Nini msimamo wa CHADEMA kuhusu Azimio la Arusha?

Nini msimamo wa CHADEMA kuhusu Azimio la Arusha?

Niwaombe radhi Mkuu Mchambuzi, Mkuu JingalaFalsafa na wadau wengine katika uzi huu kwa mambo mawili: Kuna bandiko limejenga picha mimi Highlander naegemea upande wa Chama fulani cha siasa hapa nchini. Taswira hii kama imeanza kujitokeza naomba mnisamehe kwa sababu hiyo taswira si sahihi; taswira hiyo ni co-incidental kabisa. Siongei kwa niaba ya chama chochote cha siasa! Maneno yote ambayo nimeyasema kwenye uzi huu ni ya kwangu mimi binafsi kama Highlander. Ni views personal and personal only .

Pili, Mkuu Mchambuzi, na Mkuu JingalaFalsafa mtakumbuka tumetoka mbali katika mjadala huu. leo kuna mabandiko mumeyaweka hapa yanahitaji umakini kuyajibu. Naomba mnisamehe nitachelewa kidogo kuyajadili. Kuna changamoto ya takwimu ambazo Mkuu Mchambuzi kazileta, pia kuna changamoto ya Ethical Morality katika biashara kutoka kwa Mkuu JingalaFalsafa ambayo kaichanganya na concept ya profit motive. Nitachelewa kidogo kuzijibu hoja hizi lakini nina mpango wa kuweka mchango kwenye hoja zenu. Ila sasa nikubaliane na Mkuu JingalaFalsafa kwamba Mungu wetu anaita sasa. Tutafika pazuri!

Mungu wetu anaita sasa! Asante Mkuu wangu Highlander. Kila la heri. Tuko pamoja.
 
Last edited by a moderator:
Marafiki zangu Mchambuzi, JingalaFalsafa, kmbwembwe na wadau wengine katika uzi huu, tunalo tatizo la kujua tofauti zilizopo kati ya maneno haya mawili: Usawa na Haki. Nagawa bandiko hili katika sura mbili: Sura ya kwanza inayohusu Neno Usawa na Neno Haki, na sura ya pili katika bandiko tofauti kueleza kwa nini Rushwa inadumaza uchumi na kupunguza kiwango cha mafanikio ya sera za Soko Huria ambazo wadau mnasema ni za IMF na World Bank , na ni hila za kuharibu uchumi wetu.

Usipoweza kujua tofauti ya maneno haya mawili, Usawa na Haki, huwezi kujua kwa nini Chadema haiwezi—na pengine haina hata hiyo haja ya kuliiga Azimio la Arusha jumla jumla. Nimependekeza tangu mwanzo mwa uzi huu tunaweza kuchukua maudhui mema kutoka Azimio la Arusha na kuachana na takataka zingine mule. Kulibeba kama lilivyo si kitu muafaka kabisa kwa sasa. Malengo yake hayakubaliani na malengo ya siasa zilizopo sasa.

Mkuu Mchambuzi umetoa angalizo muhimu katika huu mjadala kuhusiana na matazamio ya wananchi katika Serikali inayoweza kuongozwa na Chadema—au chama kingine mbadala wa CCM for that matter.

Napenda kukubaliana nawe kwamba watu watataka kuona Ufisadi ukiisha kesho baada ya Rais wa Chadema kuapishwa--na hilo halitawezekana. Kwa hiyo ni kweli matazamio haya ya wananchi ni bomu kwa Chadema kama watapata ridhaa ya kuongoza dola 2015, 2020 au 2025. Faraja pekee ninayoiona ni kwamba Chama hiki ni makini sana.

Watatengeza Scenarios za kushughulika kero za Wananchi, watawaelimisha kuhusu scenarios hizo ambazo zitaweka ratiba zinazoeleweka katika kila tatizo watalorithi. Vipaumbele vya mwanzo kabisa nina hakika vitakuwa a). Kuondoa udini katika nchi yetu tuishi kwa amani kama zamani; b). Kuondoa au kupunguza Rushwa; c) Kujaribu kupandisha kasi ya kukua kwa uchumi kutoka hivi viwango vya asilimia 6% au 7% vipande hadi maeneo ya asilimia 10% au hata 11%--viwango ambavyo vitalazimisha mifumukoya bei kushuka sana na watu kujua taifa limetoka. Hapa Tanzania “kutoka” ni kupata mafanikio ya kiuchumi.

Rushwa iliyoimarika katika Awamu Tatu za utawala wa CCM baada ya Mwalimu Nyerere haiwezi kumalizwa katika wiki, wala katika mwaka, pengine hata miaka 10 itakuwa bado haijesha au kupungua significantly. Nakubaliana nawe kuna bomu lakini elimu na kujizatiti kutekeleza mpango kazi zile scenario utafanya hili bomu lishindwe kulipuka. Ujamaa na kujitegemea ilikuwa siasa yenye NIA NZURI: Ilitafuta watu wote wawe sawa. Na Azimio la Arusha lilitengezwa kufanikisha lengo hilo—yaani lengo la kuleta Usawa.
Mtu anayetaka watu kuishi kwa Usawa ana Nia Nzuri. Lakini haitatokea hata siku moja chini ya jua watu wote wakawa sawa. Mungu hakupanga watu kuwa sawa ndo maana akagawa vipawa, akagawa ukubwa wa mwili, akagawa uwezo wa kufikiri, na mengine mengi yenye kuleta mseto alioutaka uwepo kwa ajili yakujitukuza yeye Mungu.

Azimio la Arusha ilikuwa Sera iliyoundwa kufanikisha Nia Njema iliyoitwa Ujamaa na Kujitegemea; nia ya kuleta usawa. Siasa za Soko Huria zinakiri binadamu tumeumbwa tofauti, tuna mahitaji Fulani-fulani ambayo ni tofauti, japo yapo ambayo kwa ubinadamu wetu lazima wote tunayahitaji: kula, kuvaa, kuishi nay ale yote yanayoainishwa katika Universal Human Rights Declaration. Wanadamu walioishi miaka ya zamani walijifunza kuwa tofauti za binadamu zilizopo zilileta vita ma mifarakano katika jamii wakagundua neno HAKI. Haki si neno jepesi kama linavyoonekana.

Pande mbili au zaidi za wanadamu wasiokuwa sawa wanalazimika kukaa pamoja kuamua ni kipi katika tofauti zao ni lazima kila mmoja awe na ulazima wa kupata. Wakishakubaliana hakuna wa kumpunja mwenzake. Anayepunja wenzake anaharibu haki.
Hata kama si kwa maneno ninayoyatumia hapa, Chadema wanasema haki ya kutumia rasilimali za Taifa Tanzania kwa faida ya Watanzaia inavunjwa kwa watu kujilimbikia mali kinyume cha makubaliano (yaani kinyume cha sheria). Wala rushwa hawalitendei Haki taifa. Azimio la Arusha lilikuwa na vipengele vilivyohusu Uadilifu. Vipengele hivi vinaweza kutumika hadi hii leo kwa malengo ya sasa ya kusimamia haki. Hii ni moja ya sababu kwa nini nilishauri vitu Fulani-fulani vinaweza kuchukuliwa kutoka katika Azimio la Arusha, hata kama jina lisiwe hilo.


Kumekuwa na ujenzi wa hoja kwamba Chadema wanatekeleza elements fulani za azimio la arusha na kadhalika. Hii ni hoja nzuri na ya msingi sana, ingawa wanachama wengi wa chadema hawataki kabisa kusikia Chama chao kuhusishwa na TANU au azimio la Arusha; Mwaka jana nilianzisha mjadala kuhusiana na mfanano na utofauti baina ya TANU na Chadema; Hoja yangu ya msingi ilikuwa ni kwamba - Chadema kufananishwa na TANU is more of a political asset than a liability, huku mfananisho huo ni more of a political liability to CCM than political asset; uzi huo kama ifuatavyo:
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/325723-chadema-na-tanu-mfanano-na-tofauti.html

Nikirudi kwenye hoja ya msingi, taifa letu kwa sasa linayumba kutokana na kukosa dira na mwelekeo ambao umekuwa digested, kueleweka na kukubalika na wananchi walio wengi; Marehemu Kolimba alijadili hili kwa kina na hoja yake inazidi kuwa na mashiko leo; Wakati wa ujamaa, kama taifa, tulikuja na maazimio kuhusiana na makubaliano juu ya nini tunataka, nini hatutaki, wapi tunataka kwenda na wapi hatutaki kwenda; Maazimio yote haya yakawekwa katika document moja ambayo ndio ilizaa azimio la arusha;jina Arusha ni kutokana na wapi kikao husika kilifanyika; maana yangu hapa ni kwamba - tusiogope neno azimio wala arusha kwani bado tunahitaji kuja na maazimio kama taifa juu ya wapi tunataka kwenda na tufiikaje katika safari tunayokudusia, na kikao juu ya hilo kinaweza fanyika Pwani, Tarime, Katavi, Simanjiro n.k; Kwa maana hii, kuna umuhimu wa kurudisha nchi katika mstari kwa kuja na azimio kwa mfano la Simanjiro iwapo tutaamua kufanyia vikao hivi muhimu huko; its as simple as that; sidhani kama kuna mwanachadema yoyote ambae anakataa kwamba nchi imekosa dira na inabidi tukae chini na kuja na maazimio na maamuzi magumu juu ya wapi tunataka kupeleka nchi yetu na njia za kufika huko tutakapochagua kwenda;

Kuna umuhimu wa watanzania kuacha kukubali propaganda kwamba mmiliki wa azimio la arusha ni TANU; Ukweli ni kwamba mmiliki huyo ni mtanzania ambae kwa wakati ule alikuja kubaliana na uamuzi kwamba tuanze na mfumo wa chama kimoja kwanza ili kujenga taifa kwa ufanisi zaidi, na hivyo mtanzania huyo alikubaliana na msimamo wa chama juu ya umuhimu wa azimio la arusha kwani ilikuwa ni njia pekee ya kutekeleza ahadi za uhuru; Mwalimu hakukurupuka kuja na azimio la arusha, the situation was so tense katika jamii, na alipoenda ziarani china kuangalia wenzetu wamefanya nini, ndipo akaja na wazo la azimio la arusha; Bottom line hapa ni kwamba – mmiliki wa azimio la arusha alikuwa ni watanzania ambao leo hii baada ya mageuzi ya kisiasa, wengine ni wanachadema, wanaccm, CUF, NCCR, CCK, TLP, huku wengine wengi wakiwa hawana ushabiki wa chama chochote cha siasa; Kwahiyo hizi views kwamba Azimio la Arusha ni la TANU/CCM sio helpful, na kuna umuhimu wa kuweka mbele utaifa wetu katika hili; Iwapo Chadema mathalani wanataka kuja na manifesto ya kurudisha nchi kwenye mstari kwa mtindo wa maazimio Fulani, wajipange tu na kuchagua wapi wafanyie kikao hicho muhimu; Kikubwa ni waepuke kufanyia kikao hicho Kanda ya Kaskazini kwani Azimio la Kilimanjaro, Arusha, Manyara au Babati, hata kama litakuwa na manufaa makubwa kwa taifa, litashambuliwa kwa hoja nyingi za ovyo na wapinzani wa chadema, hasa wana CCM wasiokuwa na mapenzi na nchi yetu;
 
Mchabuzi uko sawa, ubepari uchwara haujaleta matumaini mema kwa watanzania kama ujamaa. Bado hatujapata formula au itikadi mbadala na ujamaa.





Tiba ya IMF na World Bank inafanya kazi! Kwa takwimu zilizopo, Sera za IMF na World Bank ambazo tumezitekeleza tangu 1988 hadi hii leo, zimeleta mafanikio makubwa ukilinganisha na Mafanikio ya nyuma. Tatizo kubwa ni kwamba mafanikio yana distortions (yaani pamoja na kuonekana, hayaendi ipasavyo kwa sababu msimamizi ni mwizi. Taifa lina duka. Duka lina mali kibao. Kila jioni mwenye duka (mimi na wewe) tunaoneshwa dro imejaa hela. Kuna faida, lakini faida hii si yenyewe. Huyu msimamizi wa duka tuliyemuweka kwanza ni mwizi, pili hana akili ya kuendesha duka la aina hii.




3TZ GDP.JPG


cc: kmbwembwe, Mchambuzi, JingalaFalsafa,
 

Attachments

  • TZGDP 4.JPG
    TZGDP 4.JPG
    54.7 KB · Views: 27
Is it a corruption offence to house Ministers in Hotels?

16th March, 2013

Dr. Charles Tizeba


According to available reports, recently, the government was liable to pay over Sh100 million taxpayers money to settle hotel accommodation bills for one of its officials, the Deputy Minister for Transport, Dr Charles Tizeba who should have been allocated a government house shortly after his appointment but for some reason this never was. The government decided to house Dr Tizeba at the four-star New Africa Hotel since his appointment to the post on May 4, 2012. As of January 12, 2013, the deputy minister had stayed at the hotel for at least 247 days, bringing the total bill to $61,750 (Sh98.8 million).

It appears that the government has not learnt from its past mistakes as this is not the first time this is happening. In 2011 the Corruption Tracking System (CTS) was among the first sources to report on news that a number of cabinet ministers appointed by the President shortly after the General Elections in 2010 were being housed in uphill Hotels, for what was described as inadequate government housing facilities to accommodate the new Ministers. (Refer to Ministers still accommodated in hotels-CTS-February 2011) After serious public uproar and media rebuke, the ‘Hotel Ministers’ were finally moved into their private residences but it appears this ghost came back with Dr Tizeba in 2012.

Current Issues
 
Highlander,

Unaelekeza mjadala kuzuri sana; kwa sasa naomba nijadili kidogo suala la "haki na usawa". Wanasiasa wengi wanapenda sana kutumia dhana za natural justice na equality katika kujadili jinsi gani wanaheshimu haki na usawa wa wananchi;aidha kwa makusudi au ulimbukeni wao, wanajisahau kwamba kilicho muhimu katika haki na usawa ni social justice na equality, sio natural justice na equity; upuuzi wa equality and social justice ni foundation za liberal/bourgeois political doctrines na theories of right ambazo ndio zimeangamiza mamilioni ya binadamu for centuries kutokana na utumwa, ukoloni,vita,njaa,unyonyaji n.k; right ideology ambayo msingi wake ni equal rights have been argued over and over again na wanazuoni maarufu duniani kwamba haina mashiko katika kutambua haki na usawa wa walio wengi kwani equality among unequals is inequitable; kwa ufupi, dhana za haki na usawa ambazo ndio msingi wa ujamaa kama ulivyojadili zipo much closer to dhana za justice and equity kuliko equality of rights;

Nitarejea...


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Highlander,

Unaelekeza mjadala kuzuri sana; kwa sasa naomba nijadili kidogo suala la "haki na usawa". Wanasiasa wengi wanapenda sana kutumia dhana za natural justice na equality katika kujadili jinsi gani wanaheshimu haki na usawa wa wananchi;aidha kwa makusudi au ulimbukeni wao, wanajisahau kwamba kilicho muhimu katika haki na usawa na social justice na equality, sio natural justice na equity; upuuzi wa equality and social justice ni foundation za liberal/bourgeois political doctrines na theories of right ambazo ndio zimeangamiza mamilioni ya binadamu for centuries kutokana na utumwa, ukoloni,vita,njaa,unyonyaji n.k; right ideology ambayo msingi wake ni equal rights have been argued over and over again na wanazuoni maarufu duniani kwamba haina mashiko katika kutambua haki na usawa wa walio wengi kwani equality among unequals is inequitable; kwa ufupi, dhana za haki na usawa ambazo ndio msingi wa ujamaa kama ulivyojadili zipo much closer to dhana za justice and equity kuliko equality of rights;

Nitarejea...


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Unapojiandaa kurejea, naomba ukumbuke nimesema kwamba Azimio la Arusha lilikuwa linatafuta kuleta USAWA.
Sera zilizopo sasa ni sera zinazokubali HAKI; siyo Usawa. Kwa hiyo huwezi kurudisha Azimio la Arusha whole sell kwa sababu
'operational locus' ni tofauti.
 
Highlander,

Bandiko namba 66 nalipinga kwa nguvu zote - pale unaposema kwamba sera za worldbank zinafanya kazi kuliko za ujamaa tatizo ni wizi na usimamizi; nadhani unasahau kwamba economic crisis ya 1970s haikuletwa na ujamaa bali sababu nyingine pia ambazo zilitufanya tuwe vulnerable sababu ya our inherent weakness katika mfumo wa uchumi wetu; nitajadili baadae juu ya economic challenges of TANU ingawa I did that already huko nyuma;

Pili, ni muhimu ujue kwamba sera za worldbank na imf zilianza kuleta unafuu kidogo baada ya kufanyiwa marekebisho ambayo mengi yalirudia baadhi ya sera za azimio la arusha aidha directly or indirectly; nadhani unatambua kwamba mageuzi yalikuja 1984/5, na kufikia 1994, Tanzania chini ya mageuzi ikawa in worse situation kuliko 1985; unakumbuka kuna wakati hata misaada ilianza kusimamishwa?unakumbuka tanzania ikawa nchi ya tatu kutoka mwisho kwa umaskini? Largely ni because wahisani ambao ndio wanaipa fedha worldbank na imf walianza kukosa imani na Structural adjustment programmes kwani unlike ujamaa, haikuwa na element ya povert reduction; baada ya vuta nikuvute, IFIs wakabadilisha SAPs na kutuletea kitu kinaitwa poverty reduction strategic papers (PRSPs) ambapo tofauti na SAPs ambapo hawa IFIs ndio walikuwa waamuzi juu ya sekta gani zipewe priority n.k, PRSPs zikawa more democratic ambapo nchi maskini zikapewa uhuru kidogo wa maamuzi juu ya matumizi ya AID; and guess what, ndio tulaanza kuona serikali ikianza kurudi taratibu katika utoaji wa huduma muhimu za kijamii, nyingine bure kama ujamaa, nyingine kwa michango kidogo i.e ruzuku; hivyo ndivyo turn around ya sera za IMF na Worldbank ikaanza!!!

Ni muhimu uelewe kwamba worldbank na imf walipoanza kujali japo kidogo suala la "growth with equity", mambo ndio yakaanza badilika; ni pale walipotambulisha MDGs ambazo basically azimio la arusha ilikuwa na elements nyingi za MDGs, mambo ndio yakaanza badilika; ni waliporudi kwenye dhana ya mwalimu juu ya Uongozi Bora, siasa safi, watu na ardhi kama ndio misingi ya kunyanua watu, ndio hawa IFIs wakaleta mambo kama ya Azimio ila kwa majina kama good governance, human capital development (watu), haki za ardhi kwa wananchi, na strengthening institutions suala ambalo chini ya ujamaa lilisimamiwa na 'siasa safi' kwani hili lililenga usimamizi wa sera kitaasisi;

Ndio maana hata IFIs wanakubali Azimio had more merits than demerits na ndio maana as I discussed earlier, Rais wa WB alimwita mwalimu washington kama njia ya kumuomba msamaha kistaraabu kwa kumwambia "I have been re-reading your speeches from 1960s,na bado naona yote kimalengo ulikuwa sawa."

Nitarejea...

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Highlander,

Kuhusiana na hoja yako bandiko 69, iwapo ulitulia na kunisoma vizuri, nilijadili usawa in the context of equity, not equality, and YES, katika mazingira ya sasa, ukiachilia mbali haki (not natural justice but social,political and economic justice) Usawa (equity, not equality) isn't only possible, but also neccesary, desirable and ATTAINABLE!!

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Naomba usome bandiko namba 63 tena. Lakini kabla ya kulisoma hilo, hebu jisikilize mwenyewe hapa: Ati unasema "mageuzi yalikuja 1984/5, na kufikia 1994, Tanzania chini ya mageuzi ikawa in worse situation kuliko 1985" Hivi wewe Tanzania iliyokuwa worse unaijuwa kweli? Au unasikia tu redioni. Hii ni decade ya Mwinyi unayoiongelea hapa.

Kulikuwa ujinga mwingi sana wa rushwa na ufisadi hapa--watu wakiingiza mapombe ya Stela Artoir nchini (hata Waislamu) bila kulipa kodi, fedha zikawa zinaibwa CRDB kwa fujo ya ajabu. Unasema "kuna wakati hata misaada ilianza kusimamishwa?"
Sababu ya misaada kusimamishwa kipindi kile ilikuwa ni hofu kwamba feza zote zitaibwa. Kwa hiyo tatizo lolote unaloliona katika mtizamo wa uchumi uliopo tangu hiyo 1984/85 unayoisema ni tatizo la uongozi tu. The wrong people are managing the economy!

Unasema "IFIs wakaleta mambo kama ya Azimio ila kwa majina kama good governance, human capital development (watu), haki za ardhi kwa wananchi, na strengthening institutions." Tangu tumeanza mjadala huu nimekwambia kuna maudhui mema katika Azimio la Arusha. Hii ni kwa sababu hayo maudhui yana msaada katika kujenga uchumi unaolinda HAKI za wananchi. Taifa linalowatendea HAKI wananchi linakuwa na amani.

Kwamba IFIs wanakubali Azimio had more merits than demerits, mimi pia nimesema hili tangu mwanzo, ingawa baadaye nimefafanua kuwa sura nzuri ya Azimio la Arusha ni kwamba a) liliundwa kwa nia njema. b) Azimio la Arusha lina vipengele vinavyoweza kukuza HAKI. Kwa hiyo hatujatofautiana hapo. Mimi nina ugomvi na ufisadi tu. Ufisadi una-distort uchumi wetu.... Hilo kwa nini unalikwepa sana? Au wewe Mchambuzi ni beneficiary nini? Uniwie radhi kama nitakuwa nimekukwanza kwenye hili swali la mwisho.
 
Highlander,
Bandiko lako namba 72 unajisahau kwamba huko nyuma tulikubaliana kwamba tatizo kubwa lililopo ni kutokana na ujio wa uliberali ovyo ovyo mwaka 1984-5; yote unayojadili bandiko 72 ilitokana na marketization, liberalization and privatization kiholela huku institutions ambazo kimsingi ziliweka mambo mengi in check chini ya AR zikitupwa bila ya angalau kuzipa a transitional period ili zipunguze uholela wa soko huria; azimio la zanzibar ndio likapigilia msumari jeneza husika;

Chadema wanaposema katika katiba yao kwamba wanafuata itikadi ya uliberali mrengo wa kati inayoamini katika soko huria ambalo SIO HOLELA, maana yake wanaelewa mapungufu yaliyojitokeza,ingawa mzee wetu edwin mtei hataki kufafanua zaidi suala la uholela ambalo alilisimamia kikamilifu kwenye african desk ya IMF pale washington baada ya kupingana na Mwalimu na kuondoka nchini;

Bottom line is - unakataa kuelewa nini kiliendelea chini ya ERP na SAPs after 1984 na madhara yake kwetu ambayo yakawa obvious ten yrs later; na unakataa kuelewa SAPs zilipotelea wapi na kwanini zikaja PRSP na muhimu zaidi, growth kupewa a human face and equity under poverty reduction growth facility (PRGF) ambazo kwa pamoja ndio zimeokoa sera za worldbank na imf huku wewe ukisifia mafanikio ya uliberali bila ya umakini wa kutosha;

Mwisho, nakushauri matatui katika hili:

Moja, rejea graph yako uliyoweka humu hapo juu katika ujenzi wa hoja yako kwamba we were better in 2005 than 1985; sasa katika graph hiyo hiyo,bila ya wewe kutambua,umeweka takwimu to show jinsi gani hali ilikuwa mbaya early 1990s sawa na 1985 if not worse;soma graph yako kwa umakini;

Pili, rejea hoja yangu ya awali kuhusiana na value ya economic growth kuanzia 2000 hadi sasa ambayo obviously its impressive but that GDP haven't been produced la labour of the majority of Tanzanians hasa wakulima na wafanyakazi bali ni matokeo ya extraction ya madini yetu ambayo hayalipiwi kodi ya maana wala hakuna ajira kwa wengi sekta hiyo; ukitoa gold pdn for exports kwenye equation ya GDP for the past ten yrs, hakika GDP ya kipindi cha ujamaa wa much higher;

Na mwisho na muhimu sana sana sana, ujue kwamba-ingawa uchumi uligota 1985, our labour kwenye kilimo, viwanda na baadhi ya SOEs ilihitaji a STIMULUS PACKAGE, not reforms; Mwalimu alipingana na edwin mtei na IMF kwa kutaka stimulus package,angalia leo crisis marekani,eurozone wanavyotumia stimulus package;Mwalimu alikuwa na akili sana,na edwin mtei na imf wangefuata ushauri wa stimulus package badala ya reforms huku mabaya ya Azimio ya arusha yakitupwa na mazuri kubaki,Tanzania leo ingekuwa top five in afrika kiuchumi na kimaendeleo;

Highlander, its time you wake up and smell the coffee!!!

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Tupo pamoja highlander na sio kwamba nakwepa juu ya role ya ufisadi;nisisitize tena:

Moja, ufisadi played a big part kulihujumu azimio la arusha na nimejadili hili kwa kina hata huko nyuma;mwalimu alihujumiwa na watu aliowaamini na kuwapa uongozi mashirika ya umma,vyama vya ushirika, mawaziri ambao walikuwa bega kwa bega na mabepari wa nje na wafanyabiashara wa kiasia (baadhi, sio kina rajani au sobodo) kuhakikisha kwamba ujamaa unakufa ili kufungua uchumi kwa ajili ya mafisadi, ma--------- na mabepari wa nje waliotaifishiwa mali na AR;

Pili, ninejadili sana huko kwingine jinsi gani kundi hili hili likaendelea kuhujumu nchi kwa kuliua kabisa AR na kuja na azimio la znz mwaka 1992; miiko ya uongozi na mambo mengine kem kem ikafutwa bila ya kuwekwa kitu kipya kukidhi mazingira mapya na ni kutokana na hilo, imekuwa ngumu kupambana na ufisadi leo;

Mwisho na muhimu, katika mjadala huu, najitahidi kuangalia beyond ufisadi kwa manufaa ya ikulu ya chadema huko mbeleni; nilishajadili hili - kwamba ufisadi ni sehemu tu ya sababu kwanini wananchi maskini kwani zipo sababu nyingi; kwa maana nyingine, CHADEMA WAKIINGIA IKULU na kupunguza kabisa ufisadi, uchaguzi unaofuata au ndani ya miaka kumi,wananchi walewale wataiondoa madarakani kwani hali za wananchi zitaemdelea kuwa mbaya sana kwasababu again, umaskini wao sababu zake ni way over ufisadi; kwahiyo ni muhimu tuendelee na mjadala wa ufisadi ukipenda ingawa to me this is an atomistic hence a shallow way of looking and analyzing the rootcause of our predicament and instead the best approach ni HOLISTIC ambapo ufisadi ni sehemu tu ya sababu za umaskini wetu;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Ukimhusisha Edwin Mtei na lile soko holela la Ali Hassan Mwinyi 1985 - 1995 unakosea sana Mkuu. Ujue ile ilikuwa mwendesha baiskeli kapewa treni aendeshe. Utazamie nini kama si kulipeleka treni shimoni!

Sijui unashindwa kuelewa Kiswahili changu au vipi. Mzee Mtei kaleta baraka kubwa sana nchini. Mwache ajipumzikie uko Usa River bila shida. Bandiko namba 63 umeliona lakini? Siyo 73. Unasema CHADEMA kwa mujibu wa Katiba yao wanaelewa mapungufu yaliyojitokeza kwenye lile soko holela la Mwinyi, ingawa mzee wetu edwin mtei hataki kufafanua zaidi suala la uholela ambalo alilisimamia kikamilifu kwenye african desk ya IMF pale washington baada ya kupingana na Mwalimu na kuondoka nchini.

Maelezo ya tatizo lililojitokeza hapa Tanzania yanaelezeka bila Mtei. Dereva wa Baskeli alipewa treni kuendesha nimekwambia. Mtei wa nini hapo!

BEYOND UFISADI

Mkuu wangu Mchambuzi, unasema unajitahidi kuangalia beyond ufisadi kwa manufaa ya ikulu ya chadema huko mbeleni; kwamba ufisadi ni sehemu tu ya sababu kwanini wananchi ni maskini kwani zipo sababu nyingi; kwa maana nyingine, CHADEMA WAKIINGIA IKULU na kupunguza kabisa ufisadi, uchaguzi unaofuata au ndani ya miaka kumi,wananchi walewale wataiondoa madarakani kwani hali za wananchi zitaemdelea kuwa mbaya sana kwasababu again, umaskini wao sababu zake ni way over ufisadi; kwahiyo ni muhimu tuendelee na mjadala wa ufisadi ukipenda ingawa to me this is an atomistic hence a shallow way of looking and analyzing the rootcause of our predicament and instead the best approach ni HOLISTIC ambapo ufisadi ni sehemu tu ya sababu za umaskini wetu.

MY TAKE:

Nakubaliana na dhana ya kulijadili suala hili Holistically. Lakini wakati mi nawewe tunakubaliana kuhusu kulijadili suala hili kwa mtizamo huo, bado ni vizuri ukakubali pia kwamba unapokuwa katika vita ni ngumu kupiga maadai laki moja kwa mkupuo. Kumwondoa mmoja mmoja kama mchezo wa kubutua matofali kwenye simu inakubalika. Ukibahatika umewakuta platoon nzima ukawabutua kwa mpigo, poa. ni bahati yako hiyo. Njoeni tuanze na Ufisadi. Mengine yafaute. What is wrong with that?
 
Ukimhusisha Edwin Mtei na lile soko holela la Ali Hassan Mwinyi 1985 - 1995 unakosea sana Mkuu. Ujue ile ilikuwa mwendesha baiskeli kapewa treni aendeshe. Utazamie nini kama si kulipeleka treni shimoni!

Sijui unashindwa kuelewa Kiswahili changu au vipi. Mzee Mtei kaleta baraka kubwa sana nchini. Mwache ajipumzikie uko Usa River bila shida. Bandiko namba 63 umeliona lakini? Siyo 73. Unasema CHADEMA kwa mujibu wa Katiba yao wanaelewa mapungufu yaliyojitokeza kwenye lile soko holela la Mwinyi, ingawa mzee wetu edwin mtei hataki kufafanua zaidi suala la uholela ambalo alilisimamia kikamilifu kwenye african desk ya IMF pale washington baada ya kupingana na Mwalimu na kuondoka nchini.

Maelezo ya tatizo lililojitokeza hapa Tanzania yanaelezeka bila Mtei. Dereva wa Baskeli alipewa treni kuendesha nimekwambia. Mtei wa nini hapo!

Mbona kama unaandika na kujipinga mwenyewe? upande mmoja unakubali kwamba Bw.Mtei anahusika na kinachoendelea na upande mwingine unasema tumwache Bw. Mtei, sasa unawezaje kujadili kuhusu tukio bila kumshusisha muhusika au moja kati ya wahusika Wakuu?

Kama yeye (Bw.Mtei) alihusika ktk kuishauri Serikali kufwata sera ambazo tunazo, pia anahusika na anapaswa kutueleza zaidi na msimamo wake ulivyo sasa hasa ukichukulia kwamba yeye ni mwanzilishi wa Chama ambacho kina uwezekano wa kushika Dola, tunapaswa kuelewa yeye anasemaje?

 
Nilishaeleza huko nyuma kwa kirefu sana kwanini kuna umuhimu wa mzee wetu edwin mtei kuingia katika historia ya mema aliyoitendea nchi yetu pia kwa kujadili ujio wa ulibepari- mafanikio, makosa na changamoto kama worldbank na mwalimu walivyojadili per my post huko juu but kama wewe na yeye hamuoni haja ya kufanya hivyo, ni haki yenu na sitalijadili tena hilo ili kumwepushia kero unayoiwasilisha hapa kwa niaba yake; ila ujue tu it sends ujumbe au sumu inayosambazwa kwamba chadema na uongozi wake wana utamaduni wa kutokubali makosa na pia huwa hawakubali ushauri!!

Tuyaache ya edwin mtei, kwani nimekubali kufunga hoja ya kumjadili na naomba na wewe usimtaje tena kuanzia sasa; turudi kwenye hoja ya msingi iliyo mbele yetu na una mengi ya kunijibu katika mabandiko kadhaa hapo juu kwani nimekujibu mengi tayari; nasubiria your counter arguments kwa manufaa ya demokrasia na maendeleo ya taifa letu;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Highlander,

Naona unahimiza sana tujadili ufisadi; kumbuka, agenda hii itaisaidia chademe kuingia ikulu ila sio kubakia ikulu; lakini kama umeamua kujikita katika chadema kuingia ikulu, nipo tayari kushiriki katika mjadala wa ufisadi; lete hoja zaidi;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Nilishaeleza huko nyuma kwa kirefu sana kwanini kuna umuhimu wa mzee wetu edwin mtei kuingia katika historia ya mema aliyoitendea nchi yetu pia kwa kujadili ujio wa ulibepari- mafanikio, makosa na changamoto kama worldbank na mwalimu walivyojadili per my post huko juu but kama wewe na yeye hamuoni haja ya kufanya hivyo, ni haki yenu na sitalijadili tena hilo ili kumwepushia kero unayoiwasilisha hapa kwa niaba yake; ila ujue tu it sends ujumbe au sumu inayosambazwa kwamba chadema na uongozi wake wana utamaduni wa kutokubali makosa na pia huwa hawakubali ushauri!!

Tuyaache ya edwin mtei, kwani nimekubali kufunga hoja ya kumjadili na naomba na wewe usimtaje tena kuanzia sasa; turudi kwenye hoja ya msingi iliyo mbele yetu na una mengi ya kunijibu katika mabandiko kadhaa hapo juu kwani nimekujibu mengi tayari; nasubiria your counter arguments kwa manufaa ya demokrasia na maendeleo ya taifa letu;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

He kumbe unatumia simu ya Blackberi inaeleka una ukwasi eehh! Maana kako aghali hako kasimu
 
Mbona kama unaandika na kujipinga mwenyewe? upande mmoja unakubali kwamba Bw.Mtei anahusika na kinachoendelea na upande mwingine unasema tumwache Bw. Mtei, sasa unawezaje kujadili kuhusu tukio bila kumshusisha muhusika au moja kati ya wahusika Wakuu?

Kama yeye (Bw.Mtei) alihusika ktk kuishauri Serikali kufwata sera ambazo tunazo, pia anahusika na anapaswa kutueleza zaidi na msimamo wake ulivyo sasa hasa ukichukulia kwamba yeye ni mwanzilishi wa Chama ambacho kina uwezekano wa kushika Dola, tunapaswa kuelewa yeye anasemaje?


Sikiza mwaya...mie sijamsemea kitu chochote Mtei. Yeye ana yake na mie nina yangu. Nilichosema ni kwamba matatizo ya soko hulela yanaelezeka bila Mtei. Nikamwomba mwenzangu kwamba kwa sababu hiyo, tumwache tu mzee wa watu ajipumzikie huko Usa River. Kauli hiyo ina tatizo gani kwani.

Matatizo ya kiuchumi yaliyojitokeza 1985 - 1995 yanaelezeka kabisa, na ni natatizo Internal. Si external. Msitafute kusingizia watu kwa madhaifu yenu yote. Economics ni social science yenye sifa nyingi sana za kisayansi ujue. Zipo variables kibao LOCAL ambazo zilizosababisha kuwepo soko holela la Mwinyi; na hicho ndicho kilichokuwa Tatizo lenyewe hasa. The wrong people were given the mandate to manage the economy!
 
Sikiza mwaya...mie sijamsemea kitu chochote Mtei. Yeye ana yake na mie nina yangu. Nilichosema ni kwamba matatizo ya soko hulela yanaelezeka bila Mtei. Nikamwomba mwenzangu kwamba kwa sababu hiyo, tumwache tu mzee wa watu ajipumzikie huko Usa River. Kauli hiyo ina tatizo gani kwani.

Matatizo ya kiuchumi yaliyojitokeza 1985 - 1995 yanaelezeka kabisa, na ni natatizo Internal. Si external. Msitafute kusingizia watu kwa madhaifu yenu yote. Economics ni social science yenye sifa nyingi sana za kisayansi ujue. Zipo variables kibao LOCAL ambazo zilizosababisha kuwepo soko holela la Mwinyi; na hicho ndicho kilichokuwa Tatizo lenyewe hasa. The wrong people were given the mandate to manage the economy!

Hata 2015 pia utasema tumwache Bw.Kikwete na ufisadi wake kwani matatizo yaliyotokea huko nyuma yanaelezeka tumwache mzee Bw. JK ajipumzishie Bagamoyo!
 
Kijakazi,
Umeliweka vizuri, na inakuwa kama vile edwin mtei na highlander ni mtu yule yule, if not mtu close to him aliyepo hapa kwa kazi maalum;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Highlander,

Naona unahimiza sana tujadili ufisadi; kumbuka, agenda hii itaisaidia chademe kuingia ikulu ila sio kubakia ikulu; lakini kama umeamua kujikita katika chadema kuingia ikulu, nipo tayari kushiriki katika mjadala wa ufisadi; lete hoja zaidi;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums


Hilo nalo neno Mkuu Mchambuzi! Kwa maana hiyo, naoamba tuelekeze mjadala wetu kwa mtizamo huu:

a) Tunajua Ufisadi unaathiri uchumi kwa kufanya distortions hapa na pale. hebu tuziainishe hizo distortions.

b) Chadema ichukue vipengele gani kutoka Azimio la Arusha vitumike katika hii vita dhidi ya Ufisadi?

c) Ikulu ya Chadema iingie na vipaumbele gani? Juzi nilitoa pendekezo kuwa kufuta Udini ingekuwa priority number one,
vikienda parallel na vita dhidi ya Rushwa na Ufisadi. Na mwisho kutakuwepo kazi ya kukuza uchumi kwa umakini na uadilifu zaidi.

Unaonaje pendekezo hili la mwelekeo wa Mjadala wetu kutoka hapo tulipofika Mkuu Mchambuzi.
 
Back
Top Bottom