Nini maana ya kuoa?

Nini maana ya kuoa?

ZAmani wazazi walihusika 100%.......Binafsi nina amini MKE ni family property.
Wewe hapan'shaka...ulikuwa unapoza RIm ukaona tamu ukamfanya mke...pengine rangi na umbo vilikuvutia.....
Kama unatafuta mke usiangalie vitu hivi viwili
Angalia utu wa ndani.
 
Mimi ni kijana umri 32 Nina miaka 2 ktk ndoa sitamani tena maana Niko jela ya ndoa, je nifanyeje kutoka?
Kaa chini ongea na mwenzio tafuteni chanzo cha tatizo fanyieni kazi hilo tatizo Mungu akusaidie maana wewe ndiye kichwa cha nyumba sasa ukivurugika wewe hakuna kitakachoendelea ndani ya nyumba yako .Usikimbilie kuvunja ndoa au kuachana
 
maana yake ni kumtafuta mwenza na kuunganisha nguvu kusukuma kwa pamoja gurudumu la maisha... mnaungana na kuwa kitu kimoja kwa kila kitu..hata mtazamo wenu unatakiwa kuwa mmoja, malengo, matumaini, misimamo na kadha wa kadha... hio ndio maana nzima ya kuoana kwa mtazamo wangu.
una mtazamo chanya sana..vema.. ila wote kuwa in one parralel line!!!! MUNGU tusaidie.
 
dogo miaka 2 michache sana,,,, angalau 10 kwenda mbele,,,, nadhani ulipanda dldl bila kusoma linaelekea wapi....ndoa ni watu wawili.....wa 3 ni ibilisi.....jipange upya kuamua mustakabali wako.....
 
Pole sana. kwani ndoa yako niya mke mmoja au wake wengi?
 
ungetueleza situation ambazo zinakufanya uone machungu...yamkini inawezekana wewe ukawa ndio chanzo cha tatizo.. unajua mwanaume ndio nguzo ya familia ikitetereka tu basi familia nzima inakosa uelekeo..wewe ni baba wa familia katika hali yoyote ile hupaswi kukata tamaa dhidi ya familia yako, hakuna mtihani Mungu anaweza kumpa mwanadamu usiokuwa na majibu, kwa ushauri wangu tu unatakiwa uwe mvumilivu mwaka wa pili tu umeshaanza kukata tamaa?.. kaeni chini mtafute suluhu wewe na mke wako..unajua watu wengi tunakuwa waoga kukaa chini na kuongea vitu kwa uwazi yaani mtu yupo radhi kumueleza jambo rafiki, au kwenye mitandao lakini sio kukaa meza moja kujadili na mtu ambaye ndie anayemlenga...kaeni chini kama watu wamoja mmalize huo mgogoro..
 
Ndoa ni muunganiko mwema na wenye furaha tele kwa kipindi chote cha maisha yako endapo utaangukia katika mikono sahihi ya mtu anayejua nini maana ya ndoa na aliyekuwa tayari kuoa au kuolewa kwa wakati huo.......

Ndoa ni tukio kubwa sana katika maisha ya mwanadamu kwa hiyo linataka utayari wa nafsi na mwili vile vile na kiuchumi.....uamuapo kuoa ni lazima ukubali kubadilika kwani huwezi kuishi kama zamani kwani haupo peke yako tena.......

Unapofikiria kuoa au kuolewa huna budi kukaa pekee yako na kusema na nafsi yako je upo tayari kwa tukio hilo...???

Kuna watu wanaoa au kuolewa wakichochewa na mihemko ya balehe na ngono.....bila ya kujua kuwa ndoa ni kifungo cha maisha...

Wengine wanaoa au kuolewa kwa ajili ya mali hawa wote lazima ndoa wazione chungu na zenye kukera kwani kuna tofauti kubwa kuishi na mwenzio na kuishi peke yako.......kuishi maisha ya ndoa kunataka hekima ya hali ya juu sana ...kitu ambacho vijana wengi wamekikosa.....pia uvumilivu ni silaha kubwa kwenye maisha ya ndoa....kwani unakwenda kutumia kipindi chote cha maisha yako na mtu mwenye tabia na fikra tofauti na zako.....kuna tabia unaweza ukamuweka sawa na akakuelewa na kuna baadhi itabidi umvumilie kwani ni ngumu kubadilika.......

Vijana wanapotarajia kuoa au kuolewa inabidi wajiulize kuwa wapo tayari kwa tukio hilo kubwa....??
Be blessed Mkuu , Umenena Vyema Sana.
 
maana yake ni kumtafuta mwenza na kuunganisha nguvu kusukuma kwa pamoja gurudumu la maisha... mnaungana na kuwa kitu kimoja kwa kila kitu..hata mtazamo wenu unatakiwa kuwa mmoja, malengo, matumaini, misimamo na kadha wa kadha... hio ndio maana nzima ya kuoana kwa mtazamo wangu.
ila ni ngumu xna kuwa hivyo wanawake mmekuwa wajuaji xna.
 
ila ni ngumu xna kuwa hivyo wanawake mmekuwa wajuaji xna.
ukiona hivyo basi hata wewe utakuwa ni mjuaji... kwani wanasema wahenga Mafahali wawili hawawezi kuishi zizi moja...kujishusha mara zote ni kwa upande wote... na muda mwingine unajishusha ili kuokoa hali yawezekana hata kosa sio lako...ila ili kuleta amani kwa wakati huo unajishusha.. halafu unaweza kuliongea hilo jambo wakati mwingine mkiwa mmekaa sawa...tena ukaongelea kwa utani mmhh siku ile sijui ulipatwa na nini.. mtaongea mtamaliza hapo. lakini ukitaka kujifanya kila kitu wewe kwa vile ndio mwanaume uko juu utakuja kufail tu.
 
maliza shule kwanza ukija mtaan utayakuta, ww uwe mjuaji kila cku tu alaf yeye awe chin mtaongea badaye kiboyfrend.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom