Nini msimamo wa CHADEMA kuhusu Azimio la Arusha?

Nini msimamo wa CHADEMA kuhusu Azimio la Arusha?

GAGL

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2010
Posts
392
Reaction score
400
Nimefuatilia kwa makini sana kuhusu mwenendo wa vyama viwili vikubwa na kugundua kuwa ili nchi hii isonge mbele, ni lazima ccm iondolewe madarakani. Na chama konachostahili kushika dola ni chadema ambaye ndiye changamoto kubwa kwa ccm.

Lakini kabla sijachukua kadi ya cdm, naomba kufahamishwa kuhusu msimamo wa cdm kuhusu Azimio la Arusha kwa sababu kilichopelekea nchi hii kukosa viongozi waadilifu ni kupuuza misingi ya uongozi iliyoanishwa katika azimio hilo.

Mimi nalihitaji azimio hilo sasa sijui msimamo wa chama ninachokipenda na kutaka kujiunga kama kina msimamo huo pia.
 
Kwa kuwa Azimio la Arusha lilianzishwa na TANU iliyokuja kuzaa CCM,

Na kwa kuwa azimio la Arusha lilifanyika mwaka 1967,

Na kwa kuwa CHADEMA ilianzishwa mwaka 1992,,,

Nakushauri usiihusishe CHADEMA na hayo makitu ya CCM ni usanii mtupu. Hata katiba yao na ya nchi inaelezea habari za ujamaa na kujitegemea lakini hakuna anayetekeleza. Hata azimio la Arusha likirudi leo Chenge hawezi kurudisha mabilioni aliyoficha Jersey, Ridhiwani Kikwete hawezi kurudisha kampuni ya UDA aliyojiuzia na jamaa zake wa Simon Group kwa bei poa, Rostam Azizi hawezi kutusamehe deni la Dowans. Dawa sio azimio la Arusha, dawa ni kuiondoa CCM madarakani tuje na maazimio mengine na mipango yetu ya kimaendeleo inayoendana na mahitaji ya sasa ya kiuchumi na kitechnolojia. Usiwaingize CHADEMA kwenye maupuuzi ya CCM
 
Nimefuatilia kwa makini sana kuhusu mwenendo wa vyama viwili vikubwa na kugundua kuwa ili nchi hii isonge mbele, ni lazima ccm iondolewe madarakani. Na chama konachostahili kushika dola ni chadema ambaye ndiye changamoto kubwa kwa ccm. Lakini kabla sijachukua kadi ya cdm, naomba kufahamishwa kuhusu msimamo wa cdm kuhusu Azimio la Arusha kwa sababu kilichopelekea nchi hii kukosa viongozi waadilifu ni kupuuza misingi ya uongozi iliyoanishwa katika azimio hilo. Mimi nalihitaji azimio hilo sasa sijui msimamo wa chama ninachokipenda na kutaka kujiunga kama kina msimamo huo pia.

Naomba mtafute kamanda yeyote aliye karibu nawe Mkuu GAGL kachukue kadi yako ya CHADEMA.

Kitu ambacho wengi wanakitamani katika Azimio na Arusha si jina la azimio lile, bali wanatamani maudhui yake fulani-fulani mazuri kwa taifa hili. Si kila kitu katika Azimio la Arusha kilikuwa sawa. Azimio la Arusha lilikuwa na Utopia nyingi sana mule, nikianzia na dhana kwamba mtu anaweza kuacha profit motive kabisa, kitu ambacho hakiwezekani. Kumbe kilichotakiwa kuonekana katika Azimio la Arusha ilikuwa dhamira ya ku-moderate profit motive. Mataifa yaliyoendelea yanafanya hivyo. Unaruhusu profit motive kushamiri, ila unai-moderate. Sera za CHADEMA zinatafuta kutumia profit motive kujenga uchumi wa taifa, lakini profit motive moderated.

Spirit ya kujikana reasonably, (narudhia: kujikana reasonably), ilikuwapo katika Azimio la Arusha. Kutaka wengine nao wapate faida katika yanayofanyika ndani ya taifa, hili lilikuwapo. Uadilifu katika utendaji ndani ya chama na serikali, hili pia lilikuwapo katika Azimio la Arusha. Na haya yanahubiriwa na wataalam wa mahubiri ya siasa katika CHADEMA.

Mi nionavyo, kikubwa katika Azimio la Arusha kinachostahili kukienzi ni Maudhui ya uadilifu katika kulinda maslahi ya kwako--wewe mtu binafsi--lakini kwa mtizamo kwamba wewe ni sehemu ya walio wengi, hivyo kwamba unafanya kazi unayoifanya kwa niaba ya wengi; yaani kwamba umepewa jukumu la kulinda maslahi makuu ya Taifa kwa ujumla wake, badala ya kulinda maslahi binafsi kwanza mtu anapokuwa katika nafasi yoyote ile ya uongozi. Chadema wanahubiri haya. Linda maslahi ya taifa kwanza. Mengine yafuate. Kwa hiyo hata kama hawatafufua Azimio la Arusha neno kwa neno kwa sababu lilikuwa na kasoro zake pia, maudhui katika Azimio la Arusha yenye nia njema kwa taifa tayari wanayahubiri.

Kwa maana hiyo, kama wewe ni mpenzi wa Azimio la Arusha, nina hakika utakuwa unalipenda Azimio lile kwa sababu ya maudhui yake mema. Maudhui ya uadilifu, maudhui ya kulinda masalahi makuu ya taifa kwa ujumla wake; kulinda maslahi ya Taifa kwanza kabla ya kulinda maslahi binafsi mtu anapokuwa katika nafasi yoyote ile ya uongozi. Haya Chadema inahubiri tayari na kwa kiasi kikubwa wanajitahidi kutekeleza mahubiri yao wao binafsi. Nilisikia John Mnyika anatembelea 'Vitz kobe' ndogo badala ya Prado. Niliipenda sana hii!

Wale unaosikia wamekiacha CHADEMA na kurudi CCM ni wale ambao walienda CHADEMA kutafuta ajira; wale ambao walienda kule kutafuta mianya ya utajirisho, wakidhani CHADEMA ni kama CCM. Walipokuta pale kuna kujitolea kwingi sana wakaona hapafai na kurudi kule ambako siasa malengo yake ni ajira ya utajirisho kwa hela halali na haramu. CHADEMA inatekeleza maudhui mema ya Azimio la Arusha nionavyo mimi. Hawawezi kutekeleza kila kilichokuwapo katika Azimio la Arusha kwa sababu si kila kitu kilikuwa sawa mule. Mengine hayakuwa sawa wakati ule, hayawezi kuwa sawa leo. Lakini pia Azimio la Arusha ilikuwa sera ya TANU. Chadema si TANU, japo inaweza ikawa KAMA TANU katika mambo fulanifulani. Huwezi kuzaa mtoto akafanana na wewe kwa kiiiiila kitu. Yapo mengine yatakuwa ya kwake yeye kama yeye.

Kachukue kadi mkuu. Ingia kwenye vita ya kurudisha heshima ya nchi yetu na utajiri wake mikononi mwetu. Go!
 
Falsafa ya Chama (CHADEMA)
1. Falsafa ni fikra na mtazamo wa Chama ambayo ni kuamini katika "Nguvu na Mamlaka ya Umma" (The People's Power) katika kumiliki, kuendesha, kubuni, na kuendeleza maamuzi, mawazo, rasilimali, uchumi na siasa ya nchi yao.
2. Aidha falsafa ya "Nguvu na Mamlaka ya Umma" ndiyo msingi na chimbuko la kuundwa dola ya nchi, na kuwa, Umma ndiyo wenye madaraka ya mwanzo na ya mwisho katika kuamua hatima ya nchi na taifa pasipo kuingiliwa, kudanganywa au kughilibiwa na viongozi, watawala au wageni.
3. Ujenzi na udumishaji wa Demokrasia na Maendeleo nchini vitatokana na Nguvu na Mamlaka ya Umma wa Watanzania. Nguvu na Mamlaka ya Umma itabainishwa, kuainishwa na kulindwa katika Katiba ya nchi na Umma ndiyo utakuwa chimbuko la Katiba hiyo.
4. Historia inaonyesha kuwa "UMMA" wa Watanzania haujawahi kuwa na sauti, mamlaka na madaraka juu ya maamuzi ya hatima ya maisha ya watu. Uhuru, nguvu, mamlaka na madaraka wakati wote, tokea enzi za ukoloni mpaka leo, vimekuwa vikihodhiwa na kumilikiwa na watu wachache ambao wana mamlaka ya kuongoza SERIKALI na kuwakandamiza wananchi.
5. CHADEMA tunaamini kuwa mifumo na miundo ya utawala wa nchi yetu havijawapo kwa ajili ya kuutumikia umma, bali umma ndiyo huzitumikia serikali hizo ambazo ni mali ya watu wachache wanaopoka "Nguvu ya Umma". Sambamba na hilo, umma wa Watanzania umekuwa hauna mamlaka ya mwisho ya kuhoji maamuzi ya serikali yanayowaathiri watu, na hivyo kujikuta hauna mamlaka juu ya rasilimali, sheria, utawala, na uendeshaji wa nchi. Aidha, Katiba ya Nchi imekuwa miliki ya Serikali kwa kutumia Bunge ambalo linatawaliwa na mawazo kongwe ya ukiritimba wa enzi za mfumo wa Chama kimoja cha siasa nchini.
6. CHADEMA tunaamini na kutambua kuwa "kuchaguliwa" kuunda utawala wa kuongoza nchi hakumaanishi wachaguliwa kujitwalia mamalaka ya UMMA na kisha kuyatumia mamlaka hayo kuwakandamiza "waliowachagua" kwa sababu tu ya kutetea maslahi binafsi badala ya maslahi ya umma.
7. Hivyo basi, falsafa ya "Nguvu na Mamlaka ya Umma" ndiyo njia ya msingi ya kubadilisha fikra na uongozi unaokandamiza umma, ili kuibua fikra mpya na kuweka uongozi unaoweza kumilikiwa, kuhojiwa, na kuwajibishwa na umma kwa kutumia vyombo vilivyopatikana kwa utashi wa wengi kupitia chaguzi huru na za haki.
8. Falsafa ya "Nguvu na Mamlaka ya Umma" inalenga kuwaamsha, kuwahamasisha, kuwaelimisha, kuwashawishi na kuwaandaa Watanzania wachukue hatua ya kuimiliki, kuitawala, kuilinda na kuifaidi nchi yao tofauti na kipindi cha miaka mingi chini ya mfumo wa chama kimoja cha siasa na miaka kumi na nne ya mwanzo ya mfumo wa vyama vingi.
 
Swali zuri lakini nadhani halitajibiwa kwa sababu za kisiasa au litajibiwa kisiasa;tangia kifo cha azimio la arusha,nchi imekosa dira na tumepoteza uhuru wetu wa kujiamulia jinsi gani ya kuendesha nchi kwani madereva ni IMF na Worlbank;Kama alivyofanya Mwalimu kuomba radhi watanzania juu ya mapungufu ya azimio la arusha, Mzee Mtei nae anatakiwa azungumzie hili na pengine kuomba msamaha juu ya mapungufu ya sera za IFIs ambazo yeye alikuwa mmoja wa waasisi miaka ya mwanzo ya themanini;huo ndio ustaarabu; ni ajabu Mzee Mtei anaendelea kukaa kimya wakati ni dhahiri sasa kwamba kwa mtanzania wa kawaida,pamoja na mapungufu mengi ya ujuamaa,miaka 18 ya azimio la arusha ilikuwa bora na ya matumaini kuliko miaka 28 ya ubepari na soko huria tunayoendelea nayo leo hii; let's be objective and rational on this subject,tusiweke ushabiki wa kisiasa and display our ignorance and arrogance;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Swali zuri lakini nadhani halitajibiwa kwa sababu za kisiasa au litajibiwa kisiasa;tangia kifo cha azimio la arusha,nchi imekosa dira na tumepoteza uhuru wetu wa kujiamulia jinsi gani ya kuendesha nchi kwani madereva ni IMF na Worlbank;Mzee Mtei anatakiwa azungumzie hili na pengine kuomba msamaha juu ya mapungufu ya sera za IFIs ambazo yeye alikuwa mmoja wa waasisi miaka ya mwanzo ya themanini; ni ajabu anaendelea kukaa kimya wakati ni dhahiri sasa kwamba kwa mtanzania wa kawaida,miaka 18 ya ujamaa ilikuwa bora kuliko miaka 28 ya ubepari na soko huria tunayoendelea nayo leo hii;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Nilikuwapo wakati wa phase zote za mabadiliko ya mitizamo ya uchumi. Ni kweli kwamba Mtei amekuwapo katika tume mbalimbali zilizofanya marekebisho ya mitizamo ya kiuchumi. Ninayoikumbuka zaidi ni ile tume ya kurekebisha sera ya Kodi.
Pengine utakumbuka kwamba mara baada ya mapendekezo ya njia mpya za makusanyo ya kodi, Tanzania haikuwahi kupata kodi kidogo tena.

Mabadiliko ya kiuchumi hapa Tanzania kwa ushauri wa IMF na World Bank yameleta tija nyingi. Mlikuwa na mashirika mengi ya Umma yakiajiri watu wengi kuliko uwezo wala sababu za kuajiri watu wengi kwa idadi hizo, mlikuwa na wafanyakazi wengi katika Idara za Serikali pasipo haja ya kuwa na wafanyakazi wengi kiasi kile. IMF na World Bank walitoa ushauri idadi za ajira serikalini zipungue, idara nyingine zifutwe au kuunganishwa, Mashirika ya Umma yabinafsishwe. Haya yote, kwa mtizamo wa kiuchumi, yameleta faida kubwa kwa taifa.

Kitu pekee ambacho kimepindisha na kuvuruga matokeo mazuri ya ushauri wa IMF na World Bank ni Rushwa na upendeleo katika ajira za umma; Rushwa katika ubinafsishaji wa mashirika ilikuwa kubwa na kupotosha kabisa malengo asili ya mpango ule. Kwa hiyo Tatizokubwa hapa si IMF na World Bank. Tatizo ni Rushwa na ukosefu wa utawala bora ndani ya serikali ya chama chenu.
Mpe heshima Mtei na timu yake ya Marekebisho ya Kodi kwamba sasa Taifa linaweza hata kukusanya bilioni 400 kwa mwezi badala ya milion 200. Wape Heshima IMF na World Bank kwa ushauri mzuri kwa Taifa.
 
Kwanza acha kna kushambulia watu kwamba hawamweshimu mzee mtei. Ni wapi nimemvunjia heshima? Vinginevuo kila mara napoleta hoja hii huwa narudiwa ba hoja ya mafanikio ya mzee mtei katla kodi;Hakuna aliyesema mzee mtei hajafanyia nchi hii mazuri na wala hakuna anayesema nyerere hakufanyia mema nchi hii; unachojadili wewe ni mafanikio yake katika muktadha wa mageuzi ya kiuchumi yaliyoanzia miaka ya themanini,huku kwa mwalimu ukiponda na kutogusia mafanikio yoyote; kwa taarifa yako ni hivi - liberalisation,marketization, and privatization haitamkomboa mtanzania,kitachomkomboa mtanzania ni kuyarudia mazuri ya azimio la arusha na kuyaacha mabaya ambayo mwalimu alishaombea msamaha; ni wakati muafaka sasa wa mzee mtei kujadili mapungufu ya soko huria ambalo alishirikiana na IMF akiwa washington kuliratibu nchini Tanzania;

Kweli unathubutu kusema kwamba soko huria alija deliver kwasababu tu ya rushwa??? Soko huria katika nchi maskini is inherently problematic; sidhani kama itakuwa ni busara kuanza kupeana kisomo hapa; vinginevyo hata worldbank na imf ambao wamekuwa under pressure to reform kutokana na makosa yao katika kushauri nchi maskini wameanza kulikubali hili;

Hili la mzee mtei ni suala la uungwana tu na anajua hilo,vinginevyo kukubali mapungufu ya kiuamuzi na kimsimamo katika masuala ambayo yamekuwa yanagusa maisha ya wananchi walio wengi ni sehemu ya uongozi bora;nyerere aliganya hilo,mzee mtei ana nafasi ya kufanya hivyo au kuamua kupuuza na kuangalia tu mafanikio yake na ya soko huria holela;

Nadhani tunakwenda vizuri katika mjadala huu. Nafanya bookmark ukurasa huu sasa, ili nikujibu vizuri baadaye. Ila kwa ufupi nikubali pia kwamba unaliangalia suala hili vizuri--japo nina mashaka unataka kufunika nafasi ya rushwa katika kufifisha mafanikio ambayo yangeweza kuwapo katika soko huru pasipokuwapo tatizo la rushwa na upendeleo katika ajira ya umma.

I'll get back to you...
 
Highlander,

Wakati unajipanga kurejea katika mjadala naomba niseme hivi - Ni dhahiri kwamba bila IMF na Worldbank kuingilia,hali ingekuwa mbaya sana and may be taifa to collapse;tatizo ni kwamba intervention that aimed to rescue ilikuja kiholela sana huku hizi IFIs zikitazama zaidi faida zao kibiashara kwani worldbank na benki kama Barclays key objective ni ile ile "to maximize shareholders wealth"; ni katika hili suala la wealth "maximization "hizi IFIs zimekuwa zinaumiza maskini zaidi kuliko kuwasaidia, na ni katika suala hili hili na wealth maximization,mianya ya rushwa ikajotokeza,lakini sio kable ya kulizika azimio la arusha 1992 kwa support kubwa ya the IFIs; bottom line ni kwamba rushwa kukithiri ni matokeo ya kifo cha azimio la arusha ambalo liliuliwa as part of the liberalization,marketization and privatization process iliyoambatana bega kwa bega na ujio wa IFIs;

Mzee mtei ange acknowledge tu kwa lugha kama hiyo ingetosha,vingine kwa sisi tunaomweshimu kama mmoja wa wachumi mahiri nchini,yeye kukaa kimya wakati he's probably the only one remaining to provide us with a historical account kwa kutueleza mafanikio na chanhgamoto za soko huria na akasikilizwa; kukaa kimya maana yake ni kwamba IFIs walikuja na mwarubaini,kama hautibu watanzania walio wengi basi ni wananchi wenye mapungufu; je vijana wa leo na wa kesho tumkumbuke mzee mtei kwa namna hii?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Falsafa ya Chama (CHADEMA)
1. Falsafa ni fikra na mtazamo wa Chama ambayo ni kuamini katika "Nguvu na Mamlaka ya Umma" (The People's Power) katika kumiliki, kuendesha, kubuni, na kuendeleza maamuzi, mawazo, rasilimali, uchumi na siasa ya nchi yao.
2. Aidha falsafa ya "Nguvu na Mamlaka ya Umma" ndiyo msingi na chimbuko la kuundwa dola ya nchi, na kuwa, Umma ndiyo wenye madaraka ya mwanzo na ya mwisho katika kuamua hatima ya nchi na taifa pasipo kuingiliwa, kudanganywa au kughilibiwa na viongozi, watawala au wageni.
3. Ujenzi na udumishaji wa Demokrasia na Maendeleo nchini vitatokana na Nguvu na Mamlaka ya Umma wa Watanzania. Nguvu na Mamlaka ya Umma itabainishwa, kuainishwa na kulindwa katika Katiba ya nchi na Umma ndiyo utakuwa chimbuko la Katiba hiyo.
4. Historia inaonyesha kuwa "UMMA" wa Watanzania haujawahi kuwa na sauti, mamlaka na madaraka juu ya maamuzi ya hatima ya maisha ya watu. Uhuru, nguvu, mamlaka na madaraka wakati wote, tokea enzi za ukoloni mpaka leo, vimekuwa vikihodhiwa na kumilikiwa na watu wachache ambao wana mamlaka ya kuongoza SERIKALI na kuwakandamiza wananchi.
5. CHADEMA tunaamini kuwa mifumo na miundo ya utawala wa nchi yetu havijawapo kwa ajili ya kuutumikia umma, bali umma ndiyo huzitumikia serikali hizo ambazo ni mali ya watu wachache wanaopoka "Nguvu ya Umma". Sambamba na hilo, umma wa Watanzania umekuwa hauna mamlaka ya mwisho ya kuhoji maamuzi ya serikali yanayowaathiri watu, na hivyo kujikuta hauna mamlaka juu ya rasilimali, sheria, utawala, na uendeshaji wa nchi. Aidha, Katiba ya Nchi imekuwa miliki ya Serikali kwa kutumia Bunge ambalo linatawaliwa na mawazo kongwe ya ukiritimba wa enzi za mfumo wa Chama kimoja cha siasa nchini.
6. CHADEMA tunaamini na kutambua kuwa "kuchaguliwa" kuunda utawala wa kuongoza nchi hakumaanishi wachaguliwa kujitwalia mamalaka ya UMMA na kisha kuyatumia mamlaka hayo kuwakandamiza "waliowachagua" kwa sababu tu ya kutetea maslahi binafsi badala ya maslahi ya umma.
7. Hivyo basi, falsafa ya "Nguvu na Mamlaka ya Umma" ndiyo njia ya msingi ya kubadilisha fikra na uongozi unaokandamiza umma, ili kuibua fikra mpya na kuweka uongozi unaoweza kumilikiwa, kuhojiwa, na kuwajibishwa na umma kwa kutumia vyombo vilivyopatikana kwa utashi wa wengi kupitia chaguzi huru na za haki.
8. Falsafa ya "Nguvu na Mamlaka ya Umma" inalenga kuwaamsha, kuwahamasisha, kuwaelimisha, kuwashawishi na kuwaandaa Watanzania wachukue hatua ya kuimiliki, kuitawala, kuilinda na kuifaidi nchi yao tofauti na kipindi cha miaka mingi chini ya mfumo wa chama kimoja cha siasa na miaka kumi na nne ya mwanzo ya mfumo wa vyama vingi.
 
IMF is just a Bank, haulazimishwi kukopa, Watafuta visingizio bana? Matajiri wangi wamepitia mikopo, hata makampuni ya China yalikopa. Issue kama ukakopa kuongeza mke hutaweza kulipa.
 
Communist, hoja yako unaelekeza kwangu ama? Kama ndio,ielekeze kwa mzee mtei ambae alitofautiana na mwalimu pale mwalimu alipogomea hawa watu kwa kusema kwamba tangu lini IMF stands for International Ministry of Finance? Nyerere hakutaka kulazimishwa kokopa kwa masharti ambayo yangedumaza nchi, na sehemu kubwa ya hoja ya Mwalimu tunaona ukweli wake leo;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Nipo njiani naelekea Kawe Mkuu Mchambuzi. Pengine tumuombe Mzee Edwin Mtei, kama unavyopendekeza, kwamba aweke mchango wake katika hoja hii kama unavyoomba. Binafsi nipo njiani nashindwa kujadili jambo hili kwa kina kama ninavyotaka. Ila kwa kifupi, naona kwamba matatizo mengi ambayo yamefuatia mabadiliko ya mfumo wetu wa uchumi yametokana zaidi na kasoro ya usimamizi. Si matatizo ya mfumo wenyewe uliopokelewa jinsi ulivyo.

Baadaye nitakuambia kwamba ushahidi upo kuonesha matatizo ya usimamizi ndiyo hayohayo ambayo hata yaliufanya mfumo wa ujamaa ukawa mbaya kuzidi ubaya ambao ungeonekana kama usimamizi ungekuwa bora. Nitakuambia everything constant, yaani wasimamizi wakiwa ndo walewale, matatizo yatakuwepo no matter unatumia mfumo gani wa kuendesha uchumi.
 
IMF is just a Bank, haulazimishwi kukopa, Watafuta visingizio bana? Matajiri wangi wamepitia mikopo, hata makampuni ya China yalikopa. Issue kama ukakopa kuongeza mke hutaweza kulipa.

Hivi huwa tunadai hatulazimishwi kukopa IMF au World Bank, ni kwa sababu hakuna tamko linalosema "NI LAZIMA NCHI MASIKINI KUKOPA" au ni kwa sababu ipi? Nachofahamu huwa "TUNASHIKIWA HADI BUNDUKI ILI TUKAKOPE". Nyeupe ni nyeupe na nyeusi ni nyeusi, tuishi hivyo! NO MORE POLITICS!
Ili utazame jambo kwa mapana zaidi, ni lazima UJIKATAE kwanza. Usifungwe na chochote, isiwe chama, dini, rangi ama taifa.
Mada nzuri, tupo pamoja.....
"a4afrika" Mungu wetu anaita sasa!
 
Communist, hoja yako unaelekeza kwangu ama? Kama ndio,ielekeze kwa mzee mtei ambae alitofautiana na mwalimu pale mwalimu alipogomea hawa watu kwa kusema kwamba tangu lini IMF stands for International Ministry of Finance? Nyerere hakutaka kulazimishwa kokopa kwa masharti ambayo yangedumaza nchi, na sehemu kubwa ya hoja ya Mwalimu tunaona ukweli wake leo;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Wakuu,

Nimewasoma vyema na hoja zenu ni nzuri sana zina changamoto kubwa sn kwa wale amabao ni waelewa.

Mchambuzi na Highlander mna hoja za msingi.

Mchambuzi una hoja ya msingi:- Ya kuwa kweli waandishi wa habari watumie muda wao huu sasa nao kumuhoji Mzee wetu Mtei atuambia mazuri na mapungufu kwa uchumi wetu wa Tanzania wa Taifa letu hili changa livyosua sua.

Pia sikumbuki vyema wapi Mwl.Nyerere aliwaomba wananchi msamaa esp kwa lipi? Tukumbushe hapo japo kidogo
Nadhani mwaikumbuka Hotuba ya Mwl.Nyerere May Mosi 1995 Mbeya, Mwalimu alitamka wazi akisema na alikuwa akimwambia Basiri Mramba kuwa two yrs back wakubwa hawa(IMF & WorldBank)walimfuata wakamwambia Mwl watu wako hawa kusanyi kodi. Sasa at that Juncture nchi ilikuwa inaenda wapi? Je tulikubali mapendekezo ya hawa wakubwa (IMF & WorldBank) and then tukawa hatuyatekelezi maudhui yake. Yet hapo hapo Mwl alikuwa na mashaka ya dhati kabisa kuwa hawa wakubwa kweli twaweza enda nao sambamba?
Kweli Mwl hakupenda kukopa na kutumbukiza nchi pabaya nakubaliana nalo hilo nadhani sote hilo twaliona wazi ni kweli. na matokeo yake kweli ndio haya twayaona sasa.

Kwakuwa Kongamano lina kuja kuhusu Azimio la arusha basi ni vyema kuwaita hawa wachumi wetu mahiri Mzee Mtei pia nae awepo.
Ni muda muafa kasasa tuwekane wazi kwa kizazi kilichopo sasa na kijacho sasa tutangulize Taifa mbele kwanza

Wakuu Highlander, Communist na Mchambuzi nafurahishwa na kuhamasika sana na jinzi mnavyodadavua mambo, naomba mtambue kuwa mimi ni mmoja wa wapigania maendeleo wa taifa hili kwa kupeperusha vema kabisa bendera ya cdm, ila kwa faida ya wengi naomba muendelee kuchambua haya kwa kuyaunganisha na yale mema ya Azimio la Arusha.
 
Jethro,cagl,tupo pamoja; mkuu highlander, naunga mkono hoja, looking forward for an interesting discussion ambapo nina imani kwamba sote tutaibuka waelewa zaidi;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Wakuu GAGL,Mchambuzi, Communist, na Jethro , niwashukuru kwa mawazo mazuri yenye lengo la kujenga uelewa,na pengine kusaidia kuonesha njia ambayo taifa letu linatakiwa kuelekea kuanzia hapa tulipo.

Katika hoja ya msingi kwenye uzi huu, Mkuu GAGL anaonesha imani kuwa Chadema inao uwezekano wa kuleta uongozi mbadala, baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuonekana kukosa viongozi Waadilifu. Na wadau mmeonesha kukubaliana na msimamo huu, kwamba pana tatizo la Uadilifu katika namna nchi inavyoendeshwa.

Lakini Mkuu GAGL ameingiza suala la Azimo la Arusha katika hitimisho la hoja hii, kwa swali hili: "naomba kufahamishwa kuhusu msimamo wa CDM kuhusu Azimio la Arusha kwa sababu kilichopelekea nchi hii kukosa viongozi waadilifu ni kupuuza misingi ya uongozi [iliyoainishwa] katika azimio hilo. Mimi nalihitaji azimio hilo sasa sijui msimamo wa chama ninachokipenda na kutaka kujiunga kama kina msimamo huo pia. Mkuu Mchambuzi amelaumu Breton Woods Institutions kwa kuzorota kwa uadilifu katika utendaji wa viongozi wa CCM na Serikali yake.

Nafurahi tunakubaliana kwamba tatizo kubwa la uongozi katika nchi yetu ni kukosekana kwa Uadilifu. Sidhani kama IFIs zina sababu ya kubeba lawama. Nakubaliana na Mkuu Communist katika mtizamo wake huu: "IMF is just a Bank, haulazimishwi kukopa, Watafuta visingizio bana? Matajiri [wengi] wamepitia mikopo, hata makampuni ya China yalikopa. Issue kama ukakopa kuongeza mke hutaweza kulipa." Hili linaondoa hoja ya IFIs.

Tufanye nini kuleta uadilifu katika Serikali? Tutafute ufumbuzi tukijua kwa dhati kabisa kwamba tatizo ni internal--siyo external! Hili ndilo tunaitaji kulijadili. Mkuu GAGL, anaamini suluhisho lipo katika kurejesha Azimio la Arusha, na angependa urudishwaji huo wa Azimio la Arusha ufanywe kupitia CHADEMA, chama ambacho amesema anakipnda.

Chadema haiwezi kurudisha Azimio la Arusha kwa sababu hii ilikuwa sera ya TANU. Lakini sioni ubaya wa kuchukua maudhui mazuri ya Sera ile na kuya integrate katika sera zake. Kwa bahati nzuri naona vijidalili kama tayari wanafanya hili--kitu ambacho kinanipa binafsi faraja sana. Na ninaomba kumpe Mkuu GAGL faraja pia. Nimalizie kwa kurudia maneno ambayo niliyasema awali. Ni kamkeka karefu kidogo, lakini naomba jipe nguvu usome hadi mwisho:

Mkuu GAGL kachukue kadi yako ya CHADEMA.

Kitu ambacho wengi wanakitamani katika Azimio na Arusha si jina la azimio lile, bali wanatamani maudhui yake fulani-fulani mazuri kwa taifa hili. Si kila kitu katika Azimio la Arusha kilikuwa sawa. Azimio la Arusha lilikuwa na Utopia nyingi sana mule, nikianzia na dhana kwamba mtu anaweza kuacha profit motive kabisa, kitu ambacho hakiwezekani. Kumbe kilichotakiwa kuonekana katika Azimio la Arusha ilikuwa dhamira ya ku-moderate profit motive. Mataifa yaliyoendelea yanafanya hivyo. Unaruhusu profit motive kushamiri, ila unai-moderate. Sera za CHADEMA zinatafuta kutumia profit motive kujenga uchumi wa taifa, lakini profit motive moderated.

Spirit ya kujikana reasonably, (narudhia: kujikana reasonably), ilikuwapo katika Azimio la Arusha. Kutaka wengine nao wapate faida katika yanayofanyika ndani ya taifa, hili lilikuwapo. Uadilifu katika utendaji ndani ya chama na serikali, hili pia lilikuwapo katika Azimio la Arusha. Na haya yanahubiriwa na wataalam wa mahubiri ya siasa katika CHADEMA.

Mi nionavyo, kikubwa katika Azimio la Arusha kinachostahili kukienzi ni Maudhui ya uadilifu katika kulinda maslahi ya kwako--wewe mtu binafsi--lakini kwa mtizamo kwamba wewe ni sehemu ya walio wengi, hivyo kwamba unafanya kazi unayoifanya kwa niaba ya wengi; yaani kwamba umepewa jukumu la kulinda maslahi makuu ya Taifa kwa ujumla wake, badala ya kulinda maslahi binafsi kwanza mtu anapokuwa katika nafasi yoyote ile ya uongozi. Chadema wanahubiri haya. Linda maslahi ya taifa kwanza. Mengine yafuate. Kwa hiyo hata kama hawatafufua Azimio la Arusha neno kwa neno kwa sababu lilikuwa na kasoro zake pia, maudhui katika Azimio la Arusha yenye nia njema kwa taifa tayari wanayahubiri.

Kwa maana hiyo, kama wewe ni mpenzi wa Azimio la Arusha, nina hakika utakuwa unalipenda Azimio lile kwa sababu ya maudhui yake mema. Maudhui ya uadilifu, maudhui ya kulinda masalahi makuu ya taifa kwa ujumla wake; kulinda maslahi ya Taifa kwanza kabla ya kulinda maslahi binafsi mtu anapokuwa katika nafasi yoyote ile ya uongozi. Haya Chadema inahubiri tayari na kwa kiasi kikubwa wanajitahidi kutekeleza mahubiri yao wao binafsi. Nilisikia John Mnyika anatembelea 'Vitz kobe' ndogo badala ya Prado. Niliipenda sana hii!

Wale unaosikia wamekiacha CHADEMA na kurudi CCM ni wale ambao walienda CHADEMA kutafuta ajira; wale ambao walienda kule kutafuta mianya ya utajirisho, wakidhani CHADEMA ni kama CCM. Walipokuta pale kuna kujitolea kwingi sana wakaona hapafai na kurudi kule ambako siasa malengo yake ni ajira ya utajirisho kwa hela halali na haramu. CHADEMA inatekeleza maudhui mema ya Azimio la Arusha nionavyo mimi. Hawawezi kutekeleza kila kilichokuwapo katika Azimio la Arusha kwa sababu si kila kitu kilikuwa sawa mule. Mengine hayakuwa sawa wakati ule, hayawezi kuwa sawa leo. Lakini pia Azimio la Arusha ilikuwa sera ya TANU. Chadema si TANU, japo inaweza ikawa KAMA TANU katika mambo fulanifulani. Huwezi kuzaa mtoto akafanana na wewe kwa kiiiiila kitu. Yapo mengine yatakuwa ya kwake yeye kama yeye.

Kachukue kadi mkuu. Ingia kwenye vita ya kurudisha heshima ya nchi yetu na utajiri wake mikononi mwetu. Go!
 
Mi nafikiri wanaoisifia IMF na Benki ya dunia wangetutajia angalau nchi zilizoweza kujikwamua kiuchumi kutokana na kufata mapendekezo yao tumekuwa tukizungumzia nchi za asia ambazo miaka ya 60 tulikuwa kiwango kimoja cha uchumi lakini leo hii zina nguvu kubwa za kiuchumi zilitumia mbinu gani lakini kuna nchi kama Libya,Irak na venezuela au China ambazo wamepata mafanikio makubwa kiuchumi je walikopa au kufata masharti ya IMF kwa kifupi azimio la arusha na azimio la irak ni mojawapo ya mikakati mizuri ya kiuchumi duniani wakati Irak walifanikiwa Hugo Chavez siku zote alijisifu mafanikio yake kiuchumi yalitokana na kufata azimio la arusha tunapoudhuria kongamano la jtano tunapaswa kujiuliza pamoja na mambo mazuri ya azimio la arusha kwanini halikufanikiwa
 
Kabla sijaigusia CDM na AA, binafsi naona mambo mawili ambayo watanzania yanatusumbua!
1. Tunatambua na kuamini fika kuwa UADILIFU katika uongozi ni nguzo bora kabisa kwa ustawi wa taifa lolote! Lakini hatutaki kukubaliana na GHARAMA halisi za huo UADILIFU. Ndio maana wengi(wanafiki) watasema Uadilifu uliojengwa na AA ni SAWA, lakini kanuni/miiko ya AA ni marufuku! Tunathubutu kusema eti tuishi maudhui ya AA tu, tangu lini FANI na MAUDHUI vikatengwa? Hapa linaibuka jambo la pili.
2. Watz wengi Hatutambui mafungamano yaliyopo katika siasa, tamaduni na uchumi. Hili linatufanya TUSHINDWE KU-RELATE siasa zetu na uchumi wetu na tamaduni zetu! Yaani tunataka asali lakini hatutaki kufuga nyuki. Ni Ulimbukeni. Ni wazi kuwa kama sera za uchumi zinakinzana na za siasa ama utamaduni, hapo ni maumivu tu ni lazima kutokee mgongano utakaowaumiza raia, hasa wa kawaida.
Hayo mambo mawili ni baadhi kati ya yaliyowakuta wale walioshadadia kuvunjwa kwa AA, na yananifanya niamini wazi kabisa kuwa, wote walioshiriki kuua AA hawakutumia akili zao binafsi, walikubali kushikiwa akili na nguruwe weupe! Ni kosa lao na Mungu atawalaani milele! Hawa walikubali kurubuniwa kwa maneno matamu ya HAKI, UHURU, DEMOKRASIA, nao wakasema NDIO, pasi kuangalia mazingira yetu, imani zetu, watu wetu, n.k wakakurupuka tu na kuanza kudai Soko huria! Leo wameshndwa wanataka kuturubuni eti ni RUSHWA. Swali, kwanini hamkuchunguza kuona aina ya watu ambao mlipanga kuwapa sera zenu mfu na kujua watazipokeaje na mjipange namna ya kuwakabili? Mwenye akili(foreseer) angekuwa ameshaona Rushwa kabla ya kutushinikiza. Kigezo cha kiwango cha elimu to our degree of political consciousness tu, kingetosha kuiona Rushwa ya leo miaka kenda nyuma, matokeo yake mkaburuzwa tu kisa IMF wamesema mkatuingiza shimoni. Pumbavu!
Walioandaa AA hawakuwa wapumbavu KUMFUNGA mtanzania, waliona wazi kabisa kuwa kulingana na viwango vyetu vya elimu, historia yetu, imani zetu, mazoe, hali yetu ya kiuchumi, mitazamo yetu, n.k. ni lazima TUFUNGWE kujenga UADILIFU si katika uongozi tu bali katika maisha yetu yote kwa ujumla(kwa raia wote). Nawalaumu wana AA kwa kulegeza baadhi za vifungo, vilivyotoa mianya ya usaliti wa wanafiki.
Mkuu Mchambuzi@ anasema IMF intervention ilikuja kihole sana, ni kweli. Lakini si bahati mbaya, WALIKUSUDIA HILO, ndio maana werevu(pro-AA) waliona hlo na walipinga. Wenzetu wakafumba macho wasione HILA ZA WAZI za IMF&World Bank. Matokeo yake ndio haya Masikini hana chake tena leo! Then wanajiita wakombozi.
CDM na AA:
Mimi naamini kabisa AZ ni uozo tupu, na chochote kitokacho humo! Ilikuwako AA, ikazaliwa AZ ikaua AA na miiko yake yote, AZ(uozo) ukatoa funye mkubwa anaitwa Demokrasia mama wa uvundo wote wa leo. Kusingekuwa na CCM hii wala CDM kama uozo huu usingekuwepo. Kamwe mzoga hauwezi kutoa kimfaacho mtu kula. CDM kama ilivyo CCM inaongozwa na kufungwa na kanuni na taratibu za mzoga huo (AZ)
Kilichokuwa ndani ya Azimio la Arusha ni IMANI thabiti. Kamwe haiwezekani kuiishi nusunusu, kama moto moto ama baridi baridi. Adui wa kwanza wa imani hiyo, ndio msingi wa CDM na CCM ya leo!
a4afrika.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom