Nini maana ya 'kuoana'

Kwa mwanaume ukioa utafurahia ndoa na itadumu ila ukioana yaani mkioana kwa maana kwamba mwanamke naye amekuoa my bro ndoa yako ikifika miezi sita kaague.
Naanza kukupata..kumbe inawezekana mwanaume akaoa na yy akaolewa pia
 
Kuoa --- Mume ameoa..
Kuolewa-- mke ameolewa na mume.
Kuoana-- wote kwa pamoja wamefunga ndoa/ wameoana..


Hakuna kuoana bali kuna kufunga ndoa.

Mfano chukua neno piga hapo unapata; pigwa, pigika, pigana nk, chukua neno pigana ambapo hutumika wakati watu wawili au zaidi wanapopigana sasa linganisha pigana na neno oana ambalo limetokana na neno oa,--- katika hali halisi ya ndoa kuna "oa" na "olewa" ambapo mwanaume "anaoa" na Mwanamke "anaolewa", utaona neno pigana ni sahihi kwa upande wake lakini neno oana sio sahihi kwa upande wake na neno sahihi ni kufunga ndoa yaani ni makosa kusema mwanamke na mwanaume wameoana bali ni sahihi kusema wamefunga ndoa au wamefunga pingu za maisha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom