Nini maana ya kuoa?

Nini maana ya kuoa?

maliza shule kwanza ukija mtaan utayakuta, ww uwe mjuaji kila cku tu alaf yeye awe chin mtaongea badaye kiboyfrend.
nimalize mara ngapi mkuu nina zaidi ya miaka 5 sasa kitaani... swala ni kila mtu kusoma upepo wa hali na kumjua mtu wake...
 
ulishtumiwa na makosa gani hadi ukajikuta kwenye hiyo jela
 
kilichokufanya uingie toka mwanzo ilikuwa ni nini haswa?
 
Ndoa ni muunganiko mwema na wenye furaha tele kwa kipindi chote cha maisha yako endapo utaangukia katika mikono sahihi ya mtu anayejua nini maana ya ndoa na aliyekuwa tayari kuoa au kuolewa kwa wakati huo.......

Ndoa ni tukio kubwa sana katika maisha ya mwanadamu kwa hiyo linataka utayari wa nafsi na mwili vile vile na kiuchumi.....uamuapo kuoa ni lazima ukubali kubadilika kwani huwezi kuishi kama zamani kwani haupo peke yako tena.......

Unapofikiria kuoa au kuolewa huna budi kukaa pekee yako na kusema na nafsi yako je upo tayari kwa tukio hilo...???

Kuna watu wanaoa au kuolewa wakichochewa na mihemko ya balehe na ngono.....bila ya kujua kuwa ndoa ni kifungo cha maisha...

Wengine wanaoa au kuolewa kwa ajili ya mali hawa wote lazima ndoa wazione chungu na zenye kukera kwani kuna tofauti kubwa kuishi na mwenzio na kuishi peke yako.......kuishi maisha ya ndoa kunataka hekima ya hali ya juu sana ...kitu ambacho vijana wengi wamekikosa.....pia uvumilivu ni silaha kubwa kwenye maisha ya ndoa....kwani unakwenda kutumia kipindi chote cha maisha yako na mtu mwenye tabia na fikra tofauti na zako.....kuna tabia unaweza ukamuweka sawa na akakuelewa na kuna baadhi itabidi umvumilie kwani ni ngumu kubadilika.......

Vijana wanapotarajia kuoa au kuolewa inabidi wajiulize kuwa wapo tayari kwa tukio hilo kubwa....??

exactly....wengi wetu tunakurupuka sana, inabidi kutuliza akili sana kabla ya kufanya maamuzi au kujitia kitazi cha milele
 
Mimi ni kijana umri 32 Nina miaka 2 ktk ndoa sitamani tena maana Niko jela ya ndoa, je nifanyeje kutoka?
ukiifananisha ndoa na jela itakusumbua mmno; miaka 2 tu unalalama, tuullize sisi walioko humo zaidi ya miaka 20, ni zaidi ya undugu, na watoto wetu sasa tunawaona kama wadogo zetu kwa sababu ya ukariribu tuliojijengea
 
Mimi ni kijana umri 32 Nina miaka 2 ktk ndoa sitamani tena maana Niko jela ya ndoa, je nifanyeje kutoka?
tupe hint nini kinakusibu ili tujifunze kiongozi maana umeyuacha blank.....ndoa hizi mbona balaaa..umekosea wapi au nini kimetokea?
 
Siamini Eti hadi sasa Lowassa na Kikwete hawawasiliani wala kusalimiana!
 
Mimi ni kijana umri 32 Nina miaka 2 ktk ndoa sitamani tena maana Niko jela ya ndoa, je nifanyeje kutoka?

Solution?
= Uislam.

Hakika mada kama hizi ndipo unapojuwa kuwa Uislam ni mfumo wa maisha uliokamilika.
Hakuna taabu za namna hii katika Uislam, kila kitu kiko wazi kabisa.
 
Solution?
= Uislam.

Hakika mada kama hizi ndipo unapojuwa kuwa Uislam ni mfumo wa maisha uliokamilika.
Hakuna taabu za namna hii katika Uislam, kila kitu kiko wazi kabisa.
Dah....na hasa ile ndoa ya mkataba, inachochea sana uwajibikaji. Hakuna namna watu inabidi wabadilike waachane na hizo jela za maisha[emoji4]
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom