Nini kilimliza Jafo alipotembelea Kibiti.?

Nini kilimliza Jafo alipotembelea Kibiti.?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
371,651
Reaction score
860,930
Waziri wa TAMISEMI Ndugu Selemani Jafo alijikuta akishindwa kabisa kujizuia na kububujikwa na machozi ya kilio alipoenda Kibiti kuzindua ujenzi wa daraja la mojawapo wa vijiji vya wilaya mpya ya Rufiji....

Niliangalia ile clip kwa mshtuko na mshangao nilipomuona waziri anajitahidi sana asilie kwa sauti wakati akihutubia... Nikajawa na fadhaa baada ya camera ya mwandishi kuwageukia wananchi walioshikwa na butwaa na mshangao kumuona waziri akilia.. Pengine nao kama mimi walikuwa wanajiuliza... Analia nini?

Akiwa na siha njema na mwenye shibe alifika kijijini hapo na msafara wake... Yeye alikuwa kwenye gari jipya la kifahari VX V8, lenye kiyoyozi murua huku akilindwa na wanausalama pande zote... Njia ya kufika pale kijijini ilikuwa changamoto kutokana na ubovu wa barabara na mvua zinazoendelea lakini VX lake liliweza kumudu changamoto hiyo na kufika salama pale.

Nikaanza kujihoji kutokana na ujumbe niliouona kwenye nyuso za wakazi wa pale... Je yale machozi ya waziri yalikuwa ya nini? Si ndio kilio cha wakazi wale kimesikiwa na leo ndio ujenzi unataka kuanza?

Kwakuwa tangu kuumbwa kwa dunia hapo mahali hapajawahi kuwa na daraja ama niseme tangu kupata uhuru wa Tanganyika. Miaka yote hiyo tangu uhuru, miaka yote ya serikali za chama kimoja, miaka yote ya kubadili wabunge na wakuu wa mikoa na wilaya hawa wakazi walikuwa wamesahauliwa kabisa...

Mateso waliyopitia kipindi chote hicho si hapa, machozi waliyolia ni mengi.... Na mpaka uzinduzi unafanyika mbunge wa chama hichohicho yupo miaka yote kama wengine
Nikajikuta najiuliza hivi kweli kabisa kupata misukosuko kidogo tu Barabarani ni machozi yote yale? Ndani ya suti nadhifu na gari ya la kitajiri? Sizungumzii posho yake ya siku kwa ziara ile..

Ni nono kama mkia wa kondoo wakati wananchi wale hali zao zinajionesha wazi
Kuonesha hisia kwenye jambo lakini ni vema kuwa na tafakuri na kuchagua njia sahihi ili hisia zako zisigeuke dhihaka ama zisitafsiriwe kama usanii kwa wale uanaojaribu kuwaonsha...

Mwishowe nilijikuta namimi nalia.. Jirani yangu akashtuka na kunihoji kunani kwakuwa kuna watu wakipiga balimi mbili huangua kilio.

Kumbuka hata kilevi cha madaraka huliza....!!!!
 
Anamlilia magu asimtumbue
2.jpg
 
Ingia parliament of Tanzania nenda sehemu ya "view all MPs" ikifunguka utakuta kuna neno "search" kisha andika jina lake itatokea profile yke ikiwepo NAMBA YAKE YA SIMU, e-mail n.k. Mtwangie atakupa habari kamili kwa nini alitoa machozi ambazo ni "first hand information" humu JF utapata PERSONAL OPINIONS ambazo hazitakuwa na tija zikilinganishwa na first hand information.

Thanks mkuu!!
 
Ingia parliament of Tanzania nenda sehemu ya "view all MPs" ikifunguka utakuta kuna neno "search" kisha andika jina lake itatokea profile yke ikiwepo NAMBA YAKE YA SIMU, e-mail n.k. Mtwangie atakupa habari kamili kwa nini alitoa machozi ambazo ni "first hand information" humu JF utapata PERSONAL OPINIONS ambazo hazitakuwa na tija zikilinganishwa na first hand information.

Thanks mkuu!!
Hebu niekeze vizuri jinsi ya kuingia huko parliament Tanzania niweze kufanya hivyo... Na je ni mbali sana? Kuna kiingilio?
 
Amelia kwa sababu anajua uongo wao na Myweather kuwa ni matapeli.Wanawaumiza watanzania sn nafasi zinawasuta
 
Labda kuna Mtu wake wa karibu na aliyekuwa na ushirikiano nae wa Kutukuka wa Kibaiolojia alishawahi kuzama hapo na kutafunwa kama Karanga za Diamond na Mamba enzi hizo.
[emoji15]
 
Labda kuna Mtu wake wa karibu na aliyekuwa na ushirikiano nae wa Kutukuka wa Kibaiolojia alishawahi kuzama hapo na kutafunwa kama Karanga za Diamond na Mamba enzi hizo.
Mkuu umeadimika sana! Uwepo wako uliotukuka ulikosekana sana humu!!
 
Wewe ulitaka acheke au awazomee? Mwafrika siku zote asipowaza ngono basi atawaza majungu tu .. Tena majungu muda Wa kazi.
 
Labda kuna Mtu wake wa karibu na aliyekuwa na ushirikiano nae wa Kutukuka wa Kibaiolojia alishawahi kuzama hapo na kutafunwa kama Karanga za Diamond na Mamba enzi hizo.

Heri ya mwaka mkuu, ulipotea kidogo tukamiss uwepo wapo...
 
Waziri wa TAMISEMI Ndugu Selemani Jafo alijikuta akishindwa kabisa kujizuia na kububujikwa na machozi ya kilio alipoenda Kibiti kuzindua ujenzi wa daraja la mojawapo wa vijiji vya wilaya mpya ya Rufiji.... Niliangalia ile clip kwa mshtuko na mshangao nilipomuona waziri anajitahidi sana asilie kwa sauti wakati akihutubia... Nikajawa na fadhaa baada ya camera ya mwandishi kuwageukia wananchi walioshikwa na butwaa na mshangao kumuona waziri akilia.. Pengine nao kama mimi walikuwa wanajiuliza... Analia nini?
Akiwa na siha njema na mwenye shibe alifika kijijini hapo na msafara wake... Yeye alikuwa kwenye gari jipya la kifahari VX V8, lenye kiyoyozi murua huku akilindwa na wanausalama pande zote... Njia ya kufika pale kijijini ilikuwa changamoto kutokana na ubovu wa barabara na mvua zinazoendelea lakini VX lake liliweza kumudu changamoto hiyo na kufika salama pale
Nikaanza kujihoji kutokana na ujumbe niliouona kwenye nyuso za wakazi wa pale... Je yale machozi ya waziri yalikuwa ya nini? Si ndio kilio cha wakazi wale kimesikiwa na leo ndio ujenzi unataka kuanza? Kwakuwa tangu kuumbwa kwa dunia hapo mahali hapajawahi kuwa na daraja ama niseme tangu kupata uhuru wa Tanganyika
Miaka yote hiyo tangu uhuru, miaka yote ya serikali za chama kimoja, miaka yote ya kubadili wabunge na wakuu wa mikoa na wilaya hawa wakazi walikuwa wamesahauliwa kabisa... Mateso waliyopitia kipindi chote hicho si hapa, machozi waliyolia ni mengi.... Na mpaka uzinduzi unafanyika mbunge wa chama hichohicho yupo miaka yote kama wengine
Nikajikuta najiuliza hivi kweli kabisa kupata misukosuko kidogo tu Barabarani ni machozi yote yale? Ndani ya suti nadhifu na gari ya la kitajiri? Sizungumzii posho yake ya siku kwa ziara ile.. Ni nono kama mkia wa kondoo wakati wananchi wale hali zao zinajionesha wazi
Kuonesha hisia kwenye jambo lakini ni vema kuwa na tafakuri na kuchagua njia sahihi ili hisia zako zisigeuke dhihaka ama zisitafsiriwe kama usanii kwa wale uanaojaribu kuwaonsha..... Mwishowe nilijikuta namimi nalia.. Jirani yangu akashtuka na kunihoji kunani kwakuwa kuna watu wakipiga balimi mbili huangua kilio
Kumbuka hata kilevi cha madaraka huliza....!!!!
Tuonyeshe video hiyo basi tuone
 
Yaani umeshindwa kupiga ramli ukajua sababu au ndo magumashi na wewe pheww
 
Back
Top Bottom