Nini kilikua chanzo cha ugomvi wa Afande Sele na O Ten?

Da'Vinci

JF-Expert Member
Dec 1, 2016
35,686
106,810
Kipindi bifu limeiva Oten alimuimba Sele
Kwenye wembo wa Mimi, Oten anaimba kwamba!

Nilizaliwa Morogoro, hata siku nikifa maiti yangu iende Mor.
Naweka wazi adui yangu asinizike, hata muhuni yoyote asiyenipenda asisogee.
Kama vipi itupeni maiti yangu porini wale tai, muone mimi sifai.

Kama hujui naitwa Filipo nyandindi, na adui yangu mkubwa ni Selemani Msindi(Afande Sele)

Lakini baadae Sele na Oten walitoa ngoma pamoja inatwa Tusahau.

Oten anaimba kiitikio...

"Mimi na wewe kumbuka ni kitu kimoja, tena tumetoka moro mkoa mmoja.
Tusahau yote yaliyopita, na tugange mapya yanayokuja"

Verse 1: Oten anaimba kwamba..

Naepusha mbawa zangu kwa kuonekana mjinga, naamini mti mwema ndio unaopigwa mawe.
Kila kukicha nyandindi ndio naonelewa, nakabidhi roho yangu kwa baba aliye Mbinguni. Rafiki yako mkubwa anaweza kua adui, ila adui yako mkubwa hawezi kua rafiki ila Oten nimesamehe, ninapotoka napajua, ninapoenda sipajui, ndio maana kila siku napunguza maadui,

Verse 2: Afande akaimba..

....Na nywele ni kama akili, yule ana nywele ndefu na yule kipilipili,
Au mwingine nyekundu, na mwengine nyeusi tii
Ilimradi kuna toafauti, kati yetu ndani ya jamii
Hivi nani angetambua, kwmaba kuna kipindi mwezi unapatwa na jua
Ndio mambo yalivyo duniani, vitu kama sunami sio vigeni
Zinagongana meli, magari na ndege juu angani
Hata vidole vyetu mkononi havifanani
Hujawahi ona mama na mwana mda fulani hawaelewani, Sembuse mimi na Oten, Amkeni.

Acheni bifu za kiuni, kama kuanzisha bifu tuanzishe bifu na ukimwi
Yaliyopita sinndwele, sasa tugange ya mbele
Watu hatuna makucha vipi tunaomba Upele, hatueleweki zipi ni pumba zipi ni mchele

Wote ni walewale, kutwa kunyosheana vidole.

...Hilo halipo na kama halipo, basi nakula kiapo
Mnionapo na filipo, popote amani iwepo
Japo shetani hapendi, ila wote tuamini kwa Mungu ni zaidi ya ushindi
!
Leo filipo nyandindi, yuko pamoja na mtu pori baba abdul na selemani msindi

Wajuzi naombeni mnijuze nini kilikua chanzo kati ya Mfalme wa vina Afande na Oten wa East Cost! Je nini kiliwapatanisha..?

Enzi wanatamba hawa watu magari ya kubeba mkaa yalikua hayajaanza kufika kijijini kwetu, stori zao hatukua tunazipata!
 
O_ten mzee wa pamba bifu lilianza baada ya O_ten kutoa NGOMA ya nicheki....

Heyoo nicheki.....ninavyo ng'araaa enzi izo yupo East coast team....

O-ten alitoa NGOMA za kujisifia, kusifu ngono na pombe....
Kitu ambacho mfalme wa Rhymes 🦁 Afande Sele hakupenda.....

Umenikumbusha rafk angu tulipenda ku mwita O_ten mzee wa pamba.....
Alikua anakuja skul na cheni shingoni......
Kuna siku akatongoza mdada mmoja mzur mlokole ukawa msala....O_ten ni mtu wa bring bring... cash money 🤑🤑 umarekani mwingi...majigambo.........

Binafsi nili mpenda O_ten na staili yake ya kuflow....🤓🤓🤓

Afande alikua anawachana wanaimba nyimbo za kuchochea uvunjifu wa maadili.....
 
Afande fala anapangia watu waimbe nini. Nichek ilikuwa bonge la ngoma
Hahhaa umenikumbusha kipind hicho Dully sykes wa moto kulikua na wimbo unaitwa Nyambizi.
Nyambizi nakupenda japo mkubwa, mateso nayopata usiku ni makubwa.
Kwakua tulikua bado wadogo huu wimbo kila ulikua ukifikia wakubwa zetu wanaurusha. Sikuwahi kujua kwa nini...na sikuwahi kuusikiliza tena.

2021 nilikua nimeweka playlist ya Bongo old-school ninazo kama 1600+ ndio ukaingia huu wimbo. Nikaukumbuka nikasema ngoja niusikilize. Nikagundua kumbe ilikua ni halali walikua wanaurusha huu wimbo. Full Porn🏃🏃
 
O Ten Mtoto wa Kilakala
Afande Sele Mtoto wa Misufini
Ugomvi wao kimsingi ni Pomposity ya Sele baada ya kushinda MFALME WA RHYMES.
Aliamini yeye ni Mfalme wa Nchi na hivo pia ni Mfalme wa Moro.
O Ten aliamini yeye Mkali na kile alichopata Afande ni ktk MFALME WA RHYMES ulikuwa ni Mchingo wa akina Erick Shigongo ambao hawakutaka Taji liende kwa wakali wa DAR wakiwemo Prof. Jay, Jay Mo & Solo.
Biff likichangamka baada ya Afande kumdiss OTen kuwa "Nyimbo nzima unataja taja majina tu
Tena kwa mistari iso na vina"
Cha kufurahisha wote hao ni Walevi! Mmoja wa Pombe za Kienyeji na mwengine Majani
 
O_ten mzee wa pamba bifu lilianza baada ya O_ten kutoa NGOMA ya nicheki....

Heyoo nicheki.....ninavyo ng'araaa enzi izo yupo East coast team....

O-ten alitoa NGOMA za kujisifia, kusifu ngono na pombe....
Kitu ambacho mfalme wa Rhymes 🦁 Afande Sele hakupenda.....

Umenikumbusha rafk angu tulipenda ku mwita O_ten mzee wa pamba.....
Alikua anakuja skul na cheni shingoni......
Kuna siku akatongoza mdada mmoja mzur mlokole ukawa msala....O_ten ni mtu wa bring bring... cash money 🤑🤑 umarekani mwingi...majigambo.........

Binafsi nili mpenda O_ten na staili yake ya kuflow....🤓🤓🤓

Afande alikua anawachana wanaimba nyimbo za kuchochea uvunjifu wa maadili.....
Now I can see, sema Afande ndie Mfalme wa Rhymes kweli. Ngoma zake zote vina vimesima. Anafuata Professor Jay
 
Lile Shindano lilikuwa la SHIGONGO na lilipewa Promo na Magazeti yk yake akina KIU et al... Wasanii walikuwa wanatolewa kwa kura za Mchujo mdogo mdogo lkn nakumbuka Majina makubwa yalofika mpk Funal ni Ptof. Jizze, Juma Mchilopanga, Solo Thang Ulamaa & Sele Mwenyewe!

I stand to be corrected
Nani alimpa hilo taji, alishindanishwa na akina nani??
 
Hahhaa umenikumbusha kipind hicho Dully sykes wa moto kulikua na wimbo unaitwa Nyambizi.
Nyambizi nakupenda japo mkubwa, mateso nayopata usiku ni makubwa.
Kwakua tulikua bado wadogo huu wimbo kila ulikua ukifikia wakubwa zetu wanaurusha. Sikuwahi kujua kwa nini...na sikuwahi kuusikiliza tena.

2021 nilikua nimeweka playlist ya Bongo old-school ninazo kama 1600+ ndio ukaingia huu wimbo. Nikaukumbuka nikasema ngoja niusikilize. Nikagundua kumbe ilikua ni halali walikua wanaurusha huu wimbo. Full Porn🏃🏃
Ule wimbo ulijaa matusi, utasikia.....nimeshachoka kupiga puchu.....aaaghgggg, ptuu
 
O Ten Mtoto wa Kilakala
Afande Sele Mtoto wa Misufini
Ugomvi wao kimsingi ni Pomposity ya Sele baada ya kushinda MFALME WA RHYMES.
Aliamini yeye ni Mfalme wa Nchi na hivo pia ni Mfalme wa Moro.
O Ten aliamini yeye Mkali na kile alichopata Afande ni ktk MFALME WA RHYMES ulikuwa ni Mchingo wa akina Erick Shigongo ambao hawakutaka Taji liende kwa wakali wa DAR wakiwemo Prof. Jay, Jay Mo & Solo.
Biff likichangamka baada ya Afande kumdiss OTen kuwa "Nyimbo nzima unataja taja majina tu
Tena kwa mistari iso na vina"
Cha kufurahisha wote hao ni Walevi! Mmoja wa Pombe za Kienyeji na mwengine Majani
Ahsante kwa maelezo mkuu, daah Wengine tulikua ndanindani huko.
Vipi Oten sasa hivi yupo wapi??
Naomba uniwekee picha zake tafadhali za sasa na zamani
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom