Nini kusudi la maisha hapa duniani?

Nini kusudi la maisha hapa duniani?

Ni swali gumu sana ila kusudi unaweza kuliweka hata wewe
Sio swali gumu, how about " Satisfaction" kuridhika ndio kila tunalikusudia, katika kila jambo tulifanyalo tunataka kutimiza malengo na tukuridhika. Bahati mbaya kuridhika, hali ambayo inatuletea furaha. Kuridhika na furaha zimekuwa za mpito na muda, hubadilika, na hivyo huwa za uwongo. Lengo letu kuu ni kutafuta kuridhika na furaha ya ukweli, ambayo habadiliki, milele daima. Inaitwa njia ya maisha na uzima wa milele.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu umesha kuwa jirani na wakati mtua anayekata roho, majuto anayoyapata huwezi pima kama anataka kata rufaa, yaani achiwe hata sekunde chache atekeleze kitu fulani kabla hajakata roho. Kila kitu kina kusudi la kuwepo just look arround you, excepy you.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata kama unajiona unakusudi, hamna chochote cha ajabu unaweza fanya. Kama kufa, utakufa nakubaki mifupa tu. Wewe fanya zako kazi, kula bata maisha yaende.
 
Fuata msingi uliojengewa na wazazi wako, labda Kama kwa akili zako timamu na kwa msaada wa kimungu utajua fika kuwa hawakuwa kwenye njia halisi vinginevyo kwenda kinyume na waliokuzaa na Mungu anakukataa.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwanini afuate ya wazazi wake na siso yeye aweke misingi yake na wanae waje wafuate ?
By the way kwanini tulazimishane kufuata misingi ya wazzi.
Kila mtu awe huru akishajitambua afuate misingi anayoona yeye inafaa.
 
Hii inanitia sana mashaka, waliotuletea hizo imani na itikani wao wenyewe hawana muda nazo. Muislam wa Africa anaamin ukiwa masikini ndio unaenda mbinguni nikitazama uarabuni dubai Emirates waarabu wanaishi kafahari kama hawapo dnuiani, tajiri wa Africa anaambiwa hizo mali utaziacha duniani usiangaike nazo mtafute Mungu. Kwa hiyo jamani tufe kifukara kisa Mungu hataki watu wake tuwe matajiri au nini. Mim nilishasahau kwenda kanisani maana naona ni propaganda tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu umesha kuwa jirani na wakati mtua anayekata roho, majuto anayoyapata huwezi pima kama anataka kata rufaa, yaani achiwe hata sekunde chache atekeleze kitu fulani kabla hajakata roho. Kila kitu kina kusudi la kuwepo just look arround you, excepy you.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nadhani si kila mtu huondokwa na roho kwa namna ulivyoeleza wewe hapo labda kama umekusudia kutisha watu kama njia ya kutafuta kuhalalisha kitu fulani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usijifananishe mwenendo na wanyama mkuu binadam we are so special tukubali tukatae maisha yetu yako plan since before na kwetu sis waislam timezaliwa ili tuje kumtukuza mungu wetu kwan tunapo kuabudu anajiskia fahar pia tukimsujudia malengo yanatimia sababu mwenye zimungu anapenda sana kunyenyekewa
Hakuna kusudi lolote lakuja duniani, hakuna anaye tuongoza, wanadamu wenyewe tunajiwekea malengo, sawa na wanyama wengine, au wadudu. Wanajiwekea maamuzi yao katika maisha, kutafuta furaha na chakula ilitu kuishi sikuziende adi mda wakufa utakapofika.

Ndio maana wanadamu tumejiwekea dini, ili kutupa matumaini na muongozo wa maisha, tumejitengenezea miungu fake nakuiabudu. Ni kwa sabab tunaitaj kitu kikubwa kutuzid, na tunaitaj kuongozwa.

Hakuna cha Mungu wala Mbinguni, hakuna Mungu mjinga kiasi icho wakuacha viumbe wake wanakufa bila hatia, eti kisa kula tunda. Kama Kweli Mungu yupo, nakweli katu adhibu kutupa kifo na magonjwa eti kisa wazee wetu Adam na Eva wamekula tunda, basi uyo Mungu mpumbavu kuliko kiumbe yoyote yule. Kwa maana ata wanyama na wadudu wanajali watoto zao, sasa Mungu hajali viumbe wake aliowaumba.

So iyo ina prove Mungu hayupo au alishakufa. Means hakuna lengo la binadamu kuja duniani. Tuishi tu kusogeza siku. Nakujitafutia our own purposes. Lakina hakuna main purpose for all.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
unajiskiaje mfano ukatengeneza gari ukaona inatembea barabarani ikiwa na speed kubwa utumiaji mzuri wa mafuta japo engine ni kubwaa ipo comfortable mtengenezaji utajiskiaje kila ukiiona gari yako iko road
 
Hii inanitia sana mashaka,, waliotuletea izo imani na itikani wao wenyewe hawana muda nazo. Muislam wa Africa anaamin ukiwa masikini ndio unaenda mbinguni nikitazama uarabuni dubai Emirates waarabu wanaishi kafahari kama hawapo dnuiani, tajiri wa Africa anaambiwa izo mali utaziacha duniani usiangaike nazo mtafute Mungu. Kwaiyo jaman tufe kifukara kisa Mungu hataki watu wake tuwe matajir au nin. Mim nilishasahau kwenda kanisani maana naona ni propaganda tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Hizo dini zililetwa Afrika kama mkakati wa kibiashara.

Anayekuletea Mungu wa upendo iweje aulete kwa kukuua, kukudhulumu, kukufanya mtumwa na kila aina ya ubaya?

Miaka yote mababu zetu wameishi vizuri tu Kwani Mungu alikuwa hafamu huku kuna watu mpaka anzishe unabii na utume kutoka mashariki ya kati kwanini asianzishe unabii na utume huku huku kwetu? Kwa watu ambao tunaongea lugha moja??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unatofauti gani na kikombe ulichokitumia kunywea chai leo asubuhi, do not just put yourself down and low like that?, jiulize kwani nini huliziki hata ufanikiwapo malengo yako uliyojipangania, you still fill like there is something more which you need to do to get satisfaction.

Sent using Jamii Forums mobile app
kwa swali hilo ulitegemea nikujibu kitu gani
lakini huridhiki na kutamani kuendelea kwa sababu bado hauna mwisho hiyo ndo sababu inayokufanya ata ukipata utafute tena hakuna sababu ya ziada kwa hapo
 
Habarini Wakuu,

Binadamu tunazaliwa katika mazingira tofauti tofauti yenye mila na desturi zake, lakini pia kuna mifumo mingi inayoongoza maisha yetu bila kujua nani mwanzilishi wa mifumo hiyo na kwa kusudi gani? Na je hii mifumo ndio kila kitu katika maisha yetu?

Wengi wetu tuliaminishwa vitu vingi tukiwa wadogo tukiwa hatuna uwezo wa kuhoji tukakubali kuishi maisha hayo hata kama hatuna furaha nayo, wachache wanaenda kinyume na mifumo iliyowekwa na jamii wanaonekana ni wasaliti.

Binafsi niliacha kwenda kanisani tangu nilipopata kipaimara sikuona sababu ya kumtukuza Mungu anaechoma watu moto, msimamo huu ulinifanya niingie kwenye vita ya watu wanaonizunguka.

Wakuu nyinyi nafikiria nini juu ya kusudi la maisha hapa duniani ni kufuata utaratibu uliowekwa na kuondoka au kuna jambo lingine ila binadamu hatulijui?
Biblia inaeleza wazi wazi kwamba Mungu aliumba mwanadamu na kwamba Yeye alimumba kwa ajili ya utukufu Wake (Isaya 43: 7). Kwa hiyo, kusudi la mwanadamu, kulingana na Biblia, ni tu kumtukuza Mungu.

Swali ngumu kujibu, pengine, ni kumtukuza Mungu ina maana gani? Katika Zaburi 100: 2-3, tunaambiwa tumwabudu Mungu kwa furaha na "kujua kwamba Bwana ndiye Mungu. Yeye ndiye alituumba, na sisi ni wake; sisi ni watu wake, kondoo wa malisho yake. "kumtukuza Mungu ni inajumuisha kutambua Mungu ni nani (Muumba wetu, kwanza kabisa) na kumsifu na kumwabudu Yeye kama vile.

Tunatimiza kusudi letu la kumtukuza Mungu pia kwa kuishi maisha yetu katika uhusiano na huduma yenye uaminifu kwake (1 Samweli 12:24; Yohana 17: 4). Kwa kuwa Mungu aliumba mwanadamu kwa mfano wake (Mwanzo 1: 26-27), kusudi la mwanadamu haliwezi kutekelezwa kama Mungu hayupo ndani yake. Mfalme Sulemani alijaribu kuishi kwa ajili ya radhi yake mwenyewe, lakini mwisho wa maisha yake alihitimisha kwamba maisha pekee yenye thamani ni ya heshima na utii kwa Mungu (Mhubiri 12: 13-14).

Katika hali yetu ya kuanguka, dhambi hututenganisha na Mungu na inakua vigumu sana kumtukuza sisi wenyewe. Lakini kwa njia ya dhabihu ya Yesu Kristo, uhusiano wetu na Mungu umeunganishwa-dhambi yetu imesamehewa na haitengenezi tena kizuizi kati ya Mungu na sisi (Waroma 3: 23-24).

Kwa kushangaza, tunaweza kumtukuza Mungu kwa sababu Yeye alitupa utukufu kwanza. Daudi anaandika katika Zaburi ya 8: 4-6, "Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, Na binadamu hata umwangalie?

Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; Umemvika taji ya utukufu na heshima;

Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake. "(Hii pia inarudiwa katika Waebrania 2: 6-8.) Aya hii inaonyesha lengo lingine ambalo Mungu amempa mwanadamu: mamlaka juu ya dunia (Mwanzo 1: 28-29). Tena, hata hivyo, hii inaweza tu kutekelezwa vizuri kupitia uhusiano sahihi na Mungu.

Tunapojua zaidi Muumba wetu ndipo unampenda zaidi (Mathayo 22: 37-38), tunaweza kuejielewa vizuri na kuelewa kusudi letu. Tuliumbwa kumletea utukufu. Mungu ana mipango na makusudi ya kipekee kwa kila mtu (Zaburi 139: 13-16), lakini tunaweza kujua kwamba, haijalishi jinsi vile mipango hiyo inaonekana, hatimaye itafikia utukufu Wake (Mithali 3: 6, 1 Wakorintho 10:31).
 
Maisha ya mwanadamu yana kusudi ambalo mwanadamu halijui na hatokaa alijue. Kusudi la maisha ya mwanadamu linajulikana na aliyemleta mwanadamu.
Kwanini unaamini tuliletwa na hatukutokea tu?
 
Mungu ametuumba ili tumjue, tumpende, tumtumikie na mwisho tufike kwake juu, Amina.
 
Usijifananishe mwenendo na wanyama mkuu binadam we are so special tukubali tukatae maisha yetu yako plan since before na kwetu sis waislam timezaliwa ili tuje kumtukuza mungu wetu kwan tunapo kuabudu anajiskia fahar pia tukimsujudia malengo yanatimia sababu mwenye zimungu anapenda sana kunyenyekewa

Sent using Jamii Forums mobile app
Huo utumwa siwez, yani umezaliwa kuabudu duh. Kwangu ayo ni mateso. Mi binafsi sitakuja kusali na kuabudu
 
Biblia inaeleza wazi wazi kwamba Mungu aliumba mwanadamu na kwamba Yeye alimumba kwa ajili ya utukufu Wake (Isaya 43: 7). Kwa hiyo, kusudi la mwanadamu, kulingana na Biblia, ni tu kumtukuza Mungu.

Swali ngumu kujibu, pengine, ni kumtukuza Mungu ina maana gani? Katika Zaburi 100: 2-3, tunaambiwa tumwabudu Mungu kwa furaha na "kujua kwamba Bwana ndiye Mungu. Yeye ndiye alituumba, na sisi ni wake; sisi ni watu wake, kondoo wa malisho yake. "kumtukuza Mungu ni inajumuisha kutambua Mungu ni nani (Muumba wetu, kwanza kabisa) na kumsifu na kumwabudu Yeye kama vile.

Tunatimiza kusudi letu la kumtukuza Mungu pia kwa kuishi maisha yetu katika uhusiano na huduma yenye uaminifu kwake (1 Samweli 12:24; Yohana 17: 4). Kwa kuwa Mungu aliumba mwanadamu kwa mfano wake (Mwanzo 1: 26-27), kusudi la mwanadamu haliwezi kutekelezwa kama Mungu hayupo ndani yake. Mfalme Sulemani alijaribu kuishi kwa ajili ya radhi yake mwenyewe, lakini mwisho wa maisha yake alihitimisha kwamba maisha pekee yenye thamani ni ya heshima na utii kwa Mungu (Mhubiri 12: 13-14).

Katika hali yetu ya kuanguka, dhambi hututenganisha na Mungu na inakua vigumu sana kumtukuza sisi wenyewe. Lakini kwa njia ya dhabihu ya Yesu Kristo, uhusiano wetu na Mungu umeunganishwa-dhambi yetu imesamehewa na haitengenezi tena kizuizi kati ya Mungu na sisi (Waroma 3: 23-24).

Kwa kushangaza, tunaweza kumtukuza Mungu kwa sababu Yeye alitupa utukufu kwanza. Daudi anaandika katika Zaburi ya 8: 4-6, "Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, Na binadamu hata umwangalie?

Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; Umemvika taji ya utukufu na heshima;

Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake. "(Hii pia inarudiwa katika Waebrania 2: 6-8.) Aya hii inaonyesha lengo lingine ambalo Mungu amempa mwanadamu: mamlaka juu ya dunia (Mwanzo 1: 28-29). Tena, hata hivyo, hii inaweza tu kutekelezwa vizuri kupitia uhusiano sahihi na Mungu.

Tunapojua zaidi Muumba wetu ndipo unampenda zaidi (Mathayo 22: 37-38), tunaweza kuejielewa vizuri na kuelewa kusudi letu. Tuliumbwa kumletea utukufu. Mungu ana mipango na makusudi ya kipekee kwa kila mtu (Zaburi 139: 13-16), lakini tunaweza kujua kwamba, haijalishi jinsi vile mipango hiyo inaonekana, hatimaye itafikia utukufu Wake (Mithali 3: 6, 1 Wakorintho 10:31).
Mwanangu umeshika biblia, bible verses kama zote. Uo mda wakusoma biblia si ungesoma vitu vya maana. Dini inaonyesha kias gan dini inavyotupotezea mda.
 
Mungu ametuumba ili tumjue, tumpende, tumtumikie na mwisho tufike kwake juu, Amina.
Nisimahe mkuu kama natakuwa na kukwaza ila nipo kwenye sintofahamu......kwanini atulete duniani ? Kwanini apoteze mda kutuleta kwani huko mbinguni si tungemwabudu na kumsifu milele yote,kama anatupenda kweli na nimwenye wivu kwanini atupe akili ambayo inaweza jiuliza uwepo wake ? Kwanini aampe shetani mamlaka ya kuharibu mifumo ya mwanadamu wakuishi? Amri ya kwanza inasema mpende bwana mungu wako kama nafsi yako ila yesu anasema huezi sema unampenda mungu usiemuona huku unamchukia jirani yako unaemuona afu umpenda mungu? Bado maswali ni mengi sana je bila kifundishwa dini na uwepo wa mungu kutoka kwa wazungu ili watumikishe je tungekuwa mpaka leo tunaomba mizimu na kuamini jua ndo mungu?...... naombeni nisaidieni wakuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom