game theory, nisaidie jambo moja ni nchi gani ya Kiafrika ambayo chini ya viongozi wake imefanya vizuri zaidi katika kipindi cha miaka 23 wakati Mwalimu anatawala Tanzania? Hiyo itatusaidia kuona ni nchi gani zilipiga hatua kuuuuuuuubwa ya maendeleo kuliko Tanzania ya Mwalimu ambayo imerudi nyuma miaka 50!?
Mwanakijiji,
Mtu yeyote unayeona anasema Mwalimu,katurudisha nyuma,ni kheri kumuonea huruma tu,maana hajui alifanyalo,na wala hamjui mwalimu hata kidogo,tunaomjua mwl,sina hata la kuongea,Narudia tunaomjua mwl,basi Mungu ndiye ajuaye alitupa mtu gani?Kweli mnadiriki kusema mwl katurudisha nyuma kwa lipi?The guy was smart,na nia yake ilikua
kumkomboa mlala hoi,ndiyo maana hata yeye alikua anaishi maisha ya kawaida kabisa,haijawahi kutokea Afrika kiongozi kuishi kama maisha alioishi Nyerere,kufanya kazi kwa vitendo.Huyu mzee amelima hadi anaenda kaburini,binafsi nitembelea nyumbani kwake Butiama mara kadhaa,alikua na mashamba makubwa sana,Nyerere alikua anaenda asubuhi shambani,na kurudi saa 8 au tisa,ambapo utamkuta anacheza
bao na wazee wenzake.Alibuni sera nzuri,alichosema ukitaka kumsaidia maskini,ukitaka kufuta umaskini,ukitaka kumkomboa kila mtanzania,basi mpe elimu,na hicho ndicho alichokifanya katupa elimu ya bure,tumesoma bure,tumetibiwa bure,hakujali upuuzi wa IMF na WB,alichojali ni mtanzania anafaidika na uhuru wa nchi yake.
Kuhusu nyumba ya Butiama,navyojua mimi,hiyo nyumba alijengewa na Jeshi,tena alilipinga sana hilo suala la ujenzi wa hiyo nyumba,alisema mimi sio tembo,haka kanyumba nilikonako kananitosha.Niambie Nyerere kachukua kodi yako ipi?Ana makampuni gani?Ana viwanja gani?Ana hisa gani?Nyerere alikua ni maskini kama sisi tu,na hakutaka kuwa tajiri,mbona kama angetaka kuwa tajiri,enzi hizo watanzania tulikua tumelala,mbona angechukua kila kitu.
Kuna siku Nyerere akiwa rais wa nchi,alienda kukopa sukari,kwenye duka la mhindi,akamwambia nikipata mshahara,nitakulipa hela yako.Yule mhindi,akasema chukua mzee hiyo sukari,sitaki uje unilipe hela,Nyerere akasema kama hutaki nije kukulipa deni lako,basi hii sukari sichukui,mie sitaki bure,nitakulipa hela yako.
Eti Nyerere alikua mdini,nyie mnaongea vitu gani jamani?