Nini Kimemkuta Hasheem Thabeet?

TinyMonster

JF-Expert Member
Jun 15, 2009
248
154
Habari wanajamvi...

Nadhani kila mtanzania alifurahi sana mwenzetu Hasheem Thabeet Manka alipokuwa drafted kuingia ligi ya NBA na kutokana na uwezo wake aliouonyesha akiwa UConn tulihisi atafanya mambo makubwa sana akiwa na Mempis Grizlies. Lakini kwa bahati mbaya mambo hayakumuendea vizuri, perfomance yake ikawa mbovu hadi ikafikia wakati coach wa Griz akawa hampangi kwenye match nyingi mfululizo au kupewa dakika chache tu za mchezo. Mwanzoni nilihisi labda Coach Lionel Hollins ana chuki binafsi lakini baada ya ku-google nimegundua Hasheem ameshindwa kuonyesha uwezo wake wa UConn. Wengine imefikia hatua wanasema draft ya Hasheem Thabeet ni mbovu tangu Darko Milic. Alikuwa na wastani points 1.2 na 1.7 rebounds kwa kila mechi ambacho ni kiwango kibovu kwa mtu wa level yake.

Ninachotaka kujua kwa wana-JF mnaomfahamu huyu kijana wetu, nini kimemtokea? kwanini amepoteza kiwango chake?

Nawasilisha hoja.
 
Hasheem.jpg

Hasheem Thabeet ... - Global Publishers
 
He was punching above waight.....labda atarudi tena....ye sio wa kwanza...
 
Majivuno,kujisahau,starehe,haya tusipoyaangalia hata sie tutakuwa tunarudi nyuma,and i think this is vry serious to players,artists,acto resse(s) so forth in Tanzania
 
Hashimu nahisi hajutii kuporomoka kwake, kwa sasa kaja bongo kusalimia mama yake na atakaa kwa wiki tatu.
Cha kujiuliza, hizi wiki tatu si zingetosha kufanya mazoezi ya kutosha na kujifua ili msimu ujao walau aonyeshe kuwa anaweza??

Sasa hapa bongo wiki tatu anfanya nini?Anyway ni maisha yake binafsi,kula bata Hashimu.
 
Makocha wote wawili walikuwa hawampangi (8 min per game Memphis), wa Huston ndo kabisa(2 min per game!), at least kocha katimuliwa now maybe mambo yatabadilika.

Hasheem ni long term project anahitaji kocha ambaye analikubali hilo.

Season mpya mpaka October, so sio vibaya akikaaa wiki 3 Bongo.
 
Hashimu nahisi hajutii kuporomoka kwake, kwa sasa kaja bongo kusalimia mama yake na atakaa kwa wiki tatu.
Cha kujiuliza, hizi wiki tatu si zingetosha kufanya mazoezi ya kutosha na kujifua ili msimu ujao walau aonyeshe kuwa anaweza??

Sasa hapa bongo wiki tatu anfanya nini?Anyway ni maisha yake binafsi,kula bata Hashimu.

Kaja kukazia Mitishamba! Wabaya wake wanamwangalia jicho baya lazima afanyiwe mabo yetu ya kiasili. Am i wrong hapo? Ndo zetu, azi yuzhyooo!!
 
Nahisi ana laana ya mkataa kwao, alikuja bofongo kipindi kile, kwenye mahojiano EATV akajifanya hata Kiswahili hakipandi,.. Akawa anaongea kama wazungu wanaojifunza... Kama hujanielewa, alikuwa anazungumza kama yule Sharobaro(msanii wa Bongo Movie wa comedy). Yaani alinichefua mpaka basi, na mimi ni mmoja kati ya waliopiga dua la kuku!
 
Habari wanajamvi...

Nadhani kila mtanzania alifurahi sana mwenzetu Hasheem Thabeet Manka alipokuwa drafted kuingia ligi ya NBA na kutokana na uwezo wake aliouonyesha akiwa UConn tulihisi atafanya mambo makubwa sana akiwa na Mempis Grizlies. Lakini kwa bahati mbaya mambo hayakumuendea vizuri, perfomance yake ikawa mbovu hadi ikafikia wakati coach wa Griz akawa hampangi kwenye match nyingi mfululizo au kupewa dakika chache tu za mchezo. Mwanzoni nilihisi labda Coach Lionel Hollins ana chuki binafsi lakini baada ya ku-google nimegundua Hasheem ameshindwa kuonyesha uwezo wake wa UConn. Wengine imefikia hatua wanasema draft ya Hasheem Thabeet ni mbovu tangu Darko Milic. Alikuwa na wastani points 1.2 na 1.7 rebounds kwa kila mechi ambacho ni kiwango kibovu kwa mtu wa level yake.

Ninachotaka kujua kwa wana-JF mnaomfahamu huyu kijana wetu, nini kimemtokea? kwanini amepoteza kiwango chake?

Nawasilisha hoja.

Waswahili wanasema "alivimba kichwa" na mafanikio yake ya mwanzo. Kuna kipindi alirudi Tanzania akadai kwa majivuno "hakuna mtu aliechangia mafanikio yake". Japo sifurahii yanayomkuta, lakini kuna msemo wa Kiingereza unaosema, "Pride comes before a fall".
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom