Nini maana ya Ashakum si Matusi?

Sniper

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
1,915
709
Wadau wa lugha naomba kujuzwa nini maana ya "Ashakum si Matusi"? Au hii sentensi inatumikaje?
 
Sentensi/tungo hiyo hutumiwa aghalabu unapotaka kutamka jambo ambalo lina "tusi/utusi" ama kutamka viungo vya siri bila ya kutaka kutumia tafsida.

Mf: Ashakum si matusi, mbwa walipomdondosha Mzee Kijogoo wakaziraru korodani na mb.. yake.
 
Swali zuri lenye majibu swaafi, naomba niongezee kijiswali...'tafsida' humaanisha nn? Sorry kwa interruption.
 
Tafsida ni neno linalotumiwa kupunguza makali ya neno lingine. kwa kiingereza huitwa "euphemism". Mathalan, kujifungua badala ya kuzaa (kwa binadamu), ashakumu kujisaidia badala ya kunya/kukojoa, n.k.
 
Bado sijamuelewa.

Kama si matusi, samahani ya nini?

Kama walivyosema wachangiaji waliotangulia, 'ashakum si matusi' ni kauli fupi inayomaanisha 'Samahani kwa kauli hii, simaanishi tusi'.

Kuna maneno ambayo ukiyatumia huwa ni kama vile matusi. Ikibidi yatumike kwa manufaa, kwa mfano katika ufafanuzi, maelezo, mafunzo n.k, basi inakuwa vyema kuanza kutahadharisha kwamba hukusudii kutukana unapoyataja.

Samahani ni katika kuonyesha uungwana.
 
Kama walivyosema wachangiaji waliotangulia, 'ashakum si matusi' ni kauli fupi inayomaanisha 'Samahani kwa kauli hii, simaanishi tusi'.
Sijauliza maana ya kauli "ashakum si matusi," nimesema, ashakum si matusi, ashakum ni nini? Akasema "ashakum" ni samahani. Nikasema kama si matusi samahani ya nini?

Samahani ni katika kuonyesha uungwana.
Nilivyofunzwa mimi, muungwana anasema "samahani sikudhamiria" baada ya kitendo, ukisema samahani kabla ya kosa ina maana umekusudia. Hata njiani huwezi kumwambia mtu "ndugu nataka kukukanyaga, lakini ashakum" halafu umkanyage, si utagombaniwa? Hiyo offense ni calculated, kusudi.

"Samahani si matusi" ikifatiwa na matusi! Kama si matusi samahani ya nini?
 
Samahani sababu katika hali ya kawaida hayo maneno yanaonekana kama matusi ila kwa context unataka kutumia sio matusi. Kwa hiyo unawaomba wanao kusikiliza kutumia effort ya ziada kwa kuelewa maneno yale in the context, na wala wasichukulie kama matusi.
Maneno yanakua matusi kufatana na context, ila ukisha sema hivo yanakua ni maneno ya kawaida.
Sijui umeelewa sasa?
 
Sijauliza maana ya kauli "ashakum si matusi," nimesema, ashakum si matusi, ashakum ni nini? Akasema "ashakum" ni samahani. Nikasema kama si matusi samahani ya nini?

Nilivyofunzwa mimi, muungwana anasema "samahani sikudhamiria" baada ya kitendo, ukisema samahani kabla ya kosa ina maana umekusudia. Hata njiani huwezi kumwambia mtu "ndugu nataka kukukanyaga, lakini ashakum" halafu umkanyage, si utagombaniwa? Hiyo offense ni calculated, kusudi.

"Samahani si matusi" ikifatiwa na matusi! Kama si matusi samahani ya nini?

Kama sababu hiyo hapo kwenye rangi nyekundu, mpelekee mwalimu wako hili swali lako.
 
Sentensi/tungo hiyo hutumiwa aghalabu unapotaka kutamka jambo ambalo lina "tusi/utusi" ama kutamka viungo vya siri bila ya kutaka kutumia tafsida.
Mf: Ashakum si matusi, mbwa walipomdondosha Mzee Kijogoo wakaziraru pumbu na mb.. yake.

wewe ni mwalimu mzuri.
 
Nimeelewa somo.
 
Back
Top Bottom