pambe samanini
JF-Expert Member
- Oct 27, 2015
- 368
- 169
Mimi ni kijana umri 32 Nina miaka 2 ktk ndoa sitamani tena maana Niko jela ya ndoa, je nifanyeje kutoka?
Kuoa sio lazma lakini ni muhimuMimi ni kijana umri 32 Nina miaka 2 ktk ndoa sitamani tena maana Niko jela ya ndoa, je nifanyeje kutoka?
Pole ndugu,tafuta wadhamini wenu wa ndoa,wazee wa kiroho na wazee wa pande zote mbili watakusaidia
Mpaka mwanaume mwenye meno 32 anaongea haya nindhani ni magumu kuliko tunavyofikiria.
Humo jera ya ndoa kuna nyapara!!![/QUOT
AsanteNdoa ni muunganiko mwema na wenye furaha tele kwa kipindi chote cha maisha yako endapo utaangukia katika mikono sahihi ya mtu anayejua nini maana ya ndoa na aliyekuwa tayari kuoa au kuolewa kwa wakati huo.......
Ndoa ni tukio kubwa sana katika maisha ya mwanadamu kwa hiyo linataka utayari wa nafsi na mwili vile vile na kiuchumi.....uamuapo kuoa ni lazima ukubali kubadilika kwani huwezi kuishi kama zamani kwani haupo peke yako tena.......
Unapofikiria kuoa au kuolewa huna budi kukaa pekee yako na kusema na nafsi yako je upo tayari kwa tukio hilo...???
Kuna watu wanaoa au kuolewa wakichochewa na mihemko ya balehe na ngono.....bila ya kujua kuwa ndoa ni kifungo cha maisha...
Wengine wanaoa au kuolewa kwa ajili ya mali hawa wote lazima ndoa wazione chungu na zenye kukera kwani kuna tofauti kubwa kuishi na mwenzio na kuishi peke yako.......kuishi maisha ya ndoa kunataka hekima ya hali ya juu sana ...kitu ambacho vijana wengi wamekikosa.....pia uvumilivu ni silaha kubwa kwenye maisha ya ndoa....kwani unakwenda kutumia kipindi chote cha maisha yako na mtu mwenye tabia na fikra tofauti na zako.....kuna tabia unaweza ukamuweka sawa na akakuelewa na kuna baadhi itabidi umvumilie kwani ni ngumu kubadilika.......
Vijana wanapotarajia kuoa au kuolewa inabidi wajiulize kuwa wapo tayari kwa tukio hilo kubwa....??
Kuoa sio lazma lakini ni muhimu