Nini kifanyike kumaliza tatizo la ukatili wa kingono kwa watoto?

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,112
Salaam wana MMU

Ukatili wa kingono kwa watoto umezidi kuongezeka kadri siku zinavyokwenda. Pamoja na juhudi za serikali na jamii bado vitendo hivyo vinaendelea.

Adhabu mbalimbali hutolewa kwa wahusika wanaotenda ukatili huo lakini bado hazijaweza kuzuia mwendelezo wa vitendo hivyo.

Kila siku tunaona na kusikia kwenye vyombo vya habari, watoto wamebakwa, wamelatiwa, wamepewa ujauzito nk.

Asilimia 75 ya watoto duniani na pia Asilimia75 kwa Tanzania hutendewa ukatili huu na ndugu wa karibu, mzazi, marafiki wa familia, waalimu, viongozi wa kidini nk. Na baadhi humaliza kijamaa bila kutoa taarifa ya ukatili huo kwa vyombo vya usalama, hulipana fedha na kuyamaliza kimya kimya.

Pia zipo kesi ambazo hufika kwenye vyombo vya usalama na wakati mwingine ushahidi unakuwa ni ngumu kupatikana hivyo wahusika kuendelea kutesa mitaani hali ya kuwa watoto wananyanyasika kingono.

Wakati mwingine watoto wanalaghaiwa ili kuwaficha wahusika kwa kupewa vitisho au ahadi ya kupewa vitu vya thamani na wanaowafanyia ukatili huo hivyo inakua ngumu wahusika kichukuliwa hatua.

Je nini kifanyike ili kizuia ukatili kwa kingono kwa watoto?

1618552397207.png
 
Back
Top Bottom