Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,230
- 10,761
Kama ulidhani Mwanza kuna mambo ya samaki tu, basi chukua na hii! Jiji la Mwanza limeingia kwenye kituko baada ya Mkurugenzi wa Halmashauri kutangaza usaili wa ghafla mnamo tarehe 27 kwa askari wote wa Jiji ili kubaini & "wasio na sifa."*
Hapo ndipo wakazi wa Mwanza na Viunga vyake waliposhika vichwa! Hivi tangu lini Mkurugenzi wa Jiji akawa Mkuu wa Jeshi la Polisi au Waziri wa Mambo ya Ndani? Askari wa Jeshi la Polisi wako chini ya wizara husika, sasa huyu Mkurugenzi anayeanza kukagua sifa za askari anatafuta nini? Labda kama alimaanisha Mgambo wa Jiji wale wa kukimbizana na mama ntilie—hapo sawa. Lakini kama ni Polisi wetu wa doria, mbona kama Halmashauri inataka kuvaa viatu visivyo saizi yake?
Kichekesho kikubwa kiko hapa: mtu aliomba kazi, akafanyiwa usaili, akafaulu, akateuliwa, na amekuwa akipiga kazi miaka nenda rudi. Ghafla, mnamo tarehe 27 mwezi huu, anaambiwa, *"Wee mzee, njoo tufanye usaili tena kuona kama una sifa!" Hivi sifa huwa zinaisha muda wake kama biskuti? Ama kweli, hii kali ya mwaka! Hapo wataenda kuuliza kama una kadi ya CCM pekee.
Wadau wanalalamika na kujiuliza, yaani mgambo akose sifa akiwa tayari kazini? Kama kweli hawana sifa, aliyewaajiri mwanzo si ndiye anapaswa kufungishwa virago kwa kutuingiza mkenge?
Ukistaajabu ya Katambi utakutana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza. Hii ni noma sana. Simba akimaliza kula watoto wa Chui ataanza kula watoto wake.

"Huu utaratibu wa kukagua sifa katikati ya safari unatokea wapi? Kama mtu hana sifa, mliwezaje kumpa ajira? Huu ni upuuzi unaopaswa kufuatiliwa hadi ngazi za juu!"