Bwaga ya moyoni
Senior Member
- Aug 21, 2012
- 147
- 76
@ Cheichei2010, pengine hatutendi haki kwa wengine na tunaharibu mjadala kwa kuleta msisitizo katika mambo ya uongo kwasababu tu tunamatatizo na huyu mama. Kwa jinsi ninavyoelewa mimi na nikiwa mmoja kati ya watanzania wenye interest na ziwa Nyasa, ishu ya ushoga hapa siyo mahali pake. Isitoshe, huyu mama hajawahi kuhalalisha ushoga kama ambavyo sisi tungependa kuwaaminisha baadhi ya watanzania ambao hawana uwezo wakujitafutia habari wenyewe. Mapak sasa alichokifanya huyu mama ni ku-repeal sheria kandamizi ya vyombo vya habari na kumuondolea waziri wa habari mamlaka yakufungia gazeti kama ilivyo hapa kwetu hivi sasa. Sheria hiyo kandamizi ilitungwa na aliyemtangulia. Ameweza pia ku-repeal sheria kadha kandamizi kwa demokrasia zilizotungwa wakati wa utawala wa aliyemtangulia.
Kuhusu Ushoga, tafuta popote pale na utakachopata tu ni kuwa aliwahi kusema anafikiria ku-repeal sheria ya 'Indecency and Unnatural acts' ambayo ingeweza kuhalalisha vitendo vya ushoga lakini akawa makini kwa kusema hataweza kufanya hivyo mpaka apate kibali cha wananchi wake ambao wote kwapamoja wamekataa. Hivi sasa ameruhusu mjadala mpana kuhusu swala hili ambapo hata mawaziri wake wanazungumza hadharani kuwa hawataki. Naamini hawezi kufanya kitu kama hicho kwani akifanya hivyo atakuwa amejisafishia njia ya kuutema urais mwaka 2014. Nimeona nitowe clarification kwani ni wengi tulioingia katika mkumbo wakuamini uongo huu kuwa jirani zetu wamalawi wamehalalisha vitendo vya ushoga na hivyo kuhatarisha maisha ya vijana wetu, haswa sisi tunaozunguka Ziwa Nyasa.