Nini msimamo wa CHADEMA kuhusu Azimio la Arusha?

Nini msimamo wa CHADEMA kuhusu Azimio la Arusha?

Katiba ya CHADEMA umeisoma na kuielewa ? Ama, unataraji nani akueleze kuhusu hili? Kwa uhakika wa uimara wetu, kama taifa, misingi ya Azimio la Arusha haikwepeki; hivyo, naamini CHADEMA pia hawapingani nayo.

Asante sana Mkuu. Penye blue panakubalika sana. Mimi nilikuwa natumia maneno MAUDHUI MEMA kukubaliana nawe.
 
Katiba ya CHADEMA umeisoma na kuielewa ? Ama, unataraji nani akueleze kuhusu hili? Kwa uhakika wa uimara wetu, kama taifa, misingi ya Azimio la Arusha haikwepeki; hivyo, naamini CHADEMA pia hawapingani nayo.

Mkuu wangu, kuweka misingi kwenye katiba haitoshi. Hata CCM wanayo baadhi ya misingi hiyo lakini ndio hii CCM tunayoiona leo, ambayo imejenga thamani ya MTU kuwa KITU chake na si UTU wake. Matokeo yake, ni vita ya kupigani KITU-HULKA-KUPIGANIA UKUU/KUJIKWEZA kila ldo. Muhimu hapa, ni kupima FIKRA kuu za hivi vyama kama zinaweza kutufikisha kwenye hayo mazuri wanayoyahubiri kwenye katiba labda ama sera zao! Tunachokubaliana ni kuwa AZ ni uharo, na CCM ya leo na CDM wamezaliwa humo! TAFAKARI CHUKUA HATUA MKUU WANGU.
Wewe binafsi una nafasi muhimu katika kuleta Ukombozi kuliko hizo katiba za vyama vyenu! Kamwe MANTIKI haiwezi kukiukwa na ikatuacha salama!
Mkuu Highlander, naona ulikwepa kunijibu post yangu uliyodai nivute subira, kuhusu FAIDA na nikasubiri siku nzima! Uliporudi hukuijibu, nimekuwekea bandiko jingine, umeamua kujibu vioja badala ya hoja! Nadhani ulikuja na misimamo yako ambayo uliapa kutoivunja! Nachokushuru, umenipa nafasi ya kuyaandika mengi. Wapo watakaosoma!
Mungu wetu anaita sasa!
 
Last edited by a moderator:

JingalaFalsafa, Mchambuzi, Kijakazi, Gideon Jeremiah na wadau wengine, achaneni na Ujamaa ndugu zangu.; hiyo ni ndoto ya ndaria. Mkuu JingalaFalsafa umesomeka kama vile unataka kunikatia tamaa kwenye mjadala huu. Naomba usinikatie tamaa.

Ni kweli nina vipolo kama viwili vitatu hivi kwenye huu uzi. Hili la FAIDA naona utakuwa umesahau tu; nilikwambia umejichanganya katika tafsiri yako ya FAIDA na UTU. Wewe unaona ndo kitu kilekile, kumbe sisi tulio kwenye Soko Huriu tuna kitu kinaitwa Social Responsibilty. Soko Huria lina namna yake ya kuhudumia walio katika shida. Na kuna njia zaidi ya moja. Si kama hatutambui jukumu hilo. Social Responsibility na njia zote nyingine zenye lengo la kutambua wasiojiweza, ikiwa ni pamoja na Price Discrimination, ni sehemu ya ku-rationalize HAKI ya wanadamu wenzetu walio katika mazingira magumu kwanza kuendelea kuwa Hai, lakini pia kuona faida ya huduma tunazotoa. Biashara zote zenye uelewa mzuri wa neno biashara zinaanzishwa duniani kwa lengo la kuhudumia jamii; siyo kuinyonya jamii. Wanaoanzisha biashara kunyonya watu biashara zao zinakufa. Wanaoanzisha biashara kuhudumia jamii biashara zao zinadumu milele. Binadamu si mjinga kama vile nyie Wajamaa mnavyotaka kutuamisha. Biashara zinashamiri kwa ridhaa ya soko. Na ridhaa hiyo inaletwa kwa sababu biashara ina HUDUMIA binadamu.

UPO sawa katika jambo moja lakini: Ni kweli wanadamu hatuwezi kuishi pasipo kutegemeana. Kwa hiyo kumgawia ziada jirani yako ni kitu muhimu. Sera za Kibepari zinalijua hili ndio maana wanaanzisha kitu kinaitwa Social Responsibility. Ni kwa njia hiyo na nyingine more creative ubepari unarudisha Ziada kwa wahitaji. Inaitwa Social Responsibility. Ujamaa unatafuta kufanya Social Responsibilty pasipo mkakati mzuri wa Kuzalisha. Soko Huria linatafuta kufanya Social Responsibilty baada ya faida inayopatikana katika Mkakati mzuri wa Uzalishaji. Hebu fuatilia Nyendo za Mjasiriamali Reginald Mengi, au hata Bakhresa. Hivi kweli wewe hujasikia hata siku moja watu hawa wamesaidia watu wenye shida? Ndiyo social responsibility hiyo sasa ninakuambia habari zake.

Kwa hiyo, hata sisi watu wa IMF unaotuchamba sana tuna namna yetu ya kusaidia binadamu wenzetu waendelee kuishi. Hiyo ya Kina Mengi na Bakhresa ni direct contribution. Katika Economics kuna kitu wanaita "trickle down theory." Hii nayo ni njia nyingine wasio nacho wanapata kitu kutokana kazi nzuri ya Soko Huria--hata kama si direct, na kwamba huwa msaada huo unakuja polepole sana. Misaada kwa mabilioni ambayo mimi na wewe tumepata kutoka Marekani, Sweden, Uingereza na kwingineko ulaya miaka yote hii imeletwa kutokana fedha ya ziada kutoka kwa hawa watu wa IMF usiowataka sana hapa. Asilimia 40% bajeti ya Serikali yako inaendeshwa kwa fedha za hawa watu. Tunayo namna yetu ya kusaidia binadamu wenzetu. Achana na Ujamaa; ndoto ya ndaria hiyo; sera ya njaa hiyo....
 
Back
Top Bottom