Nini kitatokea endapo jua litazima/ litapotea?

Nini kitatokea endapo jua litazima/ litapotea?

Asubuhi ule ubaridi unakuta watu wanasubiria jua litoke ili wajianike kama kenge
Sasa likipotea kabisa kama kwenye milima ya uluguru hapo ndio utajua jua lina umuhimu wake
Ni kufa tu
Jua ndio kila kitu boss ndo linakufanya utembee, Ugegede, Ulie . Our Planet is powered by sun
 
Imagine kunapokaribia kukucha hali inakuwaje, na hapo siyo kwamba jua limepotea bali linachoma dunia upande wa pili, so still tunapata joto kwa njia ya mzunguko/muhamo wa hewa. Sasa likizimika siku ya kwanza tu temperature itafika nyuzi 0°C. Siku inayofuata viumbe wasiojisitiri ndani wataganda ya tatu tunafuata sisi
 
Kaka jaribu kuelewa nilichokiandika,naposema huwezi kuona kilicho nyuma yako,hakuhitaji shule hapo ni kwamba hapo hapo ulipo kaa na ulipo elekea huwezi kuona kilcho nyuma yako.

Pili unajengea hoja juu ya movie huku ni kufikiri kimakosa. Nini asili ya movie ni maigizo kama maigizo mengine hupunguza katika ukweli na huongeza katika ukweli,kwahiyo hii si hoja dhidi ya kile nilicho kiandika.

Tuandike ukweli na uhalisia
Mkuu Mimi sikubaliani na wewe, kama in mtazamaji wa muvi hasa kwenye miaka ya 80 na 90 utagundua kuwa vitu vingi ambavyo vilikua vinaigizwa Leo hii no real, yaani vimekua hai..
Anzia kwenye simu za mikononi, video conference, touch screen, silaha za kivita nk nk... viko vingi sana

Tegemea baada ya miaka kumi ijayo kuona haya unayoyaona sasa kwenye muvi yakiwa halisi
 
Uhai wetu na uhai wa Sayari zilizopo katika mfumo wa mzunguko wa nyota Jua wa wetu unalitegemea Jua.

Mwanga wa Jua kufika katika sayari Dunia unatumia dakika nane(8) tu. Kwa mantiki hiyo kama jua likipotea ndani ya dakika 8 tu tutajua ikawa likipotea mchana. Kama ni wakati wake wa kuchomoza( ila Jua lipo siku zote), hilo tutalijua kutokana na kanuni na nidhamu ya nyota Jua kuchomoza kwenye ada yake kuwa tofauti. Hilo likitokea kuna haya yatatokea.

Kuna kaniya gravitational pull iliyopo baina ya nyota Jua na mfumo wa Sayari inayolizunguka Jua. Hii kani inasaidia Sayari ziweze kuzunguka katika mhimili/ mzunguko wake pasipo kutoka katika mhimili( orbit). Jua kama likipotea hii kani haitakuwepo. Kutokana na kanuni na nidhamu ya Jua, mwanga wake hufika Duniani kwa dakika 8 tu; Wataalamu wanasema ndani ya dakika 8 hizohizo Dunia itahama kwenye mhimili( orbit) wake na si Dunia tu bali na Sayari zilizopo kwenye Mfumo wa Jua letu nazo zitahama. Kwa hiyo, eidha zinaweza kuelekea katika uelekeo wa "straight " au zikagongana.

Mwezi nao hautoonekana, kwa nini? Kwa sababu mwanga wa mwezi hutokana na kuakisiwa kwa mwanga wa Jua. Kwa hiyo kutakuwa ni Gizaaaa. Na ufahamu vilevile kuna kani iliyopo baina ya Mwezi na Dunia sasa sielewi sijui itakuaje.

Oxygen itakuwa ndogo. Mchakato was photosynthesis kwa mimea huzalisha oxygen, hewa ambayo tunaitumia sisi na viumbe wengine. Jua lisipokuwepo Photosynthesis itafanyikaje? Na sayari Dunia mimea nayo ipo mengi kwa kiasi chake.

Baridi na Kuganda kwa Bahari. Ukitaka kujua hili angalia Sayari zilizo mbali na Jua utafamu hili. Kingine tutashindwa kuishi si unajua baridi inamfanya binadamu kishindwa kupumia vizuri ikiwa kubwa? Waulize watu wanaoishi sehemu za juu ya Milima yenye baridi watakupa jibu murua zaidi.
 
Wadada wa kasi watapata tabu sana kutoka kwa mabosi wao wa kiume... Kama nawaona wazee wa kunyatia usiku mabeki tatu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom