Nini kinaendelea Malawi?

Inaelekea matokeo siyo mazuri, maana siku ya kwanza mbwembwe zilikuwa nyingi. Baada ya hapo media za Tanzania na Malawi ziko kimya, walioenda kujadili nao wako kimya! Hata balozi wetu aliyenza kwa majigambo sasa yuko kimya!!!
Ni lazima yawe magumu!... Tulikuwa tunamiliki sehemu ya ziwa hilo hata kabla ya makubaliano ya mwaka 1890 kati ya mjerumani na mwingereza. Kando ya ziwa kulikuwa na wanyasa upande wa malawi na wamanda, wanyakyusa, wakisi, n.k. upande wa Tanzania - kando ya ziwa. Makubaliano ya wageni yananyang'anya haki za wenyeji!!!!!!............. NINAWATAKIA KILA LA KHERI WATANZANIA WANAOSHIRIKI VIKAO HIVI WATETEE HAKI YA WATANZANIA!.. ...
 
janja ni kuwazunguka Malawi na kutafuta makampuni ya mafuta na kuyapa tenda ziwa nyasa halafu tuone kama edwadi lowasa wa malawi atasema nao wako tayari kwa vitaz
 
Hebu waeleze, internet imekuwa forum ambayo mtu anaweza kujionyesha ujinga wake mradi tu ID imefichwa.
Naomba kwanza u declare interest kuwa wewe ni mnyasa maana post zako zote hazina uzalendo nashindwa kukuelewa wewe nimtanzania waina gani!hata kama kweli ziwa ni la wamalawi tunatakiwa tuonyeshe dunia mpaka saa ya mwisho kuwa tulilidai ziwa hilo hatuwezi kuliacha likachukuliwa kiholela hata wakichukua wawe wametoa jasho!Lakini wewe inaelekea hata walivyofukuzwa City water uliuzunika ndugu yangu Nikupateje maana swala lauzalendo nikama yangeyange na kupe!
 
Last edited by a moderator:
Mie napata hisia kuwa huu mpango ni wa muda mrefu hasa baada ya ile ramani kuonyesha hilo ziwa liko Malawi.Then hizi chokochoko zilipoanza,huyu mama alikubali haraka sana wazo la mashoga.kisha mama Clinton kapay visit huko,saa hizi Blair.Pengine ni mapema sana kuliongelea hili ngoja tusubiri.Lakini nina wazo moja.Kuna yule mzee aliandika vitabu vya Jiographia na alitengeneza ATLAS, anaweza akatusaidia.Kwa watu walo karibu naye wanaweza kutusaidia kwa hilo.Anaitwa Mzee Mbando.anaweza naye akatupa mchango wake,wakati wa kuchora ile ramani ya Tz,alielekezwa mipaka ni ipi.Ni wazo langu tu.
Hapo kwenye RED ni RED kweli kweli. Kaaazi ipo!
 
Katiba ya nchi yetu haimpi mamlaka Rais, Bunge, Mahakama wala mtu mwingine yeyote ya kubadilisha mipaka ya nchi yetu. Wanaoenda kwenye mazungumzo wanafanya hivyo kufulfill requirements za kidiplomasia tu, lakini sio kuamua kama wagawe sehemu ya Tanzania. Atakayetangaza kubadilisha mpaka wa Tanzania anatafuta ugomvi na watanzania. Wamalawii wakienda mahakamani wataenda kuishitaki hewa? kwa sababu nchini kwetu sisi hakuna mtu mwenye mamlaka ya kutekeleza hukumu ya kubadili mpaka wa nchi.
Kukubali kupeleka shauri mahakamani ni ishara ya kutokuamini umiliki wa ziwa letu. Hivi wakenya leo hii wakisema mlima kilimanjaro ni wao, wakaanza kuleta kampuni la kufanya utafiti mlimani, tutasema twende mahakamani? Tangu lini nchi yetu imeanza kutegemea mahakama za kigeni kulinda mipaka yetu? Mpaka wa Tanzania na Malawi is not an exception, ulindwe kama mipaka mingine.
 
hakuna mwafaka wowote uliofikiwa mpaka sasa

It was expected.Lakini kwa mitanzania tulivyo.Hata kama tukinyang'anywa business itaendelea as usual.tutapiga unafki wetu kwenye magazeti siku mbili tatu then inajitokeza Bibi wa Loliondo na kikombe chake tunasahau kila kitu.Tanzania rahisi sana kuiongoza.Kama dhaifu ameweza nani basi atashindwa?
 
Kukubali kupeleka shauri mahakamani ni ishara ya kutokuamini umiliki wa ziwa letu.
Umeongea kinyume hapa mkuu

Wamalawi wanalitaka ziwa lote. Wamekaa na kupata mtazamo wetu.Sasa kama wanaona hoja zetu ni dhaifu na wana ushahidi wa kuishawishi ICJ, kwanini wanasuasua kufanya hivyo?

Na sisi Tanzania kama tunaona tuna ushahidi wa ngoma dro kwanini tusipate ujasiri wa kuruhusu Malawi wapeleke hili suala ICJ

Suluhisho la haki hupatikana mahakamani.Na maamuzi ya mahakama yataheshimiwa na sisi sote

MY TAKE:Ziwa limeshauzwa hilo. Kinachofanyika hapo ni pre-emptive measures. Wanasheria hao wa nchi mbili wakutane ili wajadili ni jinsi gani Werema atajitetea kama mwanasheria wetu mkuu iwapo atatakiwa afanye hivyo siku za mbele
 
Mkuu, hili swala siyo la kupeleka mahakamani.
Hivi wakenya wakisema mlima Kilimanjrao ni wao na wanataka tupeleke kesi mahakamani, utakubali?
Ndio maana nasema kukubali kupeleka shauri mahakamani ni kukubali kuwa hatuna uhakika na umiliki wetu.
Kesi ikienda mahakani ni kuipunguzia Tanzania nguvu na kuwaongezea nguvu wamalawi.
 
Lazima tuwe thabiti na hili suala, hata kama watatembelewa na Obama, lazima tugangamale, kuachia ziwa Nyasa aka Malawi kutafanya hata Mbamba Bay pia waitake, na huku Kagera wataibuka tena akina Kaguta na isitoshe Kenya pia inaweza kuja na ndoto za kuutaka Mlima Kilimamnjaro. Lazima tuwe no uthubutu hapa!
 
Mkuu, hili swala siyo la kupeleka mahakamani.
Hivi wakenya wakisema mlima Kilimanjrao ni wao na wanataka tupeleke kesi mahakamani, utakubali?
Ndio maana nasema kukubali kupeleka shauri mahakamani ni kukubali kuwa hatuna uhakika na umiliki wetu.
Kesi ikienda mahakani ni kuipunguzia Tanzania nguvu na kuwaongezea nguvu wamalawi.

Dah! Wakenya wakisema mlima ni wao hatutawapuuza tutajiuliza ni mamlaka gani inawapa nguvu ya kudai hivyo

Mkuu mahakama zimeundwa ili zitoe haki.

Unaonekana ukiwa kiongozi hutojali rule of law. Utakuwa dikteta.
 
Conclusion yako siyo sahihi. Nikiwa kiongozi sitaruhusu mahakama za nje zipewe nguvu kuamua mipaka ya Tanzania.
Kiongozi anachotakiwa kufanya ni kulinda mipaka siyo kubargain mipaka.
 
Conclusion yako siyo sahihi. Nikiwa kiongozi sitaruhusu mahakama za nje zipewe nguvu kuamua mipaka ya Tanzania.
Kiongozi anachotakiwa kufanya ni kulinda mipaka siyo kubargain mipaka.
Leo utapigana na Mmalawi, kama ulivyosema hata mlima Kilimanjaro ni controversial, kuna uwezekano wa kupigana na Mkenya

Kagera nako Waganda wanasema yao. Utapigana vita ya tatu hiyo.

Rwanda/Burundi nao watasema kabla ya mkataba wa Ubelgiji na Mwingereza wa mwaka 1920 Kigoma ilikuwa upande wao.

Je utaweza kupigana vita hizo zote nne?

Mahakama ndiyo suluhisho. Migogoro mingi ya namna hiyo imetatuliwa na mahakama

Unaweza ukatetea mipaka yako kwa vita hata tukiwashinda wanaweza wakaamua kwenda ICJ
 
Kwa hiyo leo hii mahakama ikisema Kagera ni ya Uganda wewe uko radhi kuheshimu hukumu hiyo?
By the way, kama unadhani vita is a no go zone, jeshi la nini sasa? We will do everything kuavoid vita, lakini that option can not be removed from the table.
 
Mkuu mahakama zimeundwa ili zitoe haki.

Hiyo ni nadharia tu. Unadhani wanaoshiriki kutatua mgogoro wa waisrael na wapalestina ambao ndio mgogoro mkubwa wa ardhi duniani hawajui kama kuna mahakama?
 
Hiyo ni nadharia tu. Unadhani wanaoshiriki kutatua mgogoro wa waisrael na wapalestina ambao ndio mgogoro mkubwa wa ardhi duniani hawajui kama kuna mahakama?

Labda nikuulize wewe mbona mataifa yanayoiunga mkono Palestina ni mengi kuliko yanayounga mkono Israel

Huoni kama kuna hujuma zinafanyika ili kumsaidia Muisrael?
 
Back
Top Bottom