nini kinakukera jf?

nini kinakukera jf?

Bishanga

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2008
Posts
15,321
Reaction score
10,077
jf ina raha zake (ndo mana tunaendelea kuwemo) lakini pia karaha zipo.Mdau hebu taja yanayokukera humu.
Binafsi nakerwa na yafuatayo:
1.Utakatifu: Kuna watu humu wanajitia wao ni watakatifu kuliko ma Sheikh wakuu na Maaskofu.Kwanini utake watu waishi kwa standards zako? live and let live bana.Yaliyobaki we niache na Mola wangu.
2.Ujuaji: Mtu anajikunja anarusha ka thread kake (tena maskini kalipia alfu internet cafe),we una comment '****' haki kweli? si umpotezee tu kuliko kumshushua?
3.Font: jamani font nyingine tunatumia zinaumiza macho hata kama umeandika mi pweint.
4.Hatimkato: Sa ingine mtu anaandika mambo ya msingi lakini lo lugha za sms...m2 huyu 2ro bcoz nampenda ur...jamani ndo nini sasa?
5.PM: Kuna watu humu (wanajifahamu) wame block kupokea PM,juu ya nini? saa ingine tuna maneno matamu na ya siri ya kukuPM,wewe flan wewe (name withheld) umeblock PM,unblock please nikunong'oneze kitu.

.........na wewe nini kinakukera.....?????
 
Bishanga kweli umeshindwa kumwekea ndugu yako wa damu nitonye mdhamana kwa PAW?.. Siamini!

Nakerwa na namba 4 mnoo!
 
5.PM: Kuna watu humu (wanajifahamu) wame block kupokea PM,juu ya nini? saa ingine tuna maneno matamu na ya siri ya kukuPM,wewe flan wewe (name withheld) umeblock PM,unblock please nikunong'oneze kitu.

Kudadeki, hii imenifanya nicheke..
Kwa mantiki hiyo hawa watu watakuwa wanakereka wanapotumiwa PM..
 
Bishanga kweli umeshindwa kumwekea ndugu yako wa damu nitonye mdhamana kwa PAW?.. Siamini!

Nakerwa na namba 4 mnoo!
are you serious bwanako kalambwa ban? alimtongoza nani?
 
Kudadeki, hii imenifanya nicheke..
Kwa mantiki hiyo hawa watu watakuwa wanakereka wanapotumiwa PM..
hayajakukuta mkuu? hebu jaribu kumPM......uone kama itaenda,sijui ana maana gani kublock PM.
 
Naogopa kuchakachua hii kitu, mbona ulinikimbia kwenye ule mtoko?
Tumeshatoa kero zetu hivyo ruksa kuchakachua huku tukimsubiri Bishanga azifanyie kazi...

Sikukukimbia libent, ujue wakati najiandaa kutoka nikapata taarifa kuwa nitonye kaswekwa lupango hivyo ikabidi niende kumpelekea chai... Hata hivyo bado nashughulikia dhamana!
 
Huyo nitonye ni kaka ako au?
 
Kalambwa toka ijumaa usiku asee, sijui alimtongoza nani lol.... Kwani PAW hapokei rushwa?
wala isikusumbue,ngoja niende kwa babu mlingotini.
btw kwenye mmu kuna mdau kafungua thread anauliza wanawake kwa nini mnacheat.
 
Habari yako bishanga,Mie bado mgeni sijapata la kunikera zaidi ya kufurahia kuwa member humu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom