Nini kinawakwamisha baadhi mafundi kushindwa kuwa wawazi kwa wateja?

Nov 2, 2020
68
90
Wakuu habari,

Nimekuwa najiuliza,Nini kinawakwamisha baadhi mafundi kushindwa kuwa wawazi kwa wateja?

Hali hii utokea pale fundi aidha wa ujenzi, viatu au hata nguo kushindwa kuwa muwazi kwa mteja,hasa juu ya lini kazi yake itakamilika.

Japo ifahamike si wote wenye tabia hiyo,Lakini wengi wa mafundi wekuwa si wakweli wa kutimiza ahadi kwa wakati.

Sasa mafundi,Kwani Kuna ubaya wowote kumuambia mteja wako kuwa Nimebanana na kazi , nimepokea nitaifanya kwa muda huu na mfano wake?Ili kuepusha usumbufu usio na lazima?

Youth Worker
Hardness,Teaches
 
Mafundi ujenzi waaminifu kwenye muda,kwasababu kama ni kazi muda wote anakuwa sait,ma hata akipata tatizo team yake itaendelea na kazi.
Udhaifu huwa kwenye wizi wa vifaa kwa baadhi yao,wengi hawana shida.
 
Tatizo la mafundi wengi ni kutojielewa, kushindwa kusimamia kazi zao kwa wakati, kushindwa kupangilia kipato chao na hapo hujikuta anachukuwa kazi nyingine ili apate advance itakayo msukuma kabla hajamaliza kazi aliyonayo.

Mwisho siku hujikuta amepoteza uaminifu na kuanza kumkimbia mteja. Kabla hujafikiria kumpa kazi fundi jaribu kumchunguza kidogo kabla hujaingia kwenye kero. Wapo mafundi wanaojielewa!
 
Mafundi wengi wanakuwa na tamaa. Anaweza akakubali kazi 4 kwa wakati mmoja wakati anajua hana uwezo wa kuzikamilisha kwa wakati.

N.B fundi asiye na longolongo ni kinyozi tu.
 
Back
Top Bottom