Nini Maana ya Philosophy?

FALSAFA

JF-Expert Member
Sep 10, 2014
293
56
Ndugu WanaJamii, nadhani tu wazima sisi ni jambo la kumshukuru manani. Mwenye ujuzi nilikuwa nataka atufafanulie maana ya Philosophy (Falsafa). na vipi mtu awe Philosopher (MwanaFalsafa) kama akina Robin Sharmah, Albert Einstein, Phill Collins, Francis Bacon, Isaac Newton na wengi wengineo.

Nawasilisha wana White House wa JamiiForums.
 
FALSAFA

Phylosophy/falsafa ni jaribio la kuelewa na kueleza kwa kutumia akili inayofuata njia ya mantiki. Falsafa huchunguza mambo kama kuweko au kutoweko kwa, ukweli,imani mema na mabaya, lugha, haki na mengineyo.

Tofauti na dini, imani ama itikadi, njia ya falsafa ni mantiki inayoelezea hatua zake ikiwa tayari kuchungulia upya kila hatua iliyochukua, hivyo falsafa ni njia ya maswali.

Hao uliowataja ni scientists ambao taaluma yao ya science ni mtoto wa falsafa, hii ina maana kwamba falsafa ndio mama wa elimu zote.
Miongoni mwa wanafalsafa wanaojulikana sana kwenye ulimwengu wa taaluma ni Plato, socrate, aristotle na pythagorus, hawa ni wanafalsa ya ugiriki ya kale.
 
Last edited by a moderator:
Nauliza huyu mdau hapa pichani anastahili kujiita anavyojiita?

mwanafabc.jpg
 
Falsafa imetokana na maneno ya kiyunani Philo na Sophia ambayo kwa pamoja yana maana penda hekima.

Hao uliowataja sio wanafalsafa ila wanasayansi na wengine sijui ni akina nani. Wanafalsafa ni kama akina Plato, Paschal, Nitchze, Augustine, Justin Martyr na zama za leo watu kama William Lane Craig, JP Moreland, n.k.
 
Ndugu WanaJamii, nadhani tu wazima sisi ni jambo la kumshukuru manani. Mwenye ujuzi nilikuwa nataka atufafanulie maana ya Philosophy (Falsafa). na vipi mtu awe Philosopher (MwanaFalsafa) kama akina Robin Sharmah, Albert Einstein, Phill Collins, Francis Bacon, Isaac Newton na wengi wengineo.

Nawasilisha wana White House wa JamiiForums.

Falsafa ni maelezo ya kitaalamu yenye hekima kubwa yanayoweza kumfaa mtu yeyote yule anayeishi duniani, pindi akiamua kuyazingatia na kuyafuata. Pia, mwanafalsafa ni mtu anayependa hekima, japo anaweza pia asiifuate. Kupenda kitu na kuzingatia maelezo yake ni vitu viwili tofauti!
 
By all means, marry.If you get a good wife, you'll become happy; if you get a bad one, you'll become a philosopher.
By socrates

Philosophy is the study of general and fundamental problems concerning matters such as existence, knowledge, values, reason, mind, and language.
 
Philosophy ni muunganiko wa Maneno mawili ya Kigiriki philo na sophy yakimaanisha Love and Wisdom Hii ni General field ambayo ndani yake imebeba Science Sanaa na mengineyo ambayo tunaweza kuyaelezea, Tofauti na Dini ambayo ni Imani tu
 
Nauliza huyu mdau hapa pichani anastahili kujiita anavyojiita?

mwanafabc.jpg
hahah! kwa mpicha huu, huyu anafaa kabisa kujiita mwanafalsafa, ukiangalia ilo pozi la picha utaanza kujiuliza maswa mengi sana, kwanini pozi kama hilo pichani? na kitendo cha kijiuliza maswali kichwani hapo ndipo philosophy inapoanza ujue!
 
Falsafa ni maelezo ya kitaalamu yenye hekima kubwa yanayoweza kumfaa mtu yeyote yule anayeishi duniani, pindi akiamua kuyazingatia na kuyafuata. Pia, mwanafalsafa ni mtu anayependa hekima, japo anaweza pia asiifuate. Kupenda kitu na kuzingatia maelezo yake ni vitu viwili tofauti!
Nice! Opinion brother!
 
Back
Top Bottom