Nini kusudi la maisha hapa duniani?

Nini kusudi la maisha hapa duniani?

Wayo

Senior Member
Joined
Aug 18, 2017
Posts
179
Reaction score
420
Habarini Wakuu,

Binadamu tunazaliwa katika mazingira tofauti tofauti yenye mila na desturi zake, lakini pia kuna mifumo mingi inayoongoza maisha yetu bila kujua nani mwanzilishi wa mifumo hiyo na kwa kusudi gani? Na je hii mifumo ndio kila kitu katika maisha yetu?

Wengi wetu tuliaminishwa vitu vingi tukiwa wadogo tukiwa hatuna uwezo wa kuhoji tukakubali kuishi maisha hayo hata kama hatuna furaha nayo, wachache wanaenda kinyume na mifumo iliyowekwa na jamii wanaonekana ni wasaliti.

Binafsi niliacha kwenda kanisani tangu nilipopata kipaimara sikuona sababu ya kumtukuza Mungu anaechoma watu moto, msimamo huu ulinifanya niingie kwenye vita ya watu wanaonizunguka.

Wakuu nyinyi nafikiria nini juu ya kusudi la maisha hapa duniani ni kufuata utaratibu uliowekwa na kuondoka au kuna jambo lingine ila binadamu hatulijui?
 
Fuata msingi uliojengewa na wazazi wako, labda Kama kwa akili zako timamu na kwa msaada wa kimungu utajua fika kuwa hawakuwa kwenye njia halisi vinginevyo kwenda kinyume na waliokuzaa na Mungu anakukataa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna kusudi lolote lakuja duniani, hakuna anaye tuongoza, wanadamu wenyewe tunajiwekea malengo, sawa na wanyama wengine, au wadudu. Wanajiwekea maamuzi yao katika maisha, kutafuta furaha na chakula ilitu kuishi sikuziende adi mda wakufa utakapofika.

Ndio maana wanadamu tumejiwekea dini, ili kutupa matumaini na muongozo wa maisha, tumejitengenezea miungu fake nakuiabudu. Ni kwa sabab tunaitaj kitu kikubwa kutuzid, na tunaitaj kuongozwa.

Hakuna cha Mungu wala Mbinguni, hakuna Mungu mjinga kiasi icho wakuacha viumbe wake wanakufa bila hatia, eti kisa kula tunda. Kama Kweli Mungu yupo, nakweli katu adhibu kutupa kifo na magonjwa eti kisa wazee wetu Adam na Eva wamekula tunda, basi uyo Mungu mpumbavu kuliko kiumbe yoyote yule. Kwa maana ata wanyama na wadudu wanajali watoto zao, sasa Mungu hajali viumbe wake aliowaumba.

So iyo ina prove Mungu hayupo au alishakufa. Means hakuna lengo la binadamu kuja duniani. Tuishi tu kusogeza siku. Nakujitafutia our own purposes. Lakina hakuna main purpose for all.
 
Ndiyo maana kila siku najitahd nijipatie maisha mazuri vinginevyo nitaenda tu kufa bila chochote,haya maisha we yachunguze vizri utabaini cha muhimu ni kula na kuburudika,weka lengo lolote pigania litimie basi mengine ujitahd usivunje sheria za nchi ili mzunguko wa furaha uendelee hizo zingine ni stori za kutishana au kufarijiana,

Ukifikiria tena vzr hmna shida ya stress labda ujitakie hata lisipotimia lengo kwan nini kingekukuta? Hata usipofurahi? Yaan we ishi mpaka utapoona pametosha,ila mi nimeona nijitaftie hela(means of exchange) ilo nile burudani
 
Uhusiano wa Mungu na wazazi wangu unahusiana vipi kwenye swala la maamuzi juu ya maisha yangu?

Siruhusiwi kufikiri tofauti na wao?
 
Maswali kama haya kwa baadhi ya watu ni kufuru!

Mkuu nijuavyo mpaka sasa hatujui lengo ila tunaishi tunazaana, tunakula n.k

Ktk peo zetu tunapembua mema na mabaya kutokana na vile welewa wetu ulivyo!.. binafsi naamini sheria mama za mazingira yetu ndio msingi unaotakiwa kufatwa mengine nyongeza tu!.

Navyofikiria ni kuwa ulimwengu ni mpana Sana na kuna laws nyingi hatujazijua! Siku tukifanikiwa kuyajua nyuma ya haya mengi nafikiri tutajua kinagaubaga..

Naomba nimalizie na kauli Tata!
"Huenda ukawa umeuliza swali ambalo si sahihi"

Sijui kama nitaeleweka kwa hiyo kauli..😅
 
Nadhani maana na malengo ya maisha ni swala subjective, tafuta maana yako binafsi ya maisha then ishi nayo.

Live life to the fullest until you make that great endings.
 
Binafsi naishi bila hofu wala imani japo kuna vitu navitegemea ili maisha yaende mbele zaidi vitu hivyo ni pesa na taasisi inayoniwezesha kupata kipato kinachonifanya niishi bila hofu kabisa

Lengo la mtu kuishi huenda likawepo lakini sio kwa usahihi kama tunavyojua kuhusu mungu na shetani hapo sitii neno japo uchawi na miujiza nimewahi kufanya na vitu vingine sio vya kibinadamu kabisa lakini kwakua nilifanya basi ni vya kawaida kwangu

Kikubwa duniani hapa ni kuishi tu hakuna cha ziada
 
Maswali kama haya kwa baadhi ya watu ni kufuru!
Mkuu nijuavyo mpaka sasa hatujui lengo ila tunaishi tunazaana,tunakula n.k
Ktk peo zetu tunapembua mema na mabaya kutokana na vile welewa wetu ulivyo!.. binafsi naamini sheria mama za mazingira yetu ndo msingi unaotakiwa kufatwa mengine nyongeza tu!.

Navyofikiria ni kuwa ulimwengu ni mpana Sana na kuna laws nyingi hatujazijua! Siku tukifanikiwa kuyajua nyuma ya haya mengi nafikiri tutajua kinagaubaga..

Naomba nimalizie na kauli Tata!
"Huenda ukawa umeuliza swali ambalo si sahihi"

Sijui kama nitaeleweka kwa hiyo kauli..[emoji28]
Mkuu unaweza kuliweka swali sawa ili iwe kama mwendelezo wa kujifunza vitu tofauti
 
Ni swali gumu sana ila kusudi unaweza kuliweka hata wewe
 
Mkuu unaweza kuliweka swali sawa ili iwe kama mwendelezo wa kujifunza vitu tofauti
Hiyo kauli nimeandika kwa maana hii,

Bado hatujajua laws zote kwenye huu ulimwengu hivyo huenda kuuliza kwako lengo la uhai kukawa kunapingana na hizo laws!!

I mean zenyewe hazisimami kwa lengo!!
Hizo ni fikra zangu tu!!.

Na vilevile huenda swali lako likawa linajibika ktk namna ya tofauti na vile tunavyodhania!… Ulimwengu ni mpana sana mambo ni mengi hatujayajua yote..

Usiumize kichwa hilo langu ni nadharia tu!
 
Hakuna kusudi lolote lakuja duniani, hakuna anaye tuongoza, wanadamu wenyewe tunajiwekea malengo, sawa na wanyama wengine, au wadudu. Wanajiwekea maamuzi yao katika maisha, kutafuta furaha na chakula ilitu kuishi sikuziende adi mda wakufa utakapofika.

Ndio maana wanadamu tumejiwekea dini, ili kutupa matumaini na muongozo wa maisha, tumejitengenezea miungu fake nakuiabudu. Ni kwa sabab tunaitaj kitu kikubwa kutuzid, na tunaitaj kuongozwa.

Hakuna cha Mungu wala Mbinguni, hakuna Mungu mjinga kiasi icho wakuacha viumbe wake wanakufa bila hatia, eti kisa kula tunda. Kama Kweli Mungu yupo, nakweli katu adhibu kutupa kifo na magonjwa eti kisa wazee wetu Adam na Eva wamekula tunda, basi uyo Mungu mpumbavu kuliko kiumbe yoyote yule. Kwa maana ata wanyama na wadudu wanajali watoto zao, sasa Mungu hajali viumbe wake aliowaumba.

So iyo ina prove Mungu hayupo au alishakufa. Means hakuna lengo la binadamu kuja duniani. Tuishi tu kusogeza siku. Nakujitafutia our own purposes. Lakina hakuna main purpose for all.
Mkuu umesha kuwa jirani na wakati mtua anayekata roho, majuto anayoyapata huwezi pima kama anataka kata rufaa, yaani achiwe hata sekunde chache atekeleze kitu fulani kabla hajakata roho. Kila kitu kina kusudi la kuwepo just look arround you, excepy you.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndiyo maana kila siku najitahd nijipatie maisha mazuri vinginevyo nitaenda tu kufa bila chochote,haya maisha we yachunguze vizri utabaini cha muhimu ni kula na kuburudika,weka lengo lolote pigania litimie basi mengine ujitahd usivunje sheria za nchi ili mzunguko wa furaha uendelee hizo zingine ni stori za kutishana au kufarijiana,

Ukifikiria tena vzr hmna shida ya stress labda ujitakie hata lisipotimia lengo kwan nini kingekukuta? Hata usipofurahi? Yaan we ishi mpaka utapoona pametosha,ila mi nimeona nijitaftie hela(means of exchange) ilo nile burudani
Iko sababu ya wewe kuishi, must you are missing something.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maswali kama haya kwa baadhi ya watu ni kufuru!
Mkuu nijuavyo mpaka sasa hatujui lengo ila tunaishi tunazaana,tunakula n.k
Ktk peo zetu tunapembua mema na mabaya kutokana na vile welewa wetu ulivyo!.. binafsi naamini sheria mama za mazingira yetu ndo msingi unaotakiwa kufatwa mengine nyongeza tu!.

Navyofikiria ni kuwa ulimwengu ni mpana Sana na kuna laws nyingi hatujazijua! Siku tukifanikiwa kuyajua nyuma ya haya mengi nafikiri tutajua kinagaubaga..

Naomba nimalizie na kauli Tata!
"Huenda ukawa umeuliza swali ambalo si sahihi"

Sijui kama nitaeleweka kwa hiyo kauli..[emoji28]
Taking things for granted sio poa, we unazani kwa nini una akiri ya kupambanua mambo, use it.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
binafi naishi bila hofu wala imani japo kuna vitu navitegemea ili maisha yaende mbele zaidi vitu hivyo ni pesa na taasisi inayoniwezesha kupata kipato kinachonifanya niishi bila hofu kabisa
lengo la mtu kuishi huenda likawepo lakini sio kwa usahihi kama tunavyojua
kuhusu mungu na shetani hapo sitii neno japo uchawi na miujiza nimewahi kufanya na vitu vingine sio vya kibinadamu kabisa lakini kwakua nilifanya basi ni vya kawaida kwangu
kikubwa duniani hapa ni kuishi tu hakuna cha ziada
Unatofauti gani na kikombe ulichokitumia kunywea chai leo asubuhi, do not just put yourself down and low like that?, jiulize kwani nini huliziki hata ufanikiwapo malengo yako uliyojipangania, you still fill like there is something more which you need to do to get satisfaction.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom