mfukunyunzi
Senior Member
- Mar 4, 2011
- 142
- 26
Nimekuwa nikiufuatilia huu muziki wa bongo fleva kwa muda sasa na katika kusikiliza kwangu baadhi ya nyimbo za Hamad 'Madee' aka Rais wa Manzese na Selemani Msindi 'Afande Sele' aka Mfalme sele, nimeona kama hawa wasanii wana 'bifu' la chini chini linaloendelea.
Kwa mfano:
1. Madee ana nyimbo inaitwa 'jinsi game inavyochange' kashirikiana na Godzilla na kuna mstari godzila anasema 'nyimbo zenu (hip hop) hazina swagga halafu mnang'ang'ania airtime' kisha Madee akamalizia kwa kusema 'Nadhani unamaanisha yule mwenye rasta rasta' pia ndani ya wimbo huo huo kuna mstari Madee anasema 'bado hujaona mfalme mwenye rasta chafu? (bado)'.
2. Kwa upande wa Afande Sele ana wimbo unaitwa 'Kingdom' kuna mstari unasema 'hip hop itakulipa vipi wakati unaimba matusi, unatukana ma-ras, unadiss waasisi halafu bado unadiriki kujiita rais wakati huna hata ofisi labda ni rais wa huko kwenu uwanja wa fisi'
3. Madee ana nyimbo mpya inaitwa 'nisikilize' ambayo ndani yake kuna msitari unasema 'yule mkulima alidai eti namgeza, alitamba zamani miaka hii hajaweza, anaumia kwanini mwanzo alicheza, hawezi kuosha nywele ana uhaba wa fedha'
Na kama kuna 'bifu' baina ya wawili hawa sijui chanzo ni nini?