Nini maana ya Ashakum si Matusi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini maana ya Ashakum si Matusi?

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Sniper, Apr 17, 2011.

 1. Sniper

  Sniper JF-Expert Member

  #1
  Apr 17, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,944
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Wadau wa lugha naomba kujuzwa nini maana ya "Ashakum si Matusi"? Au hii sentensi inatumikaje?
   
 2. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #2
  Apr 17, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Sentensi/tungo hiyo hutumiwa aghalabu unapotaka kutamka jambo ambalo lina "tusi/utusi" ama kutamka viungo vya siri bila ya kutaka kutumia tafsida.
  Mf: Ashakum si matusi, mbwa walipomdondosha Mzee Kijogoo wakaziraru pumbu na mb.. yake.
   
 3. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #3
  Apr 17, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Sentensi/tungo hiyo hutumiwa aghalabu unapotaka kutamka jambo ambalo lina "tusi/utusi" ama kutamka viungo vya siri bila ya kutaka kutumia tafsida.
  Mf: Ashakum si matusi, mbwa walipomdondosha Mzee Kijogoo wakaziraru pumbu na mb.. yake.
   
 4. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #4
  Apr 17, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Swali zuri lenye majibu swaafi, naomba niongezee kijiswali...'tafsida' humaanisha nn? Sorry kwa interruption.
   
 5. M

  Mwanjelwa JF-Expert Member

  #5
  Apr 17, 2011
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 961
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Mhh, mbona kama ndiyo umeongezea ugumu wa neno. Utafsiri kwa maneno yanayohitaji tafsiri?!
   
 6. Askari Kanzu

  Askari Kanzu JF-Expert Member

  #6
  Apr 17, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,526
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Ashakum = samahani kwa kauli/msemo
  Ashakum = pardon the expression

  Ashakum si matusi = samahani kwa kauli, nitakalolisema si matusi!
   
 7. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #7
  Apr 17, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  kupunguza ukali wa neno?
   
 8. Bu'yaka

  Bu'yaka JF-Expert Member

  #8
  Apr 17, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 851
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 80
  "Ashakum si matusi," ashakum ni nini?
   
 9. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #9
  Apr 17, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Nadhani utakuwa umeelewa hapo
   
 10. S

  Senior Bachelor Member

  #10
  Apr 17, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 86
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tafsida ni neno linalotumiwa kupunguza makali ya neno lingine. kwa kiingereza huitwa "euphemism". Mathalan, kujifungua badala ya kuzaa (kwa binadamu), ashakumu kujisaidia badala ya kunya/kukojoa, n.k.
   
 11. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #11
  Apr 17, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,059
  Trophy Points: 280
  Niwie radhi ninachotaka kukisema...Kama vile kumtahadharisha/kuwatadharisha msikilizaji/wasikilizaji lugha unayotaka kuitumia si nzuri hivyo wasikushangae kwa kutumia lugha hiyo.
   
 12. Bu'yaka

  Bu'yaka JF-Expert Member

  #12
  Apr 17, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 851
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 80
  Bado sijamuelewa.

  Kama si matusi, samahani ya nini?
   
 13. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #13
  Apr 17, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,282
  Likes Received: 1,432
  Trophy Points: 280
  Kama walivyosema wachangiaji waliotangulia, 'ashakum si matusi' ni kauli fupi inayomaanisha 'Samahani kwa kauli hii, simaanishi tusi'.

  Kuna maneno ambayo ukiyatumia huwa ni kama vile matusi. Ikibidi yatumike kwa manufaa, kwa mfano katika ufafanuzi, maelezo, mafunzo n.k, basi inakuwa vyema kuanza kutahadharisha kwamba hukusudii kutukana unapoyataja.

  Samahani ni katika kuonyesha uungwana.
   
 14. Bu'yaka

  Bu'yaka JF-Expert Member

  #14
  Apr 18, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 851
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 80
  Sijauliza maana ya kauli "ashakum si matusi," nimesema, ashakum si matusi, ashakum ni nini? Akasema "ashakum" ni samahani. Nikasema kama si matusi samahani ya nini?

  Nilivyofunzwa mimi, muungwana anasema "samahani sikudhamiria" baada ya kitendo, ukisema samahani kabla ya kosa ina maana umekusudia. Hata njiani huwezi kumwambia mtu "ndugu nataka kukukanyaga, lakini ashakum" halafu umkanyage, si utagombaniwa? Hiyo offense ni calculated, kusudi.

  "Samahani si matusi" ikifatiwa na matusi! Kama si matusi samahani ya nini?
   
 15. Askari Kanzu

  Askari Kanzu JF-Expert Member

  #15
  Apr 18, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,526
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  We Bu'yaka vipi, mbona mbishi sana?
   
 16. A

  Amjaribu New Member

  #16
  Apr 18, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  maana yake yakhe,tafadhari niwie radhi kwa haya nitakayosema.....
   
 17. A

  Amjaribu New Member

  #17
  Apr 18, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Maana yake uniwie radhi kwa nitakayo yatamka au kuyasikia.
   
 18. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #18
  Apr 18, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Samahani sababu katika hali ya kawaida hayo maneno yanaonekana kama matusi ila kwa context unataka kutumia sio matusi. Kwa hiyo unawaomba wanao kusikiliza kutumia effort ya ziada kwa kuelewa maneno yale in the context, na wala wasichukulie kama matusi.
  Maneno yanakua matusi kufatana na context, ila ukisha sema hivo yanakua ni maneno ya kawaida.
  Sijui umeelewa sasa?
   
 19. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #19
  Apr 18, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,282
  Likes Received: 1,432
  Trophy Points: 280

  Kama sababu hiyo hapo kwenye rangi nyekundu, mpelekee mwalimu wako hili swali lako.
   
 20. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #20
  Apr 19, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  wewe ni mwalimu mzuri.
   
Loading...