Highlander
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 3,093
- 1,077
Hata 2015 pia utasema tumwache Bw.Kikwete na ufisadi wake kwani matatizo yaliyotokea huko nyuma yanaelezeka tumwache mzee Bw. JK ajipumzishie Bagamoyo!
mmh! pagumu hapo. ngoja kwanza niwaze
Hata 2015 pia utasema tumwache Bw.Kikwete na ufisadi wake kwani matatizo yaliyotokea huko nyuma yanaelezeka tumwache mzee Bw. JK ajipumzishie Bagamoyo!
Kijakazi,
Umeliweka vizuri, na inakuwa kama vile edwin mtei na highlander ni mtu yule yule, if not mtu close to him aliyepo hapa kwa kazi maalum;
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Highlander,
Bandiko lako nadhani namba 80 has revealed wapi kuna major weakness katika mtazamo wako wa masuala ya uchumi katika muktadha wa taifa letu, lakini pia dunia ya tatu kwa ujumla:
Kwanza, it shows unasahau kwamba as of 1961, adui mkubwa wa maendeleo were umaskini,ujinga na maradhi; miaka 52 baadae, adui ni walewale; sasa tofauti na chini ya AR ambapo kulikuwa sio tu na good governance, pia there was good government; a good gvnt which aspires and provide basic social services such as education and healthcare, and once upon a time (ujamaa) serikali declared wazi na kwa vitendo hawa ndio maadui watatu wa maendeleo na kuelekeza vita huko;
Its not correct kusema we failed solely due to internal reasons,kwani kulikuwa na sababu za nje pia na nilijadili; sababu kubwa internaly were - serikali kuwa over burdened na utoaji wa huduma za kijamii na inherent weakness ya mfumo wa uchumi wetu wa produce what we don't consume and consume what we don't produce; masuala ya rushwa na poor management did not override sababu hizo hapo juu - internally; Leo hii, bado katika uchumi unaousifia, maadui watatu ni walewale tena in harshier conditions, do you know why? Its because of my next point juu ya uelewa wako mdogo wa mambo haya na ni kama ifuatavyo:
IFIs na wafuasi wao nchini wakati ule waliona njia sahihi kwenda mbele is by puting poverty, diseases and ignorance in the hands of the markets, not the state;huu ni ujuha! Wakatuambia eti the state has no business in the provision of thingns like education and healthcare, that's the business of the market and the state should just provide AN ENABLING ENVIRONMENT for businesses to do business in ignorance, poverty and diseases; mimi kuendelea kukufafanulia hapa juu ya hili nadhani ni kukupotezea tu muda kwani umeshaamua kuangalia tatizo based on internal orientation huku ukijadili mbadala based on external orientation;what a fallacy in your line of argument!!!
Pili hauna uelewa juu ya dhana ya market failures and how those were avoided in succesful cases kama thailand,singapore south korea, taiwan and to an extent brazil kwa state kuwa mstari wa mbele in planning, protectionism,infrastructure, import licensing, exchange rate controls, quotas, wage cntrols na gvnt direct investments in key sectors of the economy;haya yote were done under ujamaa na ilitakiwa tupewe stimulus package after we got hit by the 1978-9 crisis ambayo chanzo was EXTERNAL, sio INTERNAL; tuliumia internally kwa sababu kadhaa as I discussed earlier but sababu hizi hazikuwa the basic reasons why we got hit; mwalimu akaomba stimulus package, IFIs na washauri na marafiki zao "nchini" waka side with reforms ambazo ndio zimetuangamiza na zinazidi kuangamiza majority of Tanzanians leo;
Muhimu
Unaunga mkono kanuni za kiuchumi kwamba ni za kisayansi bila ya kujua kwamba ingawa most claims are grounded in economic theory, many claims rest on numerous assumptions that more often than not do not hold ESPECIALLY IN POOR COUNTRIES like Tanzania...
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Dah! Simu yangu inaniangusha vya kutosha! Naona nipo nyuma sana, lakini naomba niweke hili.
1. Mkuu Highlander, hakuna aliyekataa nafasi ya UHUJUMU/UFISADI/RUSHWA katika unyonge wetu! Hilo liko wazi! Yapo madhaifu yetu ya ndani ambayo yanafanya tuwe wasaliti wa harakati za kujenga Taifa. Lakini AA lilitushughulikia inavyostahili kuvunja mazaifu(UBINAFSI) hayo! Tulifungwa na Kusimamiwa na miiko thabiti tuichukie rushwa! IMF kupitia AZ wakaja kuua AA, wakatuingizia sera mpya zilizofungua mianya mikubwa ya Rushwa! Wapi unakoshindwa kuelewa Mkuu wangu? Mbona ndicho unachoambiwa lakini unakataa?
2. Dhana ya USAWA na HAKI: (a) Usawa katika misingi ya UTU wa mtu mweusi, si pasu kwa pasu! Kama una 2 na hitaji lako 1, nami nina 3 na hitaji langu ni 4 with reasonable qualities, MANTIKI ni kunipa hiyo 1 yako, na huo ndio UTU! Hivyo kumbe USAWA kwa misingi ya UTU wa mtu mweusi ni KUFIKIRIANA. Kupata reasonable gawio si pasu kwa pasu! USAWA under HULKA za wapumbavu nguruwe weupe wa magharibi tena mahayawani wakubwa, ni Free Competition bila kujali sifa za unaowashindanisha. HURIA! Wako tayari kumshindanisha mbio swala na kobe! Wanaita an equal opportunity kumbe ni same opportunity. Wapumbavu! (b) Katika misingi ya UTU wa mtu mweusi, HAKI yako ni kujilinda wewe! Sasa kwa vile siishi peke yangu jangwani ama msituni, ipo jamii ya watu ambayo siwezi kuikwepa kufungamana nayo, ni wazi kuwa siwezi kuwa salama kama jamii yangu haitakuwa salama, hivyo basi ninapaswa kuilinda jamii ili inilinde. Kumbe, haki yangu Kuu na ya Kwanza ni ni KUTEKELEZA WAJIBU WANGU KATIKA JAMII. Haki ni Kutekeza Wajibu! Kabla hatujakupa Haki yako, tutakuuliza kwanza kama umeshatekeleza wajibu wako! Kama laa, unastahili hata kunyimwa nafasi yako ya kufungamana nasi duniani! Kumbe basi USAWA unazaa HAKI siku zote.
3. Mkuu, hakuna anayesema humu kuwa AA libebwe tu zimazima. Tunachotaka lifanyiwe maboresho kwani sehemu yake kubwa ni bora kuliko uozo.
4. Mkuu wangu Highlander, naona unajaribu kula matapishi yako. Unadai AA halifai kwani halikubaliani na malengo ya Siasa zilizopo. Kwanza nakubaliana na hilo! Kwanini unataka AA likubaliane na siasa zilizopo? Je, si hizi ulizoziita ZIMECHAKACHULIWA? Au umesahau? Unaogopa nini kukubaliana na ukweli? Pia nikuambie tu kuwa hata AA ilitamka kujenga taifa katika demokrasia, lakini si hii iliyopo ambayo CCM ya leo na CDM wanaisujudu na wewe mwenyewe umekiri kwamba IMECHAKACHULIWA. Ndio maana nasema kuna umuhimu wa wao kujikataa.
5. Unanifurahisha sana unaposema "nina uhakika CDM itafanya ......." uhakika huo unautoa wapi Mkuu?
6. "Mungu hakupanga watu wawe sawa, ndio maana akagawa vipawa tofauti tofauti" SI KWELI na nitakwambia kwanini! Usawa si KUFANANA, nimetamka kuwa Usawa ni KUFIKIRIANA, ni kupata reasonable gawio lako katika jamii. Usawa ni kufikiriana ili kufikia faida ya maisha ambayo ni SUSTAINABILITY. Nitakupa mfano mdogo...fikiria kama itokee wote tuwe wanaume, binadamu angefutika duniani. Lakini uwepo wa KE na ME umetufanya tuwe endelevu. Uendelevu wetu unasimamiwa na MAHUSIANO yetu, mahusihano yetu ni lazima yawe yenye KUFIKIRIANA ili kuifanya dunia nzuri. Ndio maana ikitokea mwanaume kamtelekeza mke na wanae, tunashangaa!
7. Mkuu wangu unapong'ang'ania kuwa IMF imeleta Usawa wakati walijua kabisa hatuna mtaji wa kutosha, hatuna teknolojia,n.k lakini bado wakang'ang'aniza tushindane nao sokoni. We uhoni bado ni HILA umeng'ang'ana na Rushwa. Eti fursa sawa!
8. UNIVERSAL Dec. Of Human Rights-1948. Hiki kumbe ndicho kinachokufumba macho! USIDANGANYIKE mkuu, hicho ni KIINI MACHO. Ninarudia tena, HUMAN RIGHTS ni KIINI MACHO. Uwezo unao, jikane kwanza kisha zitafakari utaona hilo. Hao ndio wanaodai Faida ni ziada kwa muuzaji na mridhiko kwa mnunuzi. Chonde Mkuu wangu usimfundishe hivyo mwanao.
(9) Mkuu kumbe unaelewa kuwa, tofauti zetu zilileta mafarakano. So HAKI ikagunduliwa kuepusha hayo mafarakano. Kwanini hujiulizi leo mbona HAKI hiyohyo imekuwa mstari wa mbele kuzua hayo mafarakano? Ujagundua tu kuwa HAKI inayohubiriwa leo si hiyo waliyolenga wazee wetu? Nitakupa mfano! "Nimezaliwa Osterbay, St. Marry's to Oxford. Sijawahi kukosa dawa wala chakula nilipohitaji, wala usingizi wala starehe. Leo nina jumba la kifahari, magari lukuki uwani ya kutembelea. Nimeoa na wototo. Wewe ni jirani yangu. Umezaliwa Manzese, lipotakiwa kuwa shule mama yako alikuchukua kwenda nawe sokoni kumsaidia kuuza miguu ya kuku kwa msikini wenzenu. Hujawah kula wala kutibiwa ama kulalala kwa wakati, kuvaa inavyostahili. Umeoa leo, una watoto 5. Umejenga kabanda kako ka maboksi pembeni yangu. Leo umeamka mgonjwa, mwanao wa mgongoni naye. Wa4 na wa3 wanagaa njaa uwanjani. Wakwanza amemchukua wa2 wako stendi wakibeba mizgo ya abria, japo walitakiwa kuwa shule. Unanifuata kuniomba msaada. Eti nina uhuru wa kukupa ama nisikupe. Haki ya kutumia changu nipendavyo. NINAKUNYIMA, unaondoka. Jioni na panga lako waja niibia stoo, nakupiga risasi unakufa. Jambazi lauliwa na jamii haijali. Ndio haki hyo mkuu? UTU/MANTIKI JE?
Anaita sasa!
Jingalafalsafa,
bandiko #90 umenena yote mkuu; inasikitisha sana kuona watanzania wa hulka ya highlander wanaabudu IMF ambao walikuja kumtusi mwalimu kwa kufanyia biashara ignorance and diseases; shame on them and together tutawashinda watanzania walionunulika kwa kujua na kutojijua; hakika mungu anaita;
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Highlander, wakati nasubiri your response kwa swali langu hapo juu, naomba nisema pia yafuatayo: Kwa kweli historia ina tabia ya kujirudia lakini sio lazima ikaja na matokeo yale yale, leo inaweza kuwa baraka, ikijirudia kesho inaweza kuja na matokeo balaa; Nikiingia moja kwa moja kwa hao unaowaumini na uliberali wao kwamba ndio wakombozi, waje kutusaidia na sera zao za kuvutia wawekezaji n.k, historia ya wakati huu imejirudia na kuleta balaa; nitafafanua: Hoja kwamba jukumu la serikali katika uchumi is to create an enabling environment ni hoja ya muda mrefu sana; hoja hii ilikuja kwa mara ya kwanza mara baada ya uhuru; tuliambiwa na wakubwa wa huko nje unaowasujudia leo kwamba - the problem and the explanation of our economic backwardness and poverty ilikuwa ni uhaba wa MITAJI yani capital; lakini tulikuwa na nguvu kazi ya kumwaga yani plenty or abundant labour; wakasema kwamba, ili tuendelee, ni lazima tukaribishe na ku import mitaji; pia ili mambo yawe safi, ni lazima tuweke the neccessary incentives kama misamaha ya kodi, easy repatriation of profits kwenda nje, sheria kali za ajira kuweka nidhamu viwandani na makazini n.k; yote hayo yakatekelezwa miaka ua mwanzo kabisa ya uhuru, kwa mfano moja ya miswada ya mwanzo kabisa ya bunge chini ya serikali ya TANU baada ya uhuru ilikuwa ni foreign investmenst protection act (1962) pamoja na preventibe detection act mwaka huo huo; pia sheria mbalimbali on trade unions and anti strike zikaletwa; Highlander na waumini wote wa IMF, pamoja na yote haya, foreign investors hawakuja sana kwani kufikia mwaka 1967 mwaka wa AR kuzaliwa, kulikuwa na very little inflow ya FDI tanzania; cha ajabu ni kwamba uwekezaji kutoka nje ukaanza kwa kasi mara tu azimio la arusha lilipotangazwa pale mwanzoni; Okay - miaka ya sitini na sabini tukapitia tukapitia combination mbalimbali za import substitution and export orientation strategies za industralization kupitia state capital huku kidogo pia sekta binagsi ikichangia, huku mikopo ya wahisani wa nje na private management contracts nazo zikichangia katika mchakato huu; miradi mingi ya namna hii ikafa, partly kutokana na mismanagement, partly hujuma za waliopewa jukumu kuendesha uchumi kwa kula njama na ma--------- wa nchi na mabepari wa nje;tukiachana na hilo, kama nilivyojadili awali,katika mchakato huu, mass goods industries kama nguo, food processing, ngozi, oil etc were established with formidable success; na kwa taarifa yako, viwanda hivi havikutegemea FDI bali kodi za wakulima na wafanyakazi; Sasa tukija kwenye miungu yako IMF na WB waliokuja kwa kulazimisha tu reform na kuchukua mikopo yenye masharti nafuu huku wakikataa option given na mwalimu kutupa mikopo to bail out viwanda vyetu ambavyo bado vingeweza fufuka na kuendelea under the same approach kama ya kwao sasa huko marekani with general motors etc na pia huko eurozone, wakakataa kabisa na kulazimisha liberalization, marketization na privatization; wewe unajadili eti tatizo ilikuwa in psrc, inaonyesha uelewi kabisa kilichotokea; Sasa swali kwako - kwanini ujamaa ulileta viwanda vyenye kutoa faida na pia ajira na hivi vilihitaji tu a bail out and wake up, kwanini ujamaa led to industrilization but hao miungu wako have led to de-industrilization hadi leo? Hiyo faida ya IMF kwa wakulima na wafanyakazi unayoishabikia kwa mbwembwe ipo wapi? Kwani viwanda hivi very useful vikaenda na maji chini ya IMF and WB close supervision, na wewe unathubutu eti kusema ni psrc ndio walihusika; hivi unaelewa politics zilizozaa psrc? Na unajua IFIs walitaka psrc ifanye nini kama sehemu ya AID conditionality??? Its such a coincidence kwamba mzee kahama ndiye alikuwa mkubwa wa kwanza wa NDC kusimamia ujenzi wa viwanda na miaka 30 baadae akapewa tena ukubwa - mtu wa kwanza kupewa kazi to de-industrilize our economy in the 90s under IPC - investment promotion centre which now is TIC; Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Jingalafalsafa, bandiko #90 umenena yote mkuu; inasikitisha sana kuona watanzania wa hulka ya highlander wanaabudu IMF ambao walikuja kumtusi mwalimu kwa kufanyia biashara ignorance and diseases; shame on them and together tutawashinda watanzania walionunulika kwa kujua na kutojijua; hakika mungu anaita; Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Tarat-i-i-i-bu, Tarat-i-i-i-bu Wakuu Mchambuzi na JingalaFalsafa. Sijui kama mnaelewa lakini, kwamba "you are beating a dead horse". Ujamaa hautakaa urudi tena hapa ujue! Watanzania wenye hulka ya Highlander wapo kibao. Hapa kilichobakia ni kuwakabidhi tu wanaouelewa vizuri Uchumi wa aina hii wau-manage. Na ninakuapieni kwa jina la Mtume Mohammad (SAW), na Yesu , Na Mungu Mwenyezi, wote watatu. Hii nchi itakuwa mahali pazuri kuishi. Na sababu itakuwa SI kurudi kwa Ujamaa, bali usimamizi mzuri, usimamizi adilifu, wa Sera za Soko Huria. Hizo sera za IMF na World Bank ambazo nyie wawili mnaziponda ndo hizo hizo mkombozi wa chumi zote duniani. Hizi ndo sera zimeleta Shule binafsi ambazo zinaongoza kwa ubora wa elimu Tanzania, ndo zimeleta Maduka yaliyosheheni vitu kila mahali hadi vijijini, ndo zimeleta Hospitali binafsi zilizopunguza mzigo kwenye hospitali za serikali kusikokuwapo dawa. The list is endless. Utafanya nini na Ujamaa ambacho sekta binafsi imeshindwa. Embu acheni hizo bwana....Asante Mkuu wangu Mchambuzi. Hakika sauti ipo, inaita kwa sauti kuu! Ni sauti ya Mungu wetu aliye haia. Ninashukuru kwani mpo ambao mnaisikia pia! Heshima kwako Mkuu wangu! Pamoja sana!
....Mwanzoni niliamua kujiita Mbumbumbu/Mjinga wa Falsafa. Ni kwa sababu sikubaliani na kile kinachotetewa leo, kwangu ni UBATILI ndio maana hauachi kujenga visa, chuki na visasi kila leo. Kinachoitwa DHAHANIA leo, ndio hicho nachoamini kinaweza kuvunja hvyo visa na visasi!
WALA HUNA UMBUMBUMBU WOWOTE...WE MI NSHAKUJUA; UCHOKONOZI HASA NDO SHIDA YAKO.... HEBU NIKUSIKILIZE KWANZA....
Mkuu wangu, licha ya kukuambia kwa mifano lakini bado eti unahoji kuna uhalali gani wa wewe kunipa ziada yako?
NIKUPE ZIADA? ILI WEWE UWE UNAAMKA SAA TANO ASUBUHI AU?
Embu niambie ukweli, umekosa kabisa kuona MANTIKI yoyote kwenye mfano wa Ostebay na Manzese? Mkuu wangu Highlander nimetumia neno "REASONABLE GAWIO" reasonable! Bado unahoji kuna uhalali gani? Kuna kauli aliitoa Marx naipenda sana "From Each According to his Needs to Each According to His Needs" hiyo ndio Reasonability nayosemea!
ACHANA NA MARX KAPITWA NA WAKATI HUYO... ETI "From Each According to his Needs to Each According to His Needs". GEUZA HII ISOMEKE HIVI: "From sweat each according to His Needs." MARX ALIKUWA BABA WA UVIVU NA UTEGAJI KAZI, NDO MAANA SERA ZAKE ZIMEVUNJWA KABISA HATA KWAO.
unapong'ang'ania tutajenga wavivu, wakati nimekuambia kabisa kutegea kazi ni moja ya matendo ya HULKA/ID/UBINAFSI ambayo yanapaswa KUFUNGWA na kila kitu chetu, yaani aina ya uchumi wetu, aina ya siasa zetu na aina ya tamaduni zetu zinapaswa KUMFUNGA MWANADAMU KUTOTUMIA HULKA ZAKE BALI MANTIKI ambayo mimi naita UTU. Huwezi kupiga hatua yoyote mbele kama utaacha huru HULKA za watu. Wewe mwenyewe ni shahidi na umetamka hilo kwa kuwahusisha viongozi wa leo na kutokomaa kwa ID zao to Super Ego! Kwanini mnapenda pepo wakati mnaogopa kifo? NI LAZIMA TUFUNGWE. Nilishasema mwanzo, Watanzania wengi hatujui wala hatukubaliani na GHARAMA halisi za Ustawi wetu, ndio maana tunaburuzwa na wezi wanasiasa na mabwana zao kutoka nje! Niambie kama uhoni MANTIKI yoyote ya nilichokiandika!
KIFUNGO HAPA NI IMF TU. UKISHAWEKA IMF UMESHAFUNGA KILA KITU.... ALAMSIKI!
Mungu wetu anaita sasa!
"Maisha ni Furaha...kama haipo ni UPUUZI mkubwa. Na hakuna Furaha ya MTU binafsi bali WATU" Zingatia maneno hayo! Kwakuwa tumeandika hapa, mwanao atasoma na atahukumu kilichomo! Kila la heri Mkuu!
Mungu wetu yu tayari kutushindia vitani. Anaita sasa!