Nini kusudi la maisha hapa duniani?

Nini kusudi la maisha hapa duniani?

Mwanangu umeshika biblia, bible verses kama zote. Uo mda wakusoma biblia si ungesoma vitu vya maana. Dini inaonyesha kias gan dini inavyotupotezea mda.
Nimesoma michango nimeota una matatizo ya akili, kama sio Hayawahi, yaani hufikirii.

Nakuuliza swali moja au mawili. Kisha nitakuja kukuelekeza kitu kinachoitwa "Self Evident Truth(Bayyinah)".

1. Je dunia na vilivyomo vimejiumba au
2. Vimetokea pasi na chochote ?
 
Hakuna kusudi lolote lakuja duniani, hakuna anaye tuongoza, wanadamu wenyewe tunajiwekea malengo, sawa na wanyama wengine, au wadudu. Wanajiwekea maamuzi yao katika maisha, kutafuta furaha na chakula ilitu kuishi sikuziende adi mda wakufa utakapofika.
Inaonekana hujui chochote katika hili unali liongoelea na kuliandikia kwalo. Ngoja nikusaidie kwa mtindo huu. Ukijiangalia wewe mwenyewe kwa umakini unaona nini au unapata ishara gani ? Au ukiona gari unaona nini kwenye gari hilo au unapata ishara gani ?
Hakuna cha Mungu wala Mbinguni, hakuna Mungu mjinga kiasi icho wakuacha viumbe wake wanakufa bila hatia, eti kisa kula tunda. Kama Kweli Mungu yupo, nakweli katu adhibu kutupa kifo na magonjwa eti kisa wazee wetu Adam na Eva wamekula tunda, basi uyo Mungu mpumbavu kuliko kiumbe yoyote yule. Kwa maana ata wanyama na wadudu wanajali watoto zao, sasa Mungu hajali viumbe wake aliowaumba.
Nani alikwambia kifo ni adhabu ?

Kwahiyo kufa bila hatia ndio Mola hawajaki viumbe wake ? Inaonekana una hisi ya kuwa kifo ndio mwisho wa maisha sio ? Kufikiri kwa namna hii ni kufikiri kitoto na ujinga usiofaa hata kupigiwa mfano.
So iyo ina prove Mungu hayupo au alishakufa. Means hakuna lengo la binadamu kuja duniani. Tuishi tu kusogeza siku. Nakujitafutia our own purposes. Lakina hakuna main purpose for all.
Hapo huja "prove" ya kuwa Mungu hayupo, bali umeandika juu ya hisia zako kwazo zinaonyesha hujui chochote kuhusu Mungu, kwani uko kinyume na yale yote yanayo muhusu Mungu, hilo ni tatizo la kutojitambua, halafu unatumia mawazo kama ushahidi au ndio ukweli, hili ni tatizo la mtu kuwa mjinga sana.
 
Nisimahe mkuu kama natakuwa na kukwaza ila nipo kwenye sintofahamu......kwanini atulete duniani ? Kwanini apoteze mda kutuleta kwani huko mbinguni si tungemwabudu na kumsifu milele yote,kama anatupenda kweli na nimwenye wivu kwanini atupe akili ambayo inaweza jiuliza uwepo wake ? Kwanini aampe shetani mamlaka ya kuharibu mifumo ya mwanadamu wakuishi? Amri ya kwanza inasema mpende bwana mungu wako kama nafsi yako ila yesu anasema huezi sema unampenda mungu usiemuona huku unamchukia jirani yako unaemuona afu umpenda mungu? Bado maswali ni mengi sana je bila kifundishwa dini na uwepo wa mungu kutoka kwa wazungu ili watumikishe je tungekuwa mpaka leo tunaomba mizimu na kuamini jua ndo mungu?...... naombeni nisaidieni wakuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Sheria ya kumpenda adui yako ikigeuzwa kwa Mungu je Mungu anampenda adui yake shetani?
 
KUSUDI LA MIMI KUWEPO DUNIANI NI LIPI?

Hili ni swali ambalo lilikuwa sana katika kichwa changu kabla sijamfahamu Yesu Kristo, vilevile lipo katika vichwa vya watu wengi leo hii duniani, na nimeshaulizwa pia mara nyingi na baadhi ya watu?.. Hili swali linaibuka kutokana na jinsi watu tulivyojikuta tu ghafla tumetokea duniani bila hata ya kikao Fulani cha makubaliano, na jinsi tunavyoondoka ghafla bila hata ya taarifa zozote,.. Hapo ndipo tunajiuliza sasa maana ya Maisha ni nini? Na ni nani aliye nyuma yake?..Hivyo inatufanya kila mmoja kwa njia yake mwenyewe aanze kuchunguza na kutafiti na kujaribu kila njia na kila mbinu, ili mwisho wa siku apate jibu lake moja ambalo litampa sababu ya yeye kuwepo hapa duniani..

Hata kama ni wewe leo hii unajiuliza swali hilo, hujakosea hata kidogo kufiria hivyo, unawaza vyema kabisa.. Lakini nataka nikupe ushauri mmoja, kabla hujaanza kuchunguza kwa njia zako wewe mwenyewe embu jaribu kwanza kutafuta waliowahi kujiuliza swali kama hilo na hatua walizochukua na mwisho wao ukawaje?..Ili usije ukajikuta unarudia njia zilezile za kwao, na mwisho wa siku ukafikia pale pale walipo ukawa umepoteza muda mwingi wa utafiti ambao sio wa lazima.

Lakini leo hii nitakupa majibu ya kibiblia.. Na kitabu pekee ambacho kimetoa majibu ya maswali hayo ni kitabu cha Muhubiri..Hivyo kama unahitaji kupata jibu la swali hilo nakushauri ukisome kitabu chote kile kwa utaratibu na kwa umakini kisha utapata jibu lake mwishoni.

Aliyeandika kitabu kile ni Sulemani mwana wa Daudi, ambaye biblia inarekodi sio tu alikuwa ni mfalme mkuu sana bali pia alikuwa ni mtu mwenye Hekima kuliko watu wote waliokuwa wanaishi duniani wakati ule, na alikuwa pia ni mtu Tajiri ambaye hakukuwa na mfano wako, kabla yake na hata baada yake..

Sasa ilifikia kipindi akatamani kujua sana nini maana ya Maisha, na atafanya nini ili apate raha duniani, au apate jibu moja la uhakika kuhusu Maisha ya wanadamu,..Akasema nitajaribu kila kitu, na kila njia kwanza naanzana na Elimu, akaitafuta elimu kwa bidii, akaipata akawa na elimu kubwa ya kufahamu kila kila mnyama, na mmea, na viumbe vyote duniani (1Wafalme 4:33-34) na hekima iliyopo ndani yao, akaweza kutatua mafumbo magumu sana, akatunga mithali nyingi sana. Na akaandika vitabu vingi sana, hiyo yote ilikuwa ni kwa lengo la kupata labda jibu Fulani la Maisha pengine angegundua jambo Fulani ambalo lingemsaidia kupata kanuni rahisi ya watu kuishi duniani, au Maisha ya raha, na ya uhuru au ya furaha..lakini alipojaribu kufanya hivyo, ndivyo alivyozidi kuongezea huzuni na masikitiko anasema hivyo (Mhubiri 1:18) ..

Akasema nitajaribu wanawake..Akaenda kuoa wake 700 wazuri wanaotoka katika majumba ya kifalme tu, na Masuria 300, aangalie labda akiwa na hao atayafanya Maisha kuwa bora duniani, au ya furaha ..hilo nalo halikumletea majibu aliyokuwa anayatafuta..

Akajajiengea makasri makubwa, na kujiwekea posho ya chakula cha mwaka mzima, kila siku kwake ilikuwa ni sherehe..lakini bado hakukipata alichokuwa anakitafuta..

Akajaribu pombe, akawa anakunywa divai, lakini bado hakuna lolote aliloliona ndani yake lingeweza kufichua fumbo kubwa la maisha..akajaribu “upumbavu na wazimu” biblia inasema hivyo katika (Mhubiri 1:17), yaani mambo yote ambayo unaweza kuona ni ya kipumbavu, au wendawazimu kama vile kujitukuza, pengine kucheza dansi, n.k. lakini hakuna hata mmoja liliweza kumpa maana ya mambo yote, ..

Akajaribu kuwa na malengo makubwa akawa mfanya biashara mkubwa duniani, aione labda akishafanikiwa hapo atakipata kitu alichokuwa anakitafuta..lakini bado anasema hakukipata..

Ndipo katika dakika za mwisho, sasa katika uzee wake..Anagundua siri hii kuwa mambo yote ni ubatili, mito inapotoka ndipo huko huko inaporudi, jua linapochomozea ndipo huko huko litakuja kuchomozea tena, upepo unapovuma ndio kulekule utakaporudi kila kitu kipo katika mzunguko wake, Yule Mungu niliyeanzana naye, nitakapojitaabisha kwenda mbali naye, nitakaposema simtaki tena nataka nitafute mwenyewe akili zangu niijue ukweli wa Maisha, ndiye yule yule mwisho wa siku nitamrudia…

Unaweza Ukaona kumjua yeye kunakunyima uhuru wa kuishi..Utakwenda kutafuta unachokitaka katika moyo wako, lakini mwisho wa siku utamrudia yeye..Na hapo utakuwa umeshachelewa sana..

Ndio maana Mhubiri anamalizia kwa kusema…Jumla ya mambo yote ni UMCHE MUNGU…

Mhubiri 12:13 “Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.
14 Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya”.

Unaona,..Mhubiri ni mmojawapo wa waliotusaidia sisi kufanya utafiti, ili na sisi tusianze tena kupoteza muda mwingi kukimbizana na mambo ya Maisha tuanze kutafiti kwa akili zetu..tukidhani kuwa tutafika mahali Fulani paki pekee ambako wengine hawajafika kuhusu maisha,…kumbe tupo kwenye mzunguko ule ule wa zamani..

Leo hii tutamwacha Mungu tukatafute fedha, lakini tukishaiapata bado tutaona mbona hatujalipata lile kusudi lenyewe ndani yetu?..Tutamdharau Mungu tutasema tukatafute hekima yetu wenyewe…ni kweli tutafahamu vyote lakini mwisho wa siku swali litaendelea kubakia pale pale maana ya Maisha ni nini?

Jibu pekee la maana ya Maisha lipo kwa yeye aliyetuumba?

Mche yeye basi!… Na kumcha yeye ni kuingia katika kanuni yake.. Ambayo aliiweka tangu zamani kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwenguni.. Na kanuni yenyewe ndio hii..

Yohana 3:16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele”.

Ukimpata Yesu Kristo, hapo pekee ndipo utakapojua maana ya Maisha ni nini.. Kwasababu yeye anakupa uzima wa milele..Ukiwa na uzima wa milele wasiwasi wako utakuwa ni nini tena?….hutakuwa na hofu yoyote, na Maisha yako yatakuwa ya amani na furaha hapa duniani sikuzote..yaliyo mbali na utumwa wa hofu za Maisha..Hofu za kuogopa kesho itakuwaje..kwasababu Sulemani ndivyo alivyosema katika ..

Mhubiri 8:6 “Kwa maana kwa kila shauri kuna wakati na hukumu; kwa sababu mashaka ya mwanadamu yaliyo juu yake ni makubwa;
7 kwa kuwa hajui yatakayokuwako; kwa maana ni nani awezaye kumweleza jinsi yatakavyokuwa?

Hivyo kama na wewe bado unatafuta maaana ya Maisha, basi leo hii fahamu kuwa jibu ndio hilo hapo juu..acha kutanga tanga, mfuate YESU, akuponye nafsi yako, akupe tumaini la uzima wa milele..Uishi kwa amani siku zako zote ulizopo hapa duniani..Kwasababu kwingine kote hutapata..na kama ukijaribu kutafuta peke yako, ukweli ni kwamba utarudi hapo hapo kwa Mungu..Na wakati huo utakuwa umeshachelewa tayari.

Ikiwa upo tayari kufanya hivyo leo..Na kwamba unataka Kristo aingie ndani ya Maisha yako, akupe tumaini hilo na amani hiyo ya wokovu..

Basi uamuzi unaoufanya ni wa busara sana ambao hautakaa uujutie maisha yako yote kama ilivyokuwa hata kwetu sisi. Unachopaswa kufanya, hapo ulipo, chukua muda mchache ujitenge peke yako. Kisha piga magoti, kisha fuatisha sala hii kwa Imani, ukijua kuwa Mungu yupo hapo karibu na wewe pembeni yako kukusikia..Kisha ukiwa sasa katika utulivu Sema sala hii kwa sauti.

EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.
ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.
AMEN.

Sasa ikiwa umefuatisha sala hiyo kwa Imani ..Hatua iliyobakia kwako ni kuithitisha toba yako kwa Vitendo ikiwa ulikuwa unafanya mambo yote ambayo hayampendezi Mungu unayaacha na kujitenga nayo, Sasa Mungu akishaona umegeuka kwa vitendo basi toba yako anaipokea na atakuja ndani yako wakati huo huo na kufanya makao ya milele kwako. Vile vile unahitaji, kutafuta kanisa la kiroho ambalo utajumuika na wakristo wengine katika kumwambudu Mungu, na kujifunza biblia ili uukulie wokovu. Na vilevile ili upate ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako.

Ukizingatia hayo Bwana atakuangazia Nuru zake za wokovu daima hadi siku ile ya mwisho.

Ubarikiwe sana
 
Nawakumbusha tu Charlie Chaplin alizaliwa 1889 na kufariki 1977 akiwa na miaka 88 na filamu yake ya kwanza kutengeneza ilikuwa mwaka 1924,hii inamaanisha kwamba kulikuwepo mwaka 1889 na pia kulikuwa na mwaka 1700 na kulikuwepo na mwaka 1500 and so on hadi 100 na huku watu walikuwa wanaishi sema tu enzi hizo kulikuwa bado hakuna technology ya kuhifadhi video.

Je kabla ya mwaka 0 kulikuwa hakuna watu? Jibu ni kwamba walikuwepo, je walijiumba wenyewe? Kama walijiumba wenyewe inakuwaje wakajiumba kwa jinsia mbili yaani ke na me? Ilikuwaje automatic wajiumbe ke na me? Jibu ni kwamba kulikuwa na kitu chenye nguvu kilichofanya hayo ambaye ndio Mungu.
 
Kwanini unaamini tuliletwa na hatukutokea tu?
Hilo nimejaribu kulielezea kwenye uzi wangu wa 'ulimwengu ndani ya fikra zangu: maoni yangu kuhusu mungu, uwepo wa maisha, shetani na dhambi' uzi huu ulihamishwa jukwaa la dini sijui kama una access huko.

Ila kukujibu hilo swali nitachomoa kipande kidogo kwenye huo uzi nilipojaribu kuelezea mtizamo wangu kuhusu mwanzo wa maisha

" Kwanza, Sababu pekee ya mimi kuamini katika uwepo wa Mungu ni hii. Ili kitu chochote kiweze kuwepo ni lazima kiwe kimetengenzwa na kiumbe au kitu Fulani chenye uelewa wa juu kuliko hicho kilichotengenezwa. Mfano, magari yapo kwa sababu yupo binadamu ambayo ana ufahamu mkubwa kuliko magari ambaye ndiye aliyetengeneza magari hayo. Sasa ilikujua ni nani hasa iliyewajibika kuutengeneza ulimwengu huu jinsi ulivyo sasa tunapaswa kuurudisha muda nyuma ili kuusoma na kuona myororo wa ubuni na uumbaji. Kwa kuwa kiuhalisia hatuwezi kuurudisha muda kiyumenyume ili kuona dhahiri ni nini kilitokea, hivyo tunafannya kwa makisio, na katika kufaya hivyo tunaweza kupata majibu mawili ambayo ni; aidha kuna myororo usiokoma wa ubuni na uumbaji ama tunaweza kufika mahali mnyororo unakoma na kupata kitu kimoja ambacho kilisababisha vitu vingie vyote vitokee.

Dhana ya mnyororo wa uumbaji usiokoma hauingii akilini kwa sababu kukosekana ukomo ni wazo lililo nje ya uwezo wa fikra za mwaadamu. Na kama nilivyosema hapo awali kuwa fikra za mwanadamu zina ukomo hivyo hakuna namna zinaweza kuelewa kitu kisicho na kikomo, hivyo hilo wazo nikaachana nalo. Wazo ambalo nililikubali ni kuwa kwenye mnyororo wa uumbaji kuna mahali kuna ukomo ambapo hapo ndipo kuna kiumbe/tukio/kitu kilichosababisha matukio mengine yatokee na hatimaye kufanya ulimwengu uwe jinsi ulivyo sasa.

Hivyo kwa ufupi mimi kwa upade wangu Mungu ni tukio/roho/kiumbe/ ama kitu chochote kile ambacho kilitokea ama kwa bahati mbaya ama kwa makusudi na kusababisha ulimwengu uwe hivi ulivyo. Nadhani hadi hapo nitakuwa nimeeleweka."
 
Hakuna kusudi lolote lakuja duniani, hakuna anaye tuongoza, wanadamu wenyewe tunajiwekea malengo, sawa na wanyama wengine, au wadudu. Wanajiwekea maamuzi yao katika maisha, kutafuta furaha na chakula ilitu kuishi sikuziende adi mda wakufa utakapofika.

Ndio maana wanadamu tumejiwekea dini, ili kutupa matumaini na muongozo wa maisha, tumejitengenezea miungu fake nakuiabudu. Ni kwa sabab tunaitaj kitu kikubwa kutuzid, na tunaitaj kuongozwa.

Hakuna cha Mungu wala Mbinguni, hakuna Mungu mjinga kiasi icho wakuacha viumbe wake wanakufa bila hatia, eti kisa kula tunda. Kama Kweli Mungu yupo, nakweli katu adhibu kutupa kifo na magonjwa eti kisa wazee wetu Adam na Eva wamekula tunda, basi uyo Mungu mpumbavu kuliko kiumbe yoyote yule. Kwa maana ata wanyama na wadudu wanajali watoto zao, sasa Mungu hajali viumbe wake aliowaumba.

So iyo ina prove Mungu hayupo au alishakufa. Means hakuna lengo la binadamu kuja duniani. Tuishi tu kusogeza siku. Nakujitafutia our own purposes. Lakina hakuna main purpose for all.
Well said ..nakazia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kujifunza ili uishi ili ufe

ᴮᵉʷᵃʳᵉ ᵒᶠ ᵗʰᵉ ᶜᵒᵛⁱᵈ ⁻ ¹⁹
 
Mkuu umesha kuwa jirani na wakati mtua anayekata roho, majuto anayoyapata huwezi pima kama anataka kata rufaa, yaani achiwe hata sekunde chache atekeleze kitu fulani kabla hajakata roho. Kila kitu kina kusudi la kuwepo just look arround you, excepy you.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa yaani ulitegemea mtu akate roho then asiwe na majuto .. Wakati anaacha Mali zake .watu aliowazoea etc
Pia anaweza kuwa na majuto ambayo yana sababishwa na uongo aliojazwa kichwani kupitia masuala mbali mbali ya kiimani ...so akawa anaamini kuwa anakufa na huko aendapo anaenda kuchomwa moto kweli kumbe yuko brainwashed

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii inanitia sana mashaka, waliotuletea hizo imani na itikani wao wenyewe hawana muda nazo. Muislam wa Africa anaamin ukiwa masikini ndio unaenda mbinguni nikitazama uarabuni dubai Emirates waarabu wanaishi kafahari kama hawapo dnuiani, tajiri wa Africa anaambiwa hizo mali utaziacha duniani usiangaike nazo mtafute Mungu. Kwa hiyo jamani tufe kifukara kisa Mungu hataki watu wake tuwe matajiri au nini. Mim nilishasahau kwenda kanisani maana naona ni propaganda tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaa umeona hapo ..nia na madhumuni nikum brainwash mtu mweusi asione umuhimu wa kua na Mali ..kwa sababu ukiwa na Mali ni rahisi kuweza kuwa mtawala

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizo dini zililetwa Afrika kama mkakati wa kibiashara.

Anayekuletea Mungu wa upendo iweje aulete kwa kukuua, kukudhulumu, kukufanya mtumwa na kila aina ya ubaya?

Miaka yote mababu zetu wameishi vizuri tu Kwani Mungu alikuwa hafamu huku kuna watu mpaka anzishe unabii na utume kutoka mashariki ya kati kwanini asianzishe unabii na utume huku huku kwetu? Kwa watu ambao tunaongea lugha moja??

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaaa ...kongole

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hilo nimejaribu kulielezea kwenye uzi wangu wa 'ulimwengu ndani ya fikra zangu: maoni yangu kuhusu mungu, uwepo wa maisha, shetani na dhambi' uzi huu ulihamishwa jukwaa la dini sijui kama una access huko.

Ila kukujibu hilo swali nitachomoa kipande kidogo kwenye huo uzi nilipojaribu kuelezea mtizamo wangu kuhusu mwanzo wa maisha

" Kwanza, Sababu pekee ya mimi kuamini katika uwepo wa Mungu ni hii. Ili kitu chochote kiweze kuwepo ni lazima kiwe kimetengenzwa na kiumbe au kitu Fulani chenye uelewa wa juu kuliko hicho kilichotengenezwa. Mfano, magari yapo kwa sababu yupo binadamu ambayo ana ufahamu mkubwa kuliko magari ambaye ndiye aliyetengeneza magari hayo. Sasa ilikujua ni nani hasa iliyewajibika kuutengeneza ulimwengu huu jinsi ulivyo sasa tunapaswa kuurudisha muda nyuma ili kuusoma na kuona myororo wa ubuni na uumbaji. Kwa kuwa kiuhalisia hatuwezi kuurudisha muda kiyumenyume ili kuona dhahiri ni nini kilitokea, hivyo tunafannya kwa makisio, na katika kufaya hivyo tunaweza kupata majibu mawili ambayo ni; aidha kuna myororo usiokoma wa ubuni na uumbaji ama tunaweza kufika mahali mnyororo unakoma na kupata kitu kimoja ambacho kilisababisha vitu vingie vyote vitokee.

Dhana ya mnyororo wa uumbaji usiokoma hauingii akilini kwa sababu kukosekana ukomo ni wazo lililo nje ya uwezo wa fikra za mwaadamu. Na kama nilivyosema hapo awali kuwa fikra za mwanadamu zina ukomo hivyo hakuna namna zinaweza kuelewa kitu kisicho na kikomo, hivyo hilo wazo nikaachana nalo. Wazo ambalo nililikubali ni kuwa kwenye mnyororo wa uumbaji kuna mahali kuna ukomo ambapo hapo ndipo kuna kiumbe/tukio/kitu kilichosababisha matukio mengine yatokee na hatimaye kufanya ulimwengu uwe jinsi ulivyo sasa.

Hivyo kwa ufupi mimi kwa upade wangu Mungu ni tukio/roho/kiumbe/ ama kitu chochote kile ambacho kilitokea ama kwa bahati mbaya ama kwa makusudi na kusababisha ulimwengu uwe hivi ulivyo. Nadhani hadi hapo nitakuwa nimeeleweka."
@kiranga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nisimahe mkuu kama natakuwa na kukwaza ila nipo kwenye sintofahamu......kwanini atulete duniani ? Kwanini apoteze mda kutuleta kwani huko mbinguni si tungemwabudu na kumsifu milele yote,kama anatupenda kweli na nimwenye wivu kwanini atupe akili ambayo inaweza jiuliza uwepo wake ? Kwanini aampe shetani mamlaka ya kuharibu mifumo ya mwanadamu wakuishi? Amri ya kwanza inasema mpende bwana mungu wako kama nafsi yako ila yesu anasema huezi sema unampenda mungu usiemuona huku unamchukia jirani yako unaemuona afu umpenda mungu? Bado maswali ni mengi sana je bila kifundishwa dini na uwepo wa mungu kutoka kwa wazungu ili watumikishe je tungekuwa mpaka leo tunaomba mizimu na kuamini jua ndo mungu?...... naombeni nisaidieni wakuu

Sent using Jamii Forums mobile app
binadamu aliletwa duniani kwa sababu alikiuka sharti alilopewa na Mungu (Mwanzo; 1:16-17), kwahiyo, adhabu mojawapo ilikua ni kumfukuza bustani ya Eden ili asije kula matunda ya mti wa uzima akaishi milele ( Mwanzo; 3:22).
Akili aliyotupatia ni kwasababu alitaka mwanadamu akatawale viumbe wengine wote na ndio maana alisema tumuumbe mwanadamu kwa mfano wetu, it means unakuwa na uwezo wa kufikiri tofauti na viumbe wengine, ndio maana ata hapo unajiuliza uwepo wa Mungu;... nyani, tembo, nzi au ata mende hawawezi fikiria uwepo wa Mungu. (Mwanzo; 1:26-28)
Of course hauwezi kumpenda Mungu usiyemuona wakati unamchukia jirani yako unayemuona, kwasababu kadili unavyompenda na kumtendea wema yule unayemuona ndio hivyo hivyo unavyompendeza Mungu pia (Luka; 10; 27-37)
Hayo maswali mengine nitasaidiwa na wakuu humu.

Waroma (9; 20-21)
Lakini, ewe binadamu, u nani hata uthubutu kumhoji Mungu? Je, chungu chaweza kumwuliza mfinyanzi wake: "Kwa nini umenitengeneza namna hii? " Mfinyanzi anaweza kuutumia udongo apendavyo na kufinyanga vyungu viwili kwa udongo uleule; kimoja kwa matukizi ya heshima, na kingine kwa matumizi ya kawaida.
 
Pole Sana kwa kwenda nje ya mstari na kumwacha Mungu...Kusudi la kitu analijua aliekitengeneza...Ukiona tractor kabla hujajua kazi yake lazima utamfikiria na kumsoma mtengenezaji wake ili ujue limetengenezwa kwa kazi gani???
Mathalani lorry,,water bouzer na crane,,pia basi. Ukitaka kujua lengo lako la kuwa hapa duniani basi analo mmoja tu,,,,,Aliekuumba.Sifa zake ni Mwingi wa huruma/rehema,,mpole wa hasira na mwenye kusamehe makosa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom