Maisha ni Maigizo: Ukweli ni Upi?

Maisha ni Maigizo: Ukweli ni Upi?

bless on

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2026
Posts
741
Reaction score
1,729
Tuache kudanganyana na kupotezeana muda. Maisha haya tunayoishi ni maigizo makubwa sana ambayo tumeyakuta yameshaandaliwa. Hakuna hata mmoja wetu aliyeulizwa anataka nini kabla hajaja hapa duniani.

Sote tumezaliwa tukiwa uchi, hatuna nguo, hatuna dini, wala hatuna jina. Lakini kabla hata hujajua kupumua vizuri, watu washaanza kukulazimisha kufuata mambo yao. Mlikuta watu wanasali, mkajumuika nao. Mlikuta dini zimeshapangwa, mkazivaa kama mlivyovaa nguo mlizovishwa.

Kila upande unajiona wao ndio wako sahihi. Huyu anasema Mungu wake ni hivi, yule anasema Mungu wake ni vile. Watu wanabishana, wanachukiana, na hata kuuana kwa ajili ya vitu walivyovikuta vimeshaandikwa kwenye vitabu.

Lakini ukweli ni upi? Ukweli ni kwamba hakuna anayejua chochote! Tunadanganyana hapa duniani kwa maneno ya kurithi, lakini mioyo yetu imejaa hofu kwa sababu hatujui nini kiko upande wa pili.

Ule ukweli mnaoupigania, ule ukweli mnaoubishania, hamtaujua mkiwa bado mnakula ugali. Siku mtakapokata roho, siku macho yatakapoganda na mwili kurudi kuwa uchi kama mlivyozaliwa, ndipo utaelewa.

Kwani hamuoni? Mwanadamu alizaliwa akiwa hana kitu, lakini akili yake ikajaa hofu. Kwa sababu ya hiyo hofu ya kutojua tunatoka wapi na tunaenda wapi, binadamu wakatengeneza mifumo.

Wakaleta dini wakati ambapo hakukuwa na dini. Wakachora mipaka, wakaweka sheria, wakasema ukifanya hivi utachomwa, ukifanya vile utabarikiwa.

Hivi mnafikiri Mungu anahitaji majengo yenu ya kifahari au kelele zenu za kila jumapili na ijumaa ili ajijue yeye ni nani? Sisi ndio wenye njaa ya majibu, yeye hana njaa hiyo! Tulizaliwa uchi, tukavikwa imani za kurithi, na tutakufa tukiwa bado tunabishana kuhusu kitu ambacho hakuna aliyewahi kukipiga picha akakileta huku duniani!.

Watu wanatumia jina la Mungu kututisha. Wanatufanya tuishi kwa uoga utafikiri sisi ni watumwa. Lakini ukweli unabaki palepale mchungaji anakufa, shekhe anakufa, na tajiri anakufa. Wote wanaishia shimoni kulekule ambako hakuna anayerudi kusema jamani, kule ndani mambo yako hivi.

Mnabishana kuhusu vitabu vilivyoandikwa na mikono ya watu miaka maelfu iliyopita, wakati hamuujui hata ukweli wa dakika tano zijazo za maisha yenu. Ni upofu wa hali ya juu! Tunajifanya tunajua mbingu, wakati hata ardhi tunayokanyaga hatuielewi vizuri.
 
Ukishajua tatizo liko wapi wewe ni mshindi. Sa kwa kuwa umeshajua ilivyo unaweza ukafanya yaan ujifanye, nasema ufanye linalokuhusu au unaweza ukanywa dawa tu ulale
Tatizo lipo kwa Mungu wa mchongo
 
Ana hoja, asikilizwe

Kwangu mimi sioni igizo lolote, ila pattern ya maisha ya mtu inakuwa determined na his orher predecessors.

Mengine unaweza ukaondokana nayo kama umasikini ila mambo ya dini kidogo ni magumu yanahitaji akili iliyo makini na chetuzi

Je, nani anasimama kwenye ukweli na haki? bado tunabishana
 
Ana hoja, asikilizwe

Kwangu mimi sioni igizo lolote, ila pattern ya maisha ya mtu inakuwa determined na his orher predecessors.

Mengine unaweza ukaondokana nayo kama umasikini ila mambo ya dini kidogo ni magumu yanahitaji akili iliyo makini na chetuzi

Je, nani anasimama kwenye ukweli na haki? bado tunabishana
Mkuu najibu hapo kwenye HAKI na UKWELI kama ifuatavyo👇
Duniani hakuna HAKI ni vurugu tu Dunia inaendeshwa kimaslahi.
UKWELI unafichwa ili uongo utawale kwa maslahi ya watu wakubwa wenye nguvu mifano ipo mingi na inaonekana kwa wale walioruhusu akili zao kuwa huru.
 
Nakubaliana nawe. Dunia imejaa maigizo na unafiki. Baadhi ya watu hudanganywa na kudanganyika, baadhi ya watu hujidanganya wenyewe.

Kila mtu akionesha sura yake halisi bila kufanya unafiki, hapatakalika katu!
 
Nakubaliana nawe. Dunia imejaa maigizo na unafiki. Baadhi ya watu hudanganywa na kudanganyika, baadhi ya watu hujidanganya wenyewe.

Kila mtu akionesha sura yake halisi bila kufanya unafiki, hapatakalika katu!
Kila mtu akionesha sura yake halisi bila kufanya unafiki, hapatakalika katu!

Exactly, umeongea ukweli tupu mfano majority wastuke kwamba DINI ni utapeli aloo Dunia haitatawalika.
 
Back
Top Bottom