Nini kilipelekea vijana wa Tanzania kuteka ndege ya ATC 1982 Mwanza?

Hao watekaji walishindwa hata kuchungulia madirishani kuona wako wapi?

They were fools.

Sure, but we are greater fools. Anyway, hili lilikuwa tukio la pili la utekaji ndege . La kwanza "limefanikiwa" ndege imetuwa Heathrow airport, watekaji wamenyeshewa mvua kumi na judge mzungu hapo old Bailey. Mwalimu kapigwa butwaa, washenzi kweli hawa. Washenzi sifa maanake.
 
Hii ndege ilimalizia safari zake UK na sio ile ya Dar, ile ya maembe dodo ilikuwa ya Kisoda na wenziwe sio kina Memba, Mousa alikamatwa alipokuwa Kenya akitokea UK kuja kuangalia ustaarabu kama anaweza kurudi TZ
 
Hii ndege ilimalizia safari zake UK na sio ile ya Dar, ile ya maembe dodo ilikuwa ya Kisoda na wenziwe sio kina Memba, Mousa alikamatwa alipokuwa Kenya akitokea UK kuja kuangalia ustaarabu kama anaweza kurudi TZ

Umeeleza vema na kwa kifupi sana mkuu, safi sana!
 
rubani yoyote wa ndege ya biashara na kubwa lazima apate mafunzo ikitokea ndege kutekwa ndio utakuta code kwenye ndege kama 777, 1234 nakadhila, hata ndege ikiwa inaishiwa mafuta au kupoteza mawasilianoa au kuzima moto lazima rubani aweke code ili kupata upendeleo kwa ATC ndege yeyote yenye stress code lazima itapewa upendeleo kwenye kutua hata kama kuna ndege ya raisi basi ndege ya raisi itapelekwa holding
Wale waliojaribu kuteka walishindwa kufahamu code na kushindwa kufahamu mambo yoyote ya ndege kwahiyo rubani alibahatisha kujaribu kuwadanganya na alifanikiwa kwahilo
 

Kweli hao walikuwa washamba, wameokotana kwa maisha ya vijiweni wakaenda kuigiza kweli?

Embe dodo heheee.
 
Februari 1982 Watanzania wanne waliiteka ndege aina ya Boeing 737 ya Air Tanzania ikitokea Mwanza kwenda Dar es salaam.

Ndege ilikuwa na abiria 99. Watekaji walikuwa wakazi wa Dar es salaam mmoja wao akiwa ni dereva wa taksi, wote wanne walikuwa na umri chini ya miaka 30.

Ndege ililazimishwa kwenda kutua Nairobi. Baada ya kujaza mafuta Nairobi watekaji waliamuru marubani kuirusha ndege kwenda London.

Ilipita kujaza mafuta tena Jeddah (Saudi Arabia) kisha Athens Ugiriki kabla ya kupaa kuelekea London. Watekaji hao walikuwa tayari wametoa tishio la kuilipua ndege hiyo endapo wasingesikilizwa madai yao.

Moja ya sharti la watekaji ilikuwa kumtaka Mwalimu Nyerere ajiuzulu Urais wakisema alikuwa ameusaliti ujamaa. Baada ya ndege kutua London watekaji walitaka kujadili madai yao na watu watatu, Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje na Ulinzi wa Tanzania Ndugu Oscar Salathiel Kambona ambaye wakati huo alikuwa akiishi uhamishoni nchini Uingereza, Balozi wa Tanzania wa Uingereza wakati huo Ndugu Anthony Nyaki na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Lord Carrington. Baada ya masaa 26 ya majadiliano mateka wote waliachiwa huru na watekaji walijisalimisha
 
Ni katika mihangaiko ya hapa na pale nikakuta watu kwenye mgahawa mmoja hapa Arusha wakiongelea hili jambo. kwa kuwa nilikuwa siwatambui nikaona si uungwana kuwaingilia kwenye story yao japo nikawa natega sikio kisawasawa maana ilikuwa ikinivutia.

Mmoja anadai kuwa enzi za mwalimu kulitokea watu flani waliteka ndege yenye abiria toka Tanzania hadi Ulaya (hawakutaja nchi). Mwenye kujua hili anisaidie kama ni kweli au ni story za vijiweni tu.....
 
ni kweli ya kwanza waliteka wakatua sudani na watekaji walivunga wanamabomu kumbe maembe walitokea mwanza ya pili sikumbuki ilitokea mkoa gani lakini sikosei walifika zurichi uswiss
 
hao si akina musa membar.
vijana enzi hizo wakisoma novel wanafanya practical.ndege ilipelekwa mpaka london na vijana wakaomba ukimbizi.
 
Hiyo hapo ripoti ya NY times
 

Ni Kweli Kabisa Na Ilikuwa Ni Ndege Ya Tanzania Ambayo Ilitekwa Na Watu Wa Lebanon Ambao Walitaka Kuiteka Ndege Na Kutokomea Nayo Huko Kwao Ila Kwa Bahati Nzuri Sana Marubani Wetu Wa Kitanzania Wakati Huo Wengi Walikuwa Wakitokea Jeshini Hivyo Kuna Rubani Mmoja Ambaye Wengi Mliopanda Ndege Za ATC ( Samahani Kwa Msiopanda Ndege ) Kipindi Cha Miaka Ya Nyuma Bila Shaka Mtamkumbuka Sana Huyu Rubani Mzee Wetu Captain Mapunda ( Ambaye Sifa Zake Kubwa Ni Mbili Moja Yeye Ndiye Huvunja Utaratibu Ule Wa Ndege Ikiwa Inaondoka Na Kutaka Kuruka Ni Lazima Ivute Kasi Kwanza Lakini Kwa Captain Mapunda Hicho Kitu Kwake Kilikuwa Ni Mwiko Ambapo Yeye Akishaondoka Tu Pale Alikuwa Hasubiri Na Badala Yake Akikata Kona Tu Anaiwasha Injini Ya Pili Na Kuondoka Zake Na Sifa Yake Kubwa Ya Pili Ni Kwamba Yeye Kila Uwanja Wa Ndege Anapotua Tu Basi Ni Lazima Kwanza Atashuka Na Kuwahi Kunywa Bia Huku Abiria Mnashuka Na Kupanda Na Akitoka Hapo Ni Mwendo Mdundo ) Captain Mapunda Wakati Huo Kwa Kushirikia Kabisa Na Majeshi Ya Ulinzi Na Usalama Aliweza Kufanya Mawasiliano Ya Siri Na Labda Tu Kwa Faida Yenu Ni Kwamba Pilots Wote Huwa Wana Lugha Yao Ya Siri Ambayo Huitumia Na Watu Wa Control Tower Wakati Wa Matatizo Kama Hayo Ya Kutekwa Angani Hivyo Alichokifanya Captain Mapunda Ni Kuwazuga Wale MAPOPOMA Wa Ki Lebanon Kwa Kuwa Anawapeleka Huko Watakako Wao Kumbe KIDUME Alikuwa Anawasiliana Kwa Siri Na Watu Wa Control Tower Ambapo Kulikuwa Kuna Mzee Mmoja Wa IDARANI ( TISS ) Ambaye Baadae Alikuja Kuwa Mkurugenzi Wao Wa UWT Kwa Mambo Ya Nje ( Jina Kapuni ) Ambaye Ndiyo Alikuwa Akifanya Mawasiliano Na Kumwongoza Captain Mapunda Huku Huyo Mzee Akifanya Mawasiliano Na Majeshi Yetu Ya Ulinzi Na Usalama Na Kumpa Taarifa Zote Rais Hayati Baba Wa Taifa Na Ndipo Captain Mapunda Alipotumia Akili Ya Kuzaliwa Na Ya Kiufundi Ambapo Aliwazungusha Hapa Hapa Dar Na Maeneo Ya Rufiji Ili Kumaliza Kabisa Mafuta Ya Ktk Injini Ili Atue Kwa Tumbo Ktk Nyasi Zile Za Uwanjani Bila Kutoa Matairi Kuepusha Ndege Kulipuka Ukizingatia Ilikuwa Na Abiria Wa Kitanzania Na Kumbukeni Kuwa Ilikuwa Ni Usiku. Hivyo Walifanikiwa Na Captain Mapunda Alipoona Tu Kuwa Kamaliza Mafuta Yote Ktk Matenki Akalishusha Dude ( Ndege ) Hivyo Hivyo Kwa Tumbo Na Iliposimama Tu Akaziambia Zile NJEMBA Kuwa Ametua Mara Moja Jijini Jeddah Ili Aweke Mafuta Na Wale MAPOPOMA ( Walebanon ) Wakawa Wanashangilia Kuwa Mission Accomplished Kumbe Huku Nje Askari Wetu Hodari Na Shupavu Wa JWTZ Walikuwa Wameshaizingira Ile Ndege Na Kilichotokea Tu Ni Kwamba Captain Mapunda Aliwapa Ishara Ndipo Mmoja Wa Wale Watekaji Akajipendekeza Kuja Nje Kuchungulia Ile Anatokeza Tu Na PUA Yake Akala Za Chembe Kadhaa Ndipo Wale Wenzake Nao Wakajifanya Kuwa Wanaweza Mchezo Na JWTZ Wakajibu Mashambulizi Ndipo Wawili Kati Yao Wakauliwa Na Wale Wenzao Kuomba PO Na Mchezo Ukaishia Hapo Na Baada Ya Siku Kadhaa Captain Mzee Mapunda Akazawadiwa Tuzo Na Kupewa Gari Aina Ya Benzi Na Rais. Na Hapa Ndiyo Nimefikia Mwisho Wa UTAMU Wa FILAMU Yetu Nzuri!
 
:clap2::clap2::clap2::clap2::clap2::clap2::clap2::clap2:
 

atleast una idea ya kilichotokea but umekuwa muongo muongo sana katika hii ishu,hebu fanya utafiti kwanza ilikuwaje
 
atleast una idea ya kilichotokea but umekuwa muongo muongo sana katika hii ishu,hebu fanya utafiti kwanza ilikuwaje

Sasa Mwenye IDEA Atakuwaje Tena Na UWONGO? Nishike Lipi Hapo Mkuu? Basi Tufanye Nimekosea Hapo Hebu Wewe Tupe Ya Kwako Mkuu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…