana na kanuni/sheria za fiscal discipline ambazo wenzetu waliondelea (e.g) USA na Japan wanazifuata. Kanuni hizo ni mbili:

1. The Golden Fiscal Rule; na
2. The Sustainable Investment Rule.

Kwa upande mmoja, Golden Fiscal Rule inatamka explicitly kabisa kwamba serikali haitakopesha kwa ajili ya matumizi ya kawaida yani (current spending or expenditure kwa mambo kama posho, misharaha&#8230😉 bali kwa ajili ya investments katika maeneo yenye impact kwa maisha ya wananchi walio wengi. Nia ya kanuni hii pia ni kuhakikisha kwamba hata kama vizazi vijavyo vitakutana na deni la mababu zao, basi angalau vizazi hivyo vifaidike na madeni watakayowakuta, hasa iwapo fedha hizo zilikuwa invested kwenye sekta kama elimu, afya,maji, kilimo, viwanda kwa ajili ya ajira n.k.

On the other hand, kanuni/sheria ya Sustainable Investment Rule, compliments golden fiscal rule katika nia ile ile ya kujaribu to avoid creation ya excessive debt burden repayments kwa vizazi vijavyo kwa matumizi ambayo hayakuwahusu. Chini ya Sheria hii ya fiscal discipline, serikali inahakikisha kwamba deni linadhibitiwa katika kiwango ambacho hakita prove unsustainable or unfair kwa vizazi vijavyo.

Mwalimu alipokuwa anapingana na IMF, alilenga katika kuheshimu kanuni hizi; Kwa maana nyingine, Ujamaa chini ya Azimio la Arusha uliheshimu kanuni hizi kuliko sera za uchumi chini ya soko huria. Mifano hai ni mingi: Kwa mfano - utawala wa Mwalimu ndio uliojenga Hydro power plants, viwanda, textile mills n.k and since then hakuna any major investments katika maeneo haya ambazo zimefanywa na serikali ya mwinyi, Mkapa, na Kikwete; Sana sana over 60% ya budget allocations zimekuwa zikiishia kwenye matumizi ya kawaida (e.g. posho, salaries, procurement, ufisadi na debt servicing), kuliko kwenye matumizi ya maendeleo. Vinginevyo Mwalimu alipinga sana proposals za IMF na WorldBank in the contexts of ERP and na SAPs kwa hofu kwamba mtanzania wa kawaida angeumia. Tutazame jinsi gani Mwalimu alikuwa sahihi katika hili. Mwalimu alipata tamka wakati waku launch azimio la arusha kwamba:

"Foreign Aid is not the answer to our problems. There are many needy countries in the world. And even if all the prosperous nations were willing to help the needy countries, the assistance would still not suffice. Nor would borrowing help. Whether it is used to build schools, hospitals, house, factories etc, it still has to be repaid. Where, then shall we get it from? We shall get it from the villages and from agriculture. If we are not careful we might get to the position where the real exploitation in Tanzania is that of the town dwellers exploiting the peasants."

Miaka ya leo tunaona jinsi gani watawala wetu wanachukua mikopo ovyo ovyo tu in a non-transparent manner, mara nyingine to finance miradi ya kisiasa kuliko miradi ya kiuchumi; na anayeumia katika ulipaji wa madeni haya ni maskini (hasa wakulima);

Wadau wenzangu, Mwalimu visited the World Bank in 1998, na muda huu ulikuwa ni tosha kuweza fanya assessment juu ya mafanikio ya Ujamaa vis-a-vis Soko huria. Mwalimu alipewa mwaliko rasmi na rais wa benki ya dunia na ukumbi ulijaa WB's staff from different nations including Africa. Katika hafla hiyo, President of the WorldBank akamwambia Mwalimu maneno yafuatayo 1998 (source, Calderisi, 2006):

"I have been re-reading your speeches from the 1960s and they still ring true. Obviously there was nothing wrong with your vision. Where did we go astray?"

Mwalimu akajibu:

"I don't have full answers to that question. Some things certainly went right – we knitted a nation together, gave it a pride, and educated a large number of our children and adults. But some ideas needed to wait their proper time. People weren't ready. But you (the younger Africans) now have a chance to give those ideas new life."

Mwalimu went on to kushauri kwamba Afrika na International Financial Institutions (IFIs) i.e. World Bank and IMF should work differently together. Specifically, alisema maneno yafuatayo:

"We have had our faults, but you [the World Bank and IMF] have been running Africa for the last 10-15 years not literally, but essentially, as national budgets have shrunk, African debt has grown and political options have narrowed. Whatever mistakes we made, we made together. Now, we must find the humility to correct them hand in hand."

Mwisho one of the people from the audience akamuuliza Mwalimu ana maoni gani kuhusiana na ubinaifishaji wa mashirika ya umma. Mwalimu akajibu with confidence:

"I understand the rationale for privatization now, but part of it still strikes me as simple thievery."

Bottom line ni kwamba pamoja na mapungufu mengi ya Azimio la Arusha, Ujamaa ulikuwa na manufaa kwa watanzania walio wengi kuliko soko huria, na hili limekuwa acknowledged na wataalam wengi wa masuala ya uchumi na maendeleo. Hii ilitokana na ukweli kwamba MALENGO ya Ujamaa yalikuwa so inspiring na ushahidi wa hili ni jinsi gani wetsetn countries including the World Bank supported Tanzania wakati wa Ujamaa, tena kuna kipindi Fulani kuliko mataifa mengine yote maskini duniani;

Soko huria limemwangamiza mtanzania. Kuthibitisha hili – kwa mujibu wa afisa mmoja wa wa WorldBank anazungumzia encounter yake na Mkapa wakati akiwa rais wa Tanzania as follows:

"President Mkapa cited a survey of 50 villages showing that one in five households felt they were better off as a result of economic reforms; almost 40% thought they were worse off"

Ningependa kugotea hapa ili kuepuka kuja na uzi mrefu ambao utawachoshwa wadau kama highlander et al.

Nitarudi for more…

cc edwin mtei, cagl, highlander, EMT, nguruvi3, jingalafalsafa et al...
 
Wako wana CCM wengi hawakubaliani na chama chao kukiuka misingi mikuu ya Azimio la Arusha. Je huoni kuna haja ya cdm kutoa rasmi msimamo wake kuhusu Azimio la Arusha ili wanachama hao waweze kufana uamuzi mgumu?

Kumekuwa na ujenzi wa hoja kwamba Chadema wanatekeleza elements fulani za azimio la arusha na kadhalika. Hii ni hoja nzuri na ya msingi sana, ingawa wanachama wengi wa chadema hawataki kabisa kusikia Chama chao kuhusishwa na TANU au azimio la Arusha; Mwaka jana nilianzisha mjadala kuhusiana na mfanano na utofauti baina ya TANU na Chadema; Hoja yangu ya msingi ilikuwa ni kwamba - Chadema kufananishwa na TANU is more of a political asset than a liability, huku mfananisho huo ni more of a political liability to CCM than political asset; uzi huo kama ifuatavyo:
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/325723-chadema-na-tanu-mfanano-na-tofauti.html

Nikirudi kwenye hoja ya msingi, taifa letu kwa sasa linayumba kutokana na kukosa dira na mwelekeo ambao umekuwa digested, kueleweka na kukubalika na wananchi walio wengi; Marehemu Kolimba alijadili hili kwa kina na hoja yake inazidi kuwa na mashiko leo; Wakati wa ujamaa, kama taifa, tulikuja na maazimio kuhusiana na makubaliano juu ya nini tunataka, nini hatutaki, wapi tunataka kwenda na wapi hatutaki kwenda; Maazimio yote haya yakawekwa katika document moja ambayo ndio ilizaa azimio la arusha;jina Arusha ni kutokana na wapi kikao husika kilifanyika; maana yangu hapa ni kwamba - tusiogope neno azimio wala arusha kwani bado tunahitaji kuja na maazimio kama taifa juu ya wapi tunataka kwenda na tufiikaje katika safari tunayokudusia, na kikao juu ya hilo kinaweza fanyika Pwani, Tarime, Katavi, Simanjiro n.k; Kwa maana hii, kuna umuhimu wa kurudisha nchi katika mstari kwa kuja na azimio kwa mfano la Simanjiro iwapo tutaamua kufanyia vikao hivi muhimu huko; its as simple as that; sidhani kama kuna mwanachadema yoyote ambae anakataa kwamba nchi imekosa dira na inabidi tukae chini na kuja na maazimio na maamuzi magumu juu ya wapi tunataka kupeleka nchi yetu na njia za kufika huko tutakapochagua kwenda;

Kuna umuhimu wa watanzania kuacha kukubali propaganda kwamba mmiliki wa azimio la arusha ni TANU; Ukweli ni kwamba mmiliki huyo ni mtanzania ambae kwa wakati ule alikuja kubaliana na uamuzi kwamba tuanze na mfumo wa chama kimoja kwanza ili kujenga taifa kwa ufanisi zaidi, na hivyo mtanzania huyo alikubaliana na msimamo wa chama juu ya umuhimu wa azimio la arusha kwani ilikuwa ni njia pekee ya kutekeleza ahadi za uhuru; Mwalimu hakukurupuka kuja na azimio la arusha, the situation was so tense katika jamii, na alipoenda ziarani china kuangalia wenzetu wamefanya nini, ndipo akaja na wazo la azimio la arusha; Bottom line hapa ni kwamba – mmiliki wa azimio la arusha alikuwa ni watanzania ambao leo hii baada ya mageuzi ya kisiasa, wengine ni wanachadema, wanaccm, CUF, NCCR, CCK, TLP, huku wengine wengi wakiwa hawana ushabiki wa chama chochote cha siasa; Kwahiyo hizi views kwamba Azimio la Arusha ni la TANU/CCM sio helpful, na kuna umuhimu wa kuweka mbele utaifa wetu katika hili; Iwapo Chadema mathalani wanataka kuja na manifesto ya kurudisha nchi kwenye mstari kwa mtindo wa maazimio Fulani, wajipange tu na kuchagua wapi wafanyie kikao hicho muhimu; Kikubwa ni waepuke kufanyia kikao hicho Kanda ya Kaskazini kwani Azimio la Kilimanjaro, Arusha, Manyara au Babati, hata kama litakuwa na manufaa makubwa kwa taifa, litashambuliwa kwa hoja nyingi za ovyo na wapinzani wa chadema, hasa wana CCM wasiokuwa na mapenzi na nchi yetu;
 
Highlander,

Per bandiko namba 60 nitakurudia na takwimu,lakini ni muhimu uelewe yafuatayo:

Kwanza,GDP growth rate ya mid 1970s ilikuwa ni pro poor growth;growth ya 1970s source yake ilikuwa ni katika sectors ambazo watanzania walio wengi earned their bread; growth in the 1970s did involve labour provided the poor; miaka unayosema, hasa kuanzia 2000, growth ambayo hata wewe unaisifia kama wanasiasa wa ccm hence kuji contradict na hoja na msimamo wako wa awali juu ya wachumi uchwara wa ccm, ni growth ambayo sio pro poor bali pro rich kwani its obvious kwamba an average of almost 7% growth kwa miaka kumi na mbili mfululizo (2000-2012) havnt led to elimination of poverty kwa mafanikio kama growth ya 1965-1977;hii ni kwasababu growth ya sasa is driven by sectors that don't provide jobs kwa walio wengi,hasa wakulima i.e such growth doesn't involve labour provided by the poor; kwahiyo,rate ya nyakati hizi ya almost 7pct on avg kwa mwaka for like ten yrs haina manufaa kwa wengi kama rate ya eg 5pct average nyakati za ujamaa kwa hoja zangu hapo juu;nikupe mfano mwingine mzuri uelewe zaidi - kwa taifa kama marekani na mengine advanced kutokana na strong linkages na economic activities na walio wengi in terms of output and employment,hata a 3pct growth ina manufaa sana kwa wananchi;

Sasa nikija kwenye maeneo mengine kama literacy rate,mortality rate etc, sidhani kama nina haja ya kufafanua kwabi hoja ya hapo juu on GDP and its implications to livelihoods kwa walio wengi is self explanatory; do you think its worth it for me kuja na takwimu unazotaka kutokana na hoja yako kwamba 2005 mtanzania wa kawaida alikuwa better off kuliko mtanzania wa 1985? Note - mtanzania wa 1985 na mtanzania beyond 1985 ni watanzania wawili tofauti kabisa kihali; na mtanzania wa 1990-1994 ambapo Tanzania iligeuka kuwa nchi ya tatu kwa umaskini kuliko duniani ndani ya Economic reforms, ndio tofauti zaidi.....

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Niwaombe radhi Mkuu Mchambuzi, Mkuu JingalaFalsafa na wadau wengine katika uzi huu kwa mambo mawili: Kuna bandiko limejenga picha mimi Highlander naegemea upande wa Chama fulani cha siasa hapa nchini. Taswira hii kama imeanza kujitokeza naomba mnisamehe kwa sababu hiyo taswira si sahihi; taswira hiyo ni co-incidental kabisa. Siongei kwa niaba ya chama chochote cha siasa! Maneno yote ambayo nimeyasema kwenye uzi huu ni ya kwangu mimi binafsi kama Highlander. Ni views personal and personal only .

Pili, Mkuu Mchambuzi, na Mkuu JingalaFalsafa mtakumbuka tumetoka mbali katika mjadala huu. leo kuna mabandiko mumeyaweka hapa yanahitaji umakini kuyajibu. Naomba mnisamehe nitachelewa kidogo kuyajadili. Kuna changamoto ya takwimu ambazo Mkuu Mchambuzi kazileta, pia kuna changamoto ya Ethical Morality katika biashara kutoka kwa Mkuu JingalaFalsafa ambayo kaichanganya na concept ya profit motive. Nitachelewa kidogo kuzijibu hoja hizi lakini nina mpango wa kuweka mchango kwenye hoja zenu. Ila sasa nikubaliane na Mkuu JingalaFalsafa kwamba Mungu wetu anaita sasa. Tutafika pazuri!

Ila hili nimeshindwa kulisubirisha hadi kesho Mkuu Mchambuzi. Kwamba "kuanzia 2000, growth ambayo hata wewe unaisifia kama wanasiasa wa ccm hence kuji contradict na hoja na msimamo wako wa awali juu ya wachumi uchwara wa ccm, ni growth ambayo sio pro poor bali pro rich kwani its obvious kwamba an average of almost 7% growth kwa miaka kumi na mbili mfululizo (2000-2012) havnt led to elimination of poverty kwa mafanikio kama growth ya 1965-1977;hii ni kwasababu growth ya sasa is driven by sectors that don't provide jobs kwa walio wengi,hasa wakulima i.e such growth doesn't involve labour provided by the poor; kwahiyo,rate ya nyakati hizi ya almost 7pct on avg kwa mwaka for like ten yrs haina manufaa kwa wengi kama rate ya eg 5pct average nyakati za ujamaa.

Naomba nisikilize; at least for once. growth rate ya 7% haiwezi kuonesha impact kwa kila mtu. Utaanza kuona impact growth rate ikifikia maeneo ya 10%. Issue hapa ni why are we not getting the 10% growth rate wakati Mungu wetu katupatia kila kitu chini ya jua jamani? Kwamba CCM ina wachumi uchwara, sijabadili msimamo huo hata kidogo, ingawa inawezekana sababu ni kwamba intellectuals wanakwa sidelined na matapeli ambao wamefanikiwa kupora political power. Tatizo hasa ni mwamba you guys have hundreds of rouges in government. That is what the problem is....

Mafanikio haya tunayoyaona ni sehemu tu ya mafanikio ambayo tungeweza kuyaona kama tungekuwa na watu clean katika Government--watu waadilifu ndani ya Serikai ya CCM. Hii 7% ni efffect ya makombo tunayoachiwa na wezi.
 
"Some things certainly went right _we knitted a nation together, gave it a pride and educated a large number of our children and adults. "But some ideas need to wait their proper time. People were not ready" "But You {the younger Africans} now have a chance to give those ideas new life") Asante Mkuu Mchambuzi kwa kuzidisha mshale wa moto moyoni mwangu! Nyerere can live again! We have to make him so!
DIRA/ITIKADI/IMANI/FALSAFA KUU YA TAIFA. IMANI KUU msingi wa FIKRA ZOTE! (...nilitaka kuhoji kuhusu hili, lakini nadhani litahamisha hoja iliyopo, naomba niliulize pale tutakapofikia hitimisho la hoja hii...)!
Mungu wetu na asimamie hilo! Anaita sasa!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom