marko maluli
Senior Member
- Mar 14, 2015
- 164
- 49
Jamani haya maneno mawili yananitatiza sana naombeni tusaidizane tofauti iliyopo kati ya mapenzi na mahaba.
Mapenzi ni hisia za upendo kwa mwenza wako na mahaba ni vitendo vya kuyathibitisha mapenzi hayo!una fanya mahaba ili kudhihirisha penzi lako! mapenzi ni hisia ulizo nazo na ili kuzi onesha utafanya mahaba ,na mahaba vitakua ni vitendo mbalimbali -jinsi unavyo mwangalia kwa huba mpenzi wako,unavyomwitikia ,unavyomsikiliza ,utakavyomgusa,na hata jinsi ya kugombana nae!na mapenzi yaso mahaba sawa na nyumba iliyo sanifiwa vyema ila ikawa haina plaster ,rangi,hata dari !hakika haitapendeza!