Nini maana ya maneno haya?

Wewe ndio unanilaumu, mimi nimeelezea hali halisi. Kakangu (rip general), ulikuwa ndio usemi wake wakati tunakua. Ukifanya kitu kidogo tu anamuambia mama 'mzigo wako huu'

well, sikuwahi kuhusisha hii na muundo wa kanisa. Mtoa mada hapo juu amenipa mwanga kiasi. Naendelea kujifunza. Lakini mwisho wa siku nilidhani mtunga mithali akisema hivyo alimaanisha jukumu la malezi ni la mama zaidi. Na usisahau jamii za kale baba alitumia muda makondeni akilima na kulisha mifugo na mama akiwa nyumbani kutunza familia.

kiukweli nachukulia majukumu yoote ya kuangalia nyumba na watoto ni ya kwangu. Na naamini mume akiwa hopeless familia itaendelea tu vizuri, ila ukipata mke hopeless imekula kwako mazimaaai
 

Now your talking .......!!
 
Ni kweli unachosema, ila tasfiri unayoileta ni "plain meaning interpretation", to my understanding, in a broad sense, mstari huo unalenga, pamoja na mambo mengine, kuonyesha ni kwa jinsi gani mama anawajibika na kuwa karibu na mwana, hasa pale anapopotea. Hii ni kwa mujibu wa "mischief interpretation"...
 

Nimekupata mkuu

Mambo haya ndio yanayosababisha bond kubwa sana kati ya mama na mwana na hadi hapo umuhimu wa mama kuwa "bright" unaonekana na kile kitendo cha akina mama kuwaachia watoto wale wasichana wa nyumbani ambao hawana uhakika na makuzi yao baada ya miezi mitatu tu ya kujifungua ni hatari sana

Tujilaumu wenyewe kwa "dunia" kuharibika!
 
mnaposoma biblia mjuwe kabisa ni tofaiti sana na unavyosoma gazeti la kiu na ijumaa.

kuna kitu kinaitwa bible knowledge, ni lazima umuombe roho mtakatifu na siyo roho mtakavitu kwanza ili akuongoze unapoisoma bible.

hilo andika mnalolijadili hapa linapatika katika agano la kale kitabu cha mithali. kwa kifupi hiki ni kitabu cha hekima za Suleiman kilichosheheni mafumbo.
 

Ngoja tuone kama tutaweza kujua hasa alichokua anamaanisha!
 
Eiyer, naamini umekutana na familia zilizovunjika. Unaonaje, watoto wenye chances za kufanikiwa kimaisha zaidi wanatokea wa single dad ama kwa single moms? Sikatai kuna single moms vimeo lakini naona chances za malezi mazuri ni mama anaposimamia manake hata akiwa na mahusiano mengine hatosahau wanae.

kitu kingine, haswa kwa wazee wetu above 50, akitangulia baba chances za mama kumfuata ni kubwa sana. Lakini mama mjane anaweza kuishi miaka 30 zaidi ya afya njema akifurahia na wanae.
 
Last edited by a moderator:

Hili la watoto kufanikiwa sijalifanyia utafiti lakini ngoja nijaribu kulikagua nitakuja na maelezo kulihusu

Zaidi sana nakubaliana na wewe kuhusiana na malezi kuja kumuamulia mtu hatma yake maishani

Huyu nae alilelewa na mama .......

 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…