Nini maana ya mchamaago? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini maana ya mchamaago?

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by abrisalim, Jul 25, 2011.

 1. a

  abrisalim Member

  #1
  Jul 25, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kuna msemo usemao
  "Mchamaago hanyele huenda akwiya tena"
  Msemo huu wa kiswahili unatumika tokaenzi ya mababu namababu lakini wengi wetu hatujui maana ya maneno yaliyotumika. Nawaombeni wakuu mtueleze maana ya maneno yafuataya:
  Mchamaago,
  Hanyele,
  Akawiya.
  Naomba kila neno litungiwe sentensi ili tujue vipi kulitumia.
   
 2. mtu kitu

  mtu kitu JF-Expert Member

  #2
  Jul 26, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 316
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 60
  Wengine husema MCHAMAAGO HANYELE HWENDA AKAWIA PAPO..............
  maana : anaehama /anaendoka sehemu asitukane (kufanya mambo mabaya) pengine atarudi tena papo hapo
   
 3. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #3
  Jul 26, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  dah....hiki ni kiswahili?
   
 4. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #4
  Jul 26, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Mimi ninvyojua ni "Mchama ago hanyeli,huenda akauya papo".

  Mchama ago (msafiri aliyeweka kambi mahala fulani katika safari yake) hanyeli (hanyi hapo kambini kwa sababu anaondoka - i.e. hafanyi mabaya) huenda (kuna uwezekano) akauya (akarudi) papo (hapo hapo kwenye kambi aliyoweka mwanzo).
   
 5. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #5
  Jul 26, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Haya maneno yana falsafa kubwa sana, wanyamwezi nao wanamsemo kama huo igogo lya hakaya likashenyentelegwa ikiwa na maana karibu sawa na hiyo.
   
 6. a

  abrisalim Member

  #6
  Jul 27, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante mkuu kwa ufafanuzi wako.
   
 7. a

  abrisalim Member

  #7
  Jul 27, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante mkuu SMU.umetufafanulia vizuri sana.
   
 8. a

  abrisalim Member

  #8
  Jul 27, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu Ecoli kama ulivosema: Haya maneno yana falsafa kubwa sana, wanyamwezi nao wanamsemo kama huo igogo lya hakaya likashenyentelegwa ikiwa na maanakaribu sawa na hiyo.
   
 9. mtemiwaWandamba

  mtemiwaWandamba JF-Expert Member

  #9
  Sep 24, 2011
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 536
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  Daah!! Ahsante sana mkuu, hii methali imenisumbua tangu muda mrefu sana kuitafsiri .
  Leo nimeipata.
   
 10. M

  Mwera JF-Expert Member

  #10
  Sep 24, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mchama ago: anaeondoka ktk kambi au maeneo aliyokaa kwa muda na yakamsitiri nakumsaidia, HANYELE hapadharau au hapanyei kwakua ameshakidhi mahitaji yake, HWENDA AKAWIAPAPO: Huenda akarudi palepale pakamsitiri kuliko mwanzo,msemo huu unamaana kubwasanasanasana.nitafafanunua zaidi baadae.
   
 11. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #11
  Sep 24, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  wapendwa,

  hii methali nimewahi kuifafanua kwenye thread fulani. ufafanuzi wa SMU ni sahihi kabisa, ila naomba nifafanue vizuri zaidi hapo kwenye wino mwekundu.

  kuchamaa = kuchuchumaa
  ago= mahali pafinyu (mfano pangoni ama chini ya mti mkubwa ulioinama) ambapo huwezi kusimama wima ama kujibanza ila kwa kuchuchumaa tu. mfano wa mtu aliyekumbwa na mvua kubwa akiwa porini aweza kukimbilia kwenye kapango kadogo kaliko karibu uli kujibanzxza pale na kujihifadfhi dhidi ya mvua hiyo kubwa.

  sasa huyu aliyejibanza hapo pangoni kwa kujikunyata ama kuchuchumaa tu kutokana na ufinyu wa nafasi hapo pangoni, iwe ni kwa kujikinga na mvua, jua, baridi , wanyama wakali ama kulala wakati wa usiku nk, ndiye anayeitwa mchamaa ago! na ndiye tunayeambiwa hawezi kunya hapo maana huenda siku moja akapatwa na dharura nyingine na kujikuta akirudi kujihifadhi palepale.

  mbarikiwe sana wapendwa.

  Glory to God!
   
 12. A

  Albimany JF-Expert Member

  #12
  Sep 24, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 279
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  MCHAMA _ago, ni maneno mawili tofauti.
  KUCHAMA ndio asili ya neno, maanayake ni kuhama na Ago ni kambi kama walivyoeleza wengine hapo juu.

  MCHAMA NI KIWAKILISHI CHA MTU lakini neno hasa lilikua Kuchama.
   
Loading...