tunaanza kuwa wadaku.
Mlitaka afanyaje? Tuelezeeni kile alichokifanya na alitakiwa afanyeje!
Rafiki yangu Fair Player,
Hapa hakuna udaku, nadhani watu wanataka kupata ukweli wa hili swala na ndio maana akina Balile wamelivalia njuga, whether ni kwa manufaa ya Boss wao [mmiliki wa gazeti la Jamhuri] au ku-divert attention.
Kwenye habari za gazeti la Jamhuri, Mwalimu wa Nyerere amekiri kwamba alipinga mwanafunzi wake kupelekwa UK kutibiwa. Huyu mzee bado yuko hai.
Gachuma yuko hai na yeye alikuwa ni shahidi kwamba baada ya kusikia Mwalimu ni mgonjwa ilibidi ajitolee kumpeleka Nairobi akatibiwe na yeye amehojiwa akakubali.
Sasa hapo udaku uko wapi?
Swala la kujiuliza ni kwamba mpaka Gachuma anaamua kupendekeza Mwalimu akatibiwe Nairobi [kwa gharama za Gachuma], je Prof. Mwakyusa alikuwa wapi? Ilikuwaje mgonjwa awe anaugulia Butiama nyumbani kwake wakashindwa hata kumsogeza japo Bugando au Muhimbili, kama walikuwa wanaona ni ghali kwenda kumtibu nje?
Watu wakimtuhumu Prof. Mwakyusa kwamba alimtelekeza Mwalimu, watakuwa wanafanya makosa? Hivi kweli mgonjwa aliye serious unaweza kumwacha Butiama na ukawa uko Dar na bado ukaendelea ku-claim kwamba wewe ni Daktari unayemhudumia mgonjwa?
Nini maana ya kuitwa Daktari wa Mwalimu? Hivi leo hii JK akiugua mafua/malaria unadhani yule Daktari wake anaweza kwenda kulala nyumbani kwake akamwacha au akakaa siku 2 bila kujua JK anaendeleaje?
Hapo kwenye udaku, naomba kupingana na wewe. Tayari kuna leading clues ambazo zina point fingers kwamba kuna uzembe ulifanywa japo siwezi kujua kama ni wa makusudi au la.
Naomba nikuhakikishie kwamba hii issue ya Mwalimu haitaisha na ni mtaji wa kuelekea 2015 na atakayekuja kuitumia ni White Hair [utakuja kunikumbusha wakati ukifika maana najua uko kambi ya Lowassa].
Jamii imeaminishwa kwamba EL alikuwa na bifu na Mwalimu, na hivyo inawezekana kabisa kifo cha mwalimu kilileta faraja kwa EL. Lakini baada ya hizi tuhuma za juzi, nina uhakika EL atakuja na nguvu zote kuichimba hii issue mpaka kwenye mizizi ili kubadilisha mtazamo wa jamii kwamba kuna watu wabaya zaidi ambao walisababisha/harakisha kifo cha Mwalimu kwa uzembe au makusudi kwa manufaa yao.
Tuhuma hizi zikichimbwa vizuri sana na kuwekwa sawa, EL anaweza kuzitumia kujisafisha na kuionyesha jamii kwamba wapo watu wabaya zaidi ambao wako tayari kuharakisha vifo vya wenzao kwa manufaa yao. Kwa hiyo zile tuhuma kwamba mafisadi wa CCM wanataka kuwaua wapiganaji, zitaonekana si mali kitu ni cha mtoto ukilinganisha na watu walioharakisha kifo cha Mwalimu. Balile hawezi kukurupuka hivi hivi, lazima kuna kitu kinatengenezwa na huu ni mwaka wa uchaguzi ndani ya CCM na kampeni ndo zimeanza hivyo.
Hili swala litatumia kuua so ya Barua ya Mzee wangu Hamis Kassori [na nilitamani sana nisikie kauli yake kwenye hili sakata maana najua ana mengi sana]. Subiri hili swala litakapoanza kutumiwa na EL ndo utasema sio udaku, ila kwa sasa kwa kuwa bado ni mapema ndo maana unasema ni udaku!